Propaganda hii ni chafu haina tija kwa taifa

Propaganda hii ni chafu haina tija kwa taifa

Status
Not open for further replies.

Aman Ng'oma

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2011
Posts
968
Reaction score
542
Sasa hivi imekuwa kawaida kwa matukio ya mauji yanayotokea hapa nchini kuhusishwa na vikundi vya alqaida , alshabab au bokoharam hata kama mauaji hayo yamefanywa na majambazi au watu waliolipizana kisasi kwa wivu wa mapenzi au kudhulumiana.

Maranyingi uhusiahwaji huu unatawala zaidi kwenye midomo ya viongozi wasiokuwa makini na vyombo vya habari uchwara vilivyo biased kwenye kuriport taarifa inayohusu jamii fulani hasa anapouwawa anakuwa mkristo.Hatusikii kauli kama hizo wauliwaji wanapokuwa waislamu.

Ni muhimu kuchunguza mauaji kwa umakini ili kuepuka kupandikiza chuki kwa imani nyingine,haina tija kwa taifa.Ni mara ngapi majambazi wanauwa watu kwa kutafuta vitu wanavyohitji kwa watu/mtu waliyemuua?Hivi vikundi vya alshababy,bokoharam na alqaida tusiviombee kuingia nchini ni hatari sana.Na huko kuwatajataja ni kama kuwachafua kwa wambia wapo nchini ili hali hakuna vikundi hivyo nchini kwetu.

Unamkuta waziri mzima analopoka eti kuna alshababy,mara bokoharam,au alqaida bila hata uchunguzi.Kumbukeni mnacheza ngoma msiyoijua na ni hatari kwa umoja na mshikamano wa nchi yetu.Yani akiuwa kiongozi wa kristo tu basi kuna alshababy,hv ni viongozi wangapi wa kiislam au waislamu wangapi wameuawa hapa nchini mpaka sasa na hata tume haijaundwa kuchunguza?Inafikia wakati mpaka kuna wengine wanasema waliouwawa wamejitakia!!

Tukumbuke kuwa thamani ya uhai iko kwa wote halikadhalika uchungu wa mauti.Dr Mafingo aliuawa huko Bulongwa makete watu wakawa kimya.Kama tunaamua kupaza sauti juu ya mauaji basi tufanye hivyo kwa watu wote bila kuwa biased.

Be blessed all.
 
lini waislam wameuliwa waislam vyombo vya habari havijaandika?
 
Wivu wa ki imani,alafu kwa taarifa yako,wakristu ni waastarabu sana thats why akiuwawa unaona kunakuwa na out cry.
 
Kimsingi nakubaliana na wewe, tunatatizo la kujump into conclusions, hivi majuzi ilifikia hatua baadhi ya watu wakaanza kudai kuna mkakati wa kuhujumu watu wa mbeya wakifanya reference kwa DR Ulimboka, mtangazaji wa channel ten aliyeuwawa iringa na mtu mwingine kama sikosei.

Hii ni kitu mbaya sana, japo kwa kiasi kikubwa inachangiwa na vyombo vya usalama kutokuchukua hatua za haraka kudhibiti uharifu na kutoa taarifa kwa uma au kuonekana kwamba inaacha kutimiza wajibu wake kwa makusudi.

Nadhani watu wengi wanatoa comments zao sababu ya hasira na kutokulidhishwa na utendaji wa serikali. Hivyo ni vyema tukatafakari kama kuna kitu wananchi tunaweza kufanya kuisadia serikali yetu kutimiza majukumu yake.
 
Sasa hivi imekuwa kawaida kwa matukio ya mauji yanayotokea hapa nchini kuhusishwa na vikundi vya alqaida , alshabab au bokoharam hata kama mauaji hayo yamefanywa na majambazi au watu waliolipizana kisasi kwa wivu wa mapenzi au kudhulumiana.

Maranyingi uhusiahwaji huu unatawala zaidi kwenye midomo ya viongozi wasiokuwa makini na vyombo vya habari uchwara vilivyo biased kwenye kuriport taarifa inayohusu jamii fulani hasa anapouwawa anakuwa mkristo.Hatusikii kauli kama hizo wauliwaji wanapokuwa waislamu.

Ni muhimu kuchunguza mauaji kwa umakini ili kuepuka kupandikiza chuki kwa imani nyingi,haina tija kwa taifa.Ni mara ngapi majambazi wanauwa watu mbona kwa kutafuta vitu wanavyohitji kwa mtu waliyemuua?Hivi vikundi vya alshababy,bokoharam na alqaida tusiviombee kuingia nchini ni hatari sana.Na huko kuwatajataja ni kama kuwachafua kwa wambia wapo nchini ili hali hakuna vikundi hivyo nchini kwetu.

Unamkuta waziri mzima analopoka eti kuna alshababy,mara bokoharam,au alqaida bila hata uchunguzi.Kumbukeni mnacheza ngoma msiyoijua na ni hatari kwa umoja na mshikamano wa nchi yetu.Yani akiuwa kiongozi wa kristo tu basi kuna alshababy,hv ni viongozi wangapi wa kiislam au waislamu wangapi wameuawa hapa nchini mpaka sasa na hata tume haijaundwa kuchunguza?Inafikia wakati mpaka kuna wengine wanasema waliouwawa wamejitakia!!

Tukumbuke kuwa thamani ya uhai iko kwa wote halikadhalika uchungu wa maiti.Dr Mafingo aliuawa huko Bulongwa makete watu wakawa kimya.Kama tunaamua kupaza sauti juu ya mauaji basi tufanye hivyo kwa watu wote bila kuwa biased.

Be blessed all.
Hebu sikia viongozi na redio za watu wa imani moja wanasema viongozi wa upande mwingine wauawe!! Kabla serikali kuchukua hatua wanaanza kuuawa!!mmoja mmoja utasemaje au kufikiriaje? Pia jumbe za maandishi zinaambatana pamoja na mihadhara!utaamua lipi?
 
Hivi hao al caeda na al shabab ni ndugu zako? Kinakuuma nini hata kama wanasingiziwa?
Au wanauhusiano na dini yako?

Wivu wa mapenzi mbona alivyofariki Kanumba hatukusema al caeda wanahusika?
 
Hivi hao al caeda na al shabab ni ndugu zako? Kinakuuma nini hata kama wanasingiziwa?
Au wanauhusiano na dini yako?

Wivu wa mapenzi mbona alivyofariki Kanumba hatukusema al caeda wanahusika?

Madhara ya kusingizia vikundi vya kigaidi ni makubwa sana, tusilete mzaha katika hili, alichokisema mleta mada ni sahihi kabisa.
 
Hebu sikia viongozi na redio za watu wa imani moja wanasema viongozi wa upande mwingine wauawe!! Kabla serikali kuchukua hatua wanaanza kuuawa!!mmoja mmoja utasemaje au kufikiriaje? Pia jumbe za maandishi zinaambatana pamoja na mihadhara!utaamua lipi?
Kumbe tuna watu wa wazi kabisa wanaochochea mauaji na badala yake tunakimbilia kusema ni magaidi. vyombo vya habari na watu wanaochochea vurugu ndiyo wa kushughulikiwa mapema iwezekanavyo kabla ya kurukia kusema ni ni AL-QAEDA, BOKOHARAM n,k
 
Tumegawanywa tukagawanyika ni ngumu sana kufikia ukombozi wa kweli. Sasa itakuwa hivi: jambo likikemewa na mkirisitu muisla hataunga mkono na kinyume chake tutagawana kura2015
 
Hivi hao al caeda na al shabab ni ndugu zako? Kinakuuma nini hata kama wanasingiziwa?
Au wanauhusiano na dini yako?

Wivu wa mapenzi mbona alivyofariki Kanumba hatukusema al caeda wanahusika?
MACHAFUKO KATI YA WAISLAMU NA WAKIRISTO GEITA, MCHUNGAJI ACHINJWA HADI KUUAWA

[TABLE="class: cms_table_tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="class: cms_table_tr-caption, align: center"]Hivi ndivyo anavyoonekana Majeruhi Yasin Rajabu na hapa akiwa amelazwa katika wod namba 8 Hospitali ya wilaya ya Geita kwaajili ya kupatiwa matibabu.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="class: cms_table_tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="class: cms_table_tr-caption, align: center"]Hivi ndivyo anavyoonekana Majeruhi Said Ntahompagaze aliyejeruiwa mguu wakati wa vurugu za waislam na wakristu wachache zilizotokea leo katika kijiji cha Buseresere wilayani Chato mkoani Geita na kusababisha shughuli mbalimbali kusimama.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="class: cms_table_tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="class: cms_table_tr-caption, align: center"]Majeruhi Vicent Damon akiwa amelazwa wod na 8 hospitali ya wilaya ya Geita aliyejeruiwa wakati wa vurugu za waislam na wakristu wachache zilizotokea leo katika kijiji cha Buseresere wilayani Chato mkoani Geita na kusababisha shughuli mbalimbali kusimama.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="class: cms_table_tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="class: cms_table_tr-caption, align: center"]Majeruhi Sadick Yahaya.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="class: cms_table_tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="class: cms_table_tr-caption, align: center"]Majeruhi Ramadan aliyejeruiwa wakati wa vurugu za waislam na wakristu wachache zilizotokea leo katika kijiji cha Buseresere wilayani Chato mkoani Geita na kusababisha fukuto kubwa la vurugu zilizosababisha shughuli mbalimbali kusimama.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Machafuko makubwa yametokea leo katika kijiji cha Buseresere Wilayani Chato Mkoani Geita kati ya waslam na wakristu na kupelekea watu 10 kujeruhiwa vibaya kwa mapanga huku mchungaji wa kanisa la Pentekoste Assemblies of God Mathayo Kachila (45) akipoteza maisha kwa kuchinjwa na watu wanaodaiwa ni waumini wadini ya kiislam kisha mwili wake kutelekezwa kwenye vibanda vya maduka ambavyo vilikuwa jirani na eneo hilo.

Habari na picha kwa hisani ya Gsengo Blog

MUTAUWANA SANA MWAKA HUU WATANGANYIKA UBAYA NA CHUKI ZENU ZIDI YA WAZANZIBARI ZITAKURUDIENI WENYENU KWA EWEZO WA M/MUNGU KILA UBAYA MULIOKUSUDIA PROPAGANDA NA AGENDA CHAFU DHIDI YA WAZANZIBARI HAMUTOFANIKIWA

Wivu wa ki imani,alafu kwa taarifa yako,wakristu ni waastarabu sana thats why akiuwawa unaona kunakuwa na out cry.

Tujadili kama ni wakati muafaka kuhusisha matukio ya mauaji yanayoendelea na vikundi vya kigaidi na ndiyo mada iliyoko jukwaani, hayo ya upole wa Wakristo au Waislamu tusiyape nafasi kwa vile yanatugawa wakati sisi ni wamoja.
 
lini waislam wameuliwa waislam vyombo vya habari havijaandika?
MACHAFUKO KATI YA WAISLAMU NA WAKIRISTO GEITA, MCHUNGAJI ACHINJWA HADI KUUAWA

[TABLE="class: cms_table_cms_table_tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="class: cms_table_cms_table_tr-caption, align: center"]Hivi ndivyo anavyoonekana Majeruhi Yasin Rajabu na hapa akiwa amelazwa katika wod namba 8 Hospitali ya wilaya ya Geita kwaajili ya kupatiwa matibabu.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="class: cms_table_cms_table_tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="class: cms_table_cms_table_tr-caption, align: center"]Hivi ndivyo anavyoonekana Majeruhi Said Ntahompagaze aliyejeruiwa mguu wakati wa vurugu za waislam na wakristu wachache zilizotokea leo katika kijiji cha Buseresere wilayani Chato mkoani Geita na kusababisha shughuli mbalimbali kusimama.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="class: cms_table_cms_table_tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="class: cms_table_cms_table_tr-caption, align: center"]Majeruhi Vicent Damon akiwa amelazwa wod na 8 hospitali ya wilaya ya Geita aliyejeruiwa wakati wa vurugu za waislam na wakristu wachache zilizotokea leo katika kijiji cha Buseresere wilayani Chato mkoani Geita na kusababisha shughuli mbalimbali kusimama.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="class: cms_table_cms_table_tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="class: cms_table_cms_table_tr-caption, align: center"]Majeruhi Sadick Yahaya.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="class: cms_table_cms_table_tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="class: cms_table_cms_table_tr-caption, align: center"]Majeruhi Ramadan aliyejeruiwa wakati wa vurugu za waislam na wakristu wachache zilizotokea leo katika kijiji cha Buseresere wilayani Chato mkoani Geita na kusababisha fukuto kubwa la vurugu zilizosababisha shughuli mbalimbali kusimama.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Machafuko makubwa yametokea leo katika kijiji cha Buseresere Wilayani Chato Mkoani Geita kati ya waslam na wakristu na kupelekea watu 10 kujeruhiwa vibaya kwa mapanga huku mchungaji wa kanisa la Pentekoste Assemblies of God Mathayo Kachila (45) akipoteza maisha kwa kuchinjwa na watu wanaodaiwa ni waumini wadini ya kiislam kisha mwili wake kutelekezwa kwenye vibanda vya maduka ambavyo vilikuwa jirani na eneo hilo.

Habari na picha kwa hisani ya Gsengo Blog

MUTAUWANA SANA MWAKA HUU WATANGANYIKA UBAYA NA CHUKI ZENU ZIDI YA WAZANZIBARI ZITAKURUDIENI WENYENU KWA EWEZO WA M/MUNGU KILA UBAYA MULIOKUSUDIA PROPAGANDA NA AGENDA CHAFU DHIDI YA WAZANZIBARI HAMUTOFANIKIWA

Tumegawanywa tukagawanyika ni ngumu sana kufikia ukombozi wa kweli. Sasa itakuwa hivi: jambo likikemewa na mkirisitu muisla hataunga mkono na kinyume chake tutagawana kura2015

Tusikate tamaa, bado tuna nafasi kubwa ya kurekebisha hasa tukiwa wawazi, tuwataje hadharani wale wenye nia mbaya ya amani ya nchi yetu, awe kiongozi wa dini, mwanasiasa, mwanaharakati, au mtu yeyote hakika tutafika. Jana nimemsikiliza SHEIKH wa Dar es Salaam, hakika yule ni kiongozi wa dini ameongea vizuri sana, akasema kuna watu wanataka kuuza SILAHA na wanona njia rahisi kwa Tanzania ambapo amani imetawala ni kupitia dini kwa vile vita ya dini haina mwisho. Viongozi kama Sheikh huyu ni mfano wa kuigwa na tukiwatumia hakika hatutafika kule ambako wabaya wetu wanataka kutufikisha.
 
Hivi hao al caeda na al shabab ni ndugu zako? Kinakuuma nini hata kama wanasingiziwa?
Au wanauhusiano na dini yako?

Wivu wa mapenzi mbona alivyofariki Kanumba hatukusema al caeda wanahusika?

Umeona eee? kutokana na bandiko lake hakuna shaka yeye ni alshababu.
 
Hujamuelewa mleta mada mkuu, ameonelea matamshi ya baadhi ya makundi ya watu kuhusu wahusika wa mauaji na siyo waandishi wa habari kuandika.
asante kwa ufafanuzi,asubuhi hii viroba bado vipo kichwani
 
kaka umesema kweli nahisi watz wengi wahaijui vizuri alqaeda na hivyo vikundi vyengine lakushangaza viongozi wetuwanakurupuka kutoa hukumu kabla ya uchunguzi tena wa upande wa zanzibar tuu ni ajabu au ajenda
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom