Sasa hivi imekuwa kawaida kwa matukio ya mauji yanayotokea hapa nchini kuhusishwa na vikundi vya alqaida , alshabab au bokoharam hata kama mauaji hayo yamefanywa na majambazi au watu waliolipizana kisasi kwa wivu wa mapenzi au kudhulumiana.
Maranyingi uhusiahwaji huu unatawala zaidi kwenye midomo ya viongozi wasiokuwa makini na vyombo vya habari uchwara vilivyo biased kwenye kuriport taarifa inayohusu jamii fulani hasa anapouwawa anakuwa mkristo.Hatusikii kauli kama hizo wauliwaji wanapokuwa waislamu.
Ni muhimu kuchunguza mauaji kwa umakini ili kuepuka kupandikiza chuki kwa imani nyingine,haina tija kwa taifa.Ni mara ngapi majambazi wanauwa watu kwa kutafuta vitu wanavyohitji kwa watu/mtu waliyemuua?Hivi vikundi vya alshababy,bokoharam na alqaida tusiviombee kuingia nchini ni hatari sana.Na huko kuwatajataja ni kama kuwachafua kwa wambia wapo nchini ili hali hakuna vikundi hivyo nchini kwetu.
Unamkuta waziri mzima analopoka eti kuna alshababy,mara bokoharam,au alqaida bila hata uchunguzi.Kumbukeni mnacheza ngoma msiyoijua na ni hatari kwa umoja na mshikamano wa nchi yetu.Yani akiuwa kiongozi wa kristo tu basi kuna alshababy,hv ni viongozi wangapi wa kiislam au waislamu wangapi wameuawa hapa nchini mpaka sasa na hata tume haijaundwa kuchunguza?Inafikia wakati mpaka kuna wengine wanasema waliouwawa wamejitakia!!
Tukumbuke kuwa thamani ya uhai iko kwa wote halikadhalika uchungu wa mauti.Dr Mafingo aliuawa huko Bulongwa makete watu wakawa kimya.Kama tunaamua kupaza sauti juu ya mauaji basi tufanye hivyo kwa watu wote bila kuwa biased.
Be blessed all.