Profile picture yako ina maana gani?

Huu mjadala upo ndugu haohao wanasayansi walishachuana sana tu,mkuu zipo signals zinarushwa zaidi ya hizo na ndio zikiangukia kwa viumbe wabaya itakuwa tabu lkn ndugu unafikiri tukae tu hivihivi tusitafute changamoto..??
Asili ya binadamu ni kutaka kujua na hichi kitu kipo ndani yetu huwezi mzuia binadamu kufanya uchunguzi.. ukitaka kumfanya binadamu afanye uchunguzi mwambie hicho chumba usiingie!!! Lazima atataka kujua Kuna nini..?
Hili swala linamatokeo mawili tunaweza kupata kitu kibaya au kizuri pia muhimu kukabiliana na yote mi sisapoti kukaa tu!.

Zaidi tunatafuta intelligent life namaanisha viumbe vyenye ufahamu Kama wetu au zaidi,so hata hapa duniani ipo mitambo maalum inayodaka signals kutoka nje miaka ya zamani kuna signal ilishapatikana wakaiita Wow signal ila haikuleta majibu ilitokea wapi na maana yake,waliporudisha mitambo ktk frequency ileile hakuna kilichotokea!.. ulimwengu bado ni kimya sana..

Mi naunga mkono tafiti kuliko kukaa tu.
Nimefuatilia kwa muda kidogo mambo haya na harakati za binadamu kwa mambo ya anga kwa bahati mbaya hii bado sikuwahi kuliona! Asante ndugu yangu umenipa hamasa ya kufatilia kila engo.

Ila nimefurahi kujua mwanadamu huwa ni mtu wa kutafuta changamoto hapendi kuwa na amani yaani, inastaajabisha kwa kweli!
 
Nimefuatilia kwa muda kidogo mambo haya na harakati za binadamu kwa mambo ya anga kwa bahati mbaya hii bado sikuwahi kuliona! Asante ndugu yangu umenipa hamasa ya kufatilia kila engo.

Ila nimefurahi kujua mwanadamu huwa ni mtu wa kutafuta changamoto hapendi kuwa na amani yaani, inastaajabisha kwa kweli!
Haha! Mkuu sisi hatuna hulka ya kutulia sio kwamba hatupendi amani tunapenda Sana na ndio maana hata hapa duniani tunamantain amani japo si sehemu zote ila kwa wingi ipo,amani inatengenezwa tu.

Mkuu hivi unafikiri hata wewe ukiwa na hela hakuna kitu beunashindwa nunua tena unanunua hata kabla hakijatoka we ushaweka order!. Maisha ya hivi kila kitu unakipata kwa urahisi basi utaanza kutafuta changamoto kutumia pesa yako hiyohiyo aidha kushindana na wenye pesa wenzako ktk kufanya kitu fulani!. Ndo tupo hivyo mkuu.

Karibu Tena kwenye ulimwengu wa sayansi anga kinachoniuzi ktk huu ulimwengu anga vitu vipya kugundulika huchukua muda sana leo inakuja taarifa hii hapo mtasugua mpk kupata taarifa ya kukiki kabisa!.
Ni hulka yetu ku explore ulimwengu angalia hata historia wazungu walivyofika ktk bara letu wakajua kuwa Kuna watu wa race nyeusi na sisi tukapata kuwajua.. ni stori yenye benefit na negative effects pia!. Hatutakiwi kuogopa tusubirie mpk hao jamaa waje watatutafuna humuhumu bora tutambae hata tuhamishie vizazi vyetu ktk sayari nyengine ikibidi.

Linapokuja swala la haya Mambo sichoki kuandika mpk nijilazimishe kuacha..😂
I still typing kichwani kwangu..🤣
 
Humu jukwaani natumia jina la Kayaman, napenda na navuta sana bangi, ninatumia profile pic ya bob marley kutokana na wimbo wake wa Kaya huwa unanihamasisha sana kuvuta bangi, mwanzo nilitamani kutumia picha ya peter tosh kutokana na wimbo wa legalize it ila nikaona acha niende na bob!
Time to have Kaya now,,,kaya...kayaaa!!!

Hicho kinyimbo kinanibambaga sana katika records za Bob Marley!
 
Me mkulima na zao lililonitoa ni Pilipili hoho , nilizoea pilipili hoho za rangi ya kijani wakati fulani nilienda kutembea Dodoma nikiwa na marafiki zangu, kulikua na supermarket ikabidi tuingie kuosha macho kidogo palikua pakubwa sana ! Na ndo mara ya kwanza kuona hoho za rangi ya njano na nyekundu zilikua packed !! Nikasema hizi lazima nizilime ile kuingia mtandaoni kupata ABC nikakutana na hiyo picha ,Na ndo imekua profile pic yangu hadi leo !
 
Me mkulima na zao lililonitoa ni Pilipili hoho , nilizoea pilipili hoho za rangi ya kijani wakati fulani nilienda kutembea Dodoma nikiwa na marafiki zangu, kulikua na supermarket ikabidi tuingie kuosha macho kidogo palikua pakubwa sana ! Na ndo mara ya kwanza kuona hoho za rangi ya njano na nyekundu zilikua packed !! Nikasema hizi lazima nizilime ile kuingia mtandaoni kupata ABC nikakutana na hiyo picha ,Na ndo imekua profile pic yangu hadi leo !
So wazilima bado..?
 
Nimegundua kitu watu huwasilisha ujumbe kwa kupitia profile picture zao,na moja kwa moja aidha ujumbe husika mara nyingi huwa unamhusu mtu husika,
Kinaweza kuwa kitu unachokipenda au ambacho kinahusu maisha yako ktk namna fulani, karibuni hapa tuelezee kwa uchache tu kwanini unatumia hiyo avatar.

Binafsi avatar yangu ni GOLDEN RECORD,hii avatar niliipenda kwasababu zaidi napendelea mambo ya sayansi ya anga kwa kifupi hii golden record ni disk ambayo iliwekwa kwenye kifaa cha kisayansi kilichorushwa miaka ya zamani sana. Kifaa kilichobeba hii golden record kinaitwa Voyager 1,mpaka hivi sasa kifaa hichi kimeshapita mbali sana I mean kimeshatoka nje ya solar system yetu!. Nini kipo kwenye golden record..?
View attachment 1988481

Disk hii imetengenezwa kwa dhahabu ili iweze kutunza ujumbe uliomo kwa muda mrefu na disk hii inarekodi za sauti nyingi kutoka hapa duniani Kama mvua,sauti za wanyama,picha na salamu za lugha mbalimbali pia inaonyesha ramani ya sisi tulipo(dunia yetu).
Lengo lilikuwa ni kujulisha viumbe wengine(Kama wapo na wakibahatika kukipata kifaa husika).. ukiangalia pichani Kuna michoro kila mchoro ktk golden record unamaana yake nimeelezea kiufupi ila nishasikiliza kilichowekwa humo ni record ambayo inamasaa takribani matano!.. sikumaliza yote Kuna miziki n.k hi yote ni kututambulisha sisi kwa hao viumbe wengine.

Kwanini hiyo picha..? Kwasababu kwanza napenda "HUMANITY" pia napenda "ULIMWENGU" na sifa zake zote napenda Sana kuufahamu ulimwengu zaidi ya hivi ninavyoufahamu!. So hii picha kwangu inamaana kubwa Sana kutokana na kiu cha kupenda sayansi ya anga, kupenda kuujua ulimwengu pia napenda humanity yani jinsi tulivyo ndio maana hata ktk profile banner yangu nimeweka picha ya Adam na Eva hii ikielezea jinsi navyopenda uutu wetu na mazingira yetu kiujumla!.

Nisiwachoshe yangu ni hayo machache wewe je, profile picture yako inazungumza nini..??
Mimi natumia picha ya Chifu Mbelwa wa Tanga alieingia mkataba na mwakilishi wa Ujerumani kumpa sehemu ya Tanganyika 1884
20211002_124857.jpg
 
avatar ni ya Lupe Fiasco rapper kutoka Chicago, nilianza kumsikikiliza 2007na nilipenda album yake ya " the Cool" ilikuwa na single kama super star, hip hop saved my life, paris tokyo,dumb it down .
Pia aliwahi shirikishwa na Kanye West kabla hata Lupe hajawa maarufu ktk single touch the sky.Lupe ni anaweza kuandika lyrics kwa umahiri ,hii imechangiwa na tabia yake ya kupenda kusoma sana literature tangu akiwa mdogo pia anajua freestyle.
Kifupi namkubali Lupe Fiasco
 
Back
Top Bottom