Profile picture yako ina maana gani?

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
23,319
47,730
Nimegundua kitu watu huwasilisha ujumbe kwa kupitia profile picture zao,na moja kwa moja aidha ujumbe husika mara nyingi huwa unamhusu mtu husika. Kinaweza kuwa kitu unachokipenda au ambacho kinahusu maisha yako ktk namna fulani, karibuni hapa tuelezee kwa uchache tu kwanini unatumia hiyo avatar.

Binafsi avatar yangu ni GOLDEN RECORD,hii avatar niliipenda kwasababu zaidi napendelea mambo ya sayansi ya anga kwa kifupi hii golden record ni disk ambayo iliwekwa kwenye kifaa cha kisayansi kilichorushwa miaka ya zamani sana. Kifaa kilichobeba hii golden record kinaitwa Voyager 1,mpaka hivi sasa kifaa hichi kimeshapita mbali sana I mean kimeshatoka nje ya solar system yetu!. Nini kipo kwenye golden record?


download (1).jpeg


Disk hii imetengenezwa kwa dhahabu ili iweze kutunza ujumbe uliomo kwa muda mrefu na disk hii inarekodi za sauti nyingi kutoka hapa duniani Kama mvua,sauti za wanyama,picha na salamu za lugha mbalimbali pia inaonyesha ramani ya sisi tulipo(dunia yetu).

Lengo lilikuwa ni kujulisha viumbe wengine(Kama wapo na wakibahatika kukipata kifaa husika).. ukiangalia pichani Kuna michoro kila mchoro ktk golden record unamaana yake nimeelezea kiufupi ila nishasikiliza kilichowekwa humo ni record ambayo inamasaa takribani matano!.. sikumaliza yote Kuna miziki n.k hi yote ni kututambulisha sisi kwa hao viumbe wengine.

Kwanini hiyo picha..? Kwasababu kwanza napenda "HUMANITY" pia napenda "ULIMWENGU" na sifa zake zote napenda Sana kuufahamu ulimwengu zaidi ya hivi ninavyoufahamu!.

So hii picha kwangu inamaana kubwa Sana kutokana na kiu cha kupenda sayansi ya anga, kupenda kuujua ulimwengu pia napenda humanity yani jinsi tulivyo ndio maana hata ktk profile banner yangu nimeweka picha ya Adam na Eva hii ikielezea jinsi navyopenda uutu wetu na mazingira yetu kiujumla!.

Nisiwachoshe yangu ni hayo machache wewe je, profile picture yako inazungumza nini?
 

kayaman

JF-Expert Member
Aug 3, 2013
4,430
9,851
Humu jukwaani natumia jina la Kayaman, napenda na navuta sana bangi, ninatumia profile pic ya bob marley kutokana na wimbo wake wa Kaya huwa unanihamasisha sana kuvuta bangi, mwanzo nilitamani kutumia picha ya peter tosh kutokana na wimbo wa legalize it ila nikaona acha niende na bob!
 

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
23,319
47,730
Humu jukwaani natumia jina la Kayaman, napenda na navuta sana bangi, ninatumia profile pic ya bob marley kutokana na wimbo wake wa Kaya huwa unanihamasisha sana kuvuta bangi, mwanzo nilitamani kutumia picha ya peter tosh kutokana na wimbo wa legalize it ila nikaona acha niende na bob!
Dah! Ndugu upo vizuri aisee nataka nije nitest siku moja kuonja hii kitu sijui nitafanya kituko gani..🤣
 
13 Reactions
Reply
Top Bottom