Mkuu kwani tatizo liko wapi, mpaka hapa TFF, Vilabu na kamati ya ligi hawana cha kupoteza, siku zote ligi ilikuwa haionyeshwi na hakuna kilichoharibika na wala vilabu hawakupata hela; Azam wametoa hela na ligi wanataka waonyeshe ili waingize hela wao sasa hapo wewe unaathirika vipi endapo watashindwa kuonyesha? Ni kama mtu anataka kuja kununua mahindi kwako ingawa hujawahi kuona akiwa na kifaa cha kubebea hayo mahindi lakini akakwambia mimi nitakupa hela na muda ukifika nitakuja kuchukua hayo mahindi, hela umeshapata kazi inakuwa ni kwake kuja kuchukua hayo mahindi asipochukua wewe huathiriki na chochote. TFF, kamati ya ligi na Vilabu (isipokuwa Yanga na Manji) wanachotaka ni hela na Azam wametoa, sasa mlitaka waseme tunataka kwanza tuone mkirusha matangazo ndo tuwape hii Zabuni wakati wenye kurusha matangazo tayari hawana uwezo wa kutoa hizo hela?