Profesa Kabudi: Kikwete na Mkapa haifai kuwataja kwenye kashfa sababu tunatunza heshima yao

bora Magu angewakaanga hawa jamaa, halafu yeye tukamsamehe, lakini na yeye anaingia kwenye makaburi yale yale, kuna siku itafika
 
Hao wana heshima gani kuzidi Marais wa Brazil ,Korea Kusini n.a. Marekani walioshitakiwa n.a. kung'olewa madarakani? Kweli maajabu hayataisha Tz.
 
Kwastaili hiyo ukiwa raisi kullaaaa uwezavyo heshima yako italindwa ki kilakitu...afrika tutachelewa saaaaanaaaaa!! Tunaujinga na unafiki wahali yajuu.
Tunaomba basi waombe hâta radhi kwa walotufanyia maana wengine tumelia saaanaaaa. Wapo walopoteza maisha kwa kukosa Dawa...wengine wamekufa njaa....wengine wameteseka kwakukosa elimu...wengine wamejiua kwa kushindwa na maisha magumu...wadada wamejiuza...wajane wamehangaika na watoto...kinamama na maji km 30...vijana wameuwawa kwa ukibaka!!!! Nimengi mnooooo khaa!
 
Waziri wa Sheria Prof. Plamagamba Kabudi amesema haifai kuwataja marais Mkapa na Kikwete kwa kuwa heshima yao inatunzwa kwa kuwa wamekuwa wakuu wa nchi, wakuu wa serikali na maamiri wajeshi wakuu na heshima hiyo inafaa kutunzwa kikatiba, kisheria, kimaadili, kiutamaduni na kiutu na ndio maana hata ripoti haijawataja sehemu hata moja


Ni wapi palipoandikwa mwizi aheshimiwe
 
Hapo ndipo tunapoharibu Watanzania.

Waziri wa Sheria Prof. Plamagamba Kabudi amesema haifai kuwataja marais Mkapa na Kikwete kwa kuwa heshima yao inatunzwa kwa kuwa wamekuwa wakuu wa nchi, wakuu wa serikali na maamiri wajeshi wakuu na heshima hiyo inafaa kutunzwa kikatiba, kisheria, kimaadili, kiutamaduni na kiutu na ndio maana hata ripoti haijawataja sehemu hata moja

Hivyo haifai kuacha kujadili mambo yaliyo mbele yetu na kuwajadili wakuu hawa wastaafu

 
Hakuna kujadili watu
Hapa tunajadili Kuikomboa nchi tu
Kwani nchi inakombolewa na miti? Si watu ndio wanajitoa kwa dhati na si kidrama drama kam hizi tunazoziona. Heri angefanya kimya kimya kwa mashauriano ya kina ambako ndio tunaelekea kama alitaka kutunza heshima ya viongozi waliopita!
 
Marekani Rais anashitakiwa sio baada hata akiwa madarakani sisi hapa hooo ushuzi mtupu yaani wameharibu halafu tuwaenzi nchi bhana
vita ya madini haijawahi kumuacha mtu salama
 
Ule unabii wa Mwl JK Nyerere ndio unatimia sasa na ndio mimi nina ulewa sasa, kwamba "upinzani wa kweli utatatoka ndani ya ccm yenyewe" Kumbe ilikuwa ni ccm mumo kwa mumo na wala sio ccm uhamie sijui cdm au cuf. Ni ccm wenyewe kwa wenyewe, kama vile naota.


Na washawasha!
 
Kilimo:-
tumefeli (sio tena uti wa mgongo wa taifa letu) kilimo kwanza iliyeyuka stock ya ma powertiller ilipokwesha.

Rushwa:-
Ndio imepamba moto mpaka wabunge wanalishwa mlungula.

Utawala bora:-
Wamezalisha watumishi hewa wa kutosha!!!
Wafanyakazi wa Tra wameigeuza tra ni mali yao.

Uwekezaji:-
Umegubikwa na wizi rushwa na mizengwe mtindo mmoja.

Madini:-
Mrahaba 4%
!!!!!!!!!!!!!!

Walikuwa wanafanya kazi gani iliyotukuka kustahili kutokubughudhiwa?
 
Hata mimi naunga mkono hoja. Tusiwajadili Marais wetu wastaafu na hata aliyeko madarakani. Urais ni taasisi sio kitu cha kuchezea. Full stop.
Lakini, tunaweza kuwajadili makamu, PM, Spika, Naibu spika, na mawaziri wooote pamoja na wabunge woote. Mkitaka kumjadili Dr Kikwete, mjadilini alioyafanya akiwa waziri kuleeeee. Mkitaka kumjadili Dr Mkapa, mjadilini aliyoyafanya kuleee kabla ya uraisi.
Mkitaka kumjadili Dr John, mjadilini kuleeee sio leo. Leo tunampongeza kwa kuwa mzalendo wa kuthubutu kutufungua macho tukaona tunavyo ibiwa.
Ushauri, Ili tusijewaingiza kwenye msaragambo huu, tuachane na kutafutana, iundwe tume, iwachunguze kwa siri, iwakamatie kile cha juu walichotuibia, wakirejeshe hazina kuu, na wasiruhusiwe kulalamika. Jiulize, ni nini maana ya tume ya utumishi na maadili ya viongozi?? Watu huenda kuapa nini? Watu huenda ku declare nini pale? Ati naingia uwaziri na shs 100 na nyumba nusu sijamalizia kupaua. Ukitoka na nyumba 100 baada tu ya uwaziri wa miaka 5 si lazima uulizwe??
Najiuliza, nyiye mliotuaminisha kuwa mtawachunguza hawa viongozi, mlikuwa wapi?? Nyiye nanyi ni majipu. Mwafaa mtumbuliwe. Nisiseme mengi, yale ya bwana yulee DAB na magari ya kifahari na viwanja 120 miji mbali mbali aliyovitaja Mh Musukuma yameishia wapi?? Hicho kitengo ni jipu lililoiva mno.
Mkuu umejitahidi sana kuandika lakini bahati umeandika ujinga mtupu
 
Haiingii akilini kumuadhibu subordinate alafu boss wake aliyekuwa akimtuma afanye alichofanya unasema unamtunzia heshima. Waziri ni mshauri tu wa rais
 
Waziri wa Sheria Prof. Plamagamba Kabudi amesema haifai kuwataja marais Mkapa na Kikwete kwa kuwa heshima yao inatunzwa kwa kuwa wamekuwa wakuu wa nchi, wakuu wa serikali na maamiri wajeshi wakuu na heshima hiyo inafaa kutunzwa kikatiba, kisheria, kimaadili, kiutamaduni na kiutu na ndio maana hata ripoti haijawataja sehemu hata moja

Hivyo haifai kuacha kujadili mambo yaliyo mbele yetu na kuwajadili wakuu hawa wastaafu


Bado sana tulidhani sasa hii tungekuwa serious kama wenzetu kwenye kutatua matatizo yetu kumbe bado....haya tusubiri nabii mwingine hii itaishia bla bla bla kama tulivyozoea.
 
Tumeshindwa kabla hatujaanza! Wahojiwe! Vinginevyo na wengine waachwe! Hao ndo waelelezaji wakuu! Wengine ni watelezaji tu!
Wasafishwe na mahakama wala si vinginevyo! Wakiachwa hawa joka la makengeza litakuwa limepata mpenyo!
Hawa wahusika wakuu wawili tusiwaonee aibu Bali wahojiwe! Kuna mmoja Kati yao yuko kimyaaa! Utafikiri hajui kinachoendelea! Ni aibu yake?
 
Back
Top Bottom