Sijui kwanini awamu hii kumekuwepo na ongezeko kubwa la wajinga!Profesa Assad akiwa mjumbe wa Bodi ya NSSF miaka michache iliyopita na tena akiwa ni mjumbe kwenye kamati ya Bodi ya uwekezaji ya NSSF(MIC) alijinufaisha katika kununua nyumba za NSSF huko Tanga bila kujali conflict of interest.
Nyumba hizo zilizouzwa pia kuna Mkurugenzi mmoja wa NSSF, Bwana Kidula ambaye nae alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tenda ya Menejiment ya NSSF naye alijitwalia nyumba kadhaa za Tanga na Dodoma.
Katika kipindi cha Dau NSSF, mauzo ya nyumba yalifanyika kwa upendeleo mkubwa ili watu wake wazinunue. Mfano nyumba za Kijichi zilipata wateja wengi ila waliambiwa zimeisha kumbe ni uongo ili ziweze kugawiwa jamaa zake kupitia majina ya wake zao na jamaa zao.
Kwa mfano kuna mtoto wa profesa Mlawa (rafiki wa dau) ambaye yuko NSSF alijipatia hizo nyumba kwa usiri mkubwa. Zoezi la kuwauzia nyumba wafanyakazi wa NSSF lilifanyika kwa ubaguzi maana wale makafiri au wagalatia kama walivyokuwa wanaitwa na wenzao( wakati huo) walifichwa kuhusu uuzaji huo.
Hayo yote aliyajua Prof Assad lakini hakuchukua hatua zozote tena zaidi alikuwa Mwenyekiti wa BOARD YA AUDIT COMMITEE.
Huyo ndo Assad ambaye anataka sasa kufanya kazi zake kwa weledi mkubwa akisahau wakati wa Dau NSSF ilikuwa na madudu ya kufa mtu.