Profesa Assad ni muongo, duniani 73% ya ndege zote za biashara hununuliwa kwa pesa taslimu

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,355
17,321
Nimesikitika kuona msomi kama Assad aki-personalize tofauti zake na Hayati Magufuli kwa kusema mtu kichaa tu ndie ananunua ndege kwa cash, profesa akasema mikopo/lease ndio njia sahihi.

Binafsi sijui hizo takwimu amezipata wapi za kua vichaa tu ndio wananunua ndege kwa pesa tasilimu ama cash.

Utafiti unaojulikana Duniani kote uliofanywa na Chase & Associate unaonyesha kua ndege zote za biashara 73% hununuliwa kwa cash ama wanaita outright purchase. Je, wote hao 73% ni vichaa? Ama profesa ndie ana akili kuwazidi?

Profesa anataka kuaminisha umma kua njia pekee na ya lazima ya kununua ndege ni kwa mkopo, kwa cash unakua kichaa, hivi huyu jamaa ana akili kweli?

Profesa ameongea kama mtu ambae hakwenda shule, profesa analazimisha mtazamo wake ndio uwe mtazamo wa watu wote.

Nilikua namkubali profesa lakini hii la ku-personalize tofauti zake na Magufuli na kumshambulia marehemu kua ni kichaa tena kwa mtazamo wake binafsi imesababisha nimemuondoa akili profesa Assad.

Hivi profesa yeye kwenye maisha ama kwenye public settings ameweza kufanikisha lipi?, Amewahi kua mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa NBC, enzi za utawala wake benki ilikua inaelekea kufa/kufilisika kabisa. Bila yeye kuondolewa bank isingekuwepo sasa hivi. Asijionyeshe kua no brainy saana, alipewa nafasi mbona hakutuonyesha huo u brainy wake?

Analalamikia kua hakupewa nyaraka za SGR, JNHP, ATCL, kwa nini hakujiuzuru kuonyesha credibility? Maana hapo ni sawa na kua alizuiwa kutekeleza majukumu yake ya msingi kwa maslahi mapana ya nchi, kwa nini hakujiuzuru?

 
Unanunuaje cash wakati wafanyakazi wako umewakazia more than 5 yrs hakuna nyongeza, vijana ajira hamna, amesema cash ina matumizi yake kwa issue kama hzo unapiga mkopo, hakuna haja ya kulaza njaa watu alaf unaenda kununua Boeing Kwa keshi unakuja kuliweka ardhini haliendi popote linakula hela ya maintenance, huku vijana mtaani wanakomaa na vibanda umiza, kwa dharau unawaambia wajiajiri na unasepa chato kutengeneza uwanja wa ndege wa kimataifa.

Serikali ya Pombe imekopa 1.2 Trillion kutoka World Bank kwa ajili ya ujenzi wa madarasa alafu at the same time serikali ya Pombe imenunua ndege kwa cash sh. 1.5 Trillion most of them zipo ground zinanyewa na popo huku fast jet Kwa hujuma ipo out of action.....Alaf Mimi msinikumbushe habari za jiwe kabisa aisee...the worst president ever

1618134582033.gif
 
Kwa wewe mtu mmoja kumuondoa haimpunguzii credit zake.

Hamshambulii marehemu anashambulia utendaji wa marehemu na iwe angalizo kwa watu wajao na waliopo.

Kuwa kiongozi si kuwa ndio unajua kila kitu na wenzio ni magarasa tu.

Hebu pita vizuri, nami nilikua nakukubali ila kwa chuki yako hii kama ya kidini nadhani nimekudharau.
 
Kwa wewe mtu mmoja kumuondoa haimpunguzii credit zake,
Hamshambulii marehemu anashambulia utendaji wa marehemu na iwe angalizo kwa watu wajao na waliopo,

Kuwa kiongozi si kuwa ndio unajua kila kitu na wenzio ni magarasa tu,

Hebu pita vizuri, nami nilikua nakukubali ila kwa chuki yako hii kama ya kidini nadhani nimekudharau
Safi kabisa
 
Hivi alikumbuka kuwaambia kuwa mtu ukikopa gharama zinakuwa juu zaidi ya uñunuzi wa hizo ndege kwa cash? Na pia kwa mfano kipindi chote cha corona ndege zilikuwa haziruki, kama zingekuwa zimekopwa hela ya kulipa hayo madeni ingetoka wapi? Pathetic profools, nilikuwa namwelewa lkn kwa hili naona kavuka mipaka. Aache unafki.
 
Kwa wewe mtu mmoja kumuondoa haimpunguzii credit zake.
Hamshambulii marehemu anashambulia utendaji wa marehemu na iwe angalizo kwa watu wajao na waliopo

Kuwa kiongozi si kuwa ndio unajua kila kitu na wenzio ni magarasa tu,

Hebu pita vizuri, nami nilikua nakukubali ila kwa chuki yako hii kama ya kidini nadhani nimekudharau
Tuliomuondoa akili ni wengi na wenye akili. Majuha kama nyie mnashabikia tu hamkuona kama amekosea.
 
Back
Top Bottom