Mzee makoti
JF-Expert Member
- Jul 27, 2016
- 2,587
- 3,060
Sakata la uuzaji wa nyumba za Serikali limeibuliwa upya na aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Musa Assad akikosoa utaratibu uliotumika kuziuza.
Dodoma. Utaratibu uliotumika kuuza nyumba za Serikali umekosolewa kutokana na kutolihusisha Bunge kama chombo cha wawakilishi wa wananchi.
Hayo yameelezwa na aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), Profesa Musa Assad ambaye amesema mchakato huo ulihusisha Baraza la Mawaziri na Makatibu wakuu huku Bunge likiwekwa pembeni.
Akizungumza kwenye mdahalo ulioandaliwa na Mtandao wa Asasi za kiraia uliojikita katika kuchagiza uwajibikaji kwenye uziduaji (Hakirasilimali) katika wiki ya Azaki inayofanyika mjini Dodoma.
Amesema Serikali imeuza nyumba hizo na mchakato ulikuwa ni baraza la mawaziri wakishauriwa na makatibu kutengeneza waraka na kupeleka kwa Rais ili akubali kuuza nyumba hizo.
“Nani kakuruhusu? Ni mawaziri na makatibu wakuu. Kwanini halizungumzwi sasa jambo hilo. Lingekuwa wazi tungesema hilo haliwezekani lakini tumekaa kimya na hakuna mtu ambaye amesema hili jambo lazima lirudi bungeni tulizungumze ili tutoe ruhusa maalum jambo hili lifanyike ama lisifanyike,” amesema Profesa Assad
Chanzo: Mwananchi