Uwezi kuwa maharufu bila kuihusisha serikali na haijalishi nikwa mabaya au kwa mazuri na hasa kama unaona unapoteza mwelekeo njia ya CUF iliyobaki ni karata ya muungano kwani karata ya amani na usawa zanzibar imeshatatuliwa na Maalim seif kuwa madarakani!!Kilichobaki ni chokochoko!
Mtakuwa mna wazimu sana! Hebu angalia kama si uwepo wa Zanzibar kwenye Muungano mgefanya wizi huu? Mgefanya kwa njia gani nanyi mipaka yenu ya bahari inkingwa kila upande? Mkienda kusini mnakuta Msumbiji na mkienda juu Kaskazi mnakutana na Kenya niambie mgedai wapi hizo maili mnazotaka mzidishiwe?Barubaru na Wana JF,
Hivi nina swali, ni wananchi wangapi wanajua au kuusoma ule Muungano wa Kwanza waliofikia akina Mwalimu Nyerere na Karume ???? Kwa jinsi nilivyosoma hii post/topic/mada na kuielewa kuna Harufu ya Ubaguzi na Zanzibar kutaka kujitenga.
Angesema Jamhuri ya Tanganyika na sio Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Maana Tanganyika, Zanzibar na Pemba ndio zilizozaa TANZANIA. na penye Tanzania angesema Tanganyika.
Sisi Watanganyika wao Wazanzibar, wakitengana hawatakaa salama, watasema Wao Wapemba na sisi Wazanzibar
My Take: Mbona sisi hatudai Tanganyika yetu ??? Hili suala naliona ni kubwa na linalohitaji tuelimishwe zaidi na zaidi
Mtoto akililia wembe mpe ...........
Nawakilisha
Mamlaka ya JMT ni kamili. Eneo la jamhuri ya Muungano ni eneo zima la bara na visiwani. Hakuna eneo lolote la 'nchi ya Zanzibar' ambalo si eneo la JMT. Kama lipo niambie. Katiba ya ZNZ inaweza kusema lolote lakini ikipingana na ile ya Muungano vipengele vyake ni batili. Zanzibar ni nchi kwa Wazanzibari tu; siyo nchi inayotambulika mahal popote duniani. Kuwa na jeshi, mahakama, na rais (mihimili mitatu ya dola) hakuifanyi ZNZ kuwa nchi vinginevyo miye ningetamba niko "nchi" ya Michigan! Kuongeza eneo la bahari kutakuwa na manufaa kwa Zanzibar na kwa Tanzania nzima. Wananchi wa ZNZ yawapasa wafurahi na kuunga mkono uamuzi huu wa serikali ya JMT.
Lakini hili nalo ni kosa la msingi, unaliita kushirikiana lakini ni dereliction of duty na kutapanya mamlaka, Mama Waziri amekosea na amevunja Katiba. Hii inatokana complexity ya structure of Union inayofanya watu kutoelewa nguzo zinazounda Muungano.Nadhani hapa mtamuonea bure tu huyu mama....Lakini vile vile kwa wanaofahamu mchakato wa mambo haya wanajua kabisa kuwa maamuzi haya ya kimataifa toka chini ngazi za wataalamu hadi inapofikia ngazi ya mawaziri serikali zote mbili hushirikiana vizuri sana.
Ambayo ndio hii conclusion uliyoifikia hapo bila kujijua: kwamba, kama swala la Tanzania, la Muungano, halina haja ya kushirikisha Baraza la Wawakilishii wa Zanzibar basi hata ile petition yenyewe ya kuongeza mipaka haikutakiwa kushirikisha serikali ya Zanzibar.Sioni mahali popote ambapo pana msingi wa kuliuliza Baraza la Wawakilishi juu ya hili kwani suala la eneo la Muungano ni eneo zima la Tanzania. Hakuna bahari ya Zanzibar!
Nina wasi na Uraia wenu! Kwa nini munajenga hofu kubwa ya kurejeshwa nchi ya Tanganyika! Jengine ni kwamba musijitie UJUA wa kutokuona mambo, akili zenu zichuchuzeni kidogo ili zione mbali kabla hazijalemaa; Wapemba (Wazanzibari) hawapo Tanganyika tu bali wameekeza duniani kote.
Ata vile Zanzibar ni mkoa. Nadhani JK amelegea fulani katika kuitumikia JMT na ndo maana watu wa Z wamejisahau kuwa hiyo si nchi bali ni mkoa. Nadhani kila mkoa wa JMT huwe na tawala kama za Z ili tupeleke maendeleo kwa wananchi. Mf. Serikali ya mkoa wa Z, Serikali ya Mkoa wa Dar, n.k.natamani ningekuwa rais ningeifanya zenj mkoa na hao vimbelembele kama jusa ningewarudisha kwao uaharabuni, hawa ndio wanaotududisha nyuima. Tanahitaji raisi mbabe ndio tuendelee. La sivyo hatutafika mahali. Huyu jussa ni ni mtu hatari na si mzalendo kabisa ni mamluki
Naomba nikuweke sawa kidogo kwani kuna mambo umeyasahau kidogo.
Tanganyika na Znz zimeungana kimkataba na sio kikatiba. Kuna mambo yamo katika mkataba huo nayo ndio mambo ya muungano. Suala la ardhi na makazi si suala la Muungano na ndio maana Znz kuna waziri wa wizara hiyo na Bara yupo.
Kumbuka kuwa Mamlaka ya Tibaijuka mwisho wake ni Chumbe akiwa Znz hana mamlaka yoyote ukilinganisha na waziri wa mambo ya nje au mambo ya ndani. hawa wana malka kote kote.
Kumbuka vile vile Znz ni nchi kamili yenye mamlaka kamili na hilo limebainishwa katika katiba ya Znz. Kwa msingi huo Katiba hiyo hiyo imeanisha eneo la Znz kiufasaha kabisa. sasa kwa ombi hilo la Tibaijuka ni lazima katiba ya Znz itabidi ibadilike kwa kuongeza eneo la milki yake au kupunguza miliki yake na hapo ili kubadilisha kipengele hicho cha katiba lazima BLW litahusika vilivyo kwani wao ndio wtunzi wa sheria za Znz na mambo yote yaliyo nje ya muungano.
Kumbuka kuwa katika Picha walopiga kule UN wakti wanawakilisha alikuweo Tibaijuka, balozi wa Tz katika UN, Mbunge wa Mafia na Katibu wa wizara kutoka Znz. Kwa mantiki hiyo inaonekana wazi Prof Tibaijuka alipata baraka zote za Bunge la Muungano dio maana akachukua muwakilishi wa Bunge.
Sasa upande wa BLW hawakuwa na taarifa zozote ongezeka hilo officially na aliku husishwa kwa lolote lile kitu ambacho Jussa amehoji. Ikumbukwe kuwa maombi haya yakifanikiwa lazima BLW litahusishwa katika kupitisha sheria za ongezeko la eneo la miliki la Znz.
sasa labda tujiulize.
Je Znz itaongezewa kiasi gani katika hicho kilicho ombwa? hilo ni suala ambalo limegubikwa na utata mkubwa na alijabainishwa katika mkataba au mbi hilo.
Lakini pia lazima ufahamu kuwa Tz na Znz zote zinaongozwa na Rules of Law. Na mihimili yote mikuu inajipambanua yaani Serikali, Bunge na Mahakama bila kuingilia katika utendaji kazi wake. Kila muhimili unajitegemea.
Limeanza baraza la wawakilishi kuhoji Serikali ya Znz kisha uzi utafuata. Kwani majibu ya Serikali ndio yatatoa mwangaza kwa sakata hilo. Lakin all in all Tibaijuka lazima ajiuzuru hapo.
Kwani mtiririko wa jambo hili unakuwa sawa kabisa na ule wa Tz kujiunga na OIC.
Kilichowafikisha hapa viongozi wa Zanzibar ni chaguzi na matokeo ya kijinga. Sasa hivi wanachukua madaraka kwa ridhaa ya Maalim Seif na Jussa. Hili nalo lina mizizi yake huku bara. CCM bara imekuwa ikiwapelekea Wazanzibar wagombea ambao sio chaguo lao.Tatizo la msingi ni kwamba baadhi ya viongozi wa Zanzibar wamepoteza uwezo wa kuongoza. Hakuna viongozi ambao wana ujasiri wa kusimama dhidi ya watu kama kina Jussa na kuwaambia ukweli; hakuna viongozi Zanzibar wenye uwezo wa kusema na kutetea hoja zao au kupendekeza hoja tofauti na za kina Jussa. Huko kwenye BLW hakuna viongozi wenye ujasiri wa kusimama na kusema hapana!
Wazanzibari wanalazimishwa kuwa na fikra za aina moja na kuwa wasioneshe tofauti yoyote ya mawazo; huu ndio mwanzo wa ule udikteta wenyewe. Wachache ambao wanaweza kuwa ni pro-union wanaogopa kusimama na kuwapinga hawa separasists kama kina Jussa. Hawawezi kwa sababu wamekubali kuingia katika political pandering kwamba kila mmoja akitaka kuonekana ni kiongozi mzuri basi lazima awe against the union, deparaging watu wa bara, kebehi ya Nyerere n.k Matokeo yake watu wenye ujasiri wamekosekana na muungano wao unatokana na chuki sasa.
Hawa Wazanzibar ndugu zetu umoja wao uko kwa sababu wanaonekana kuchukia Muungano na kuichukia Tanzania bara; wanaamini kuwa ni Tanganyika ndio tatizo lao wakati kwa kila kipimo wako wanajiamulia mambo yao mengi wao wenyewe. Wanajiaminisha kuwa wao ni nchi na ina mambo yake na wanataka wawe nchi wakiwa bado kwenye muungano! Bahati mbaya ukweli wameambiwa mara nyingi lakini hawataki kuamini - Zanzibar siyo nchi mahali popote pale isipokuwa kwa Zanzibar yenyewe.
KUna nchi nchi moja tu nayo ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Ibara ya 1) ya Katiba Ya Muungano. Na Katiba hiyo inasema wazi kuwa eneo la JMT ni eneo lote la Tanzania Bara na Eneo lote la Tanzania Visiwani na bahari yake! Wazanzibari hawaamini kuwa wao siyo nchi! Wakati umefika tuanze kuwahakikishia ndugu zetu kuwa wao ni sehemu ya Muungano na ni wananchi wa Tanzania. Kama kweli wanaona muungano hauwafahi au ni tatizo wajitokeze tu na kudai kuwa wanataka kutoka nje ya Muungano.
Lakini wafanye hivi kwa kujiuzulu kwanza nafasi zao kwenye Muungano ili wapiganie kujitenga kwa Zanzibar! Haiwezekani upande mmoja wanafurahia matunda ya Muungano wakati huo huo hawautaki!
Huu Muungano ni pasua kichwa!
Haya manung'uniko, malalamishi na "kutunishiana misuli" vitaisha lini?