Prof. Tibaijuka ashauri wabunge wasiwe Mawaziri!

Prof. Tibaijuka ashauri wabunge wasiwe Mawaziri!

CCM ni watu wa ajabu sana!

Humphrey Polepole alimaliza kazi,siku ya Mdahalo wao kuwa,ccm wanskataa mfumo huo kwa kuwa utawakosesha nyadhifa zile za kupeana baada ya kumsaidia Rais kupiga debe,pili zitawafanya wakose mafungu ya kujitajirisha kwa kuwa chama chao kibaruhusu ukwapuaji na kujitajirisha.

Kitendo cha kuweka kifungu cha 16 kinachozuia kuweka fedha nje,wabunge kutokuwa Mawaziri wakajua siasa itakuwa haina maana,

Kitendo cha kuhakikisha Mbunge anapigiwa kura ya kuondolewa ubunge akiunga mkono hoja inayowaonea wapigakura wake,ccm ikajua kuwa kwa kuwa chama lengo lake kuu kuwahakikishia wawekezaji ulinzi na sie kutupatia fungu la kumi tutaumia tu,lazima tuikatae ili tuwe salama.

Ndio maana bila aibu siku hiyo walicheza ngoma ndani ya ukumbi wa bunge bila aibu,wakisema tumewauaaaa!
 
Ahaa... anatia aibu kabisa kabisa hyuyu mama. Wakati wa kuandika ile katiba yao feki chini ya jambazi lililokubuhu Chenge mbona hakusema?
 
Watu hujifunza kutokana na makosa, hebu tujaribu kuwasikiliza watu wa aina ili tujifunze jambo. AISIFUYE MVUA IMEMNYEA.
 
Aliyekuwa Waziri wa Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Makazi Prof Anna Tibaijuka ameibuka na kusema Mbunge anapokuwa Waziri kama ilivyo sasa, anakuwa anafanya kazi za kuitetea Serikali badala ya kuisimamia.

Mbunge huyo wa jimbo la Muleta Kusini amesema pia anakosa nafasi ya kuwatumikia ipasavyo wananchi wa jimbo lake ambao ndio wamemchagua kuwasilisha matatizo yao Serikalini kwa ajili ya utatuzi.

Prof Tibaijuka ameibuka baada ya kuvuliwa wadhifa wake wa uwaziri na Rais Jakaya Kikwete kufuatia kupokea Bil 1.6 kutoka kwa James Rugemalira kinyume na masharti ya maadili kuhusu zawadi kwa mtumishi wa UMMA.

Prof Tibaijuka amesema sasa amerudi jimboni kwake Muleba Kusini kuwatumikia Wananchi. Amesema moja ya changamoto ambayo alikumbana nayo alipokuwa Waziri ni kuwa hakupata muda wa kutosha kuwatumikia Wananchi wa jimbo lake.

Muda mwingi alikuwa analazimika kufanya shughuli za Serikali badala ya kuisimamia Serikali ili itekeleze mahitaji ya wananchi wa jimbo lake kwa wakati. Hivyo kwa kuwa sasa yeye sio Waziri tena, basi anao muda wa kutosha kutatua kero za wananchi.

Ikumbukwe jambo hili la Mawaziri wasitokane na Wabunge lilipendekezwa kwenye rasimu ya pili ya katiba iliyokuwa imewasilishwa bungeni na iliyokuwa tume ya Katiba chini ya aliyekuwa Mwenyekiti wake Jaji Joseph Warioba.

Hata hivyo jambo hilo lilipingwa na bunge la katiba, na wengi waliopinga pendekezo hilo ni wabunge wa Chama cha Mapinduzi akiwemo Prof Anna Tibaijuka.

Sasa ni jambo la kushangaza kumuona Prof Tibaijuka leo anatoa kauli hiyo wakati alipokuwa kwenye bunge la katiba hakusema chochote na alipiga kura ya ndio vipengele vyote vya katiba iliyopendekezwa.
 
Kipindi cha Nipashe cha Radio One Stereo kimeripoti kuwa akiwa jimboni kwake akiongea na wananchi wa huko Mama Profesa Anna Tibaijuka amenukuliwa akisema kuwa serikali sasa iangalie uwezekano wa mawaziri kutokuwa wabunge kwani kunawakosesha fursa ya kuwa karibu na wananchi (wa majimbo yao).

Hapo ndiyo nikabaki kujiuliza hivi huyu Bibi kavurugwa eeh? Yeye si alikuwa sehemu ya kuandaa hiki kinachoitwa katiba inayopendekezwa?! na kwa kujibu wa katiba yao hiyo pendekezwa, ibara ya 111-1(d) inatamka bayana kuwa:



111.-(1) Mtu atateuliwa kuwa waziri au naibu waziri wa serikali ya Jamhuri ya Muungano ikiwa:

(d)ni mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.


Maswali ninayojiuliza hapa:
Mama Tibaijuka amesahau walichokipendekeza kwenye katiba yao pendwa?
Au alijua anahutubia majuha?

50.JPG

 
Anawalilia wananchi wake wampe kura mwakan hana lolote.......alikua wapi kwenye bunge la.katiba mpk.issue ikapita kama.sio umbea?
 
Unafiki na nikuchanganyikiwa huko.Ni afadhari akae atulie maana ni kama Kadata vile.
 
Haya ya mwanaye je
 

Attachments

  • 1419596588387.jpg
    1419596588387.jpg
    56.3 KB · Views: 248
Mbona anakuja kuzungumza haya baada ya kuachishwa uwaziri?
Ina maana miaka 4 yote hajaweza kuwatumikia wananchi wake vyema.
 
Back
Top Bottom