Aliyekuwa waziri wa ardhi na makazi wa Tanzania mh. Anna Tibaijuka anaitaka serikali kubadirisha utaratibu wa mbunge kutokuwa waziri ili wabunge waweze kuwahudumia wapiga kura wao badala ya kutumia muda mwingi kufanya kazi za serikali.
Wadau kama sio uchizi ni nn hiki au ndio kapagawa baada ya kufutwa kwake?
Hilo lilikuwemo ktk rasimu ya katiba mpya kwa wingi wao CCM wote walilipinga sasa imekuwaje baada ya kutolewa alione ni suala la msingi,hiyo inaonyesha kuwa CCM wengi wameburuzwa kumbe wana matakwa yao binafsi na sio kufuata matakwa ya chama hata kama huridhii.
Mkuu tupe chanzo cha habari maana wengine tunatumia ubongo kuchambua jambo/mambo kuliko wengi wao wanotumia HISIA TU! Nitakuja na comments baada ya kupata source ya hizi habari.