1. Loliondo hakuna anayehamishwa, bali imewekwa mipaka kati ya kilomita za mraba 2,500 na 1,500 ambazo jumla ni kilomita za mraba 4,000.
2. Ngorongoro wanaohamishwa ni kutokana na wingi wao wa sasa, usalama wao na kukiuka masharti ya uhifadhi kwa kujenga nyumba za kudumu, kufanya kilimo na mengine mengi.
3. Prof. Shivji anasahau kuwa waliopo Ngorongoro si wazaliwa, bali walihamishiwa hapo mwaka 1958 kutoka Serengeti.
4. Prof. Shivji anapaswa kutambua haki ya urithi kizazi hadi kizazi. Ndani ya Ngorongoro sheria ya NCA iko wazi kabisa hawamiliki ardhi, hivyo hawana cha kurithisha watoto wao.
5. Mimi nami nimebaki na swali litakalonikosesha usingizi, hivi Prof. Shivji hayajui haya au kuna kitu nyuma ya pazia?