Prof. Mwandosya atoa ufafanuzi juu ya elimu yake

CCM ACHENI UKILAZA WA MWENDO KASI. NANI KASEMA MALISA KAPATA FOUR?? MALISA HAJAWAHI KUSOMA MINAKI HAYO MATOKEO MNAYOSAMBAZA SI YAKE. BOTH O LEVEL NA A.LEVEL KASOMA MOSHI. MATOKEO YAKE HAYA HAPA.

O.LEVEL,

GODLISTEN MALISA DIVISION 1 POINTS 16

J.K NYERERE SECONDARY SCHOOL, MOSHI 2007

CIV-C HIS-D GEO-C KIS-B ENG-B PHY-B CHE-B BIO-B BAS-C

http://www.matokeo.necta.go.tz/csee/S1038.htm

Mna swali jingine? CHADEMA imejaa vichwa, ukilaza wa mwendo kasi waachieni kina Jesca na magamba wa Lumumba.
Hahahaha dah huyu jamaa kumbe ndio wale wale, yuko hapa anaropoka ropoka bila staha za Kiongozi mkuu wa nchi? Fumbafu thana
 
Kwani kuna mahali popote alitiliwa mashaka kuwa Elimu yake ni ya Mwendokasi ya kama ya mtoto wa Baba Jesca?

Sipingani na Maelezo na historia ya Prof.Mwandosya ila sasa yeye amefikaje hapa? Maana labda kuna kitu sikielewi.
Ndio! Kuna jambo huelewi! Na japo huelewi unajifanya kuelewa na kutoa maneno yasiyo ya maana. Hapa anamjibu mtu anayeitwa Malisa aliyeandika na kupotosha kuhusu elimu ya Mwandosya na hao wengine. (wakati anazungumzia kuhusu wanafunzi wa diploma ya Chuo kIkuu Dodoma). Alikuwa anafanya reference kwa kina Mwandosya lakini akajikuta napotosha kuhusu elimu yao. Hapo ndipo Prof. Mwandosya alipoweka sawa.
 
Tatizo la Malisa ni kupost majina ya watu wasiohusika na huu mjadala badala ya jina moja alilokuwa anazungumzia. Wakati huo yeye pia ni kilaza wa kutosha tu. Matokeo ya Malisa Godlisten ya pale Minaki Form IV 2007: 0044,M,GODLBISTEN MALISA,27,IV,CIV-C HIS-F GEO-D KIS-D ENG-D PHY-D CHE-D BIO-D BAS-D. Link: http://www.matokeo.necta.go.tz/csee/S0133.htm
Kuna Uzi niliomba kesi za mtu mmoja mmoja sifutwe, tunakosa busara na kuanza kushambuliana, taratibu tunaanza kuleteana aibu zetu na huenda tusipone hadi kila mmoja wetu amedhalilika!
 
Mzee wangu Prof Mwandosya ni hoja ipi ya Malisa uliyoijibu ? Kama ni hili la vilaza kama baba Jesca anavyosema sijaona uhusiano kabisa ,au kuna Hoja nyingine ya Malisa tofauti na hii ya vilaza wa maskini??
Mkuu angalia usiingie chaka kwa ajili ya ushabiki. Alichojibu Prof. Mwandosya sio kumtetea Jesca au Magufuli bali ni ku-clarify jinsi yeye na hao wengine walivyosoma (jambo ambalo Malisa katika kuwatetea wanafunzi wa UDOM alifanya reference kwa kina Prof. Mwandosya na kusema walipomaliza four four walienda direct chuo kikuu)
 
@2Kimo,Asante...Nimeelewa.Maana niliuliza baada ya kuona mambo ya Baba Jesca na Elimu ya Mwendokasi na Prof.Mwandosya wapi na wapi tena?
 
Kwani kuna mahali popote alitiliwa mashaka kuwa Elimu yake ni ya Mwendokasi ya kama ya mtoto wa Baba Jesca?

Sipingani na Maelezo na historia ya Prof.Mwandosya ila sasa yeye amefikaje hapa? Maana labda kuna kitu sikielewi.
Ukiona hivi ujue hoja imegonga utosi! Kesho utasikia matamko meeengi kutoka kwa watu na heshma zao.
 
Wakati niko CoET, Prof Luhanga alinifundisha na kipindi hikohiko alikuwa VC wa UDSM, alikuwa anasema maprof wako wawili tu pale UDSM ni yeye na Prof Mwandosya,
Ikanipa wasaa wa kutafuta machapisho yake, yalikuwa ni machapisho bora yenye citations za hali ya juu kabisa. kwa wale wasiomuelewa mwandosya wafanye review kidogo tu kujua ni mtu wa aina gani
 
malisa amesoma jk nyerere au minaki?
 

Attachments

  • malisa jk nyerere au minaki.docx
    53.7 KB · Views: 30
Mwaka 1967 Serikali, kupitia Wizara ya Elimu ya Taifa ilianzisha sera ya kuwa na shule ambazo zingechukua wanafunzi wenye vipaji, waliofanya vizuri na kupata alama za juu kwenye masomo ya sayansi na hisabati katika mitihani ya kidato cha nne.

Katika mfumo huo taasisi/shule mbili, Chuo cha Ufundi Dar es Salaam, na Sekondari ya Kibaha, zilichaguliwa kudahili wanafunzi waliopata alama za juu katika hisabati, fizikia, na kemia, kuchukua masomo ya Hisabati, Hisabati, na Fizikia (Pure Mathematics, Applied Mathematics, and Physics) kidato cha tano na cha sita(Advanced Level au A-Level).

Chuo cha Ufundi Dar es Salaam kilichaguliwa kuanzisha masomo ya kidato cha tano na cha sita mbali na mafunzo ya kawaida ya cheti(Full Technician Certificate). Kozi hizi mbili zilienda sambamba lakini zilikuwa tofauti. Masomo ya kidato cha tano na sita yalilenga katika kuwatayarisha wanafunzi ambao baada ya kumaliza na kufaulu wangeenda vyuo vikuu kusomea uhandisi.

Mbali na mchepuo wa Hisabati, Hisabati na Fizikia, wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita Chuo cha Ufundi Dae es Salaam walichukua masomo ya ziada ya Uchoraji katika Uhandisi (Engineering Drawing) na mazoezi ya karakana (Workshop Practice).

Masomo haya yalitolewa katika azma ile ile ya kuwatayarisha wanafunzi kuchukua uhandisi vyuo vikuu lakini hawakutahiniwa katika masomo haya ya ziada. Mchepuo huu ulianza mwaka 1968 na pamoja na mafanikio makubwa ulihitimishwa mwaka 1972.

Baadhi ya wanafunzi waliopitia mchepuo huo ni Profesa Mathew Luhanga, Profesa Lunogelo Mwamila, Profesa Mark Mwandosya, Eric Mugurusi, Majani(RIP), Profesa Maurice Mbago, Kassim Mpenda, na wahandisi na wataalamu wengi mashuhuri.

Kwa kumalizia, si kweli kwamba Profesa Mwandosya alipata cheti cha ufundi halafu akaenda Chuo Kikuu cha Aston Uingereza, bali alipata alama za juu kidato cha sita katika mchepuo wa Hisabati, Hisabati, na Fizikia (Pure Mathematics, Applied Mathematics, and Physics), msingi uliomwezesha hatimaye kupata shahada ya uhandisi umeme daraja la kwanza( First Class Honours), Chuo Kikuu cha Aston, Uingereza, na hivyo kuruhusiwa kufanya shahada ya uzamifu (PhD), Chuo Kikuu cha Birmingham, Uingereza, moja kwa moja bila kupitia shahada ya uzamili(Masters).

Rafiki yangu yeyote wa fb anayemfahamu Ndugu Malisa GJ,mwandishi na mchangiaji wa makala katika mitandao ya kijamii, tafadhali mpatie taarifa hii. Shukrani.

Mark Mwandosya.
Tunashukuru kwa taarifa
 
Mkuu angalia usiingie chaka kwa ajili ya ushabiki. Alichojibu Prof. Mwandosya sio kumtetea Jesca au Magufuli bali ni ku-clarify jinsi yeye na hao wengine walivyosoma (jambo ambalo Malisa katika kuwatetea wanafunzi wa UDOM alifanya reference kwa kina Prof. Mwandosya na kusema walipomaliza four four walienda direct chuo kikuu)
Asante Mkuu na sijaingia chaka ndio maana hapo kwenye statement yangu nimeuliza ni hoja ipi ,kuna hoja ya Malisa inayotembea humu ndani kumuhusu Jesca ,

Ni wapi nilipo onyesha ushabiki ?? Kuita mtoto wa mwingine kilaza wakati una wa kwako ni kilaza zaidi yao unataka niunge mkono hilo ?
 
Sijaelewa,,,,,anamjibia Jesca ama ni vipi. Kama ni Jesca basi mzee kaenda chaka.........
Halafu wazee kama hawa naanza kuwatilia mashaka. Maana kuna mambo hajaendi sawa ila wako kimya tu
Sukari, Lugumi, Bunge Live, Udikteta wa Dr.Tulia.......na sasa VILAZA na UDOM
Mi wazee wanaonufaika na mfumo huwa siwaamini sana
Mkuu unategemea hao wategemezi wa ccm waseme lolote la kuikosoa ccm?
 
Yaani tumesahau Lugumi kabisa....tunadiscuss matokeoa ya watu...

Huko fb ndo watu wanachafuana mbaya...though muwe makini katika kupost matokeo feki ya watu.....

Manake mtu atasimama na wewe mahakamani kwa staili hii....

Mwenye yangu ayalete
 
Tatizo la Malisa ni kupost majina ya watu wasiohusika na huu mjadala badala ya jina moja alilokuwa anazungumzia. Wakati huo yeye pia ni kilaza wa kutosha tu. Matokeo ya Malisa Godlisten ya pale Minaki Form IV 2007: 0044,M,GODLBISTEN MALISA,27,IV,CIV-C HIS-F GEO-D KIS-D ENG-D PHY-D CHE-D BIO-D BAS-D. Link: http://www.matokeo.necta.go.tz/csee/S0133.htm
Kumbe huyu jamaa nae ni KILAZA anashinda anatupigia kelele tu hapa...!!
 
Back
Top Bottom