Prof. Mwandosya atoa ufafanuzi juu ya elimu yake

Dusko Tadic

Senior Member
Nov 22, 2014
171
96
Mwaka 1967 Serikali, kupitia Wizara ya Elimu ya Taifa ilianzisha sera ya kuwa na shule ambazo zingechukua wanafunzi wenye vipaji, waliofanya vizuri na kupata alama za juu kwenye masomo ya sayansi na hisabati katika mitihani ya kidato cha nne.

Katika mfumo huo taasisi/shule mbili, Chuo cha Ufundi Dar es Salaam, na Sekondari ya Kibaha, zilichaguliwa kudahili wanafunzi waliopata alama za juu katika hisabati, fizikia, na kemia, kuchukua masomo ya Hisabati, Hisabati, na Fizikia (Pure Mathematics, Applied Mathematics, and Physics) kidato cha tano na cha sita(Advanced Level au A-Level).

Chuo cha Ufundi Dar es Salaam kilichaguliwa kuanzisha masomo ya kidato cha tano na cha sita mbali na mafunzo ya kawaida ya cheti(Full Technician Certificate). Kozi hizi mbili zilienda sambamba lakini zilikuwa tofauti. Masomo ya kidato cha tano na sita yalilenga katika kuwatayarisha wanafunzi ambao baada ya kumaliza na kufaulu wangeenda vyuo vikuu kusomea uhandisi.

Mbali na mchepuo wa Hisabati, Hisabati na Fizikia, wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita Chuo cha Ufundi Dae es Salaam walichukua masomo ya ziada ya Uchoraji katika Uhandisi (Engineering Drawing) na mazoezi ya karakana (Workshop Practice).

Masomo haya yalitolewa katika azma ile ile ya kuwatayarisha wanafunzi kuchukua uhandisi vyuo vikuu lakini hawakutahiniwa katika masomo haya ya ziada. Mchepuo huu ulianza mwaka 1968 na pamoja na mafanikio makubwa ulihitimishwa mwaka 1972.

Baadhi ya wanafunzi waliopitia mchepuo huo ni Profesa Mathew Luhanga, Profesa Lunogelo Mwamila, Profesa Mark Mwandosya, Eric Mugurusi, Majani(RIP), Profesa Maurice Mbago, Kassim Mpenda, na wahandisi na wataalamu wengi mashuhuri.

Kwa kumalizia, si kweli kwamba Profesa Mwandosya alipata cheti cha ufundi halafu akaenda Chuo Kikuu cha Aston Uingereza, bali alipata alama za juu kidato cha sita katika mchepuo wa Hisabati, Hisabati, na Fizikia (Pure Mathematics, Applied Mathematics, and Physics), msingi uliomwezesha hatimaye kupata shahada ya uhandisi umeme daraja la kwanza( First Class Honours), Chuo Kikuu cha Aston, Uingereza, na hivyo kuruhusiwa kufanya shahada ya uzamifu (PhD), Chuo Kikuu cha Birmingham, Uingereza, moja kwa moja bila kupitia shahada ya uzamili(Masters).

Rafiki yangu yeyote wa fb anayemfahamu Ndugu Malisa GJ,mwandishi na mchangiaji wa makala katika mitandao ya kijamii, tafadhali mpatie taarifa hii. Shukrani.

Mark Mwandosya.
 
28051e336ff0b786102433fc98dba722.jpg
 
Tatizo la Malisa ni kupost majina ya watu wasiohusika na huu mjadala badala ya jina moja alilokuwa anazungumzia. Wakati huo yeye pia ni kilaza wa kutosha tu. Matokeo ya Malisa Godlisten ya pale Minaki Form IV 2007: 0044,M,GODLBISTEN MALISA,27,IV,CIV-C HIS-F GEO-D KIS-D ENG-D PHY-D CHE-D BIO-D BAS-D. Link: http://www.matokeo.necta.go.tz/csee/S0133.htm
duh... JF noma, kumbe ni kama ya Jesca
 
Tatizo la Malisa ni kupost majina ya watu wasiohusika na huu mjadala badala ya jina moja alilokuwa anazungumzia. Wakati huo yeye pia ni kilaza wa kutosha tu. Matokeo ya Malisa Godlisten ya pale Minaki Form IV 2007: 0044,M,GODLBISTEN MALISA,27,IV,CIV-C HIS-F GEO-D KIS-D ENG-D PHY-D CHE-D BIO-D BAS-D. Link: http://www.matokeo.necta.go.tz/csee/S0133.htm
Haya sasa tunapoelekea tutaaza kuchunguzana tulipataje wake na waume na watoto baba zao halisi
 
Kwani Jesca John Magufuli alipata alama za juu kiasi cha kudahiliwa UDOM?
Prof. Mwandosya namheshimu sana lakini kwenye hili akae mbali au aende Mwakaleli kubuni miradi ya maendeleo maana barabara ya Katumba-Mwakaleli-Lufilyo haipitiki na yeye amemaliza miaka 15 madarakani bila kufanya lolote kwenye miundombinu na kuwaacha raia wakibebwa kwenye malori kama ndizi na mihogo
 
Sijaelewa,,,,,anamjibia Jesca ama ni vipi. Kama ni Jesca basi mzee kaenda chaka.........
Halafu wazee kama hawa naanza kuwatilia mashaka. Maana kuna mambo hajaendi sawa ila wako kimya tu
Sukari, Lugumi, Bunge Live, Udikteta wa Dr.Tulia.......na sasa VILAZA na UDOM
Mi wazee wanaonufaika na mfumo huwa siwaamini sana
Hebu jiridhishe na hoja kwanza kabla ya kumshutumu!
Malisa alimtolea mfano Mwandosya kuwa elimu yake ni form 4, then akaingia certificate na diploma kabla hajaenda University! Alichokifanya hapa ni kuleta usahihi wa taarifa yake tu, sidhani kama amegusia jambo lolote la Jesca! Wewe umekuwa mvivu kufuatilia taarifa na umekurupuka na majibu na shutuma kwa Mwandosya!
 
CCM ACHENI UKILAZA WA MWENDO KASI. NANI KASEMA MALISA KAPATA FOUR?? MALISA HAJAWAHI KUSOMA MINAKI HAYO MATOKEO MNAYOSAMBAZA SI YAKE. BOTH O LEVEL NA A.LEVEL KASOMA MOSHI. MATOKEO YAKE HAYA HAPA.

O.LEVEL,

GODLISTEN MALISA DIVISION 1 POINTS 16

J.K NYERERE SECONDARY SCHOOL, MOSHI 2007

CIV-C HIS-D GEO-C KIS-B ENG-B PHY-B CHE-B BIO-B BAS-C

http://www.matokeo.necta.go.tz/csee/S1038.htm

Mna swali jingine? CHADEMA imejaa vichwa, ukilaza wa mwendo kasi waachieni kina Jesca na magamba wa Lumumba.
 
Back
Top Bottom