Prof. Mwandosya atoa ufafanuzi juu ya elimu yake

Prof. Mwandosya atoa ufafanuzi juu ya elimu yake

Ndio! Kuna jambo huelewi! Na japo huelewi unajifanya kuelewa na kutoa maneno yasiyo ya maana. Hapa anamjibu mtu anayeitwa Malisa aliyeandika na kupotosha kuhusu elimu ya Mwandosya na hao wengine. (wakati anazungumzia kuhusu wanafunzi wa diploma ya Chuo kIkuu Dodoma). Alikuwa anafanya reference kwa kina Mwandosya lakini akajikuta napotosha kuhusu elimu yao. Hapo ndipo Prof. Mwandosya alipoweka sawa.

Nyie watu sijui matatizo yenu ni nini tu!!

Je, ni kwa sababu hamtaki kukubaliana na ukweli kuwa Rais amepotoshwa na yeye kupotoka sana kwa ishu ya vijana hawa wa UDOM?

Na kuhusu Mark Mwandosya, binafsi sidhani kama ni ishu hapa.

Kilicho cha ukweli ni kuwa, wapo wasomi wengi katika viwango tofauti tofauti vya elimu kuanzia maprofesa, madaktari, wenye shahada moja, mbili au stashahada ya juu, stashahada ya kawaida ambao walipitia njia sawa sawa na hawa vijana wanaosomea diploma maalum ya ualimu wa masomo ya sayansi pale UDOM ambao leo wanetukanwa na Rais kwa kuitwa "vilaza!!"

Si hivyo tu, bali hata miaka ya 1980 hadi 1990 kulikuwa na vyuo ambavyo vilikuwa vinachukua vijana waliomaliza kidato cha nne moja kwa moja kwenda kusomea stashahada ya ualimu!!

Mfano wa vyuo hivi ni kama Shinyanga TTC (wakati huo kikiitwa SHY - COM kwa sbb kilikuwa ni maalumu kwa walimu wa masomo ya biashara i.e Commerce & Book Keeping), Chang'ombe TTC, Korogwe
TTC nk. Hawa tuliwaita wanaenda kusomea nusu kombi!!

Tofauti na wanafunzi waliomaliza kidato cha sita (form six) waliokuwa wanachaguliwa kwenda kusomea Stashahada ya ualimu kwa miaka miwili, hawa waliomaliza kidato cha nne course duration yao ilikuwa ni miaka miatatu badala ya miwili!!

Huyu aliyemaliza kidato cha sita na kwenda kuchukua diploma yake alikuwa sawasawa na huyu aliyemaliza kidato cha nne na kwenda kusomea nusu kombi ndani yake anasoma na ualimu!!

Sasa leo kwa hawa vijana wa special diploma pale UDOM cha ajabu ni nini
eti??

Labda tofauti na kasoro pekee ambayo mimi binafsi naiona ni kuchukua hadi wale waliopata alama mbaya za ufaulu tofauti na standards zilizowekwa

Hii kamwe haikupaswa kuwa kesi kubwa kwa kiasi ambacho ikafikia hatua ya hadi Rais kulisemea hili kwa kutumia lugha isiyo na staha wala kupendeza hata mbele ya ummajambo linaloishusha credibility yake!!

Hii inasababisha watu kuanza kujiuliza kulikoni huyu ndugu yetu Rais? Huwa anafikiria kweli kabla ya kusema jambo? Au ndo mizuka yenyewe hii?
 
Mzee Mwandosya katafuta style ya nitoke ipi, kaja na kitanga's style. Bora aendelee kupotea tu kwenye media kwanza anatafuta nini tena kama ni majukumu hapati Magu amesema wazee hawataki wanakula rushwa, aendelee kuangalia migomba yake tu.
 
CCM ACHENI UKILAZA WA MWENDO KASI. NANI KASEMA MALISA KAPATA FOUR?? MALISA HAJAWAHI KUSOMA MINAKI HAYO MATOKEO MNAYOSAMBAZA SI YAKE. BOTH O LEVEL NA A.LEVEL KASOMA MOSHI. MATOKEO YAKE HAYA HAPA.

O.LEVEL,

GODLISTEN MALISA DIVISION 1 POINTS 16

J.K NYERERE SECONDARY SCHOOL, MOSHI 2007

CIV-C HIS-D GEO-C KIS-B ENG-B PHY-B CHE-B BIO-B BAS-C

http://www.matokeo.necta.go.tz/csee/S1038.htm

Mna swali jingine? CHADEMA imejaa vichwa, ukilaza wa mwendo kasi waachieni kina Jesca na magamba wa Lumumba.
Lete matokeo ya mbowe na kubenea hapa
 
Sijaelewa,,,,,anamjibia Jesca ama ni vipi. Kama ni Jesca basi mzee kaenda chaka.........
Halafu wazee kama hawa naanza kuwatilia mashaka. Maana kuna mambo hajaendi sawa ila wako kimya tu
Sukari, Lugumi, Bunge Live, Udikteta wa Dr.Tulia.......na sasa VILAZA na UDOM
Mi wazee wanaonufaika na mfumo huwa siwaamini sana

Mleta mada alitakiwa aseme kuwa Prof. Mwandosya anamjibu Malisa aliyesema kwamba Profesa Mwandosya alipata cheti cha ufundi halafu akaenda Chuo Kikuu cha Aston Uingereza, akijaribu kuhalalisha watoto wa Form IV kwenda UDOM moja kwa moja. Nadhani Prof. ameisikia ndio anatoa ufafanuzi sio kwamba anajibu issue ya Jesca. Naona kwa sasa kaamua kupumzika siasa.
 
Watu kama hawa wanaojiita wasomi wakubwa hawana faida kwenye hii nchi ni wachumia tumbo tuu. Bora vilaza tuu sometime huwa wanamsaada mkubwa kwa jamii.
Mtu kama hyu prof anashindwa kubuni mikakati dhabiti ya kukinyanyua chuo chake cha Mbeya University of Science and Technology anakalia kujibizana na vihoja visivyo na maana hafai kabisa. Siasa za chama tawala zinawaharibu sana hawa wazee. Wapumzike tuu nchi wawachie wengine wenye damu changa waiongoze wenyewe waneshindwa.

Hii ni aibu kubwa kwa watu wenye uwezo mkubwa kushindwa kutatua kero za watanzania na kutuletea bla bla nyingi.
Shame on them.
 
Kwani kuna mahali popote alitiliwa mashaka kuwa Elimu yake ni ya Mwendokasi ya kama ya mtoto wa Baba Jesca?

Sipingani na Maelezo na historia ya Prof.Mwandosya ila sasa yeye amefikaje hapa? Maana labda kuna kitu sikielewi.
Ben nimekuelewa
 
Kazi kweli kweli hii nchi inahitaji mifumo bora ili kuzuia vigogo kujimilikisha nchi.
 
Hii "vita" ya ukilaza na elimu za mwendokasi itawafukunyua wengi kutoka huko walikojificha.Kumbe Prof. Mwandosya hana Master's degree?

Wakati mwingine ni bora mtu kukaa kimya tu kuliko kutoa maelezo yasiyo na tija na kujiharibia CV.
 
Mzee Mwandosya ni brain haba sana kuipata hata kama ni Marekani. Taifa lilitumia pesa nyingi ili aje atumike kuleta maendeleo nchini. Nasikitika, taifa limem-missuse. Anazeeka sasa bila ya ku-utilize at least 50% ya uwezo wake mkubwa ambao yeyote atakaye pinga uwezo alionao anastahili kitanda cha kudumu MIREMBE!
kosa lake ni kuwa mwanasiasa...ukishakuwa mwanasiasa inabidi ufuate muongozo wa chama hata kama ni wa hovyo
 
Mwaka 1967 Serikali, kupitia Wizara ya Elimu ya Taifa ilianzisha sera ya kuwa na shule ambazo zingechukua wanafunzi wenye vipaji, waliofanya vizuri na kupata alama za juu kwenye masomo ya sayansi na hisabati katika mitihani ya kidato cha nne.

Katika mfumo huo taasisi/shule mbili, Chuo cha Ufundi Dar es Salaam, na Sekondari ya Kibaha, zilichaguliwa kudahili wanafunzi waliopata alama za juu katika hisabati, fizikia, na kemia, kuchukua masomo ya Hisabati, Hisabati, na Fizikia (Pure Mathematics, Applied Mathematics, and Physics) kidato cha tano na cha sita(Advanced Level au A-Level).

Chuo cha Ufundi Dar es Salaam kilichaguliwa kuanzisha masomo ya kidato cha tano na cha sita mbali na mafunzo ya kawaida ya cheti(Full Technician Certificate). Kozi hizi mbili zilienda sambamba lakini zilikuwa tofauti. Masomo ya kidato cha tano na sita yalilenga katika kuwatayarisha wanafunzi ambao baada ya kumaliza na kufaulu wangeenda vyuo vikuu kusomea uhandisi.

Mbali na mchepuo wa Hisabati, Hisabati na Fizikia, wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita Chuo cha Ufundi Dae es Salaam walichukua masomo ya ziada ya Uchoraji katika Uhandisi (Engineering Drawing) na mazoezi ya karakana (Workshop Practice).

Masomo haya yalitolewa katika azma ile ile ya kuwatayarisha wanafunzi kuchukua uhandisi vyuo vikuu lakini hawakutahiniwa katika masomo haya ya ziada. Mchepuo huu ulianza mwaka 1968 na pamoja na mafanikio makubwa ulihitimishwa mwaka 1972.

Baadhi ya wanafunzi waliopitia mchepuo huo ni Profesa Mathew Luhanga, Profesa Lunogelo Mwamila, Profesa Mark Mwandosya, Eric Mugurusi, Majani(RIP), Profesa Maurice Mbago, Kassim Mpenda, na wahandisi na wataalamu wengi mashuhuri.

Kwa kumalizia, si kweli kwamba Profesa Mwandosya alipata cheti cha ufundi halafu akaenda Chuo Kikuu cha Aston Uingereza, bali alipata alama za juu kidato cha sita katika mchepuo wa Hisabati, Hisabati, na Fizikia (Pure Mathematics, Applied Mathematics, and Physics), msingi uliomwezesha hatimaye kupata shahada ya uhandisi umeme daraja la kwanza( First Class Honours), Chuo Kikuu cha Aston, Uingereza, na hivyo kuruhusiwa kufanya shahada ya uzamifu (PhD), Chuo Kikuu cha Birmingham, Uingereza, moja kwa moja bila kupitia shahada ya uzamili(Masters).

Rafiki yangu yeyote wa fb anayemfahamu Ndugu Malisa GJ,mwandishi na mchangiaji wa makala katika mitandao ya kijamii, tafadhali mpatie taarifa hii. Shukrani.

Mark Mwandosya.

Tuweke kumbukumbu sawasawa.
Serikali ilianza na darasa mahsus la wanafunzi wa 1967 walionza kwanza kusoma "Ordinary Technician Diploma" ya "City & Guilds"-- miaka 3,darasa lao likijulikana "TDE 67. Idadi yao ikiwa 17. Sambamba na hiyo, hawa walisoma vilevile London GCE--Pure, Applied Maths na Physics miaka 2(wakati huo shule zingine zikifanya Cambridge). Walimu wakiwa Mr. Goode kutoka Minaki na Mr. Burtchard kutoka Ihungo.Hawa walipata vyeti viwili wakati wanamaliza miaka yao 3 pale Tech.College 1969.

Hawa wa Form V per se walianza1968 kwa miaka 2. Nao walifanya vizuri tu
 
Mzee Mwandosya katafuta style ya nitoke ipi, kaja na kitanga's style. Bora aendelee kupotea tu kwenye media kwanza anatafuta nini tena kama ni majukumu hapati Magu amesema wazee hawataki wanakula rushwa, aendelee kuangalia migomba yake tu.
Huyo mzee ni mlalamishi sana hata kule Dodoma ndiye aliibua issue ya Kikwete kwenda na majina matano Mfukoni akitaka Membe awe Rais kisha watawale Nchi kifalume kwa upande huo alisema Ukweli, lakini kwa upande wa UDOM anachemsha tena ataamsha Majipu yake ambayo watu walimtunzia Siri kutokana na yeye kuwa Profeselii na si profesa olijino ni aina ya Wasomi wajanja janja kama Lipumba ambaye licha ya kujidai msomi alirubuniwa na Div 4 Nape na Div zero form six January Makamba akachukua pesa toka kwa Membe akawakacha Ukawa kwa visingizio vya kishamba tu, ni wakati wa kuwachunguza hawa watu wanaojiita Maprofesa na ma-Dr maana wengi wamesomea ufisadi kama Mwakyembe kwenye mabehewa na Tibaijuka kwenye Escrow na wenzao wengi wapiga Madili.
 
Nimeshaona vijana waliosoma FTC ya woodwork wanaoleta tija kubwa kuliko wasomi wengi wenye PhD.

PhD wetu wengi wanabakia kutisha watu kuwa wamesoma na kusahau kutumia elimu yao kuleta maendeleo.

Bora hata mama ntilie
 
Tatizo la Malisa ni kupost majina ya watu wasiohusika na huu mjadala badala ya jina moja alilokuwa anazungumzia. Wakati huo yeye pia ni kilaza wa kutosha tu. Matokeo ya Malisa Godlisten ya pale Minaki Form IV 2007: 0044,M,GODLBISTEN MALISA,27,IV,CIV-C HIS-F GEO-D KIS-D ENG-D PHY-D CHE-D BIO-D BAS-D. Link: http://www.matokeo.necta.go.tz/csee/S0133.htm
Huyu jamaa hana hata sifa za kuwa mmoja wa wanachama wa JF, sasa hapo D zimepangana kama bibi mwenye mimba, u-FreatThinker utatoka wapi?
 
Kwani kuna mahali popote alitiliwa mashaka kuwa Elimu yake ni ya Mwendokasi ya kama ya mtoto wa Baba Jesca?

Sipingani na Maelezo na historia ya Prof.Mwandosya ila sasa yeye amefikaje hapa? Maana labda kuna kitu sikielewi.
hembu na wewe tuwekee matokeo yako hapa watu wayaone...........naona ishakuwa fashion siku hizi
 
Hii "vita" ya ukilaza na elimu za mwendokasi itawafukunyua wengi kutoka huko walikojificha.Kumbe Prof. Mwandosya hana Master's degree?

Wakati mwingine ni bora mtu kukaa kimya tu kuliko kutoa maelezo yasiyo na tija na kujiharibia CV.
Halafu hicho chuo alichosoma Mwandosya si miongoni mwa vyuo bora huko UK, yaani ni ka chuo fulani kalimfanyia upendeleo wa hovyo kusoma Phd bila kuwa na master. Heri angekaa kimya, sikulijua hili kuwa Mwandosya hana masters.
 
Mkuu rejea tena ukweli wa post yako Malisa unayembambika ukilaza si aliyetoa hoja hapa. Hapa kasoma Old Moshi na matokeo ya ni Div 1. Unajilinganisha na Jesca nini?
Huyu Malisa naye kilaza tu, matokeo yake yapo hadharani ana 4.27, halafu kidume mzima anakomaa kumtusi Dada Mwenyekiti 4.30.
 
Back
Top Bottom