Prof. Mwandosya atoa ufafanuzi juu ya elimu yake

Prof. Mwandosya atoa ufafanuzi juu ya elimu yake

Mkuu prof alikuwa anakujibu juu ya kipande cha elimu yake ulichoandika , alikuwa anasahihisha! sehemu iliyo muhisu yeye tuu!

Haya mengine naomba nimtetee mzee wangu please!
 
Juzi niliweka andiko hapa kutoa ufafanuzi juu ya wanafunzi wa UDOM waliokua wakisoma Diploma maalumu ya Ualimu wakitokea kidato cha 4. Baadhi ya watu walihoji Uhalali wa wanafunzi hao kusoma Chuo Kikuu wakitokea kidato cha 4. Yani ilionekana ni maajabu kwenda Chuo kikuu bila kupita kidato cha tano na cha sita.

Nikatoa maelezo nikiwatetea vijana hao nikasema kwamba utaratibu wa kwenda Chuo kikuu bila kupita A-Level ni utaratibu rasmi unaotambulika nchini. Na wapo wengi waliotumia utaratibu huo na wakafika mbali. Katika kutoa mfano wa mmoja wa watu waliotumia utatatibu huo nikamtaja Profesa Mark Mwandosya, kwamba yeye baada ya kumaliza kidato cha nne alijiunga na chuo cha ufundi (DIT) kisha akadahiliwa chuo kikuu.

Jana nikapata taatifa kuwa Profesa Mwandosya amenijibu. Nikatumiwa taarifa ya majibu yake. Sikutaka kuamini taarifa hiyo kwa haraka hadi ndugu Gabriel Mwang'onda alipowasiliana nami na kunihakikishia kuwa ni majibu halisi kutoka kwa Profesa Mwandosya mwenyewe.

Kwanza nimpongeze Profesa Mwandosya kwa kuona umuhimu wa kunijibu. Ni viongozi wachache sana wanaotambua nguvu ya mitandao ya kijamii. Kwahiyo kama hoja yangu ilimfikia kupitia mitandao na akaweza kisoma na kujibu ni jambo la kupongezwa.

Lakini maelezo ya Mwandosya hayajajibu hoja ya msingi badala yake ametoa ufafanuzi juu ya elimu yake. Ingekuwa mahakamani Mwandosya angekua amejadili suala ambalo sio sehemu ya mjadala (matter which is not in dispute).

#MAELEZO_YA_MWANDOSYA

Mwandosya anakiri kwamba ni kweli alisoma chuo cha Ufundi Dar (DIT) lakini anasema kuwa si kweli kwamba hakusoma A-Level. Anasema akiwa DIT alisoma ufundi wakati huohuo akisoma masomo ya form five na six.

Anasema serikali kwa wakati huo ilianzisha mpango maalumu wa kuchukua wanafunzi wenye ufaulu wa juu ktk masomo ya sayansi na kuwasajili katika tasisi mbili ambazo ni sekondari ya Kibaha na Chuo cha Ufundi Dar (DIT) kwa masomo ya sayansi.

Mpango huo ulidumu kwa miaka mitatu kati ya mwaka 1968 na mwaka 1971. Kwa mujibu wa Mwandosya katika "mpango huo maalumu" wanafunzi walisoma masomo ya ufundi (FTC) wakati huohuo wakisoma masomo ya A-level. Hii ilimuwezesha yeye kudahiliwa chuo kikuu cha Aston nchini Uingereza kwa kuwa alikuwa amehitimu pia kidato cha sita nje ya masomo ya ufundi aliyokua akisomea.

Profesa Mwandosya ametaja baadhi ya maprofesa wenzake waliopita kwenye utaratibu huo maalumu ambao ni pamoja na Prof.Mugurusi, na Prof.Mathew Luhanga etc.

#HOJA_YA_MSINGI

Hoja ya msingi haikua Elimu yaProfesa Mwandosya. Hoja ya msingi ilikua utaratibu wa kwenda chuo kikuu bila kupita A-Level. Mwandosya alitumika tu kama mfano, kama ambavyo ningeweza kutumia mfano wa mtu mwingine.

Kwahiyo nilitegemea Mwandosya ajibu kwamba utaratibu huo UPO ila mfano uliotumika kwake si sahihi, au akanushe kwamba utaratibu huo HAUPO. Yani aseme hakujawahi kuwa na utaratibu wa kwenda chuo kikuu kwa kutokea FTC bila kupita A-Level, kwa hiyo maelezo ya Malisa ni ya uongo. Lakini Mwandosya hajafanya hivyo.

Alichofanya ni kutoa ufafanuzi juu ya elimu yake kana kwamba tulikua tuna hofu na elimu yake. Hakuna mtu mwenye hofu na elimu ya Profesa Mwandosya, tunajua yeye ni msomi mzuri anayetambulika kimataifa.

Ambacho alitakiwa kueleza ni kujibu hoja ya msingi then akanushe mfano uliomhusu yeye. Kwa mfano angeweza kusema "utaratibu wa kwenda chuo kikuu bila kupita A-level ni utaratibu rasmi unaotambulika ila mimi sikutumia utaratibu huo" kisha ndo akaeleza yeye alitumia utatatibu gani.

Lakini andiko lake kuwa alidahiliwa chuo kikuu kwa matokeo yake ya form six na sio cheti cha FTC ni kama vile anasema huwezi kwenda chuo kikuu ukitokea chuo cha ufundi (FTC) au vyuo vingine vya kawaida jambo ambalo si kweli. Yawezekana Mwandosya hakukusudia kumaanisha hivi lakini ndivyo watu walivyomuelewa.

Hoja ya msingi ni je, hivi haiwezekani kwenda chuo kikuu bila kupita A-level? Kama Mwandosya anasema yeye alipita A-level, je hakuna wengine waliofika chuo kikuu bila kupita A-level??

Ktk maelezo yake Mwandosya anasema utaratibu wa kusoma elimu ya ufundi (FTC) na masomo ya A-level kwa pamoja ulikua ni "mpango maalumu" uliodumu kwa miaka mitatu tu (1968 hadi 1971).

Maana yake ni kwamba kabla ya mwaka 1968 wanafunzi wa DIT walikua wakisoma FTC tu bila kuchanganya na A-level, na baada ya mwaka 1971 wanafunzi waliendelea kusoma FTC tu bila masomo ya ziada ya A-Level. Kwahiyo waliofanikiwa kusoma "two in one" yani FTC na wakati huohuo wakisoma A-Level ni akina Mwandosya tu (1968 - 1971).

Sasa je Mwandosya anataka kutuambia kuwa wale waliomaliza FTC kabla yao, au baada yao je, hawakupata nafasi za kwenda vyuo vikuu kwa sababu hawakuwa na masomo ya A-level?? Jibu si kweli.

Mimi binafsi nawafahamu wasomi wengi tu wazuri waliosoma FTC na walipomaliza wakadahiliwa vyuo vikuu bila kusoma A-Level kama Mwandosya. Na utaratibu huu umekua ukitumika kwa muda mrefu hadi serikali ilipobadilisha mtaala wa FTC kuwa Ordinary Diploma.

Na hadi sasa hivi wahitimu wa kidato cha 4 waliofanya vizuri masomo ya sayansi wanadahiliwa kusoma Ordinary Diploma kwenye vyuo vya ufundi kisha wanajiunga na vyuo vikuu kusomea shahada mbalimbambali za Uhandisi bila kupita A-Level.

Kwahiyo nihitimishe kwa kusema kwamba maelezo ya Profesa Mwandosya ni mazuri lakini ametoka nje ya hoja. Kama yeye alisoma FTC na A-Level kwa pamoja, haimaanishi kuwa hakuna waliosoma FTC peke yake na wakaenda vyuo vikuu. Wapo waliosoma FTC na walipohitimu wakaenda vyuo vikuu bila kufanya masomo ya ziada ya A-Level kama yeye.

Hivyo basi kwa kuwa inawezekana kwenda chuo kikuu bila kupita A-Level, hatuwezi kuwahukumu wanafumzi wa UDOM waliotoka kidato cha 4 kwenda kusomea Diploma maalumu ya ualimu wa sayansi kwa miaka mitatu. Utaratibu waliotumia upo sahihi kabisa na wakimaliza wanaweza kujiunga na vyuo vikuu wakasomea Shahada (degree) bila tatizo lolote.

Mnaweza kumfikishia salamu hizi baba yangu Profesa Mwandosya as matter for noting.

Asanteni,
Malisa G.J
Sasa huyu mwenye 4 malisa na profesa wapi na wapi madogo mbona kuota nywele za kwapa imekua shida?
 
Kwani mwenyekiti wao kaomba kwenda kusoma? Vyama navyo vinachuja wasomi siku hizi? Ingekuwa hivyo watu kama Kawawa, Lusinde na Lusinde wa sasa wasingekuwa na nafasi kwenye vyama? Tutofautishe siasa na uhalisia. Siasa zimetufikisha hapa tulipo ndo maana nadhani tufute hata vyama tuishi bila chama sababu sisi tusiokuwa na vyama tunateseka sababu ya vyama vyenu. Mwenzangu wazazi wako kijijini wameletewa maji na chama? dawa, huduma za wazee je?? oh vyama too much jamani.
Sory mkuu uliposema lusinde wa sasa ulimaanisha goodluck milinga au sor lakin
 
Naona Malisa na Saanane wamechiz toka washindwe uchaguzi.

Kila kitu kwao ni kibaya hakuna jema wanaloona ktk serikali hii ya awamu ya Tano.

Nawasihi wajitathmin upya chama wanakiua,watanzania huwaambii kitu kwa Magu
Magu hupi huyu baba jesca kilaza?
 
Sory mkuu uliposema lusinde wa sasa ulimaanisha goodluck milinga au sor lakin
Tuna lusinde wangapi mjengoni na kama siyo hivyo mzee lusinde una cv zake na je si alikuwa mkulu wa chama Dom mpaka anastaafu mbona hakuulizwa degree zake? Kumbuka siasa haviendani elimu vinaendani. Kama unatunga sheria kama bungeni elimu elimu elimu na uelewa. Ukija kwenye uhamasishaji ndo unakuta yule wa Mtera. Simple mind hawahitaji vichwa kuchanganyikiwa wanahitaji ngonjera na vigeregere. Bungeni ili mtu aheshimiwe ni kichwa na ndipo tabu inakoanzia sababu wapiga vigeregere na pambio na ngonjera wamejazwa ili kidumu.
 
Hakuna popote ambapo Professor Mwandosya amemjibu huyo Malisa.
Facebook wall ya Prof. Mwandosya inaonyesha bandiko la mwisho liliwekwa tarehe 14 May, 2016.
 
Hakuna popote ambapo Professor Mwandosya amemjibu huyo Malisa.
Facebook wall ya Prof. Mwandosya inaonyesha bandiko la mwisho liliwekwa tarehe 14 May, 2016.
Hata kama kajibu ni kuweka kumbukumbu sawa kuwa yeye hakupitia mfumo wa FTC kama ambavyo Malisa ameelezea katika posting yake. Jamii forums isiwe jamii ghetto! Kama angezunzumzia issue ya eligibility ya kuingia chuo kikuu kuwa ni A level pekee hata Mimi ningempinga kwa Hilo. Nashangaa Malisa kaja tena na argument ingine eti Prof hajajibu issue aliyozungumzia na hata wengine kumdhihaki wakati yeye katoa ufafanuzi tu kuhusu jinsi alivyoingia chuo kikuu. Nasimama kumtetea Prof kuwa hajatendewa haki na watu ambao kila jambo hulichukulia kwa misimamo ya kisiasa. Malisa aangeukubali huo ukweli aliotoa Prof na kisha kumuuliza msimamo wake katika issue hii. Nina hakika 150% Prof angesema FTC wako wengi tu walioingia chuo kikuu moja kwa moja maana kawafundisha. Vinginevyo issue ya Malisa na hao wengine wanaomsakama Prof hawajamtendea haki. Kama Malisa kalielewa hili amwombe msamaha Prof. Andishi la Malisa lilikuwa zuri sana ila hilo la Prof sio haki.
 
Mwaka 1967 Serikali, kupitia Wizara ya Elimu ya Taifa ilianzisha sera ya kuwa na shule ambazo zingechukua wanafunzi wenye vipaji, waliofanya vizuri na kupata alama za juu kwenye masomo ya sayansi na hisabati katika mitihani ya kidato cha nne.

Katika mfumo huo taasisi/shule mbili, Chuo cha Ufundi Dar es Salaam, na Sekondari ya Kibaha, zilichaguliwa kudahili wanafunzi waliopata alama za juu katika hisabati, fizikia, na kemia, kuchukua masomo ya Hisabati, Hisabati, na Fizikia (Pure Mathematics, Applied Mathematics, and Physics) kidato cha tano na cha sita(Advanced Level au A-Level).

Chuo cha Ufundi Dar es Salaam kilichaguliwa kuanzisha masomo ya kidato cha tano na cha sita mbali na mafunzo ya kawaida ya cheti(Full Technician Certificate). Kozi hizi mbili zilienda sambamba lakini zilikuwa tofauti. Masomo ya kidato cha tano na sita yalilenga katika kuwatayarisha wanafunzi ambao baada ya kumaliza na kufaulu wangeenda vyuo vikuu kusomea uhandisi.

Mbali na mchepuo wa Hisabati, Hisabati na Fizikia, wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita Chuo cha Ufundi Dae es Salaam walichukua masomo ya ziada ya Uchoraji katika Uhandisi (Engineering Drawing) na mazoezi ya karakana (Workshop Practice).

Masomo haya yalitolewa katika azma ile ile ya kuwatayarisha wanafunzi kuchukua uhandisi vyuo vikuu lakini hawakutahiniwa katika masomo haya ya ziada. Mchepuo huu ulianza mwaka 1968 na pamoja na mafanikio makubwa ulihitimishwa mwaka 1972.

Baadhi ya wanafunzi waliopitia mchepuo huo ni Profesa Mathew Luhanga, Profesa Lunogelo Mwamila, Profesa Mark Mwandosya, Eric Mugurusi, Majani(RIP), Profesa Maurice Mbago, Kassim Mpenda, na wahandisi na wataalamu wengi mashuhuri.

Kwa kumalizia, si kweli kwamba Profesa Mwandosya alipata cheti cha ufundi halafu akaenda Chuo Kikuu cha Aston Uingereza, bali alipata alama za juu kidato cha sita katika mchepuo wa Hisabati, Hisabati, na Fizikia (Pure Mathematics, Applied Mathematics, and Physics), msingi uliomwezesha hatimaye kupata shahada ya uhandisi umeme daraja la kwanza( First Class Honours), Chuo Kikuu cha Aston, Uingereza, na hivyo kuruhusiwa kufanya shahada ya uzamifu (PhD), Chuo Kikuu cha Birmingham, Uingereza, moja kwa moja bila kupitia shahada ya uzamili(Masters).

Rafiki yangu yeyote wa fb anayemfahamu Ndugu Malisa GJ,mwandishi na mchangiaji wa makala katika mitandao ya kijamii, tafadhali mpatie taarifa hii. Shukrani.

Mark Mwandosya.
Ingekuwa busara elimu aliyoipata kuwapa wengine kuliko kukimbilia siasa.
 
Yaani na ignorance ya watu imewafanya watu wasijue kuwa watu walioenda vyuo vya ufundi ndio waliokuwa vipanga! Hiyo ilikuwa sera ( I hope sere hii imefutwa ) maana iliwachanganya sana hata wanafunzi wenyewe. Kwani walichukuliwa mageneous, wakasoma miaka 3 halafu kwenda Chuo Kikuu wakawa wanambiwa inabidi wasome miaka 4 kama wenzao. hii iliwakatisha tamaa baadhi na Unfortunately ( hasa zamani) bila Degree unaonekana kama hujasoma hivyo wengi wao waliishia kuwa dissapointed esp. wale ambao hawakutaka tena ' poteza' 4 years. Hivyo watu wanapaswa kuelewa mambo yalivyokuwa! Natumaini imebadilishwa hii maana huenda kwa wakati ule ilikuwa na tija lajkini waliochaguliwa somehow walikuwa kama wamekuwa victimised!
 
Sielewi huyu Malisa anashindwa kuelewa kitu gani kwenye majibu ya Prof. Mwandosya.

Back
Top Bottom