Prof. Mwandosya atoa ufafanuzi juu ya elimu yake

Prof. Mwandosya atoa ufafanuzi juu ya elimu yake

Tatizo la Malisa ni kupost majina ya watu wasiohusika na huu mjadala badala ya jina moja alilokuwa anazungumzia. Wakati huo yeye pia ni kilaza wa kutosha tu. Matokeo ya Malisa Godlisten ya pale Minaki Form IV 2007: 0044,M,GODLBISTEN MALISA,27,IV,CIV-C HIS-F GEO-D KIS-D ENG-D PHY-D CHE-D BIO-D BAS-D. Link: http://www.matokeo.necta.go.tz/csee/S0133.htm

Umeaibishwa muongo wewe!
 
Mwaka 1967 Serikali, kupitia Wizara ya Elimu ya Taifa ilianzisha sera ya kuwa na shule ambazo zingechukua wanafunzi wenye vipaji, waliofanya vizuri na kupata alama za juu kwenye masomo ya sayansi na hisabati katika mitihani ya kidato cha nne.

Katika mfumo huo taasisi/shule mbili, Chuo cha Ufundi Dar es Salaam, na Sekondari ya Kibaha, zilichaguliwa kudahili wanafunzi waliopata alama za juu katika hisabati, fizikia, na kemia, kuchukua masomo ya Hisabati, Hisabati, na Fizikia (Pure Mathematics, Applied Mathematics, and Physics) kidato cha tano na cha sita(Advanced Level au A-Level).

Chuo cha Ufundi Dar es Salaam kilichaguliwa kuanzisha masomo ya kidato cha tano na cha sita mbali na mafunzo ya kawaida ya cheti(Full Technician Certificate). Kozi hizi mbili zilienda sambamba lakini zilikuwa tofauti. Masomo ya kidato cha tano na sita yalilenga katika kuwatayarisha wanafunzi ambao baada ya kumaliza na kufaulu wangeenda vyuo vikuu kusomea uhandisi.

Mbali na mchepuo wa Hisabati, Hisabati na Fizikia, wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita Chuo cha Ufundi Dae es Salaam walichukua masomo ya ziada ya Uchoraji katika Uhandisi (Engineering Drawing) na mazoezi ya karakana (Workshop Practice).

Masomo haya yalitolewa katika azma ile ile ya kuwatayarisha wanafunzi kuchukua uhandisi vyuo vikuu lakini hawakutahiniwa katika masomo haya ya ziada. Mchepuo huu ulianza mwaka 1968 na pamoja na mafanikio makubwa ulihitimishwa mwaka 1972.

Baadhi ya wanafunzi waliopitia mchepuo huo ni Profesa Mathew Luhanga, Profesa Lunogelo Mwamila, Profesa Mark Mwandosya, Eric Mugurusi, Majani(RIP), Profesa Maurice Mbago, Kassim Mpenda, na wahandisi na wataalamu wengi mashuhuri.

Kwa kumalizia, si kweli kwamba Profesa Mwandosya alipata cheti cha ufundi halafu akaenda Chuo Kikuu cha Aston Uingereza, bali alipata alama za juu kidato cha sita katika mchepuo wa Hisabati, Hisabati, na Fizikia (Pure Mathematics, Applied Mathematics, and Physics), msingi uliomwezesha hatimaye kupata shahada ya uhandisi umeme daraja la kwanza( First Class Honours), Chuo Kikuu cha Aston, Uingereza, na hivyo kuruhusiwa kufanya shahada ya uzamifu (PhD), Chuo Kikuu cha Birmingham, Uingereza, moja kwa moja bila kupitia shahada ya uzamili(Masters).

Rafiki yangu yeyote wa fb anayemfahamu Ndugu Malisa GJ,mwandishi na mchangiaji wa makala katika mitandao ya kijamii, tafadhali mpatie taarifa hii. Shukrani.

Mark Mwandosya.

Kabla hatujatoka povu zaidi tufahamishe wewe ulie post hapa Prof. anajibu swali gani.
 
Utaahira hauna gharama zaidi ya kukumbatiwa na vilaza. Kweli hoja ya malisa CCM na JPM hawatakaa wailewe kwa sababu yote wanayoyafanya kwa kujikanganya ni matokeo ya ukilaza pamoja na uprof na Phd za Kichina. Niwaambie tu hao ndio wanafanya mstakabali wa elimu yetu kuwa duni. ENIMIES OF STATE
 
Huyu naye hajielewi kabisa
Mzee Mwandosya ni brain haba sana kuipata hata kama ni Marekani. Taifa lilitumia pesa nyingi ili aje atumike kuleta maendeleo nchini. Nasikitika, taifa limem-missuse. Anazeeka sasa bila ya ku-utilize at least 50% ya uwezo wake mkubwa ambao yeyote atakaye pinga uwezo alionao anastahili kitanda cha kudumu MIREMBE!
 
Mzee Mwandosya ni brain haba sana kuipata hata kama ni Marekani. Taifa lilitumia pesa nyingi ili aje atumike kuleta maendeleo nchini. Nasikitika, taifa limem-missuse. Anazeeka sasa bila ya ku-utilize at least 50% ya uwezo wake mkubwa ambao yeyote atakaye pinga uwezo alionao anastahili kitanda cha kudumu MIREMBE!
Mkuu suala siyo Mwandosya suala ni kujikanganya kwa mkulu kuita watoto wa wanyonge vilaza wakati wa kwake ni kilaza anaefaidi mfumo kilaza. By the way Prof anaeacha uprofesa na kujiunga na siasa hizi za hovyo utamwitaje?

Ndiyo maana tunaongozwa na dr mkemia ambaye hajawahi kushika wadhifa wo wote wa kisiasa hata kwenye ngazi ya tawi.
 
Mbona hajajibu hoja yoyote..... kweli ccm mnahali mbaya sana
Nawe hukutoa hoja bali uliandika riwaya inayomhusu kimakosa sasa kakusahihisha.
Muungwana angesema akhasante nasahihisha taarifa zako. Mwandosya inaijua historia yake vizuri kuliko mtu yeyote. Sasa wewe unataka tukufuate wewe badala ya mwenye historia yake.
 
Wakati niko CoET, Prof Luhanga alinifundisha na kipindi hikohiko alikuwa VC wa UDSM, alikuwa anasema maprof wako wawili tu pale UDSM ni yeye na Prof Mwandosya,
Ikanipa wasaa wa kutafuta machapisho yake, yalikuwa ni machapisho bora yenye citations za hali ya juu kabisa. kwa wale wasiomuelewa mwandosya wafanye review kidogo tu kujua ni mtu wa aina gani
Mkuu, angebaki UDSM anatutengenezea brains zingine. Alipoingia kwenye siasa hapo nchi ikamtumia vibaya. Ni kama Dk. Bilali, ujuzi alionao na uwezo ni mkubwa sana. Tungewatumia hao effectively ungekuta hatuingii gharama za kuwapa tenda wachina hata ya kuchimba shimo la choo
 
Ndio! Kuna jambo huelewi! Na japo huelewi unajifanya kuelewa na kutoa maneno yasiyo ya maana. Hapa anamjibu mtu anayeitwa Malisa aliyeandika na kupotosha kuhusu elimu ya Mwandosya na hao wengine. (wakati anazungumzia kuhusu wanafunzi wa diploma ya Chuo kIkuu Dodoma). Alikuwa anafanya reference kwa kina Mwandosya lakini akajikuta napotosha kuhusu elimu yao. Hapo ndipo Prof. Mwandosya alipoweka sawa.
Weka kitu kamili tujue aliongea nini na akapotosha nini na huu ufafanuzi wa Prof Mwandosya unafuta vipi hoja ya Malisa. Kijana haukuwa unashiriki debate wakati unasoma?
 
Ngoja nisogeze kiti. Maana toka mada imeanza sijaona nzi wa Lumumba wakitia mguu humu sijui nini kimetokea.
 
Tatizo la Malisa ni kupost majina ya watu wasiohusika na huu mjadala badala ya jina moja alilokuwa anazungumzia. Wakati huo yeye pia ni kilaza wa kutosha tu. Matokeo ya Malisa Godlisten ya pale Minaki Form IV 2007: 0044,M,GODLBISTEN MALISA,27,IV,CIV-C HIS-F GEO-D KIS-D ENG-D PHY-D CHE-D BIO-D BAS-D. Link: http://www.matokeo.necta.go.tz/csee/S0133.htm
kumbe ndio hawa hawa wanataka kwenda chuo kikuu kwa njia ya mkato
 
Sijaelewa,,,,,anamjibia Jesca ama ni vipi. Kama ni Jesca basi mzee kaenda chaka.........
Halafu wazee kama hawa naanza kuwatilia mashaka. Maana kuna mambo hajaendi sawa ila wako kimya tu
Sukari, Lugumi, Bunge Live, Udikteta wa Dr.Tulia.......na sasa VILAZA na UDOM
Mi wazee wanaonufaika na mfumo huwa siwaamini sana
Ndo maana hata mtoto wao kaanza kuwalaumu hawa wazee-anasema hawa ndo wametuweka hapa pabaya.
 
Mkuu umesababisha nijiulize hivi tunaweza kuwa na Prof. Kilaza????;
Sasa unajiuliza swali la msingi. Ukilaza si kiwango cha elimu kwangu mimi ukilaza ni kushindwa kutumia ralimali akili kupata matokeo ya kukubalika. Kwa kingereza

Kilaza is not equivalent to Ignorance but it is a manifestation of stupidity(non delivery). In Tanzania we are prone to stupid decisions. Definitely we have adequate literacy(Not ignorant).
 
Back
Top Bottom