Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 15,576
- 23,385
Je, Hili jina la scholarship ni sahihi?
Je, Marais wengine walipewa majina kwenye mkopo ambao fedha ni za walipa kodi?
Je, nani alaumiwe, kama kuna lawama, kwa kila kitu kukiita ch aRais hata kama yeye mwenyewe hajaagiza hivyo?
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatangaza programu ya Ufadhili iitwayo SAMIA SCHOLARSHIP kwa masomo ya shahada ya kwanza kwa wanafunzi waliopata ufaulu wa juu katika mitihani ya Kidato cha Sita mwaka 2023 iliyoendeshwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) katika Tahasusi za Sayansi (PCB, PCM, PGM, CBG, CBA, PMC na CBN).
SAMIA SCHOLARSHIP itagharamia kwa asilimia mia moja (100%) masomo ya Elimu ya Juu kwa wanafunzi hao ambao wamepata udahili katika fani za Teknolojia, Uhandisi, Hisabati na Tiba.
Ili kupata ufadhili yampasa mtoto kuwa:
1. Awe Mtanzania;
2. Awe na ufaulu wa juu kwenye mitihani ya taifa ya kidato cha sita mwaka 2023 iliyoendeshwa na NECTA katika tahasusi za sayansi;
3. Awe amepata udahili katika Chuo cha Elimu ya Juu hapa nchini kinachotambuliwa na Serikali katika programu za Sayansi, Teknolojia, Uhandisi, Hisabati au Tiba ambazo zimetajwa katika kundi la kwanza (Cluster 1) katika Mwongozo wa utoaji mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa mwaka 2023/2024 unaopatikana kupitia www.heslb.go.tz
4. Awe ameomba ufadhili kwa usahihi kwa njia iliyoelekezwa.
3.0 MAENEO YA UFADHILI
Ufadhili utazingatia viwango na miongozo ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ya kugharamia maeneo yafuatayo:
a. Ada ya Mafunzo
b. Posho ya chakula na malazi
c. Posho ya Vitabu na Viandikwa
d. Mahitaji Maalum ya Vitivo
e. Mafunzo kwa Vitendo
f. Utafiti
g. Vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu
h. Bima ya Afya
4.0 MUDA WA UFADHILI
Wanafunzi watakaofadhiliwa, watagharimiwa kati ya miaka mitatu (03) hadi mitano (05) kulingana na programu husika walizodahiliwa.
soma majina ya wanufaika wa huo MKOPO , ambao sijui kama ni wa kurudisha, maana HESLB ndio unakopeshwa na kurudisha.