Prof. Mussa Assad: Asilimia 60 ya viongozi wana uwezo mdogo

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,568
44,785
Dar es Salaam. Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Profesa Mussa Assad amesema kuna haja ya kuanza na safu mpya ya viongozi serikalini, kwa kile alichokidai kuwa waliopo wengi hawana uwezo mzuri kiutendaji.

Profesa Assad amesema hayo leo Aprili 10, 2021 wakati wa uzinduzi wa mfululizo wa midahalo kwa umma itakayokuwa ikiandaliwa na Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM).

Amesema kwa mtazamo wake asilimia 60 au 50 ya viongozi ndani ya Serikali sio wazuri, hivyo wanapaswa kupumzishwa ili mambo yaanze upya.

“Viongozi wengi sio wazuri au hawakidhi kiwango kinachohitajika, tatizo langu ni moja tu inapofika mahali unaona mtu anakosea na huwezi kusema kama mtu anakosea, unakuwa umefika mahali pabaya sana,” alisema Profesa Assad na kuongeza:

“Sio lazima umkosoe wazi wazi, lakini angalau basi andika kwamba mheshimiwa nimeona umefanya jambo hili na hili, lakini nafikiri kimsingi jambo hilo halikuwa sawa; rai yangu turekebishe hapa na hapa, akipata rai kwa mtu mmoja atakasirika, akipata rai hiyo kwa watu 10 kwenye cabinet (baraza) yake lazima asikilize”

Amesema tatizo ni kwamba watu wote wamekuwa waoga; imefika mahali watu wengine wananyamaza tu.

“Ndiyo maana nasema tuanze upya tuanze na hao wachache ambao wanakwenda vizuri, hilo pia ni somo kwamba ambao nao ‘in the future’ (baadaye) watakuwa wa ovyoovyo, dawa yao ni hiyo ya kuwaweka kando na kuanza upya,”amesema.
 
Yupo sahahi kabisa; inawezekanaje wewe mtaalam ukatumia taarifa ya feasibility study ya 1970 ukajenga mradi mkubwa wa JNHP? kama siyo utahira ni nini? kisa kiongozi flani amesema kua mradi uanze feasibility study itakuja nyuma.

Sidhani kama tunapaswa kuendelea na viingozi wa namna hii
 
Prof pekee asiepelekeshwa na tumbo lake, sio kama kina Prof Kalamaganda Kabugi na watapia tumbo wenzake.

Prof Assad anajua kuipa ngumi za uso serikali kisawasawa, alidiriki hata kumpa ngumi za uso Magufuli na utemi wake, sambamba na kile Kibonge cha Bungeni (Ndugai).
 
Dar es Salaam. Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Profesa Mussa Assad amesema kuna haja ya kuanza na safu mpya ya viongozi serikalini, kwa kile alichokidai kuwa waliopo wengi hawana uwezo mzuri kiutendaji.

Profesa Assad amesema hayo leo Aprili 10, 2021 wakati wa uzinduzi wa mfululizo wa midahalo kwa umma itakayokuwa ikiandaliwa na Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM).

Amesema kwa mtazamo wake asilimia 60 au 50 ya viongozi ndani ya Serikali sio wazuri, hivyo wanapaswa kupumzishwa ili mambo yaanze upya.

“Viongozi wengi sio wazuri au hawakidhi kiwango kinachohitajika, tatizo langu ni moja tu inapofika mahali unaona mtu anakosea na huwezi kusema kama mtu anakosea, unakuwa umefika mahali pabaya sana,” alisema Profesa Assad na kuongeza:

“Sio lazima umkosoe wazi wazi, lakini angalau basi andika kwamba mheshimiwa nimeona umefanya jambo hili na hili, lakini nafikiri kimsingi jambo hilo halikuwa sawa; rai yangu turekebishe hapa na hapa, akipata rai kwa mtu mmoja atakasirika, akipata rai hiyo kwa watu 10 kwenye cabinet (baraza) yake lazima asikilize”

Amesema tatizo ni kwamba watu wote wamekuwa waoga; imefika mahali watu wengine wananyamaza tu.

“Ndiyo maana nasema tuanze upya tuanze na hao wachache ambao wanakwenda vizuri, hilo pia ni somo kwamba ambao nao ‘in the future’ (baadaye) watakuwa wa ovyoovyo, dawa yao ni hiyo ya kuwaweka kando na kuanza upya,”amesema.
 
Kunapokuwa na mfumo wa kulindana ni rahisi kuwa na viongozi wengi wenye uwezo mdogo, na silaha kubwa ya viongozi wengi wenye uwezo mdogo, ni kutumia mabavu kuficha udhaifu wao. Sababu kubwa hasa kwangu niionayo ya kuwa na viongozi wenye uwezo mdogo inachangiwa na hii katiba yetu. Katiba ambayo inayompa rais madaraka makubwa ya kuchagua viongozi wa taasisi zote za kimamlaka kwa utashi wake, na viongozi hao wanajikuta wana deni kwa hisani ya rais, na sio kuwajibika kisheria, wala kikatiba, kibaya zaidi rais huyo hawezi kushitakiwa. Hapo kunabeba 50% ya ubovu wa mfumo wetu wa uongozi.
 
muongo sample aliyochukua kubwa mno hawezi ku justify lakini kwa kuwa yeye ni mhasibu namsamehe

Angesema mfano asilimia 60 ya mawaziri hapo sawa

Kusema asilimia 60 ya viongozi wote serikali ni uongo hawezi justfy hizo takwimu sample kubwa mno .A narrow down

Alichosema hakina credibility kitakwimu
 
Back
Top Bottom