Prof. Muhongo ni mtu makini ninayemjua

Prof. Muhongo ni mtu makini ninayemjua

........"Unajua kwa nini Tanzania inaendelea kuwa maskini?" alihoji na kutaarifu: "Kwanza Serikali haitaki kuongeza wataalamu, pili hata mchango wa wataalamu wachache waliopo hautiliwi maanani na tatu baadhi ya wataalamu siyo waaminifu, wanapotosha mambo kwa makusudi na msingi wa yote hayo ni rushwa." .........

....Serikali yetu inatakiwa ifanyie kazi KUBWA kauli hii......na hili ndio jibu kwanini Tanzania ni maskini
 
........ Wawekezaji wengi wa kigeni wanafuata sheria na kila wanalofanya huwa lina ushauri wa kisheria wakati maafisa wa Tra huendesha mambo yao kwa utashi, wanaya koroga halafu ndo wanakimbilia kwa wanasheria kuomba ushauri matokeo yake kesi nyingi Tra huwa wanashindwa tu. Bwana Nyoni kule Mwanza ana lazimisha hata fedha za project work financing nazo zitozwe capital gain. Ukimwambia hizi ni project costing hakubali hata chepe, sasa akasome hii hukumu ajiulize mara mbili mbili.

Hilo ni tatizo kubwa sana tulilonalo.......tunajidnaganya sana na personalities badala ya kufuata misingi ya sheria......na hii inatokana na mijitu kuwepo sehemu fulani kwa upendeleo wakati ni VILAZA kama huyo mtajwa hapo juu......

the bottom line ni kwamba sheria/regulations zetu inabidi ziwe makini ili kulinda maslahi yetu.....na wanaosimamia wanatakiwa wawe na UELEWA ULIO MAHIRI....na sio kujaza nafasi kwa kujuana......
 
Mkuu Ogah hili Serikali hii dhalimu inalijua sana, lakini pia wanajua mtaji wao mkubwa wa kuendelea kuwafisadi Watanzania na kubaki madarakani milele ni ujinga mkubwa wa baadhi ya Watanzania. Hivyo hili la kuongeza Wataalam kwao halina priority yoyote ile.

....Serikali yetu inatakiwa ifanyie kazi KUBWA kauli hii......na hili ndio jibi kwanini Tanzania ni maskini
 
Last edited by a moderator:
Najibu hoja nilizotia red bila kufuata mtiririko so bear with me:

1. Kuhusu South Africa nadhani unamaanisha mpango wa Black Economic Empowerment al maarufu kama BEE. Sijui takwimu zako ulizotumia kufikia conclusion kuwa mpango huu ulifanikiwa umezitoa wapi, lakini kwa ninavyojua mimi mpango huu kimsingi umefeli. BEE imetengeneza utajiri wa ghafla kwa vigogo wa ANC na washirika wao tu na sio watu weusi wote kiujumla. Mpaka sasa impact ya BEE ni ndogo sana kwa jamii ya watu weusi kwa ujumla nchini SA. Laiti wangejua, wangetumia system ya Muhongo badala ya BEE kwenye uchumi wao.
Hebu angalia hapa: waziri wao mwenyewe wa fedha anapinga, na hapo chini kuna kiongozi wa entity kama hii TPSF ya huko SA naye pia anapinga BEE, wewe unaionaje nzuri?

"In 2010 Pravin Gordhan, the minister of finance, said: "BEE policies have not worked and have not made South Africa a fairer or more prosperous country." In the same year, Lawrence Mavundla, the president of the National African Federated Chamber of Commerce and Industry, said BEE and preferential procurement had marginalised small businesses instead of helping them. It had also promoted "tenderpreneurs who were tender thieves because they got their tenders through [political] connections".

source: 'BEE is flawed and should be scrapped' | Business | Business | Mail & Guardian

2. Ninakubali haja ya kupendelea wazawa ipo, tena sana, lakini sio kwa kufanya vitu vya hovyo hovyo kama BEE, au kugawa vitalu kwa vigogo kama Nigeria na Angola cosmetically, ili tu tukitaja matajiri nchini kwetu tutaje na ngozi nyeusi mbili tatu. Economic emancipation ni kwa ajili ya watu wote na sio wachache kwa niaba ya wengi. Vitalu/gesi ni ya watanzania wote, itakuwaje eti baadhi yetu wapewe upendeleo? kama wao ni wafanyabiashara kweli na wana mitaji mikubwa kuliko "ya kutengeneza juisi", si washindane kwenye soko huria na matajiri wenzao toka nje? Kwa upande mmoja wanadai uwezo wanao, lakini hapo hapo hawataki ushindani, wanataka upendeleo sasa which is which?


3. kuhusu mimi kuwa "slow thinker": Kwa mawazo yangu sidhani hilo ni tatizo. A slow thinker mara nyingi huwa anathink deeper, wakati fast thinker mara nyingi huwa anakurupuka tu ili aje na majibu fasta fasta halafu asifiwe kuwa ali-think fast.

4. hayo mengine ya social backgrounds sitayajibu kwa sababu ni relative. For example, kwa maneno yake mwenyewe "Dr" Mengi alikuwa analala kwenye zizi la ng'ombe/mbuzi kwa umasikini, leo hii ni tajiri mkubwa, je huyu social background yake, kwa definition yake itakuwa ni low au high? Akiongea tumchukuliaje? wewe jikite kwenye hoja achana na hizo social background


Thats why I LOVE JF.!! wallah!....yaani hapa nawasoma Myanguneni jMali na masopakyindi Lole Gwakisa.....na wengine......nafarijika sana.....

In short kinachokuwa debated na wandugu wengi ni 'models' .....ni modeli ipi bora kuliko nyingine...........

NB: ...tuwapongeze viongozi wetu pale inapostahili...... ukiangalia tangu Prof ateuliwe.....ni mshike mshike inaibuliwa....which is very good......then tuwekane sawa.....Ingekuwa Ngeleja's au Yona's type wala msingesikia chochote.....
 
Last edited by a moderator:
Hawa wazungu walikuwepo kabla ya Muhongo nyie ndo mwawashtukia leo !! Tehteh binadamu bana!
 
Kama Tanzania tunataka maendeleo ya kweli, basi tunamhitaji Pro Sospeter Muhongo kwa mengi zaidi kuliko haya ya nishati. Kwa mwaka 2015 aafaa kuwa mgombea uraisi wa Tanzania kuliko mtu mwingine yeyote iwe upinzani au chama tawala. Hakuna zaidi ya yeye, wengine wote ni uwongo tu.
 
Thats why I LOVE JF.!! wallah!....yaani hapa nawasoma Myanguneni jMali na masopakyindi Lole Gwakisa.....na wengine......nafarijika sana.....

In short kinachokuwa debated na wandugu wengi ni 'models' .....ni modeli ipi bora kuliko nyingine...........

NB: ...tuwapongeze viongozi wetu pale inapostahili...... ukiangalia tangu Prof ateuliwe.....ni mshike mshike inaibuliwa....which is very good......then tuwekane sawa.....Ingekuwa Ngeleja's au Yona's type wala msingesikia chochote.....
Mkuu Ogah pamoja na pongezi zako, nazikubali but with a pinch of salt.
Muhongo is on record kudharau ujasiriamali wa watanzania , ati ni wa kusindika juice na matunda tu, thats very low thinking indeed.
Na ndio maana mijadala hii inaibuliwa kuvindicate hilo tamko, kunawanaoli validate hilo tamko, hivyo kukubaliana na mawazo finyu.
 
Last edited by a moderator:
THANK YOU Mkuu masopakyindi mchango wako umetulia na umejaa hekima na busara tele. :yo: :yo: :yo:


Tatizo la watu wenye akili ndogo kama ninyi ni kufikiri kila anayepigania haki ya watanzania kushiriki katika uchumi wa nchi kwa kuwafikiria kwanza basi ni mtu wa Mengi.

Nyie slow thinkers wala hamuoni the bigger pictuer of economic emanciipation for Tanzanians kwa vile mnaridhika baada ya kununua vigari used vya dola elfu nne au tano!

Soth Africa kwa kuwa na viongozi wenye uelewa mpana wa tatizo hilo, ilianzisha programme mahsusi ya kuwaendeleza waafrika kushiriki kikamilifu katika uchumi wa nchi yao, na mpango huo una mafanikio makubwa.

Nimeeleza kwa kirefu kidogo lakini sidhani kama wewe na mtoa mada mtaelewa sana kwa sababu ya upeo mdogo, worse still kuingia kwenye matusi inaelezea mtu with a very low social backgroung and even lower social projections.
 
Last edited by a moderator:
If you dont see tha flaw in the argument , basi we ni kati ya wale nasema si slow thinkers tu, but low ceiling achievers.
Wish you good luck!
Yes, luck, because you dont have to work to be lucky!
Probably some day the muzungu will think of releasing you from economic bondage.
Na kwa bahati mbaya hilo ndio somo hata maprofesa linawashinda!

Typical of Prof Muhongo language......lakini in a different way.......

Mkuu Ogah pamoja na pongezi zako, nazikubali but with a pinch of salt.
Muhongo is on record kudharau ujasiriamali wa watanzania , ati ni wa kusindika juice na matunda tu, thats very low thinking indeed.
Na ndio maana mijadala hii inaibuliwa kuvindicate hilo tamko, kunawanaoli validate hilo tamko, hivyo kukubaliana na mawazo finyu.

wote mnaweza kuwa na hoja makini sana....lakini nijinsi gani mnaziwakilisha na kwa lugha gani....tofauti yako na Prof inaweza kuw ani ndogo sana ambayo ni hiyo......

lakini hoja ya msingi ni.....models zipi mnazoziona zinatufaa Watanzania......pamoja na yote hayo binafsi ninalia na sheria/regulation zinazo-govern uwekezaji......hatuna haja ya ku-invent kwneye haya mambo....ziko nchi kibao tunaweza kujifunza kutoka kwao na ku-tailor/fabricate za kwetu kwa mazingira yetu......

Ni kweli ni makosa kumfikiria Mengi kila unapojadili kupendelea wazawa......lakini siwalaumu sana wanaofikir hivyo kwani.....the typical of Mengi et al...wameshatuumiza sana...simply kwa sababu ya UJINGA wetu.....lakini Ujinga wetu usitufanye tu-generalize mambo kirahisi......
 
Typical of Prof Muhongo language......lakini in a different way.......



wote mnaweza kuwa na hoja makini sana....lakini nijinsi gani mnaziwakilisha na kwa lugha gani....tofauti yako na Prof inaweza kuw ani ndogo sana ambayo ni hiyo......

lakini hoja ya msingi ni.....models zipi mnazoziona zinatufaa Watanzania......pamoja na yote hayo binafsi ninalia na sheria/regulation zinazo-govern uwekezaji......hatuna haja ya ku-invent kwneye haya mambo....ziko nchi kibao tunaweza kujifunza kutoka kwao na ku-tailor/fabricate za kwetu kwa mazingira yetu......

Ni kweli ni makosa kumfikiria Mengi kila unapojadili kupendelea wazawa......lakini siwalaumu sana wanaofikir hivyo kwani.....the typical of Mengi et al...wameshatuumiza sana...simply kwa sababu ya UJINGA wetu.....lakini Ujinga wetu usitufanye tu-generalize mambo kirahisi......
Mkuu nia yangu ni kwajolt watanzania vijana ku think big!
Tusikubali kuwekewa ceiling na vikwazo katika malengo tuanayojiwekea kimaisha/kibiashara

Otherwise nakubaliana na wewe, the road to economic freedom for Tanzanians is very long and winding.
 
Pamoja na changamoto zote zinazomkabili waziri huyu katika wizara yake ama kwa hakika ukilinganisha na waliopita utaona kwamba anajitahidi sana katika madini kwa wachimbaji wadogo na umeme vijijini.

Sasa kijijini mtu akiuza kuku wake watatu tu anaweka umeme ipo haja ya kumpongeza waziri huyu,kila asemacho kina hoja na ushahidi,,tusihukumu kwa kuangalia na kusikia upande mmoja.

Nenda prof watanzania makini tupo nyuma yako.
Yani hivi ndo umeonyesha kuwa unamjuwa Mhongo?daah!
 
Hata Dr Slaa anafaa kuwa Rais kwa wachache sio wote, pia hata Mbowe ni kiongozi mzuri kwa wana CDM sio wote, nadhani kwa msingi huo huo hakuna kiongozi ambae anafaa kwa wote au unasemaje Bulldog?

Hata Jk anafaa kuwaongoza msoga ila si nchi nzima
 
Umejitahidi ku argue mkuu, though I do not get your end game kwa hatma ya kujitegemea kiuchumi kwa kila mtanzania.
You seem to rest your case kuikabidhi nchi kwa wazungu-Muhongo style, and hope for the best!

Pengine angekuwepo Mwalimu na kujiandikia tena chapter ya KUJITEGEMEA KIUCHUMI, pengine ndo mngeelewa zaidi.

Narudia tena watu si slo thinkers tu, lakini hamna solutiohn kwa tatizo lililopo, la kuwakabidhi nchi wazungu na kutegemea the best out of it.

kulaumu, every Tom, Dick and Harry can do it, mbayazaidi upeo wa kufikiri unaishia kwa Mengi.
I am in business, real and big time, and I know tha ukikabidhi njia kuu za uchumi kwa wawekezaji unaishia si tu kutopata kodi stahiki, bali vile vile umasikini hauishi.
mfano uliotolewa na gazeti la Mwananchi if anything, should be an eye opener. zTunakabidhi rasilmali zetu kwa wazungu and then literally BEG kulipwa kodi!
Umasikini mbaya sana wa mawazo huo.

Na ndio maana nikasema ukiwa na upeo mdogo kimaisha, basi mzungu ndio suluhisho!
what rot.

Pengine umepekua tu programme ya Bkack empowerment huko SA, na kwa makusudi badala ya kutazama the positive attributes ukaamua kusoma comments za Mail na Guardian, any fool will tell you that displacing a mzungu from his economic base, which has been for a long time so, one should expect a fight back.

Check your facts as to who is the biggest investor in SA, the same person who must be displaced!

Check your facts too about Nigeria and its NEEDS programme, na uone juhudi za waafrika wenzetu wenye vichwa sahihi juu ya mabega yao.

Leo uchumi wa Nigeria unapaa kutokana na kujiwezesha na kuwezeshwa wananchi wake.
No wonder tuna akina Dangote.

Nasisitiza its not the time for slow thinkers and low achievers, jaribuni kujipanua pale Mwalimu alipoishia, Kujitegemea kiuchumi maana yake nini kwa siku na wakati wa sasa.

Mkuu, nitajitahidi kujibu hoja zako zenye red:

1. You seem to rest your case kuikabidhi nchi kwa wazungu-Muhongo style: Nadhani labda kuna haja ya wewe kutueleza ni vipi unaelewa modeli ya Muhongo kuhusu uchumi wa gesi. kwa sababu napata mashaka kuwa wanaompinga Muhongo labda wanaielewa tofauti na sisi wengine.
Muhongo kasema vitalu vyote ni mali ya Taifa. Taifa linamiliki vitalu hivi kupitia TPDC. anayetaka kuchimba gesi awe mzawa au mgeni anaruhusiwa kushirikiana kwa ubia na TPDC kwa vigezo vilivyo sawa kabisa. Hapa kuna mambo mawili ya kuzingatia:
  1. Watanzania WOTE (including: wewe na mimi, muuza bar, baamedi, mpiga debe, mtoto wa mbwa....) wote tunamiliki vitalu vya gesi kupitia TPDC.
  2. Wawekezaji wanaokuja wanachaguliwa kwa vigezo vya nani bora zaidi ya wote, tenda huru na haki, na hivyo mmiliki wa gesi (ambaye ni sisi watanzania) tutapata maslahi bora zaidi

Honestly, katika hali hiyo unasemaje kuwa modeli hii ya watanzania WOTE kumiliki gesi tafsiri yake ni "kuikabidhi nchi kwa wazungu"?

Kwa upande wa pili, modeli unayo-advocate for, inasema kuwa eti baadhi ya vile vitalu vitengwe exclusively kwa ajili ya wafanyabiashara "wazawa". Huoni kuwa modeli yako ndio mbovu kwa sababu moja kwa moja inamaanisha "kuikabidhi nchi kwa wachache"?

2. and I know tha ukikabidhi njia kuu za uchumi kwa wawekezaji unaishia si tu kutopata kodi stahiki, bali vile vile umasikini hauishi: Kutokupata kodi stahiki ni matokeo ya usimamizi mbovu wa serikali, sera mbovu, rushwa, ufisadi n.k hili halina uhusiano wowote na modeli ya uchumi, ingekuwa hivyo nchi maskini duniani zingetanguliwa na marekani na ulaya ambazo njia kuu za uchumi ziko kwa watu binafsi.

3. "Pengine umepekua tu programme ya Bkack empowerment huko SA, na kwa makusudi badala ya kutazama the positive attributes ukaamua kusoma comments za Mail na Guardian...": Mkuu, kama watu tunaojiona kuwa ni great thinkers naomba tusiandikie mate, WEWE lete takwimu zozote zile zinazoonyesha ufanisi wa program hii. Mimi nimeleta comments toka kwa WAZIRI WA FEDHA WA SOUTH AFRICA YENYEWE akiiponda BEE. Nadhani labda wewe unajua zaidi ya wasauzi wenyewe. Tusaidiane kwa hilo.

4. Check your facts: respectfully i say CHECK YOUR FACTS AGAIN. uchumi wa Nigeria unaopaa, unapaa kwa vigezo vya nani? Bahkresa, Mengi, Rostam? Jiulize kwa nini Lowassa wakati ule alisema uchumi unapaa watanzania wa kawaida hawakumuelewa. Ni kwa sababu uchumi ule haukuwa equitably distributed kwa kila mtu. kama mtanzania mmoja ataongeza pato lake kutoka dola moja hadi labda 5, hapo kweli "uchumi umepaa". Lakini kama yeye atabaki pale pale halafu "wazawa" wachache watapata matrilioni kupitia kuuza hisa za vitalu vyao uchumi utapaa kiuhalisia kwenye akaunti zao na familia zao, lakini uchumi utapaa kwenye makaratasi tu kwa sisi wengine (kupitia takwimu kama GDP etc).
cc: Ogah Lole Gwakisa.
 
Last edited by a moderator:
"Biggest Investor in South African Stocks Wants Local Ownership
By Janice Kew and Franz Wild Apr 7, 2014 1:00 AM GMT+0300

Maintaining local ownership of South African companies is the best way to boost economic growth, said Elias Masilela, who heads a fund manager that holds shares worth 11 percent of the market value of stocks traded in Johannesburg.

Masilela’s state-owned Public Investment Corp. drew criticism last year when it opposed CFR Pharmaceuticals SA (CFR)’s 12.8 billion rand ($1.2 billion) offer for Johannesburg-based Adcock Ingram Holdings Ltd. (AIP) CFR, Chile’s largest drugmaker, said Dec. 17 that the PIC’s opposition to its takeover was for nationalist reasons.

“When you talk of growing an economy and empowering your people it is important that as you grow the economy you keep your people in control of the economy,” said Masilela, 49, in an April 1 interview in Johannesburg. “The logic is, you’ve built up this investment and if you can run it, why don’t you run it yourself.”
Source: www.bloomberg.com

Mkuu dont speak for South Africans, they can speak for them selves.

Hebu tuangalie vizuri:

1. Mimi nimemleta waziri wa fedha wa south africa. Ambaye serikali yake ndio iliyoleta hii sera.
"In 2010 Pravin Gordhan, the minister of finance, said: "BEE policies have not worked and have not made South Africa a fairer or more prosperous country." source: 'BEE is flawed and should be scrapped' | Business | Business | Mail & Guardian

2. wewe unamleta "mzawa" anayefaidika na sera hii mbovu. Je unataka aipinge?


3. Nadhani wengi tumeisoma hii habari kwa haraka haraka, nashauri tupitie the whole article tuone hasara za mifumo ya "kizawa" kama BEE.

"In 2012 Gwede Mantashe, the ANC secretary general, criticised preferential procurement too. He said: "This thing of having a bottle of water that you can get for R7 procured by the government for R27 because you want to create a middle-class person who must have a business is not on … It must stop."


Moeletsi Mbeki, the brother of former president Thabo Mbeki, has also repeatedly criticised BEE. In his book, Architects of Poverty: Why African Capitalism Needs Changing, published in 2009, he wrote that BEE "strikes a fatal blow against black entrepreneurship by creating a small class of unproductive but wealthy black crony capitalists made up of ANC politicians". It thus robbed South Africa of the key to economic and industrial development: an entrepreneurial bourgeoisie. "These are the businessmen, industrialists, risk-takers and private investors who alone can create a developed, -modern state."

Habari nzima iko hapa: 'BEE is flawed and should be scrapped' | Business | Business | Mail & Guardian
 
pro kiboko ya bongo lala na sikia mzee wa itv kazuia vyombo vyake kumuandika kwa uzuri,marufuku
 
Hakuna kitu alichofanya huyó ni Muhongo kweli
 
Ubaya wa mhongo uko wapi hapa??
1
TAARIFA KWA UMMA
ZABUNI YA 4 YA KUNADI VITALU VYA
UTAFITI WA GESI ASILIA
Utangulizi.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Shirika la Maendeleo
ya Petroli Tanzania (TPDC), tarehe 25/10/2013 ilizindua rasmi zabuni ya
nne ya vitalu vya utafiti wa mafuta na gesi asilia vilivyoko bahari kuu na
ziwa Tanganyika kaskazini. Uzinduzi wa zabuni hii ulihusisha vitalu 7
vilivyoko bahari kuu (deep offshore blocks) pamoja na kitalu cha ziwa
Tanganyika kaskazini (Lake Tanganyika North). Vitalu vya bahari kuu vipo
katika kina cha maji kati ya mita 2000 na 3000 wakati kitalu cha ziwa
Tanganyika kinafikia kina cha mita 1500. Mchakato wa zabuni utafungwa
rasmi baada ya miezi sita na Zabuni zitakazowasilishwa kabla ya saa nne
asubuhi ya Alhamisi ya tarehe 15 mwezi Mei mwaka 2014. Zabuni
zitafunguliwa kwa uwazi mbele ya washiriki wa mnada watakaopenda
kuwepo ama kuwakilishwa siku ya ufunguzi.
2
Majina ya vitalu vinavyonadiwa ni kama inavyooneka katika jedwali hapa
chini.
Nambari Jina la kitalu Eneo (mita za Mraba)
1 Block 4/2A 3630
2 Block 4/3A 2620.3
3 Block 4/3B 3045.0
4 Block 4/4A 2963.3
5 Block 4/4B 3048.9
6 Block 4/5A 2545.3
7 Block 4/5B 3052.6
8 Lake Tanganyika North 9670.2
Faida za Ugawaji wa Vitalu vya utafiti kwa njia ya Zabuni
Utaratibu huu wa kutoa maeneo kwa kutumia zabuni hutumika sehemu
nyingi duniani zikiwemo nchi nyingi za Bara la Afrika, Asia, Ulaya, Marekani
(kusini na kaskazini). Umuhimu wa kugawa vitalu kwa njia ya zabuni ni
pamoja na:
 kuhakikisha kuwa mchakato mzima unafanyika kwa njia ya uwazi;
 kutoa vitalu kwa utaratibu mzuri ili kuweza kuendeleza rasilimali kwa
gharama nafuu endapo ugunduzi utafanyika;
3
 kupata wawekezaji bora wenye mitaji, utaalamu na uzoefu wa
kufanya utafutaji;
 kutoa nafasi kwa wawekezaji wazalendo kushiriki katika shughuli za
utafutaji wa mafuta na gesi; na
 kutoa fursa kwa makampuni mengi na wataalamu mbalimbali kuona
takwimu (data) zilizopo na hivyo kupata kwa wingi maoni mbali mbali
ya kitaalamu kuhusiana na uwezekano wa kuwepo mafuta na/au
gesi.
Gharama za kushiriki kwenye Zabuni
Gharama za kushiriki kwenye zabuni zinajumuisha ada isiyorejeshwa ya
ushiriki kwenye zabuni, gharama za kununulia kifurushi cha zabuni
yenyewe, gharama za kununulia vifurushi vya data za mitetemo cha lazima
kwa waomba zabuni wa vitalu zilivyopo bahari kuu na ziwa Tanganyika
kaskazini na gharama za kununulia ‘data' za nyongeza za hiari kadri
mshiriki atakavyoona inafaa.
Ada ya ushiriki kwenye zabuni isiyorejeshwa ambayo ni Dola za Marekani
50,000. Gharama halisi ni kama zilivyonyambuliwa hapa chini:
Gharama kwa muombaji wa vitalu vya baharini
i. Gharama za kununulia kifurushi cha lazima cha zabuni za vitalu
vya bahari kuu (Bidding Round Data Package (BRDP) for deep
offshore blocks) ni Dola za Marekani 750,000 kwa kila kifurushi.
4
ii. Gharama za kununulia kifurushi cha lazima cha taarifa za
mitetemo ya ‘Mandatory 2D SPAN' ni Dola za Marekani milioni
3.375 kwa kila kifurushi.
iii. Gharama za kununulia taarifa za hiari za mitetemo ya ‘Optional 2D
SPAN data' ni Dola za Marekani 750 kwa kila kilomita moja ya
urefu.
Gharama kwa muombaji wa kitalu cha kaskazini ya ziwa
Tanganyika
i. Gharama za kununulia kifurushi cha lazima cha zabuni ya kitalu
cha ziwa Tanganyika kaskazini (BRDP for Lake Tanganyika North)
ni Dola za Marekani 350,000 kwa kila kifurushi
ii. Gharama za kununulia taarifa za hiari za mitetemo ya ‘Optional
Phase I and Phase II data' ni Dola za Marekani 220 kwa kila
kilomita moja ya urefu.
Waomba zabuni ni lazima waoneshe ushahidi wa kununua taarifa (data)
kwa kuambatisha risiti ya manunuzi pamoja na mkataba wa kutunza siri
waliosaini katika zabuni watakazo rejesha.
Kabla ya kushiriki katika uombaji zabuni, makampuni yote ni lazima
yaweze kutimiza masharti ya zabuni yaliyowekwa. Makampuni inabidi
yanunue kifurushi cha zabuni husika (Bid Round Data Package – BRDP).
5
Kifurushi cha zabuni (Bid Round Data Package – BRDP)
Katika kifurushi hiki kuna vitabu vya zabuni pamoja na maelekezo ya
taratibu za kushiriki na kuwasilisha zabuni [Bidding Instructions]; maelezo
ya jinsi ya kutathini zabuni [Evaluation Criteria]; vipengele vya tathmini ya
uwezo kifedha [Fiscal Terms]; mfano wa mkataba wa kugawana mapato
wa 2013 [Model Production Sharing Agreement]; Sheria inayosimamia
utafiti na uzalishaji ya mwaka 1980 [Petroleum (Exploration and
Production) Act 1980]; Sheria ya Hifadhi ya Mazingira [Environmental
Management Act 2004]; Sera ya Nishati ya 2003 [Energy Policy of 2003];
na Sera ya Gesi Asilia ya 2013 [Natural Gas Policy].
Sababu za kuuza data
Data za utafutaji mafuta na gesi huuzwa kwa sababu gharama za
kukusanya data ni kubwa sana, hivyo mauzo hufidia gharama za
ukusanyaji data hizo za awali na kufanya miradi ya ukusanyaji data kuwa
endelevu.
Kwa upande wa baharini inabidi kukodi meli maalumu zenye mitambo ya
kukusanyia data. Meli hizi zinabeba mitambo na kompyuta maalumu
zinazotumia teknolojia ya hali ya juu kurekodi tabia za miamba za kuakisi
mawimbi ya sauti chini ya ardhi (reflection seismic methods). Meli hizi
huweza kukaa baharini kwa hadi miezi mitatu au zaidi zikifanya shughuli za
ukusanyaji data na zinahudumiwa kimahitaji kwa kutumia helikopta na meli
6
ndogo za kutoa huduma. Ulinzi pia kujikinga na maharamia huhitajika.
TPDC na wabia wake hugharamia zoezi la ukusanyaji data. Ni wazi kwamba
gharama hizi huwa ni kubwa sana, hivyo inabidi data zinazopatikana
ziuzwe ili mwekezaji na TPDC waweze kurejesha gharama zao.
Kwa upande wa nchi kavu napo pia gharama ni kubwa. Gharama huanza
kwa kutengeneza mikuza, kulipa fidia, kulipa makandarasi wa kipima
mikuza, kusafisha mikuza na kurekodi tabia za miamba za kuakisi mawimbi
data za mitetemo.
Tunahitaji makampuni yatumie data hizi kutathmini sehemu ambazo
zinaweza kuwa na hifadhi za mafuta na gesi asilia. Tathmini hizo zitatumika
kusaidia wataalamu kupima uwezo wa makampuni na kuchagua kampuni
stahili kupewa vitalu.
Utazamaji wa Takwimu/ Taarifa - Data Viewing
Utazamaji wa taarifa za kijiofizikia na kijiolojia (data viewing) unaweza
kufanywa kwenye ofisi za Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania (TPDC).
Mtazamaji anapaswa kuweka miadi ‘appointment' ya kutembelea chumba
chenye hizo taarifa kupitia:
Shirika la Mendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)
Tower A, Benjamin William Mkapa, Pension Towers Building,
Plot 23/90-23/92 Azikiwe/Jamhuri Streets,
Dar Es Salaam,
Tanzania.
7
Mkurugenzi Mkuu, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania
Simu ya mezani : +25522 2200103/4
Barua pepe :tpdc4thround@tpdc-tz.com
Tovuti :Tanzania Petroleum Development Corporation
Mtazamaji atapata nafasi ya kuona taarifa zilizomo kwenye kifurushi cha
zabuni cha vitalu vya bahari kuu (BRDP), kifurushi cha zabuni cha ziwa
Tanganyika, ‘data' za lazima za mitetemo zenye jumla ya kilometa 4500 za
urefu, na taarifa nyinginezo za mitetemo kama zitahitajika na pamoja na
seti ya ‘data' za zamani zilizoboreshwa.
SEHEMU A: USHIRIKI WA WAZAWA
Maelezo kuhusu fursa sawa katika kushiriki kwenye mnada wa vitalu vya
utafiti wa mafuta na gesi ni kwa mujibu wa Sheria ya Ununuzi wa Umma
ya mwaka 2004 (Public Procurement Act, 2002).
Ingawa Zabuni iko wazi kwa makampuni ya ndani na ya nje kushiriki,
Utaratibu umewekwa utakaotoa upendeleo kwa makampuni ya ndani
yaliyosajiliwa kwa sheria za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na
kumilikiwa na wazawa kwa asilimia zisizopungua 50 ikiwa yatatimiza vigezo
vilivyowekwa kuviwezesha kupata huo upendeleo.
Vilevile ushirikiano wa
ubia kwa makampuni yanayomilikiwa na wazawa na yale ya nje utapewa
upendeleo ikiwa utatimiza vigezo vilivyowekwa ambavyo vinataka pamoja
8
na mambo mengine; kuthibitisha kuwa atafanya kazi zenye thamani
isiyopungua asilimia 10 ya gharama ya kazi na kuwa atapata mgawo
usiopungua asilimia 20 ya faida itakayopatikana.

Mambo ya kufanya ili kushiriki kwenye Zabuni
Kampuni inayotaka kununua data na kushiriki kwenye zabuni inaweza
kuwasiliana na:
Mkurugenzi Mtendaji,
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania,
Tower A, Benjamin William Mkapa Pension Towers Building, Plot 23/90-
23/92 Azikiwe/Jamhuri Streets,
S.L.P. 2774,
Tel: +25522 2200103/4
Dar Es Salaam, TANZANIA
Barua pepe: tpdc4thround@tpdc-tz.com
Wazabuni watarajiwa wanaweza kutuma maswali ya ufafanuzi kuhusiana
na zoezi la zabuni.
Muombaji anapaswa kurejesha kwa mkono nakala 2 pamoja na nakala
halisi vikiwa vimefungwa na kuviweka katika sanduku la zabuni lililopo
katika ofisi kuu za Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, (Tower "A")
chumba numbari 401 kilichopo gorofa ya nne, jengo la Benjamin William
Mkapa Pension Towers, Kitalu nambari 23/90-23/92, Azikiwe/Jamhuri
9
Streets, Dar es Salaam, au itumwe kwa huduma ya kutuma vifurushi
vilivyoandikishwa (registered post/mail) kwenda kwa:
Katibu wa Bodi ya Zabuni ya Shirika la Maendeleo ya Petroli
Tanzania S.L.P. 2774, Dar-es-Salaam.
Mshiriki katika zabuni pia anaweza kushiriki katika zabuni kwa kuwasilisha
zabuni yake siku ya ufunguzi kabla ya saa nne asubuhi kwa masaa ya
Tanzania siku ya Alhamisi tarehe 15 mwezi Mei mwaka 2014 kama
ilivyoelekezwa kwenye muongozo wa zabuni uliokwishatolewa na unaweza
kuuona kwenye tovuti maalumu iliyoandaliwa kwa ajili ya zabuni ya
ugawaji wa vitalu: The 4th Tanzania Offshore Licensing Round
Tathimini za Zabuni za vitalu zilizopokelewa
Zabuni za vitalu ni zabuni za kimataifa na za wazi kwa makampuni yenye
nia ya kufanya shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi asilia. Zabuni hizo
hazibagui asili ya makampuni, kampuni yaweza kuwa ya kitaifa au ya
kimataifa. Utoaji wa zabuni huzingatia mambo makuu matatu;
 uwezo wa kampuni kifedha;
 uwezo wa kampuni kitaalamu; na
 mgawo wa rasilimali kwa Taifa endapo gesi na mafuta vitagunduliwa.
10
Zabuni zitakazopokelewa zitafanyiwa tathimini kufuatana na vigezo
vilivyowekwa kulingana na kazi za kitaalamu ambazo muomba zabuni
atakuwa ameahidi kuzitekeleza kwa vipindi vyenye jumla ya miaka 11
(4/4/3) ya utafiti kama vilivyo kwenye sheria inayosimamia shughuli za
utafiti na uzalishaji wa mafuta na gesi Tanzania. Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika ataunda Kamati ya kufanya tathimini kwa mujibu wa sheria
inayosimamia manunuzi ya umma.
Mapendekezo ya Kamati ya tathimini hupitiwa na Bodi ya Manunuzi ya
Shirika ambapo mapendekezo ya Bodi ya Manunuzi huwasilishwa kwa
Mkurugenzi Mtendaji ambaye naye huyawasilisha kwenye Bodi ya
Wakurugenzi wa Shirika ili kuandaa mapendekezo yatakayopelekwa kwa
Waziri kwani ndiye mwenye dhamana ya kutoa leseni za utafiti. Kama
Waziri atakubaliana na mapendekezo aliyoletewa ataiagiza kampuni
iliyoshinda itaarifiwe na kujiandaa kwa mazungumzo na timu ya washauri
wa serikali kuanza kwa nia ya kusaini mkataba wa kugawana mapato.
Mkataba huu pindi unaposainiwa pamoja na majukumu hutoa haki za
kipekee kwa kampuni iliyoshinda zabuni kufanya shughuli za kutafuta
mafuta na gesi asilia kwa kipindi kilichowekwa katika eneo husika.
Kampuni iliyoshinda hupewa kuendesha leseni ya utafutaji na Waziri wa
Nishati na Madini kwa niaba ya TPDC kama mkandarasi. Kampuni hiyo
itapaswa kufanya kiasi cha kazi za kitaalamu za kitafiti zitakazo husisha
shughuli za kijiofizikia, kijiolojia na kijiochemia kama ilivyo kwenye
mkataba.
11
Kazi hizo huhusisha uchukuajia wa data za mitetemo za 2D na 3D,
uchimbaji wa visima vya utafiti, uchimbaji wa visima vya kuthibitisha kiasi
ya hazina ya gesi au mafuta iliyopatikana na pia uchimbaji wa visima vya
uendelezaji wa maeneo hazina ilipogunduliwa.
Makadirio ya gharama za mfano kwa kiwango cha chini kufanikisha
shughuli za utafiti mpaka uendelezaji zinaweza kuwa kama zilivyoainishwa
hapa chini:
12
Dola za
Marekani
Tathimini za kijiofizikia na kijiolojia 10 milioni
Ukusanyaji wa takwimu za 2D na 3D 5 - 25 milioni
Jumla kwa Tathmini zote za kimazingira (EIAs) 12 milioni
Uchimbaji wa visima 3 vya utafiti (@ 170 mill) 510 milioni
Uchimbaji wa visima 6 vya tathmini (@ 150 mill) 900 milioni
Uchimbaji wa visima 10 vya uendelezaji (@ 100 mill) 1000 milioni
Jumla ya gharama isiyohusisha miundombinu Dola za Marekani
milioni 2437 (2.4 Bn)
Makadirio haya hayahusishi gharama za kuweka miundombinu ya
kuwezesha uzalishaji, usafishaji, uchakataji, uuzaji na gharama zinginezo.
Gharama hizi zinaonesha makadirio ya gharama za awali za shughuli za
utafutaji wa mafuta na gesi asilia. Gharama za uendelezaji kuweka
miundombinu hadi kufikisha gesi kwa mtumiaji huweza kufikia hadi Dola za
Marekani bilioni 15 (US$ 15Bn).
Baada ya kusainiwa kwa mkataba, mshindi wa zabuni atatakiwa kutekeleza
mambo aliyoahidi wakati wa vipindi vya utafiti.
13
Akichimba kisima na kugundua mafuta au gesi, atapaswa kufanya utafiti
zaidi ili kujiridhisha kuwa kiasi kilichogunduliwa kinaweza kuzalishwa kwa
faida. Katika utafiti huo, mwenye leseni analazimika kuchimba visima zaidi
pamoja na kufanya thathmini za kijiofizikia na kijiolojia zaidi.
Akijiridhisha, kuwa hazina iliyogunduliwa inaweza kuzalishwa kwa faida,
anapaswa kuomba leseni ya uzalishaji ambao hutakiwa kuambatanisha
maombi yake na mpango kabambe wa kuendeleza hazina iliyopo (mafuta
au gesi). Waziri akiridhika na mpango uliowasilishwa na kampuni, huipa
hiyo kampuni leseni ya uendelezaji inayompa haki mwenye leseni
kuendeleza na kuizalisha hazina aliyoipata kwa kipindi cha miaka 25 na
inaweza kuongezwa kwa kipindi kingine cha miaka 20.
Mauzo ya kinachozalishwa hutumika kurudishia gharama zilizowekezwa
kwenye shughuli zote za mradi na faida hugawanywa kwa namna
iliyokubalika katika mkataba wa kugawana mapato.
Taarifa hii inatolewa ili kuelimisha umma kuhusiana na zabuni za ugawaji
wa vitalu iliyozinduliwa tarehe 25/10/2013 na haipaswi kuchukuliwa kama
maelekezo kwa wanaotaka kushiriki kwenye zabuni (Invitation to Bid).
Maelekezo ya namna ya kushiriki kwenye zabuni yanapatikana kwenye
mtandao ufuatao:
(http://www.tz-licensinground.
com/pdf/Invitation%20for%20Bids%2031%20Oct%202013.pdf).
14
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) linayaalika makampuni ya
wazawa yenye uwezo wa kifedha na kitaalamu kushiriki katika zabuni
iliyotangazwa ya kutafuta wawekezaji wa vitalu vya utafiti sambamba na
makampuni ya nje.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na:
Idara ya Utafutaji, Uzalishaji na Huduma za Kiufundi,
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania
Tower A, 9th Floor; BWM Pension Tower
Azikiwe/Jamhuri Street
P.O. Box 2774
Dar es Salaam, Tanzania
simu: +255 22 2200103/4, 2200112
fax: +255 22 2200113
Barua pepe: tpdc4thround@tpdc-tz.com
 
Back
Top Bottom