Prof. Mkumbo: We should not compare Magufuli with Mwl. Nyerere

Prof. Mkumbo: We should not compare Magufuli with Mwl. Nyerere

Mkuu lazima uangalie Nyerere alitawala kipindi gani na changamoto zake. Ni baada ya ukoloni ambapo kila mtu alitaka lion share. Kama utakubuka 1964 mutiny inaeleza ni kwanini mwalimu alichukua some of drastic measures.

Kumbuka Mwalimu alikuwa na kazi ya kujenga Utaifa na umoja na kisha kutoa uelekeo
Kinyume chake tungekuwa na coup de tat kila siku kama ilivyokuwa Ghana na Nigeria

Mwl alifanya mengi kuweka policy za nchi sawa, na kujenga utamaduni wa kukubaliana bila kupigana.

Mwinyi akawa na changamoto za kuweka Taifa pamoja katika mfumo wa vyama vingi. Alikuwa mvumilivu sana hata kuonekana kana kwamba alishindwa kazi.
Hakuwa na visasi wala hakutumia madaraka yake kulipa hasira kwa wanaompinga

Mkapa hakuzuia demokrasia hata ilipomuudhi. Alikuwa tayari kutoa lugha mbaya wakati akicahia demokrasia ifanye kazi yake. Kuna nyakati aliwajibu waliompinga kwa matendo na si visasi na chuki

JK aliaacha demokrasia ishamiri ingawa alikuwa anauma kwa upande kukuweka sharia

Magufuli amekuta kila kitu kipo sawa, kuanzia misingi ya uchumi, siasa, jamii na kila kitu
Haya tunayoyaona katika demokrasia hayana ulazima wa aina yoyote

Inafika mahali watu wanatafuta sababu zingine zikiwa hazina maana lakini zinabeba uzito

Ukiwalinganisha wawili hao, Mwalimu na Magufuli hakuna ulingano wa jambo lolote isipokuwa moja tu, wote ni wanadamu.
Watu wana mlinganisha sana Dr Magufuli na wengine ili aonekane tu kuwa anabana demokrasia.

Kwasababu amekuta kila mtumishi hasa wenyewe nafasi kubwa ni kama samaki aina ya kambale kila mmoja ana sharubu hujui nani baba,mama au mtoto.

Na matokea yake ubadhirifu umekithiri sana kila kona.

Nyerere na Magufuli wote ni wanadamu kila mmoja ana mazuri yake na madhaifu yake.

Dr John Magufuli Fanya kazi kama ulivyojipanga na ulivyokusudia kuipeleka nchi ndiyo awamu yako hii.
 
Watu wana mlinganisha sana Dr Magufuli na wengine ili aonekane tu kuwa anabana demokrasia.

Kwasababu amekuta kila mtumishi hasa wenyewe nafasi kubwa ni kama samaki aina ya kambale kila mmoja ana sharubu hujui nani baba,mama au mtoto.

Na matokea yake ubadhirifu umekithiri sana kila kona.

Nyerere na Magufuli wote ni wanadamu kila mmoja ana mazuri yake na madhaifu yake.

Dr John Magufuli Fanya kazi kama ulivyojipanga na ulivyokusudia kuipeleka nchi ndiyo awamu yako hii.
Kwanza nchi haipelekwi kwa jinsi anavyotaka bali kwa mujibu wa sheria. Elewa hilo

Pili, unachanganya kati ya kuwajibika na demokrasia.
Kuwajibika ni suala la usimamizi wa kile kinachopaswa kusimamiwa kwa mujibu wa sheria

Demokrasia ni namna gani wewe unapata uhuru wako kikatiba, unautumiaje katika kusikiliza, kusikilizwa, kushiriki na kushirikishwa katika maamuzi yanayokuhusu kwa mujibu wa sharia

Ni namna wananchi wanavyopata fursa ya kujadili, kujadiliana , kukosoa au kukosolewa ndani ya sharia zilizoanishwa

Huwezi kuzuia uhuru wa habari, kukusanyika, kukosoa au kukosolewa, kunyima haki ya kusikiliza na kusikilizwa ukasema unasimamia demokrasia.

Na wala hayo si mapungufu ya kibinadamu ni mapungufu yasiyotarajiwa

Nyerere hana mfano kwasasa, si kwa waliopita bali anayemkaribia mama yake hajamaliza kindergarten. Nyerere is an icon, statesman, visionary leader and a man of principles

Narudia tena uelewe kwa lugha rahisi, jukwaa litakalomweka Nyerere alinganishwe na mwingine, miti ya kulijengea haijaota na wala shamba la kupanda halijapatikana. Period
 
nyerere angetaka butiama kuwa kama New york angeweza kwa 100% na angetaka familia yake kuwa matajiri hamana familia yyte ingewashinda wangekuwa kama familia ya kenyatta
 
Kumkaribisha kiongozi anaekalia nchi nyingine kimabavu. Falsafa za Nyerere ni ukombozi ndio maana alisaidia nchi nyingi za Africa kupata uhuru.
JPM yeye anakumbatia madikteta na wakolon.
Nyerere alimrudishia wafungwa Gadafi!
 
Wana JF wanahoji hela za misaada zielekezwe kwa wahanga iweje pesa ibadilishwe matumizi?tunaomba majibu ya kujitosheleza tuache kujibu kiwepesi wepesi maswali magumu!
 
Ahsante sana Mkuu Nguruvi3 kwa mchango wako mzuri sana uliojaa busara na hekima tele.

Inasikitisha sana kuona hii Serikali ilivyo na watendaji wenye roho mbaya na ukatili wa hali ya juu. Iko tayari kulipa mapesa chungu nzima kununua ndege kwa cash lakini wakati huo huo ikashindwa kutoa kati ya bilioni 15 na 20 ili kuwasaidia raia wake waliokumbwa na maafa. Pamoja na hayo wanaomba misaada ndani na nje ya nchi huku wakitangaza misaada hiyo ni kwa ajili ya kusaidia wahanga. Wanakusanya misaada na kubadili kauli yao kwamba misaada hiyo sasa haitasaidia tena wahanga bali itakuwa ni kwa ajili ya taasisi za Serikali. Kisha bila aibu wala woga wanaiba pesa zilizokusanywa ambazo ni zaidi ya bilioni 15 na kuudanganya umma wa Watanzania kwamba pesa walizokusanya ni 5.4 billioni wakati UK imetoa 6.7 billioni Uganda imetoa 450 millioni.

Serikali ya huyu aliyejigamba kujitoa mhanga kuwapigania wanyonge nchini kumbe yeye ndiye wa kwanza kuwakandamiza na kuchukua pesa zao kwenda kutoa rushwa kwa Wabunge wa CCM ili wapitishe mswaada wake wa kidikteta ili kuminya uhuru wa habari nchini.
Milion 10 waliyopewa wabunge wengi wataimaliza kwenye michepuko kwa sababu ni pesa haramu yenye laana ya wananchi wa kagera.
 
Mkuu Pohamba, naunga mkono hoja, hata vidole havifanani lakini ile vyote kuitwa vidole tayari ni mfanano.

Kitu ambacho nakubaliana na Prof.Kitila, kama kigezo chake cha mfano ni falsafa tuu, then ni kweli Magufuli hafanani na Nyerere, lakini kuna mambo mengi tuu Magufuli ni kama Nyerere.
1.Wote wanatoka Kanda moja na wanaasili moja.
2.Wote ni waalimu.
3.Initial za majina yao ni J.
4.Wote ni Wakristu Wakatoliki
5. Wote wanasali St.Peter.
6. Wote ni wapiga ngoma.
7. Wote ni wakali sio watu wa mchezo mchezo.
8. Wote wanaichukia rushwa.
9.Wote ni watu wa watu.
10. Wote ni ma dikiteta. ...Wazalendo.

Karibu mnitembelee mitaa hii nimefanya a simple comparison and contrast kati ya Magufuli na Nyerere

Magufuli Kama Nyerere: Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi, Ni Kazi Tuu, Ila Pia sio Kama Nyerere!

Paskali
hawafanani kwa mengi sana kumbuka Nyerere alitawala kwa changamoto nyingi sana huku akiandaa nchi, huku ukombozi wa Africa, huku vita za uganda, huku mapinduzi na njama nyingi za kumpindua madarakani hivyo udikteta wa Nyerere ulijitokeza ili kuwadhibiti wale waliokuwa wakimwandama kumpindua, lakini siku hizi wimbi la kupindua serikali halipo Wapinzani wengi wapo kwenye nguvu ya Hoja tu cha ajabu kipindi hiki Wapinzani hawana uhuru wa kufanya mikutano wala kukosoa chochote.
 
hawafanani kwa mengi sana kumbuka Nyerere alitawala kwa changamoto nyingi sana huku akiandaa nchi, huku ukombozi wa Africa, huku vita za uganda, huku mapinduzi na njama nyingi za kumpindua madarakani hivyo udikteta wa Nyerere ulijitokeza ili kuwadhibiti wale waliokuwa wakimwandama kumpindua, lakini siku hizi wimbi la kupindua serikali halipo Wapinzani wengi wapo kwenye nguvu ya Hoja tu cha ajabu kipindi hiki Wapinzani hawana uhuru wa kufanya mikutano wala kukosoa chochote.
Mkuu Ushu, kuna aina nyingi za kumfananisha kutegemea na vigezo vya mfanano unavyovitumia.
Tukitumia kigezo cha gender, chama, dini, thehebu, kanisa, na asili, then Magufuli ni kama Nyerere 100% chini ya 100%.

Hata udikiteta, pia wanafanana ila kwa vile tuko kwenye mchakato wa kumtangaza Nyerere kuwa ni Mwenye Heri ambayo ni hatua moja kabla hajatangazwa Mtakatifu, watu humu wanaujustify udikiteta wa Nyerere kutokana na hali halisi ya kipindi hicho na ndivyo tunavyo ujustify udikiteta wa Magufuli kuwa ni dikiteta mzalendo anayafanya udikiteta kwa nia njema ya kusafisha uozo wote wa nchi hii uliotufikisha hapa, nchi ikiisha Nyooka ndipo tuikumbatie tena demokrasia.

Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

Paskali
 
Wanasiasa wa ACT maendeleo siyo wa kuwaamini kabisa wanachokizungumza.
 
Prof. Kitila Mkumbo "It is totally wrong to compare mwl with Maguful, mwalimu was philosophically well packed".
 
~~~~~~~RambiRambi Za Kagera~~~~~~~~~
Uingereza Bil.6 [emoji777]
Marekani Bil.5[emoji818]
Kenya Mil.200[emoji777]
Korea 1.5Bil[emoji777]
Wadau mbalimbali 5.4Bil[emoji777]
Sirikali.
TOTAL 5.4 Bil
Sijui Umenielewa Apo?
Mama yangu!!
 
Back
Top Bottom