Ni kweli huwezi kumlinganisha Rais Magufuli na Mwl. Nyerere kwa sababu hawa ni binadamu wawili tofauti lakini pia tuache kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa!
Hiyo demokrasia ya Mwl. Nyerere inatoka wapi wakati aliongoza taifa kwa kutumia kauli mbiu ya ''Zidumu Fikra za Mwenyekiti wa chama Taifa''.
Mwl. Nyerere alituambia katiba ya Tanzania inampa madaraka makubwa lakini kwa vile alipenda madaraka makubwa ndiyo maana hakuibadilisha ili kupunguza hayo madaraka.
Mwl. Nyerere aliwafanya baadhi ya Watanzania kukimbia uhamishoni wengine kupewa house arrest.
Inawezekana neno demokrasia lina maana nyingine zaidi ya alichokuwa anakifanya Mwl. Nyerere kwa sababu alishawahi kunukuliwa akisema, “Developing nations need democracy, but the need and necessity of democracy should come from within according to geographical necessity, maturity etc …’’
Kama hoja ni masuala ya kifalsafa, hata Adolf Hitler alikuwa mwanafalsafa mzuri sana.