Prof. Mkumbo: We should not compare Magufuli with Mwl. Nyerere

Prof. Mkumbo: We should not compare Magufuli with Mwl. Nyerere

Na sifa ya Wanafalsafa hawakurupuki wanaamini katika reasoning kabla ya kufanya maamuzi ndo maana mambo yalikuwa mujarabu.
 
Ni kipi kinachomfanya Mkumbo aseme Magufuli hana falsafa?...

Falsfa ni nini?

Ni utaratibu upi aliokiuka Magufuli hadi sasa?

Kungekuwa hakuna demokrasia nchini Mkumbo angepewa nafasi kwenye TBC kubwabwaja?
SASA UNAMUULIZA NANI?JIBU HOJA??
 
Salamu kwenu,
Katika kipindi cha this week in perspective TBC, Prof Kitila Mkumbo ameasa watu waache kumlinganisha Rais Magufuli na Hayati Baba wa Taifa,rais wa kwanza wa Tz.
Mwalimu alikuwa ni mtu wa mawazo ya kifalsafa na vitendo kwa kufuata taratibu.
Mwalimu hakuwa kidhani na demokrasia.
Amemalizia kwa kusisitiza ni watu wawili wanaopishana kwa ulekeo tofauti.
Ingawa rais anapambana na rushwa,lakini asiibane demokrasia maana ndio pekee itamfanya afanikiwe dhima yake.
Huyu bwana amesema iliyo kweli ama ni vile yupo ACT.?
wanaomlinganisha wengi hata hawamjui mwalimu vizuri. Tuu kwa kuona vipande vya hotuba zake.
 
Sasa mbona lugumi, kivuko chakavu, mabehewa ya mwakyembe, bomba la gesi, kiwanda hewa cha cement lindi, billion 600 ukarabati uwanja wa ndege na madili kibao kama hayo ya kula pesa za huko kagera hawajatumbuliwa?

Haya yote ya metokea katika kipindi cha mwaka1 wa hii sirikali ya awamu ya tano?

Na washawasha!
 
Nyerere hakuwahi shuhudia wabunge wa ccm wakihongwa milioni kumi na hata yeye hakuwahi pata mgao dhalimu kama huo.

Kweli wanatofautiana Sana Kati Nyerere na J.P.M

Hivi, hili la Wabunge wetu kuhongwa lina ukweli? Mbona mamlaka na wahusika wamenyamaza kimya kana kwamba hawajapata kusikia madai haya mazito kuliko jambo lingine lolote lilopata kutokea katika nchi hii? Inawezekana kweli Wabunge wetu kuhongwa na serikali yao? Ili wafanye nini? Wahujumu wapiga kura wao? Hivi kwaniniwatawala wanaotuhumiwa na kitendo hiki wamenyamaza kimya? Hii ndiyo 'criminal state' aliyopata kuzungumzia mwandishi mmoja nguli wa nchi hii?
 
Kitila aache unafki wa Ki ACT, Sifa kuu ya kufananisha vitu ni lazima viwe tofauti ili upate baadhi ya yanayowiana. Mwl Nyerere na Magufuli ni watu wawili tofauti lakin Wenye baadhi ya mambo wanashabihiana.

1) Ukali, wote walikuwa wakali na wanaogopwa na wasaidizi wao.
2) Ubabe, wote walikuwa wababe na wakat Mwingine kuingilia mifumo rasmi ya kiutendaji cha Msingi wanayotaka yapite

3) Wote hawashauriki, kwa wale watu wazima wnzangu wanakumbuka kwanini Mwl aliitwa Bwana haambiliki.
4) Kuminya Demokrasia
5) Kupitisha Sheria kandamizi dhidi ya media, Nyerere alipitisha 1976 na Magu anaipitisha 2016
6) ......

Nyerere amekuwa kama hirizi ya kisiasa katika nchi hii; mtu haamini kuwa anachokifanya kinaweza kukubalika na umma bila kujiegemeza kwa Nyerere. Tuliopata nafasi ya kumfahamu Nyerere tunajua wazi kuwa kuanzia chama alichoasisi hadi viongozi wake wa sasa ni kinyume kabisa na kila kitu Mwalimu alichojinasibisha nacho. Tunajua jinsi Nyerere alivyokuwa mnyenyekevu kwa wananchi wake. Tunajua jinsi alivyochukia ubaguzi wa aina yoyote. Alifanya jaribio la kujenga demokrasia ya chama kimoja lakini akawa wa kwanza kugundua kuwa mfumo huo ulikuwa na kasoro nyingi kuliko faida. Nyerere akijua kuwa jukumu lake la kwanza ni kujenga utaifa,wakati mwingine lililazimu baadhi ya mambo yasimamiwe kwa njia tofauti ili kufunikisha lengo hilo adhimu. Utaifa huo uliojengwa na Nyerere ndio huu sasa ambao kwa namna ya kushangaza tunafanya jitihada zote kuubomoa huku tukijidanganya kuwa ndiyo siasa za ushindani. Tumwache Nyerere apumzike badala ya kushirikisha kwenye upuuzi wetu wa kubomoa nchi aliyotuachia.
 
Jamani hivi Kambona alikimbilia Uingereza wakati wa awamu ipi? Kina Tuntemeke Sanga walichaniwa vyeti vyao awamu ipi? Akina Kassangatumbo walijengewa vituo vya polisi vijijini mwao ili kuwazuia hata kwenda sokoni awamu ipi? Akina Abdu Jumbe walinyamazishwa na kuwekwa vizuizini kwa kudai serikali 3 awamu ipi?

Mnapomuangalia Nyeree jadilini na kivuli chake. Stop Deifying Nyeree, God is watching u.

Nyerere alikuwa anajenga utaifa katika kipindi ambacho kilikuwa kigumu. Kazi hiyo alifanya kwa uaminifu na kwa maslahi ya umma wote wa Tanzania na siyo kikundi kidogo kinachosukumwa na lengo moja tu: kuhodhi madaraka ya dola. Na baada ya kutujengea utaifa, Nyerere akabaini kuwa mfumo wa kisiasa uliokuwepo ulikuwa na kasoro nyingi kuliko faida na akabaini siyo endelevu. Ndiyo maana, kinyume na matarajio ya wana-ccm wenzake akawa wa kwanza kutetea mfumo wa vyama vingi.
 
Ni kipi kinachomfanya Mkumbo aseme Magufuli hana falsafa?...

Falsfa ni nini?

Ni utaratibu upi aliokiuka Magufuli hadi sasa?

Kungekuwa hakuna demokrasia nchini Mkumbo angepewa nafasi kwenye TBC kubwabwaja?
NDUGU yangu yafaa uenda ukagoogle ili uelewe falsafa/philosophy ni nini, na kiongozi akiwa nayo anakuaje, uongozi wake unakuwaje na mengine ya msingi. Yafaa usibishane kwa sababu hujui, bishana kwa sababu unajua na una hoja.
 
Mwalimu yupo juu zaidi ya kina Mandela kawaacha mbali sana sasa ukimfananisha huyu na Nyerere ina maana pia yupo sawa na kina Mandela? utani huo..
 
Ni ukichaa kufanya hiyo comparison ..nimetumia utafiti 1 kati ya 4
 
Amesema kweli, wamuache mwalimu Nyerere apumzike na siyo kumfananisha na watu asio endana nao hata kidogo
 
Katika uumbaji Mungu alifanya kitu kinaitwa exceptional uumbaji ulikuwa tendo takatifu sana ambalo kila kilichotengenezwa kilipewa upekee wake sasa mimi wakati mwingine nawashangaa sana mnapofananisha na kulinganisha utendaji kazi wa watu hautakuja kufanana kamwe na hapo exception huanzia! So white is white and black is black!
 
Back
Top Bottom