Prof. Mkenda, Waziri bora na wa mfano

ila anapenda sana kujionyesha kwenye tv.
aache show of, achape kazi, wananchi wanataka kuona matokeo sio maneno mengi na kuonekana kwenye tv.
bado safari ni ndefu, muda wa kujipongeza bado sana.
 
Ni mnyenyekevu
Msomi
Hajikwezi
Mchapakazi.
Anayebisha asikilize kipindi cha dk.45 ITV na radio one leo hii.
Tunataka kiongozi mwenye kuleta matokeo chanya kwa wananchi sio hizi sifa zisizotusaidia sisi wananchi

Bei ya pembejeo imepaa kweli kwelikweli afu unasifia upuuzi
 
Tunataka kiongozi mwenye kuleta matokeo chanya kwa wananchi sio hizi sifa zisizotusaidia sisi wananchi

Bei ya pembejeo imepaa kweli kwelikweli afu unasifia upuuzi
Kitendo cha kupanda bei ya mafuta ya magari na mitambo kinasababisha bidhaa zingine zipande tu.
Ila swala la ushirika wakulima hawataki aje na ufumbuzi sio kurithi mawazo yasiyo tija
 
Kama ni Mchaga hapana aisee kuwa Rais
1. Iwapo tuna hitaji kufanikiwa kiuchumi ni kumteuwa Adolf Mkenda kuwa waziri wa fedha. Hili likifanyika hatutajuta.

2. Vikwazo vyote wanavyowekewa wapinzani vitolewe kwa kuwa "kelele za mlango hazimnyimi mwenye nyumba usingizi"

3. Mambo mengine ambayo hayana tija yatatudidimiza kama taifa. Tufungue ukurasa mpya tusonge mbele.

4. Kelele hizi za ukandamizwaji wa haki za binadamu na upinzani siyo afya kuendelea kusikika kwenye makisio ya ndani na kimataifa. Tuvumiliane tusemane, tukosoane sisi kwa sisi.

5. Tusibambikiane kesi za uongo. Ufa hujenga ukuta, tujihadhari na hatari tunayoijenga wenyewe kwa kiburi chetu wenyewe na kwa choyo na nchu wa madaraka.

6. Tusiharibu sifa yetu ya manukato kama taifa tuwe wazalendo.

7. Kikwete u wapi? Uliyaweza haya bila papara na kelele. Busara zako ni muhimu kipindi hichi, uongozi wako wa kidiplomasia ni nguzo kuu kwa mshikamano wa taifa letu.

8 Kikwete piga kelele na nchi yetu itapona.

9. Kikwete ulishawahi kusema "Wazee ni grisi" naomba haya yanoyotokea kemea kwa upendo na unyenyekevu na upendo na watakusikiliza.

10. Mungu ibariki Tanzania.
 
Kaachivu Jambo gani ambalo limeleta matokeo chanya katika kilimo,maana Nasikia pembejeo za kilimo zimepanda Bei Sana.Naomba mnisaidie maana Tanzania akitokea mwanasiasa akawa anajua Sana kujieleza basi anakua bora,naomba ufafanuzi
Pembejeo zimekuwa za moto huo ubora uko kwenye kuongea au kutatua changamoto? Hopless kabisa hakuna kitu pale mbolea 80000 50kg gunia la mpunga 5000tsh mahindi 25000tsh
 
Ni mnyenyekevu
Msomi
Hajikwezi
Mchapakazi.
Anayebisha asikilize kipindi cha dk.45 ITV na radio one leo hii.
Namkubali sana huyu prof.

Anavyowasilisha hoja zake unaona kabisa ile intellect yake. Yuko vizuri, halafu ana exposure kubwa sana.

Halafu,ni mtu wa decision and action. Mawaziri wote wangekuwa hivi,tungesonga mbele kwa kasi kubwa sana!
 
Bado hatujaona mageuzi kwenye kilimo zaidi ya maneno tu.
wakulima na watanzania wanataka kona mabadiliko sio weledi wa kuzungumza!!
wamepita kila aina ya mawaziri ktk wizara hiyo lkn hakuna mabadiliko.
taasisi za utafiti wa kilimo kama NALIENDELE n.k zipozipo tu hazina tija yoyote kwenye maendeleo ya kilimo.
mambo mengi sana ktk kilimo bado yanaenda kimazoea.
Mkenda anazunguka sana sehemu mbalimbali lkn hakuna tija wala mabadiliko kwenye kilimo
 
Kaachivu Jambo gani ambalo limeleta matokeo chanya katika kilimo,maana Nasikia pembejeo za kilimo zimepanda Bei Sana.Naomba mnisaidie maana Tanzania akitokea mwanasiasa akawa anajua Sana kujieleza basi anakua bora,naomba ufafanuzi
Wewe utakuwa hufuatilii mambo ya kilimo. Ungekuwa unafuatilia usingekuwa na mtizamo huo.

Kuhusu kupanda kwa mbolea,ni tatizo la Dunia. Mbolea imepanda bei sana kwenye soko la Dunia kutokana na athari za janga la korona. Hata hivyo,Prof Mkenda amejitahidi sana kuchukua hatua mbalimbali ambazo zimepunguza mno athari za ongezeko hilo la bei hapa nchini.

Kusema ukweli,prof Mkenda ni waziri bora kabisa.
 
Namkubali sana huyu prof.

Anavyowasilisha hoja zake unaona kabisa ile intellect yake. Yuko vizuri, halafu ana exposure kubwa sana.

Halafu,ni mtu wa decision and action. Mawaziri wote wangekuwa hivi,tungesonga mbele kwa kasi kubwa sana!
Hamzidi jiwe kwa akili bana
jiwe alikuwa anajua idadi ya samaki na mayai yake kwenye kila ziwa. Anajenga gorofa lenye floor nne pale UD kwa 50m. Huyo Propesa atawezaaa
 
Hamzidi jiwe kwa akili bana
jiwe alikuwa anajua idadi ya samaki na mayai yake kwenye kila ziwa. Anajenga gorofa lenye floor nne pale UD kwa 50m. Huyo Propesa atawezaaa
Unajua nyinyi ndio mnasababisha watu wamsemeseme mwendazake bila sababu badala ya kumuacha apumzike.

Katika watu wenye rekodi ya kuwa na akili unamuweka na jiwe? Acha kuchekesha watu. Inawezekana wewe huna akili kwa hiyo wenye akili zinazochemka huwezi kuwajua!
 
Bado hatujaona mageuzi kwenye kilimo zaidi ya maneno tu.
wakulima na watanzania wanataka kona mabadiliko sio weledi wa kuzungumza!!
wamepita kila aina ya mawaziri ktk wizara hiyo lkn hakuna mabadiliko.
taasisi za utafiti wa kilimo kama NALIENDELE n.k zipozipo tu hazina tija yoyote kwenye maendeleo ya kilimo.
mambo mengi sana ktk kilimo bado yanaenda kimazoea.
Mkenda anazunguka sana sehemu mbalimbali lkn hakuna tija wala mabadiliko kwenye kilimo

..Mkenda kasema anakwenda kuongeza bajeti ya utafiti ktk vituo vyote vya kilimo hapa nchini.

..mkakati wake ni kuongeza uzalishaji wa mbegu bora hapa nchini.

..pia ameweka lengo la kuboresha huduma za maafisa ugani ili waweze kutoa elimu bora kwa wakulima.

..kipaumbele chake ni kuongeza uzalishaji per hectare kwa wakulima wetu.

..Napendekeza Mkenda na Bashe wapewe miaka 3 ya kutekeleza VISION yao ya kuinua uchumi. Wakishindwa waondolewe.
 
Tatizo sio kuongeza bajeti ya fedha, miaka mingi fedha zinatolewa lkn hakuna cha maana zaidi ya kula fedha za umma.
tunataka wataalamu wetu.wawe wazalendo wa kweli kwa nchi yao, wajitume vilivyo hata kama pesa ni kidogo, kuna maeneo wala hayahitaji pesa bali yanatakiwa kujituma tu.
tuache porojo tuchape kazi kwa manufaa ya Taifa letu.
NALIENDELE, n.k
Chuo kikuu cha kilimo cha SOKOINE kimekuwa kikizalisha lundo la wataalamu wa kilimo lkn hakuna tija kwenye kilimo hadi leo.
 
Back
Top Bottom