Prof. Mbarawa arudi kuwa Waziri wa Ujenzi, tutegemee nini katika sekta hii?

Professor Mbarawa alishawahi kuwa waziri wa Ujenzi na kwa mujibu wa Magufuli alisema hadharani kuwa ile wizara ilimshinda na hivyo kumuhamishia wizara ya maji. Ghafla leo analetwa tena wizara hiyo hiyo ya Ujenzi, kuna kitu gani kipya atafanya?
Wizara ya maji kule ilikuwa kuwakomoa komoa makandarasi aliowaacha ujenzi.
 
Naona aligusa penye maslahi yako panapoumiza kweli, maanake nakumbuka wakati huo ulimwanzishia mada kama hii ya leo.

Huko kwenye kandarasi zenu naona kuna uozo mkubwa sana msiopenda uguswe. Sijui Magufuli mlimpendea nini, au ilikuwa ni kumwogopa, maanake sijawahi kusikia mkimlalamikia yeye. Pengine ni kwamba mlijua jinsi ya kula na kipofu?
Wakandarasi wanajifikiria wao tuu kuna sehemu moja Prof Mbarawa alikuta TEMPERARY OFISI imejengwa kwa mabati kama kiosk million mia moja alikuwa huyu jamaa ndio maana anamchukia Ila Waziri Mbarawa na mchapakazi Sana hapendi rishwa
 
Ama kweli dunia tambara bovu.

Prof Makame Mbarawa siyo siri, ni adui mkubwa wa Makandarasi katika sekta zote za Ujenzi na hata hapo mwisho Maji.

Mbarawa ni kama mtu wa kisirani na mara nyingi hana focused objectives.

Tutegemee nini sasa sekta hii ya ujenzi maana huku mwishoni aliwaita makandarasi kuwa wezi na akataka miradi yote ya Maji ifanywe kwa Force Account.

Karibu Mbarawa.

View attachment 1935511
Kwani hili ya kuinflate estimates za ukandarasi c lilikuwa linaonekana na mifano ii wazi.huyu mzee tatizo ni mtu wa maadili na mkweli sana,sasa kuna sekta hazitaki mtu wa namna hiyo maana ndio vichochoro vya upigaji.sasa ndio kama ulivyosema "usiyemtaka karudi tena" na uzuri serikali hii mawaziri wanafull powers over taasisi zao,vile viburi vya watendaji wakuu kufahamiana na mamlaka na kuleta dharau kwa mawaziri kwishney.
 
Ama kweli dunia tambara bovu.

Prof Makame Mbarawa siyo siri, ni adui mkubwa wa Makandarasi katika sekta zote za Ujenzi na hata hapo mwisho Maji.

Mbarawa ni kama mtu wa kisirani na mara nyingi hana focused objectives.

Tutegemee nini sasa sekta hii ya ujenzi maana huku mwishoni aliwaita makandarasi kuwa wezi na akataka miradi yote ya Maji ifanywe kwa Force Account.

Karibu Mbarawa.

View attachment 1935511
Tutaelewana saana mwaka huu...bora yeshee ahaaa
 
Barua hiyo ni kichaka tu cha dhamira iliyojificha.
Hakuna mtu anaandika barua kuwa atawakomoa na mtakoma ubishi.
Lakini barua hiyo inaelekea huko.
Mkuu 'Masopa', ninakuaminia sana na kukuheshimu, lakini sijaona jibu la kuridhisha kuhusu kanusho la yaliyoandikwa ndani ya barua hiyo.

Sioni kwa nini Prof Mbarawa atake, kwa maksudi tu kuwakomoa makandarasi wazawa, huku wakifanya kazi nzuri ya kulijenga taifa letu.

Ikidhihirika kuwa hivyo ndivyo, hata mimi nitaanza kumdharau huyu Prof., ambaye nilishasema humu kuwa ni kati ya mawaziri niliokuwa nawapa heshima kwa utendaji wao wa kazi na kujali maslahi ya nchi yetu.

Kama lipo linalojulikana kinyume na haya, liweke hapa wote tulisome na kulitolea maoni. Hili la "kukomoa" bila sababu ya msingi halieleweki kabisa.
 
Professor Mbarawa alishawahi kuwa waziri wa Ujenzi na kwa mujibu wa Magufuli alisema hadharani kuwa ile wizara ilimshinda na hivyo kumuhamishia wizara ya maji. Ghafla leo analetwa tena wizara hiyo hiyo ya Ujenzi, kuna kitu gani kipya atafanya?
Alisema hadharani kuwa "wizara imemshinda"?

Kama hii ni kweli, atakubali vipi kurudishwa kwenye wizara ambayo haiwezi?

Au mazingira ya wakati huo, yakihusiana na mteuzi wake ndiyo yalifanya kazi yake iwe ngumu huko wizarani; na kwa kuwa sasa yupo mteuzi mwingine ambaye hana watu wa kuwakingia kifua huko wasiguswe na waziri ndio yanayobadilisha hali ya mazingira?

Lazima kutakuwepo na sababu muhimu ndani ya wizara hii inayofanya mawaziri wawe na wakati mgumu kuiendesha.

Na huyo aliyeondolewa sasa Chamulilo, na yeye kuna sababu zipi?
 
Jamaa hana upendo na makandarasi wazalendo, na kandarasi za ujenzi ndiyo maisha yetu.
Kwa upande wa ujenzi wa barabara sidhani kama force account itafanikiwa kwa sababu nyenzo nyingi za ujenzi zipo kwa wakandarasi.
 
Wakandarasi wanajifikiria wao tuu kuna sehemu moja Prof Mbarawa alikuta TEMPERARY OFISI imejengwa kwa mabati kama kiosk million mia moja alikuwa huyu jamaa ndio maana anamchukia Ila Waziri Mbarawa na mchapakazi Sana hapendi rishwa
Tatizo la watu kupenda sifa.
Haulizi temporary shed kama imeshajengwa bali atatafuta kukomoa tu.
Pale aliambiwa kitajengwa hapa, yeye akachukulia banda la mabati ili kumwadhiri mtu na ajipatie sifa.
Mkandarasi akifika site kwa mara ya kwanza anakuta nyasi tu na vichaka, sasa simnti ya kwanza unaweka wapi kma siyo banda la bati ambalo baadaye unajenga a better shed.
Hayo tumeyapitia makandarasi lakini kwa vile mtu ana moyo huo wa kukomoa komoa kila aachoona, hayo ndiyo matokeo yake
 
Prof. Mbarawa tunakuomba acha upole, kuwa mkali.
tunakufahamu wewe ni mfuatiliaji mzuri sana ila tatizo una kaupole, wapigaji na wabadhirifu huwa wanapenda sana kusimamiwa na mtu mpole ili wapate namna ya kupiga vizuri.
hivyo tunakuomba ongeza ukali ili miradi isonge kwa kasi.
 
Kwa upande wa ujenzi wa barabara sidhani kama force account itafanikiwa kwa sababu nyenzo nyingi za ujenzi zipo kwa wakandarasi.
Wewe kaa chonjo waswahili husema hasidi haachi asili!
Tutaona vituko vyake huyu jamaa na chuki yake!
 
Prof. Mbarawa tunakuomba acha upole, kuwa mkali.
tunakufahamu wewe ni mfuatiliaji mzuri sana ila tatizo una kaupole, wapigaji na wabadhirifu huwa wanapenda sana kusimamiwa na mtu mpole ili wapate namna ya kupiga vizuri.
hivyo tunakuomba ongeza ukali ili miradi isonge kwa kasi.
 
Kivipi kuhusu Chamuriho,au alikuwa apokei rushwa
alikuwa hawajibiki kabisaa, yani yupo kama hayupo......wizara ili dorora, alikuwa anazuga tu, bora kawekwa benchi.

Sasa Prof Mbarawa ni Mfuatiliaji mzuri, ila tunamuomba awe mkali, tunafahamu kuwa hapo wizarani kuna vidudu watu, tunawafahamu kwa majina yao.
 
Back
Top Bottom