Prof. Mark Mwandosya Amlipua Apson Mwang'onda Bungeni

Prof. Mark Mwandosya Amlipua Apson Mwang'onda Bungeni

Mjenga Nchi ni mwananchi na walalamishi siku zote si wajenga Nchi, kwani wanatumia mda mwingi kupika majungu na Ulalamishi kisha kusahau kujenga Nchi, Mwandosya ni Mlalamishi ni mkabila hana jipya bado yupo Analogia hata ukipima uongeaji wake ni wa ki-analogia full , hii ndio Tanzania kila Mtu anadhani anaweza Kuwa Rais ! Ebu jiulize kwa mbinu hizi za Mwandosya ikitokea akawa Rais itakuaje? Visasi na kukomoana vitaingizwa kwenye katiba,Mwandosya,membe,Sita Dr kigwangwala na wenzenu Urais si pahala pa majaribio ingawa Tanzania kila kitu kinawezekana lakini kwa Hawa Kuwa Ma-Rais haiwezekani kwani ni rahisi kwa Nyangumi kupenya kwenye Tundu la sindano kuliko hao Kuwa Rais.
 
Wadau, akitoa mchango wake wakati wa mjadala wa sura za Rasimu ya Katiba, Waziri Prof Mark Mwandosya amewataka wakuu wa vyombo vya dola kujiepusha na siasa pindi wanapostahafu kwenye utumishi. Anasema kuwa wakuu hao wa vyombo vya dola hususan Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Mkuu wa Majeshi na Mkuu wa Polisi wakiwa wakiwa kwenye nyadhifa zao wanamiliki mafaili, Dossier za wanasiasa wote. Hali hiyo inawaweka kwenye position ya kuwajua in and out wanasiasa wote hususan wale wanaotarajia kugombea nafasi za juu hasa ya Urais.

Mwandosya anasema kuwa kitendo cha Wakuu hao baada ya kustahafu kujihusisha na siasa kwa kuamua kugombea nafasi za kisiasa au kuwaunga mkono baadhi ya wanasiasa wanaogombea nafasi za kisiasa kunawaweka kwenye nafasi ya kukiuka maadili ya kazi zao. Anasema kuwa ijapokuwa wanapostahafu wanaacha mafaili ofisini, wanaondoka na kumbukumbu moyoni.

Pia anasema kuwa wakuu hao bado wanakuwa na mahusiano na watumishi waliopo hivyo inakuwa ni jambo jepesi kwao kujijenga au kumjenga mtu wanayemuunga mkono kupitia watumishi wa vyombo hivyo wenye mahusiano mema nao. Pia anasema kuwa wakuu hao wanaweza kumbomoa adui wao kirahisi kwa kwa sababu hizo hizo.

Ijapokuwa Prof Mwandosya hakutaja moja kwa moja majina ya anaowalenga, lakini kwa mtiririko wa matukio ya hivi karibuni, anamlenga Apson Mwang'onda. Kwa nini nimefikia hitimisho hilo? Kwa siku kadhaa nimekuwa nikiripoti taarifa zinazomhusu Apson Mwang'onda akijihusisha na Mtandao wa Lowasa.

Kwamba, Apson Mwang'onda ni Mwenyekiti wa Kamati ya Wezesha Lowasa aende Ikulu na kwamba amekuwa akifanya vikao na wanasiasa kadhaa wanaomuunga mkono Lowasa. Vikao hivyo vimekuwa vikifanyika nyumbani kwa Apson na Mtoto wake Jimmy ambavyo pia vimekuwa vikihusisha matumizi ya kiasi kikubwa cha fedha. Apson Mwang'onda amesikika akisema kuwa yeye kwa sasa ni mstahafu hivyo si tatizo kwake kujihusisha na siasa.

Kilio cha Mwandosya hakikuanza leo. Katika Kitabu alichoandika kijulikanacho Sauti ya Umma ni Sauti ya Demokrasia, Prof Mwandosya ameeleza jinsi alivyohujumiwa na baadhi ya watendaji wa serikali na chama na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa, Apson Mwang’onda. Katika kitabu hicho, Profesa Mwandosya ametaja mlolongo wa viongozi na watendaji wa serikali katika kitabu hicho, miongoni mwa majina hayo limo la Apson.

Katika kitabu hicho Profesa Mwandosya anasema kuwa alipekewa ujumbe na mzee Jimmy David Ngonya kwamba amekuwa anamlaumu Apson kwamba hakumuunga mkono katika harakati za kuwania urais mwaka 2005, jambo ambalo alisema ni hoja iliyofinyangwa kimkakati ili kujenga uhalali wa kumwandama na kumhujumu katika harakati za kuwania nafasi ya NEC kwa mkoa wa Mbeya mwaka 2007.

Katika kinyang’anyiro cha nafasi ya NEC mkoa wa Mbeya Profesa Mwandosya alipambana na Thom Apson Mwang’onda ambaye 2005 alikuwa kambi yake katika kuwania tiketi ya urais kupitia CCM. Katika kitabu hicho Profesa Mwandosya, anaelezea jinsi alivyofanyiwa fitna, hujuma na kila aina ya mizengwe wakati wa mchakato wa uchaguzi kwa mwaka 2007 mkoani Mbeya.

Katika ukurasa wa 21, ameelezea baada ya Chimwaga, siku moja aliyekuwa naye karibu sana Mwalimu Jimmy David Ngonya alimtembelea nyumbani kwake Kibisi Tukuyu mwaka 2006, na kumpa ujumbe wa Apson ambao alimpa baada ya kufanya naye mazungumzo katika hoteli ya Land Mark iliyopo mjini Tukuyu.

Katika kitabu hicho pia ukurasa wa 141 wa Profesa Mwandosya anaeleza taarifa alizopata za matumizi makubwa ya fedha katika uchaguzi wa nafasi ya NEC mkoa wa Mbeya. “Makadirio ya fedha walizotumia yalikuwa kati ya Sh. milioni 300 hadi bilioni moja,” anaeleza Profesa Mwandosya kwenye kitabu hicho wakati akielezea mchuano ulivyokuwa katika kinyang’amyiro cha ujumbe wa NEC mkoa wa Mbeya. Anasema kuwa katika mazingira ya matumizi makubwa ya fedha ulikuwa ni ushindani kati ya ‘Goliati’ mwenye fedha na ‘Daudi’ asiye na fedha.

SO, WHAT??
Kama ana faili zao za uchafu awaache waingie IKULU? Kwa sababu alizotoa Prof. Mwandosya (ninayemuheshimu sana) itakuwa vyema kuwaruhusu watu kama Apson kuingilia kwa kuweka sawa mambo isipokuwa wasiruhusiwe kugombea.
Kinachoonekana ni kutaka kuingia IKULU na uchafu!

Anjo
 
Pesa, hasa inayopatikana kwa njia ya uhalifu, kwa watu wenye madaraka makubwa inawajengea kiburi fulani hivi.
Ningekuwa Apson ningekaa kimya kuliko kuja kuumbuka, maana watu tunajiuliza akiwa Mkurugenzi TISS alifanya biashara gani hadi kutajirika hivyo?
Kuna matajiri wakubwa kama Bakhressa ambao wako kimyaa!!
Na wana siasa wana biashara gani ya kuwa na pesa nyingi????
 
SO, WHAT??
Kama ana faili zao za uchafu awaache waingie IKULU? Kwa sababu alizotoa Prof. Mwandosya (ninayemuheshimu sana) itakuwa vyema kuwaruhusu watu kama Apson kuingilia kwa kuweka sawa mambo isipokuwa wasiruhusiwe kugombea.
Kinachoonekana ni kutaka kuingia IKULU na uchafu!

Anjo
Umenena vyema,nchi zote intelijensia huusika kwa kiasi kikubwa sana katika michakato ya uchaguzi na uongozi
 
Nami nina tuswali twa uchokozi; hivi hawa wakuu anaowasema Prof. Mwandosya walikuwa wanaripoti kwa nani? Na je hao waliokuwa wanapewa ripoti na sasa wamestaafu vipi? Na wao wakae kimya? Je mtu kama unaamini ni msafi na huna kashfa, woga wa nini? Je Waziri Mkuu mstaafu? Je Jaji Mkuu mstaafu? Je mkuu wa TAKUKURU mstaafu? Vipi gavana wa Benki Kuu? Je Mwanasheria Mkuu wa serikali mstaafu? Je Mkuu wa Jeshi mstaafu? Kwa nini iwe Mkuu wa Usalama au Mkuu wa Polisi ndio watajwe? Nafikiri Prof. Mwandosya kachanganyikiwa...namshauri astaafu akapumzike na kama anaogopa joto, dawa ni kukaa mbali na jiko.
 
Amran Kombe (aliyekuwa mkurugenzi wa Usalama wa Taifa) naye alijihusisha na siasa hasa alikuwa na Mrema na kumpa siri mbalimbali inasadikiwa hata bomu la million 900 enzi hizo Mrema alipata datails kutoka kwake na alikuwa ameshastaafu.
Lakini kwa bahati mbaya mapolisi waliomfuatilia kutoka Dar walimuua maeneo ya Maili sita moshi wakidhani alikuwa ni jambazi, ijapokuwa Kombe alijisalimisha kwa kuinua mikono yake juu lakini aliuwawa. Na hao maaskari waliomuaa waliachiwa kwa msamaha wa raisi....wengine wanasema waliachiwa kipindi cha Mkapa wengine kipindi cha Kikwete. Maoni yangu hapa ni kwamba anaweza tu kujihusisha na siasa kama Kombe alivyojihusisha na siasa baada ya kustaafu kwani hamna shida kabisa
.
Hayo yalitokea kipindi hicho wigo na Uhuru wa kuchagua na uhuru wa kuonyesha Fikra ulikuwa Mdogo sana, sasa Tz umebadilika kidogo Uhuru wa kuonyesha nia upo, hata uhuru wa kuonyesha unayemsapoti Pia upo na wala si Dhambi ! Tatizo ni Mchecheto kwa wale wasiojiamini ambao hutumia mda mwingi kuwaza namna ya kumzuia Lowasa asiingie ikulu ,wanapika majungu na fitna pasipo kutafakari matokeo yake watajikuta mda mwingi umepotelea humo kwenye uzushi kisha wanakumbuka shuka kumekucha huku Lowasa akichanja mbuga kuelekea paleeeee...magagoni kwa upolee.... Chezea lowasa wewe...
 
aliyemuua Kombe ni huyu Apson. Alihofia haya anayofanya yeye. Kwa hiyo kama Kombe aliuawa kutokana na kumsupport Mrema, huyu Apson mbona anafanya yaleyale ya Kombe?
Una uhakika ndo aliyemuua?kwa hiyo naye auwawe???
 
Apson anatakiwa kutiwa stiki kwa mambo ya kihuni anayofanya kwenye siasa za tanzania ni mzee wa ajabu sana.
 
Amran Kombe (aliyekuwa mkurugenzi wa Usalama wa Taifa) naye alijihusisha na siasa hasa alikuwa na Mrema na kumpa siri mbalimbali inasadikiwa hata bomu la million 900 enzi hizo Mrema alipata datails kutoka kwake na alikuwa ameshastaafu.
Lakini kwa bahati mbaya mapolisi waliomfuatilia kutoka Dar walimuua maeneo ya Maili sita moshi wakidhani alikuwa ni jambazi, ijapokuwa Kombe alijisalimisha kwa kuinua mikono yake juu lakini aliuwawa. Na hao maaskari waliomuaa waliachiwa kwa msamaha wa raisi....wengine wanasema waliachiwa kipindi cha Mkapa wengine kipindi cha Kikwete. Maoni yangu hapa ni kwamba anaweza tu kujihusisha na siasa kama Kombe alivyojihusisha na siasa baada ya kustaafu kwani hamna shida kabisa
.
Mkuu naona huna akili kama mkuu wa usalama anayo mafaili yote ya wanasiasa na viongozi wa nchi hii leo unasema eti hakuna shida akijihusisha na siasa akistafu napata shida na akili yako kama ungemsikiliza vema mwandosya usingesema haya unayosema kama juha,Apson amekosea sana anatakiwa naye auawe kama kombe tu.
 
Nami nina tuswali twa uchokozi; hivi hawa wakuu anaowasema Prof. Mwandosya walikuwa wanaripoti kwa nani? Na je hao waliokuwa wanapewa ripoti na sasa wamestaafu vipi? Na wao wakae kimya? Je mtu kama unaamini ni msafi na huna kashfa, woga wa nini? Je Waziri Mkuu mstaafu? Je Jaji Mkuu mstaafu? Je mkuu wa TAKUKURU mstaafu? Vipi gavana wa Benki Kuu? Je Mwanasheria Mkuu wa serikali mstaafu? Je Mkuu wa Jeshi mstaafu? Kwa nini iwe Mkuu wa Usalama au Mkuu wa Polisi ndio watajwe? Nafikiri Prof. Mwandosya kachanganyikiwa...namshauri astaafu akapumzike na kama anaogopa joto, dawa ni kukaa mbali na jiko.

Mwandosya kakosa Ujanja wa kujitangaza kaamua kuja na Gia ya Rivas na Majungu akiamini Vitamsaidia kupanda chati, Sijui washauri wake ni akina nani? Lakini Nadhani yupo upande wa akina Mzee Mengi na Timu yake, mwandosya tafadhali Urais usiuwazie kabsa ! Huna nafasi Watanzania wa Leo hawataki mtu wa Slow,slow, wanataka mtu mchapa kazi ,asiyependa uzushi uzushi mwenye kujali maisha bora kwa watanzania.
 
Hamna jipya nyie!!. Mnaanza kuweweseka mapema, wasi wasi wangu inawezekana jamaa Apson ndo alikuwa anapanga deal za kung'oa watu kucha na kuwateka sasa wameanza kumhofia akitumia techniques hizo dhidi ya watu wao.

Kelele zenu wengine wala hazituhusu, endeleeni kujunguana tu!
 
Mkuu naona huna akili kama mkuu wa usalama anayo mafaili yote ya wanasiasa na viongozi wa nchi hii leo unasema eti hakuna shida akijihusisha na siasa akistafu napata shida na akili yako kama ungemsikiliza vema mwandosya usingesema haya unayosema kama juha,Apson amekosea sana anatakiwa naye auawe kama kombe tu.
Utaanza kufa wewe kabla ya wengine, iweje uwe na roho mbaya hivyo? Yaani mtu akimuunga Mkono mwenzake auliwe ? Acha hizo usifuge Kichwa kwa ajili ya kuotesha Nywele,Ndevu,na mzuzu ,fuga kichwa kwa kutambua Kuwa kila mwanadamu ana Haki ya kuishi hadi afariki kwa mapenzi ya Mungu si kwa mapenzi yako.
 
Mkuu wa mtaa wa wekundu, hapa unachanganya, linganisha ujio wa Kitine kwenye system na ujuo wa Amran Kombe. Apson Ni Sawa na Kombe, ila Kitine alikuja kivyake na hao DCs,RCs na wengine Ni wateuliwa tu. Tusichanganye
Inaonekana unaijua vizuri story ya kombe,tujuze basi nani aliyemuua!
 
Hapa yataongelewa mengi sana lakini Ukichunguza kwa Undani sana utagundua kiini cha Haya yoote ni Urais 2015 , lakini wenye wasiwasi ni wale wapinzani wa Lowasa ,wanahaha kwa gharama kubwa kumchafua huku wakijaribu kuwavunja moyo wasaidizi wake,marafiki zake na wafuasi wake,lakini wanasahau Kuwa wateuzi wa jina la mgombea Urais ni kamati kuu ya ccm na wao wana Akili zao na mapenzi Yao , hizi haraka za mwandosya sijui anaogopa nini mpaka kaanza kuchachawa ! Mambo bado mabichi huu mziki bado saana ! Mechi hii ya Lowasa,January , mwigulu VS Sita,membe,Kigwangala na mwandosya ilishachezwa nje ya Uwanja matokeo yanajulikana ndio Maana waliofungwa wanachachawa saaana.
 
Ulalamishi mwingi ni dalili ya kushindwa , hata kule Zenji maendeleo yamechelewa kwa Sababu watu wanatumia Mda mwingi kupiga Porojo,majungu,fitna na Uzushi na kusahau Maendekeo,Mwandosya kakosa Sera ya kuwashika watanzania kaamua kupandia kupitia Mgongo wa Mzee Apson ,mbinu ambayo imefeli kwani haitamsaidia kupaa juu na nyota yake kung'aaa ,Mwandosya kajipange upya kwani Umebugi men.
 
Turudini kujadili mada husika sasa Mwandosya now days ameonesha unafiki wa waziwazi kabisa utadhani siyo Profesa.

Ukishakuwa CCM huwezi kuutumia uprofesa wako ,ni sawa na samaki msafi ukimtumbukiza kwenye ndoo ya samaki walioharibika hawezi kuwabadilisha samaki hao kuwa wazuri Bali naye ataishia kuharibika tu.
 
Mtoa uzi umekosa cha kuandika?
Kuna mambo meni ya kuangalia na kufanya kama vijana wa Tanzania.

Tuache kulisha watu maneno!
 
Ukishakuwa CCM huwezi kuutumia uprofesa wako ,ni sawa na samaki msafi ukimtumbukiza kwenye ndoo ya samaki walioharibika hawezi kuwabadilisha samaki hao kuwa wazuri Bali naye ataishia kuharibika tu.

Profesa Bongo? Si unawaona ma-profesa akina Kapuya vitendo vyao ! Ujue Tanzania kila Jambo linawezekana,Hapa Tz Mtu anaweza kusoma kwa kuiba mitihani au kununua mitihani kuanzia std 7, form 4,Six,chuo kikuu ,degree,masters,phd hadi huo Uprofesa.Elimu ya Tz ni ya Ujanja ujanja tu, ni wachache sana wenye Taaluma na Elimu Harisia .jaribu kujiuliza ufanisi wa kazi wa Maprofesa wa Tz linganisha na watu wenye Elimu ya kawaida utapata jawabu. Mwandosya Nadhani ni aina ya wasomi wale waliosoma kijanja -janja na kujiita maprofesa wakiwa hawana Tofauti Profesa Maji marefu.
 
Amran Kombe (aliyekuwa mkurugenzi wa Usalama wa Taifa) naye alijihusisha na siasa hasa alikuwa na Mrema na kumpa siri mbalimbali inasadikiwa hata bomu la million 900 enzi hizo Mrema alipata datails kutoka kwake na alikuwa ameshastaafu.
Lakini kwa bahati mbaya mapolisi waliomfuatilia kutoka Dar walimuua maeneo ya Maili sita moshi wakidhani alikuwa ni jambazi, ijapokuwa Kombe alijisalimisha kwa kuinua mikono yake juu lakini aliuwawa. Na hao maaskari waliomuaa waliachiwa kwa msamaha wa raisi....wengine wanasema waliachiwa kipindi cha Mkapa wengine kipindi cha Kikwete. Maoni yangu hapa ni kwamba anaweza tu kujihusisha na siasa kama Kombe alivyojihusisha na siasa baada ya kustaafu kwani hamna shida kabisa
.

Nimekuelewa kabisaaaa.. Duh! Hatari
 
Profesa maji Marefu ni mjanja kuliko profesa Mwandosya , kwanza baada ya kuugua Taaluma yote aliyosoma ilfutika kichwani pengine kasalia na STD 7 tu ,si unajua sasa kazeeka vibaya na kile alichokisomea hakifanyii kazi hivyo Taaluma yake aliyosomea keshaisahau hata akipewa mtihani wa Darasa la 7 wa Juzi atafeli tu. chezea Elimu ya Tz wewe......
 
Back
Top Bottom