Mkuu mie mwana CCM mchapa lapa, sina uhusiano wowote na hao wakubwa.Riz one kuwa mwanasheria wa kawaida tu ametoa wapi utajiri kiasi hicho? kabla hujauliza swali jiangalie kwanza na angalia wanaokuzunguka ndio uje na swali tena.
Ushauri wako umejaa busara ya hali ya juu sana. Kama wahusika watasikia na kuuzingatia, itakuwa jambo jema sana
Wadau, akitoa mchango wake wakati wa mjadala wa sura za Rasimu ya Katiba, Waziri Prof Mark Mwandosya amewataka wakuu wa vyombo vya dola kujiepusha na siasa pindi wanapostahafu kwenye utumishi. Anasema kuwa wakuu hao wa vyombo vya dola hususan Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Mkuu wa Majeshi na Mkuu wa Polisi wakiwa wakiwa kwenye nyadhifa zao wanamiliki mafaili, Dossier za wanasiasa wote. Hali hiyo inawaweka kwenye position ya kuwajua in and out wanasiasa wote hususan wale wanaotarajia kugombea nafasi za juu hasa ya Urais.
Mwandosya anasema kuwa kitendo cha Wakuu hao baada ya kustahafu kujihusisha na siasa kwa kuamua kugombea nafasi za kisiasa au kuwaunga mkono baadhi ya wanasiasa wanaogombea nafasi za kisiasa kunawaweka kwenye nafasi ya kukiuka maadili ya kazi zao. Anasema kuwa ijapokuwa wanapostahafu wanaacha mafaili ofisini, wanaondoka na kumbukumbu moyoni.
Mimi nilisema tangu mwanzo kuwa Apson amekosea sana kujiingiza kwenye siasa ametia aibu heshima yote aliyokuwa nayo itapotea ngoja kampeni zianze mtaniambia wenyewe,mwandosya kafanya vema.
Mwandosya asiweweseke leo, wakati vyama vya upinzani, hususani CDM walipolalamika kuwa idara hiyo ya usalama inatumiwa na CCM kuihujumu CDM, wanaCCM walikuwa wanacheka. Sasa imekuwa mkuki kwa nguruwe. Walikuwa wakiwatumia TISS kuwahujumu CDM, sasa yale mabomu waliyoyatumia kulipua wengine yanawalipukia wao wenyewe na kuwadhuru. Viongozi wa juu wa CCM kama Mwandosya hawapaswi kuyasema hayo leo hii kwa sababu madhara ya hayo wanayoyalalamikia yalipokuwa yanasikika kwa CDM waliona kuwa CDM wameishiwa. WanaCCM mnavuna mlichopanda
Kwa akiki hii, sishangazwi na ccm walipomuuwa Kombe kwa kushirkiana na Mrema baada ya kustaafu ukuu wa usalama wa Taifa!
Huyu hawewezi kwasababu anamsapoti gamba mwenzao mwenye nguvu kubwa waliyeshindwa kumvua gamba!
Hawana njaa bali wana tamaa ya kuwa matajiri kupindukia.Mkuu, binafsi siamini kama hawa wakurugenzi wastasfu wana njaa
Kwamba alishiriki hilo la Kombe, sina details zozote hapo. Nafahamu tu mafisadi wa ccm walishiriki.aliyemuua Kombe ni huyu Apson. Alihofia haya anayofanya yeye. Kwa hiyo kama Kombe aliuawa kutokana na kumsupport Mrema, huyu Apson mbona anafanya yaleyale ya Kombe?
Kumleta kutokea wapi?First lady hajakosea kutuletea Membe?