Prof. Mark Mwandosya Amlipua Apson Mwang'onda Bungeni

Prof. Mark Mwandosya Amlipua Apson Mwang'onda Bungeni

Kwa akili hii ya Mwandosya, sishangazwi na ccm walipomuuwa Kombe kwasababu ya kushirkiana na Mrema.

Wakati huo Mrema akigombea urais kupitia NCCR Mgeuzi mwaka 1995. Mrema alikuwa akilipuwa mabomu ya kashfa na siri za ufisadi. Hii ilikuwa baada ya Kombe kustaafu ukuu wa usalama wa Taifa kama ilivyo kwa Mwang'onda!

Wakaona kuwa siri hizo Mrema anazitoa kwa Kombe!

Huyu Mwang'onda hawamwezi kwasababu anamsapoti gamba mwenzao mwenye nguvu kubwa waliyeshindwa kumvua gamba!

Je Mwandosya alisapoti kitendo kile dhidi ya Abdulrahman Kombe?

Msimamo wake huu dhidi ya Mwang'onda, hauna tofauti na msimamo wao dhidi ya Kombe!

Pamoja na kuwa ni muhimu Sheria iweke zuio kwa baadhi ya maafisa waliofikia cheo Fulani jeshini ,usalama ,IGP,CGP..kugombea Siasa ...lakini ni ngumu Sheria Hiyo kuwazuia kumuunga mtu mkono ...kwa sababu ..wanayo haki ya kupiga kura ...Sasa ukiwa Mpiga kura unaweza kuombwa kura ...na kuamua kumuunga mtu mkono....
Saa Huyu mgombea ambaye wakuu wote wa zamani wa hivi vyombo UKianza na Kitine na wengine ..hawamuungi mkono..Ana kasoro gani ..?..Kwani lazima awe yeye Rais ..si kuna watu milioni 45 ..kwani lazima hata huyo Lowassa awe Rais ?
 
Kwa kutajwa tu kuhusika na michezo michafu, napendekeza Membe na Lowasa wote watoswe
 
Mimi nilisema tangu mwanzo kuwa Apson amekosea sana kujiingiza kwenye siasa ametia aibu heshima yote aliyokuwa nayo itapotea ngoja kampeni zianze mtaniambia wenyewe,mwandosya kafanya vema.

Salamu zimfikie mzee Apson popote alipo na washirika wake.

Tulieni mnyolewe, Apson hajawahi kugombea cheo chochote cha kisiasa bali waliofanya hivyo ni Hans Kitine, Robert Mboma na Tibaigana na Mahita kama sikosei.

Tulieni dawa iwain vizuri.
 
Nilimsikia Mwandosya akizungumza bungeni,akili ilinijia ghafla kuwa baada ya muda Chabruma atareport alichokisema Mwandosya hapa JF,na nilipatwa na hisia kuwa hilo likitokea basi sitakuwa na shaka kuwa Chabruma ndo Mwandosya mwenyewe.......au mwanae
 
Kwanini azuiwe jamani...? Lets be fair..kama katiba inamkataza sawa lakini sio mtu anakuja na mawazo fulani asiingie siasa no way...hata akiwa nani katiba kwanza mambo binafsi baadae...
 
Mkuu vipi hajazungumzia mgombea wenu anayeletwa na WAMA... Nafkiri ni jambo la msingi aongeze page moja ili akemee mke wa rais kutuletea mgombea ambaye kamwe hawezi kushnda hata kwa dawa

mwaka huu msipouana dunia itashangaa sana !
 
Kwanini azuiwe jamani...? Lets be fair..kama katiba inamkataza sawa lakini sio mtu anakuja na mawazo fulani asiingie siasa no way...hata akiwa nani katiba kwanza mambo binafsi baadae...

Hans Kitine alikuwa mkurugenzi wa Usalama wa Taifa na akaja kugombea ubunge na Mkapa akamchaguwa kuwa waziri. Mwandosya anaweweseka tu ni Profesa uchwara tu.
 
Nilimsikia Mwandosya akizungumza bungeni,akili ilinijia ghafla kuwa baada ya muda Chabruma atareport alichokisema Mwandosya hapa JF,na nilipatwa na hisia kuwa hilo likitokea basi sitakuwa na shaka kuwa Chabruma ndo Mwandosya mwenyewe.......au mwanae
Hahahahahahahaaaaaaaa! JF ina burudani sana
 
Hans Kitine alikuwa mkurugenzi wa Usalama wa Taifa na akaja kugombea ubunge na Mkapa akamchaguwa kuwa waziri. Mwandosya anaweweseka tu ni Profesa uchwara tu.

Angekuwa wa maana sana kama angeshawishi bunge la katiba limnyime rais madaraka ya kuteuwa waziri asiyekuwa na wizara maalumu kama yeye alivyo........haya ndio madhara ya kuwa na waziri asiye jua kazi yake ipasavyo
 
Hans Kitine alikuwa mkurugenzi wa Usalama wa Taifa na akaja kugombea ubunge na Mkapa akamchaguwa kuwa waziri. Mwandosya anaweweseka tu ni Profesa uchwara tu.
Mkuu, kitendo cha Mkapa kumteua Kitine kuwa Waziri ni yale yale aliyoona Mwandosya. Kauli yake leo bungeni bado ni valid na ni cut across. Hata yeye Kitine inamhusu
 
Baba nape kwa nini usitundike daruga katika siasa rudi UDSM ndiko utakakoheshimika na uprofesa wako. Huko nsiasani u taendelea kupata stress tu hadi ufe muda si wako. Hivi huko kwenye siasa kuna uhondo gani hadi kina prof. kama mwandosya wang'ang'anie hadi wanaugua lakini bado tu utadhani luba. Babu Mwandosya nashauri urudi Tukuyu ukalee wajukuu wanaku-miss sana.
 
Yaonekana una chuki binafsi na Mwandosya. Ila alichosema leo Bungeni kila mwadilifu anamsifu
 
Wadau, akitoa mchango wake wakati wa mjadala wa sura za Rasimu ya Katiba, Waziri Prof Mark Mwandosya amewataka wakuu wa vyombo vya dola kujiepusha na siasa pindi wanapostahafu kwenye utumishi. Anasema kuwa wakuu hao wa vyombo vya dola hususan Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Mkuu wa Majeshi na Mkuu wa Polisi wakiwa wakiwa kwenye nyadhifa zao wanamiliki mafaili, Dossier za wanasiasa wote. Hali hiyo inawaweka kwenye position ya kuwajua in and out wanasiasa wote hususan wale wanaotarajia kugombea nafasi za juu hasa ya Urais.

Mwandosya anasema kuwa kitendo cha Wakuu hao baada ya kustahafu kujihusisha na siasa kwa kuamua kugombea nafasi za kisiasa au kuwaunga mkono baadhi ya wanasiasa wanaogombea nafasi za kisiasa kunawaweka kwenye nafasi ya kukiuka maadili ya kazi zao. Anasema kuwa ijapokuwa wanapostahafu wanaacha mafaili ofisini, wanaondoka na kumbukumbu moyoni.

Pia anasema kuwa wakuu hao bado wanakuwa na mahusiano na watumishi waliopo hivyo inakuwa ni jambo jepesi kwao kujijenga au kumjenga mtu wanayemuunga mkono kupitia watumishi wa vyombo hivyo wenye mahusiano mema nao. Pia anasema kuwa wakuu hao wanaweza kumbomoa adui wao kirahisi kwa kwa sababu hizo hizo.

Ijapokuwa Prof Mwandosya hakutaja moja kwa moja majina ya anaowalenga, lakini kwa mtiririko wa matukio ya hivi karibuni, anamlenga Apson Mwang'onda. Kwa nini nimefikia hitimisho hilo? Kwa siku kadhaa nimekuwa nikiripoti taarifa zinazomhusu Apson Mwang'onda akijihusisha na Mtandao wa Lowasa.

Kwamba, Apson Mwang'onda ni Mwenyekiti wa Kamati ya Wezesha Lowasa aende Ikulu na kwamba amekuwa akifanya vikao na wanasiasa kadhaa wanaomuunga mkono Lowasa. Vikao hivyo vimekuwa vikifanyika nyumbani kwa Apson na Mtoto wake Jimmy ambavyo pia vimekuwa vikihusisha matumizi ya kiasi kikubwa cha fedha. Apson Mwang'onda amesikika akisema kuwa yeye kwa sasa ni mstahafu hivyo si tatizo kwake kujihusisha na siasa.

Kilio cha Mwandosya hakikuanza leo. Katika Kitabu alichoandika kijulikanacho Sauti ya Umma ni Sauti ya Demokrasia, Prof Mwandosya ameeleza jinsi alivyohujumiwa na baadhi ya watendaji wa serikali na chama na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa, Apson Mwang’onda. Katika kitabu hicho, Profesa Mwandosya ametaja mlolongo wa viongozi na watendaji wa serikali katika kitabu hicho, miongoni mwa majina hayo limo la Apson.

Katika kitabu hicho Profesa Mwandosya anasema kuwa alipekewa ujumbe na mzee Jimmy David Ngonya kwamba amekuwa anamlaumu Apson kwamba hakumuunga mkono katika harakati za kuwania urais mwaka 2005, jambo ambalo alisema ni hoja iliyofinyangwa kimkakati ili kujenga uhalali wa kumwandama na kumhujumu katika harakati za kuwania nafasi ya NEC kwa mkoa wa Mbeya mwaka 2007.

Katika kinyang’anyiro cha nafasi ya NEC mkoa wa Mbeya Profesa Mwandosya alipambana na Thom Apson Mwang’onda ambaye 2005 alikuwa kambi yake katika kuwania tiketi ya urais kupitia CCM. Katika kitabu hicho Profesa Mwandosya, anaelezea jinsi alivyofanyiwa fitna, hujuma na kila aina ya mizengwe wakati wa mchakato wa uchaguzi kwa mwaka 2007 mkoani Mbeya.

Katika ukurasa wa 21, ameelezea baada ya Chimwaga, siku moja aliyekuwa naye karibu sana Mwalimu Jimmy David Ngonya alimtembelea nyumbani kwake Kibisi Tukuyu mwaka 2006, na kumpa ujumbe wa Apson ambao alimpa baada ya kufanya naye mazungumzo katika hoteli ya Land Mark iliyopo mjini Tukuyu.

Katika kitabu hicho pia ukurasa wa 141 wa Profesa Mwandosya anaeleza taarifa alizopata za matumizi makubwa ya fedha katika uchaguzi wa nafasi ya NEC mkoa wa Mbeya. “Makadirio ya fedha walizotumia yalikuwa kati ya Sh. milioni 300 hadi bilioni moja,” anaeleza Profesa Mwandosya kwenye kitabu hicho wakati akielezea mchuano ulivyokuwa katika kinyang’amyiro cha ujumbe wa NEC mkoa wa Mbeya. Anasema kuwa katika mazingira ya matumizi makubwa ya fedha ulikuwa ni ushindani kati ya ‘Goliati’ mwenye fedha na ‘Daudi’ asiye na fedha.

We chabruma una akili kama ya kunguni.una wivu kama shoga
 
Mimi nilisema tangu mwanzo kuwa Apson amekosea sana kujiingiza kwenye siasa ametia aibu heshima yote aliyokuwa nayo itapotea ngoja kampeni zianze mtaniambia wenyewe,mwandosya kafanya vema.

Ila MAHITA na yule Muhaya kule kagera walipo Gombea Ubunge kwa tiketi ya CCM walipatia?
 
Mkuu, kitendo cha Mkapa kumteua Kitine kuwa Waziri ni yale yale aliyoona Mwandosya. Kauli yake leo bungeni bado ni valid na ni cut across. Hata yeye Kitine inamhusu

Sasa mbona Ccm ni chama cha kijeshi au wewe ni mfuata mkumbo tu hujui kitu?

Ona hawa Luteni kanali Kikwete, Kanali Kinene, Luteni Makamba Captain Komba, Brigedia Ngwilizi an likes

Wakuu wa mikoa wamejazwa wanajeshi na kwenye ya usalama hata Membe na Pinda nao wanapaswa kukaa pembeni hawa wote ni makachelo
 
Back
Top Bottom