Prof. Maghembe adhulumiwa mali ya bilioni !

Nawapa ushauri wa bure,wote waliofanywa vivuli wa kumiliki mali ya watawala kwa mtindo huu wachangamkie fursa hii,msipokuwa matajiri msimlaumu mtu,hawa mafisadi ni kuwaosha kama walivyoosha kodi zetu.
 
Huu uzi ni kama umeandikwa na mtu aliyekuwa anatweta baada ya mbio ndefu za kukimbia kujiepusha na adhabu fulani na akasimamishwa ghafla aeleze alichoeleza. Namshauri mleta uzi atulie na kuandika vizuri alichokusudia tukijue wadau.

inaonekana wewe ndio slow learner,yani umeshindwa kutoka na kitu hapo?
 
Hivi ninyi kwa akili zenu mnadhani kuna kiongozi wa juu yeyote ccm msafi!
mh............! am tired na hiki kitu kinachoitwa ccm.
 
Mwizi kaibiwa

Hivi kwa nini Mawaziri wengi ni mamilionea? Hakuna sheria inayowabana kutofanya biashara?
Nasikia hata Mramba mzee wa kula nyasi naye alilizwa pesa ndefuu na mwenye mabasi ya Kilimanjaro Express.
 
Huyu waziri ni mwizi, je amepataje mali hizo, je kama ni mali halali kwanini anazificha??????
Kikwete, mulika mwiziiiiii meeeeeeeeen
Sharo.jpg
 
SALAM WANABODI
Mbunge wa Jimbo la Mwanga na Waziri wa Maji Mh. Profesa Jumanne Abdala Maghembe amedhulumiwa mali yenye thamani ya zaidi ya Tsh bilioni moja na swahiba wake ambaye ni Diwani wa Kata ya Shighatini Mh. Enea Mrutu.
Mali hizo ni mabasi makubwa ya kubebea abiria aina ya UTONG na Moja aina ya Scania yanayaofanya safari kati ya Dar na Arusha na malori mawili aina ya Mitsubishi FUSO ambayo kwa sasa Mh. ameyapeleka huko Kahama . Mabasi (KIRUMO CHARO) ambayo mheshimiwa Mbunge alikubaliana na Mhe. Diwani kuwa kwa kuwa yeye (enea) ana kampuni ya mabasi anaomba kutumia jina la Kampuni yake ya CHARO GENERAL SUPPLY LTD ili kufanya biashara hiyo kutokana na sababu za kiutumishi wake serikalini(kama mbunge na waziri). Ukichukulia status yake ya maisha hapa nchini haieleweki kwani alikuwa mtafiti huko malawi ndo akaja kugombea ubunge hapa mwanga tangu mwaka 2000.
Sakati hili lilianza baada ya Mheshimimiwa Eneah kutumia kiasi kikubwa cha fedha wakati wa Kampeni za uchaguzi wa CCM kwenye jumuiya za Wazazi, UVCCM na Chama kwenye nafasi ya MNEC ambapo jumla ya Tsh 56,000,000 zilitumika kama Rushwa kwa wajumbe na kubahatika kushinda Jumuiya ya UWT tena kwa mbinde na wizi mkubwa wa kura. Mh. enea kwa sasa anatamba mtaani kuwa maghembe hana cha kumfanya kwani hawezi kwenda mahakamani kuhofia kuumbuliwa kuwa ni fisadi.
naomba kuwasilisha.

SOURCE: MHUDUMU WA OFISI YA CHARO GENERAL SUPPLY NA MIMI MWENYEWE

Ama kweli KIFUMWA NI VANTU
 
Back
Top Bottom