Prof. Lipumba: CHADEMA wamepoteza dira

Prof. Lipumba: CHADEMA wamepoteza dira

kama hoja ilikua kumkataa kumnadi Lowassa angenadi hata wabunge na madiwani wa ukawa,kosa alilofanya ni kuwakimbia watu wakiwa katika kipindi kigumu cha uchaguzi,c ajabu kwa ushawishi aliokua nao kwenye ukawa wabunge na madiwani wangeongezeka,nilimwamini sana Lipumba lakini kwa sasa namfananisha na mtu aliyeaminiwa kugombea nafasi akashindwa kurudisha fomu,cuf tutakosea kumpa nafasi ya juu chamani
 
mcubic unadhani tatizo letu kama taifa ni "ukemeaji" wa masuala ya Rushwa? Tatizo letu ni dhamira ya dhati ya kupambana na rushwa. Na rushwa ya tanzania ni ya kimfumo bila ya kuufumua huo mfumo tutaishia kuwa na matamko yasiyoisha na kuoneana bila ya sababu. Agenda dhidi ya ufisadi CHADEMA walikuwa wanaifanya kuwa ni ya taifa nyie mmeigeuza kuwa ilikuwa ni ya CHADEMA. Aibu ilioje!!

Ilikua ya Chadema na ikapata uungwaji mkono na watanzania wengi nikiwamo mimi hivyo hoja ikageuka kuwa ya kitaifa. Rushwa ni suala kubwa linaloigharimu nchi hii katika kupiga hatua za kimaendeleo, kwa hiyo kwa yeyote anayepinga Rushwa kwa vitendo (rais magufuli) mimi ntamuunga mkono kabisa bila kuangalia ninafuata itikadi zipi.

Kinachoshangaza ni kuona baadhi ya watu wanabeza hatua hizi kwa kejeli, wakati wao ndio walikuwa wapigaji kelele wakuu dhidi ya rushwa. Kuna watu wanasema au kutaja neno mfumo bila kuelewa maana yake......hebu tuone maana ya neno mfumo kwa kiingereza:


"A set of detailed methods, procedures and routines created to carry out a specific activity, perform a duty, or solve a problem"

Kwa tafsiri isiyo rasmi mfumo ni : "Aina ya mbinu mbalimbali zinazofanywa khaua kwa hatua na mara kwa mara katika shughuli fulani, kufanya kazi au kutatua matatizo"

Kwangu mimi mfumo wa kwanza ambao ungepelekea sisi kufanya shuguli mbali mbali ili kufikia malengo tuliyojiwekea ni Katiba ( huu ndio muongozo mkuu kwa taifa lolote lile). Mimi ninakubali kuwa katiba yetu tuliyonayo imepitwa na wakati haitufai....baada ya katiba kuna mifumo mingi na tofauti tofauti ambayo watu huifuata katika kutekeleza majukumu yao.

Tuchukulie mfano kwenye mpira wa miguu ni kwanini tanzania hatufanikiwi na wenzetu wanafanikiwa? Jibu ni rahisi tu ni kua hatupitii katika hatua muhimu ambazo wenzetu wanapitia katika kuandaa wacheza mpira.....mathalani mtoto anakiwa kusoma elimu ya mpira kinadharia na vitendo tangu akiwa kijana mdogo katika shule za michezo ambazo nazo zinatoa taaluma nyingine.

katika kufanya mfumo wowote ufanye kazi basi usimamizi, uwajibikaji na nia ya dhati ya kutaka mfumo ufanye kazi ni mambo muhimu......haiwezekani wengine wanapigia kelele rushwa na kuanza kuchukua hatua wengine wanakejeli wakati huo huo tunasema mfumo mbovu, hatujui kuwa na sie tunaokejeli tunafanikisha mfumo usifanikiwe.....Matu anayekemea jambo kwa dhati ya moyo anasaidia kwa namna moja ama nyingine kusaidia mfumo kufanya kazi
 
Mwambieni akiwa muongo asiwe msahaulifu. Clip za mapokezi ya Lowasa Ukawa zinaonyesha ushiriki wake ila lililomuuma ni kule kuenguliwa katika kazi yake ya kudumu ya " Mgombea Urais"

kujiuzuru kwake kunamsafisha
 
Kama Prof alikosa uzalendo kwenye UKAWA na matokeo yake CUF kupitia UKAWA wamepata wabunge na madiwani wengi ikilinganishwa na kipindi chake hii inaonesha kuwa Prof alifail katika mission yake. Sasa kama anarudi na slogan ya HAPA HAKI TU hiki ni kichekesho kingine. Nashauri CUF wakimaliza issue yao ya Zanzibar wamtimue mapema kwani kwenye chama huyu bwana ni liability.
 
Wakati akiongea kupitia AzamTwo Television, Prof. Lipumba amesikika akisema, CHADEMA kimepoteza dira ya kisiasa kutokana na mtafaruku uliojitokeza ndani ya UKAWA baada ya kumpokea Lowassa na kumfanya mgombea Urais wa Tanzania.

Prof. Lipumba amesema, ''Sisi ndani ya CUF tunaweza kukijenga vizuri chama chetu kwa sababu msingi wetu ni kusimamia haki kwa wote lakini wenzetu wa CHADEMA wamepoteza dira kwa sababu itakuwa ni vigumu kuzungumzia suala la mapambano dhidi ya ufisadi''.

''Msingi wa sera zetu ni Haki Sawa Kwa Wote, Rais Magufuli anasema HapaKaziTu na sisi tunasema Hapa ni Haki Tu'' Alisema.

Aliendelea kusema, ''Tuna mahala pazuri pa kuanzia, kutazama namna ya kuikosoa serikali katika kutekeleza hizi sera za HapaKaziTu, Je tunalinda haki za kila mmoja wetu, tunafuata utaratibu mzuri wa sheria''

Alimalizia kwa kusema, ''wenzetu CHADEMA wamepoteza dira''.

VIDEO:


Ni kweli kabisa CHADEMA wamepoteza dira yao na sijui watatoa wapi jeuri ya kuongelea ufisadi tena.
 
Last edited by a moderator:
Allen Kilewella

Kwa hiyo ajenda yenu ni ipi?
CCM wanakemea ufisadi.....mmeporwa hoja yenu.

ACT- utu, miiko na uzalendo

CUF- haki sawa kwa wote....hapa haki tu.

Madiliko lowasa lowasa mabadiliko kaz yao kuzungusha mikono badala ya kuzungusha akil
 
Last edited by a moderator:

"A set of detailed methods, procedures and routines created to carry out a specific activity, perform a duty, or solve a problem"

Kwa tafsiri isiyo rasmi mfumo ni : "Aina ya mbinu mbalimbali zinazofanywa khaua kwa hatua na mara kwa mara katika shughuli fulani, kufanya kazi au kutatua matatizo"

Mimi ningetafsiri hivi "Mfumo ni Mbinu yakinifu, utaratibu na kanuni zilizobuniwa kufanikisha shughuli fulani, kutimiza wajibu, au kutatua tatizo" Kwa maana hii ni lazima kwanza mfumo ubuniwe, pia ndani yake kuwe na utaratibu wakufuatwa na kanuni za kuzingatia katika kutatua tatizo. Kwa tafsiri hii yangu sidhani kama kushughulika na watu ni kushughulika na mfumo!

Nakubaliana na wewe kwamba Katiba ni chanzo kikuu cha mfumo wa kuendesha mambo katika taifa letu, na ndiyo maana sisi wengine tunaamini bila kwanza Katiba kubadilishw bila shaka haya anayoyafanya Magufuli zitakuwa ni mbio za Sakafuni.
 
Prof Lipumba alisusa uongozi Maalim Seif akasema hewala leo kaona upinzania umeshamiri anataka kuurejea uenyekiti kinyamela hafai hata kidogo askari anayekimbia vitani adhabu yake ni kifo.
 
Yaani baada ya cdm kumsaidia kupata idadi ya wabunge ambayo hajawai kuipata muda wake wote wa uenyekiti leo anarudi na hii gear, au naye kapewa assignment nyingine siku alipotembelea magogoni!?
 
Lipumba hana hata aibu. Anadai sisi CUF ................... CUF ipi wakati alijitoa kabla ya kupigwa boot!!

Dhambi ya usaliti inamtesa ............ hata Yuda alitaka kurudisha vile vipande 30 vya sarafu ili jamaa wamuachie Yesu lakini ilikuwa too late ............ mwisho wa siku akajinyonga!!!
Prof. Lipumba bado ni mwanachama wa CUF.

Nani alikuambia kupingana na uamuzi wa chama ni usaliti?
 
Amezungumza jana wakati akimpokea Mnyaa mbunge wa Cuf aliyeshinda ubunge wa Afrika Mashariki.
Prof Lipumba amesema kama chadema iliweza kumuuza Dr Slaa aliyekipigania chama hawatashindwa kumuuza Maalim seif.

Pia amewachana chadema kuwa ni chama kilichopoteza dira na misingi yake, Prof Lipumba amesema sasa hivi watuhumiwa wa ufisadi, kuuza madawa ya kulevya, uchawi, ukwepaji kodi wote hao kimbilio lao ni chadema.!!

Prof Lipumba amebaki na mshangao tunu, miiko, dira na miiko ya chadema iko wapi??
 
PROF LIPUMBA yupo sahihi SLAA alipigania chama sana ila alilipwa mabaya ila ipo siku chadema watajuta dhambi walio ifanya itawarudia
Inasikitisha chadema kuuzwa kwa mafisadi
 
Lipumba anavyouharibu upinzani kwa uswahili na unafki hawezi kuinyooshea mkono CDM . Ametumika vibaya na hata akiachiwa hiyo Cuf haiwezi tena kusimama dhidi ya wanaomlipa(CCM)

Awaache CDM wafanye yao naye aendelee kuichuuza CUF huko Lumumba
 
Lipumba anavyouharibu upinzani kwa uswahili na unafki hawezi kuinyooshea mkono CDM . Ametumika vibaya na hata akiachiwa hiyo Cuf haiwezi tena kusimama dhidi ya wanaomlipa(CCM)

Awaache CDM wafanye yao naye aendelee kuichuuza CUF huko Lumumba
Kati ya Lipumba na Mbowe nani yuko bize kupokea majizi na wauza madawa ya kulevya??
 
Back
Top Bottom