Prof. Kitila Mkumbo arejea rasmi CCM

Prof. Kitila Mkumbo arejea rasmi CCM

Kwamba kwa level ya profesa huwezi kufanya maisha nje ya siasa?! Hii nchi ya ajabu kama tutakua tumefikia huko
Nimemquote Mh Lawrence Masha, alisema anawatoto, acha aangalie mbele. Ndiyo maana akaondoka Chadema.
 
Baada ya kushindwa kwa mission yake ya kuiua CHADEMA ameamua kurejea alikotoka.

Kila la heri lakini ukumbuke kila kazi ina malipo yake
Chadema itajiua yenyewe kwa usajili mbovu wa mafisadi. You can fool some of the people for sometimes,but you can't fool all the people all the time!
 
Kutoka Sebuleni na kuingia chumbani ndani ya nyumba moja ni kuihama nyumba?

Danganyeni watoto.
 
Nimecheka sana hakuna kitu kibaya kama kuamua kuweka akili zako mfukoni,

Naona ameamua kubeba kichwa chake kichwani kama mzigo juu ya mabega.

Le professeli kweli njaa ya kuanzia kichwani kuelekea tumboni ni mbaya sana, Njaa ingeanzia tumboni tungempa chakula.

Maprofesa wa kitanzania ni majanga kama majanga mengine. Ni muhimu kubadili huu mfumo wetu wa elimu, watu hawajawahi fanya jambo la maana wanasoma tu makaratasi na kuitwa maprofesa.

Shame On them
Mbona una hasira sana?
 
Sidhani kama Zito alitambua kuwa amezungukwa na viongozi wa namna hii.

Mwenyekiti wa Chama na mgombea urais wa Chama, katibu wa Chama, na mshauri mkuu wa Chama.

Wawili Wamehama, mwingine yuko na nafasi ya kiserikali.
Hawa ndio ilikuwa nguzo kuu ACT na waasisi wake.

Sasa ni kama wamemtelekeza nadhani angejua hili bora hata angebaki CHADEMA.

Je hao waliobaki wamemuzunguka wako salama?
nahodha mahiri hufa na chombo chake.
 
Kuna mambo yanachekesha Sana aiseeee, ukiacha Afisaelimu wa Wilaya moja ya Daaaahhh na Yule Mwalimu wa Muheza na Lushoto kwa uchache kuna huyu mwingine nae.
IMG-20171116-WA0072.jpg
 
upinzani umebaki Yatima. hawana sera;hawana hoja; wataendelea na vioja; ccm inazidi kuwa imara
 
Kitila amefanya "gamble" ya kisiasa inaweza ikamlipa au akapotea mazima kisiasa.

Kitila afahamu kwamba kilichomfikisha hapo ni vitu viwili

1. "Rarity" yake ndani ya serikali, yeye kama mtu aliyetoka chama cha upinzani lakini akaaminiwa kuwa ndani ya cycles za mamlaka, rarity hii ilimpa uthamani wa pekee ndani ya kundi la wengi.

2. Constructive criticisms alizokuwa akizitoa wakati akiwa nje ya serikali naamini zilizivutia mamlaka za uteuzi

Kwa yeye kuwa mwanaCCM anapoteza ile "rarity", ameingia katika kundi la wengi, kaungana nao sasa hana ule uspecial ambao angeendelea kuupata kwa kuwa mwanachama wa chama cha upinzani lakini akawemo serikalini.

3. Kwa kuwa sasa ni mwanaCCM anaweza kufanya constructive criticism ndani kwa ndani ila nje kwenye public hawezi, na hata huko ndani siyo rahisi kuwa bold na free kama huku nje kwa hiyo sioni ni kwa vipi hii ya pili itamnyanyua tena kisiasa mbele ya umma zaidi ya hivi alivyo kwa sasa.

Kwa hiyo naiona njia ngumu sana ya kisiasa mbele ya profesa Kitila kama karata zake hatazichanga vizuri, kwa sababu hana mtaji wake wa kisiasa wa kusimama yeye kama yeye.
 
Back
Top Bottom