Prof. Kabudi: Zoezi la kutafsiri Sheria kwa lugha ya Kiswahili linaendelea

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi amesema Wizara nyingine pamoja na Taasisi zinaendelea na zoezi la kutafsiri Sheria zinazosimamia ili ifikapo Desemba 2021 Sheria zote ziwe zimetafsiriwa kwa Kiswahili.

Amesema Mahakama ipo katika hatua za mwisho kutafsiri Kanuni zaidi ya 50 zilizotayarishwa na Jaji Mkuu. Kwa upande wa Bunge, tayari imetafsiri Sheria inazosimamia.

Amewataka wale ambao bado hawajaanza zoezi hilo kufanya hivyo mara moja ili kuendana na Mpango Kazi na kumaliza kazi hiyo kwa wakati.
 
Kesi za kbambikizwa hapo hakuongelea?

Mh. Rais aliagaza kesi zisizo na ushahidi zifutwe. Hadi leo hakuna utekelezaji.

Ingekuwa ni mwenda zake aliagiza siku ile ile wange tekeleza.

Sasa tumuombe Mh. Rais aondoke na huyu wa jalalani aje mwenye kutii mamlaka.
 
Iwapo mawaziri na wakuu wa Taasisi na idara zote wataendelea kuhudumu wateule wa mwendazake mama asitegemee matokeo chanya
 
Hiyo Kazi itachukua miaka 200

Yaani sheria zitungwe kwa kiingereza kwa miaka 70, halafu zitafsiriwe ndani ya miaka miwili mitatu?

Hawa wanapoteza muda, labda cha kufanya waangalie ni sheria zipi zinatumiwa na wananchi zaidi kama vile sheria za ndoa ndo watafsiri hizo

Ila kuanzia sasa kwenda mbele sheria zianze kuandikwa kwa kiswahili
 
Back
Top Bottom