Prof. Kabudi: Watanzania tuache uoga, hakuna atakayeshitakiwa na ACACIA

Pamoja na yoote hayo mazuri anayoyasema Kabudi !!. Ni awamu ya tatu ya Ben iliyotuiingiza ktk matatizo makubwa na sasa kupitia kwa Mkulu ni kuwa hata majina yao tusiyataje!!. Halafu ndiyo mashujaa eti wamefanya makubwa!!! Bila kuwajibishana hakuna lolote hasa kwa watawala
 
Kwa akili yako unaamini kwamba kesi ya masamaki taifa lilishindwa??? Hakuna hukumu ya kwamba taifa lilishindwa kesi hiyo ila ni watu tu waliamua kupiga dili na watuhumiwa
Lakini Tanzania ililipa au uzembe wa waziri aliyekuwepo na tena ni Raisi kwa sasa na phd yake feki leo hii Tanzania masikini wanaendela kuzidi

Go back to school Dude

Swissme
 
Wameshatunyonya sana acha mikataba yote irudiwe upya. Na siyo ya madini tu nahisi kwenye gasi ndo kumejaa uozo. Mikataba yote irudishwe bungeni.

Ila wabunge haswa wa CCM hata siwaelewi, ni kama bendera fuata upepo tu. Wao walikaa na kupitisha miswada yote ya madini kwa kura ya ndiyo. Wapinzani walipowapinga wakabakia kuzomea. Sasa hivi walichokuwa wanahoji wapinzani ndo kinawatokea puani.

Tukiacha mihemko na uchama tukaweka nchi yetu mbele nina uhakika kabisa Taifa letu litasonga mbele. Ila kama sheria zitapitishwa tu kwa sababu tunataka ushabiki wa chama chetu ushinde tutatambukia shimoni.

Nakubaliana kabisa Prof Palamagamba alichosema ni vyema tukaenda mbele kwa ujasiri mkubwa na kuangalia upya mikataba iliyowekwa ya madini na kutengeneza mikataba mipya kuliko kuweka mkia katikati ya mapaja.

Liwalo na liwe tu. Ama zao ama zetu. Hata tukiliwa basi tujuwe pia tumejaribu kurudi kwenye mstari ikashindikana na siyo kubakia kulia lia tu.

Ditto!

Kuhusu CCM na wabunge wao, hilo ni kweli.

Ni CCM pekee ndo waliotufikisha hapa tulipo.

Na umekuwa msimamo wangu wa muda mrefu sasa kwamba CCM wanapaswa kutuomba radhi Watanzania.
 
Kwa maana hiyo Lissu was right kusema tatizo ni sheria na mikataba na sasa review inaaza na Professor anatambua athari za Ghana na Tz hapo awali Lissu ni resource
Hakuna ambaye alisema tatizo sio sheria.

Hata mapendekezo ya Kamati zote mbili zilizoundwa na Rais Magufuli zilisema tatizo ni sheria na taratibu ndio maana moja ya mapendekezo ilikuwa ni kufanya mabadiliko ya sheria.

Mapendekezo hayo yamezaa miswada mitatu ya sheria ya madini kama ilivyowasilishwa na Prof. Kabudi.
 
Kama umejua prof. anakuchezea akili, achana naye! Shughulika na hoja za watu wasiokuchezea akili!

Umejuaje kama hatuwezi kuwashitaki iwapo mazungumzo hayatafanikiwa?

Kwa nini unataka negotiations zifanyike baada ya acacia kupatikana na hatia? Kwenye masuala ya madai, hata mahakama huwa zinawaomba wadai wafanye mazungumzo nje ya mahakama kabla ya kushitakiana mahakamani kwa sababu ya kupunguza gharama za mashitaka.

..Prof anazungumza kana kwamba acacia peke yao ndiyo wenye haki ya kutupeleka mahakamani/miga, wakati siyo kweli. Na ndiyo maana nasema hata wakati akisema ukweli, Prof anadanganya humohumo. Na huko ndiko kuchezea watu.

..Napendekeza Acacia wakashtakiwe miga kwasababu ripoti mbili za tume za Raisi zimethibitisha kwamba wametuibia. Na kama wametuibia basi mahali panapowastahili ni miga ili Tanzania tukapate haki yetu.Kwa maoni yangu acacia wakishapatikana na hatia Tanzania tutakuwa na leverage kubwa zaidi tunapo-deal nao ktk meza ya mazungumzo.
 
Tunajua sana kuongea, kulaumu, na kunung'unika.

Watu tumelalamika weee...sasa hayo malalamikio yanafanyiwa kazi, watu wanaanza kutetemeka [tena baadhi ya hao wanaotetemeka eti wanajiita sijui wasomi-mawakili]...ooh mmeona waliopo kwenye bodi ya sijui Acacia...mara sijui tutashitakiwa...mara hivi...mara vile!

Okay, fine...but so what?

You would think it's Armageddon the way some of these people tremble in apprehension!

Huna jipya ww na Kabudi sioni tofauti wote mnaishia kuingiza maneno ya kizungu kuwakoga majuha lakini hayana tija. Lengo na matumaini ya wananchi ni kulipwa 108t na wala sio kuogopwa kushitakiwa. Watu tumebaki na matumaoni makubwa kuhusu kulipwa na wala sio hofu ya kushitakiwa. Lengo la kuzuia makinikia ilikuwa ni kulipwa madini tunayoibiwa. Tukaishia kubezana humu majukwaani na nchi kwa ujumla huku kuanzia mkulu mpaka wafwata mkumbo wakionyesha tunalipwa tena hela nzito. Kwa hiyo yale maandamano ya kumpongeza rais na wengine wakaishia kusema rais aongezewe muda ni hiyo kuzuia kushitakiwa na Acacia? Najua umejitosa kwenye hii mada lakini unasikia aibu ya mwaka. Hoja ni kulipwa 108t na sio kuogopa kushitakiwa. Sasa imedhihirika hata hayo tunayojadili hayawahusu wezi wa sasa bali ni wapya watakao kuja anbao hatuna hakika kama watakuja.
 
Hawa ACACIA wameamua mpaka kufungua site maalumu kujibu/kutolea ufafanuzi madai yote na kila tuhuma wamejibu tena kwa kutoa nyaraka huku wakitushaangaa kwa kutoa madai ambayo sio realistic kwa mfano hilo la kudai ACACIA hawajasajiliwa kuchimba madini wakati kumbe ACACIA haichimbi hayo madini bali ni kampuni tanzu za ACACIA ndio zinahusika na ndio zenye leseni ya uchimbaji.

Baadhi ya madini tunayodai yako kwenye huo mchanga kumbe hata hayapo kabisa.Mtu unasoma maelezo yao mpaka unaona aibu na kujiuliza wanatuchukuliaje hawa watu.

soma haya maelezo ya ACACIA kuhusu baadhi hayo madini tulodai yapo kwenye makinikia na ambayo ni madini adimu(REE)

  • REE deposits are not found with gold deposits of the style of Buzwagi and Bulyanhulu
  • Ytterbium is a minor component of most REE deposits
  • The findings imply that there 9.8 tonnes per annum of Ytterbium being produced; this would make Acacia likely equivalent to the current largest known producer in the World
  • Acacia believes that the Ytterbium is 1ppm or 0.0001% in the concentrate
  • We do not get paid for this miniscule amount as it is not commercially extracted and therefore no royalty is due
Soma zaidi kupitia hii link:

http://www.acaciamining.com/export-ban-facts/disputed-key-facts/english.aspx

kuibiwa tumeibiwa kisheria na labda kwenye kukwepa kodi ingawa nako huko wametoa nyaraka zote kuonyesha ambavyo wamekuwa wanalipa kodi serikalini.
 
Msemaji ukweli sitaki kuamini yale matumaini mliyowapa watu saa mnatuona majuha mnaanza kugeuza hoja ni kutokushitakiwa. Hoja ilikuwa ni kulipwa na wala sio hofu ya kushitakiwa. Mliiaminisha watu tutalipwa 108t, leo mnaanza kutuletea hadithi za kutoshitakiwa? Halafu nimejaribu kufuamfuatilia Kabudi, nimegundua hana jipya, kila mara akiongea anaishia kuongea historia na kiswangilish kisicho na tija lakini hana suluhisho la matatizo ya nchi.

Kwa ufupi huyo huyo Kabudi ni mwalimu wala sio mtu wa kumtegenea kwenye uchumi wetu. Pamoja na maelezo yake yote na kutumia vijimaneno vya kizungu hakuna mahali anapozungumzia hizo hela za malipo zaidi ya kuonyesha hatutashitakiwa. Kwani hao Acacia lengo lao ni kutushitaki? Wao iwapo wataendelea kuvuna hawana muda wa kutushitaki ila iwapo tutawazuia kuvuna wanaweza kutushitaki.

Nimegundua hata hiyo mnayosema sijui hawajasajiliwa Brela si lolote si chochote kwani mpaka sasa Acacia wapo nchini na wanaendelea na kazi zao. Hivi ingekuwa ni kampuni ya mtanzania na haswa mpinzani itamkwe haijasajiliwa leo ingekuwa bado inaendelea kufanya kazi? Tuliaminishwa baada ya wiki hao Barrick wanarudi kuja kujadili kurudisha chetu, mpaka hawajatokea, badala yake tunakimbizana na miswaada ya dharura kumbe hata yenyewe ni ya wawekezaji wapya na wala sio hawa mnaowata wezi. Duuuu aibu gani hii, na kwa kauli hizi sintoshangaa yale macontainer 277 ya makinikia tukalipishwa gharama za kuyazuia.
Tindo
Hakuna aliyesema tutalipwa 108 trilioni. Kuwa na madai ni suala moja, kukubaliwa madai ni suala jingine.

Rais alisema tutafanya majadiliano ili kufikia muafaka wa madai yetu.

Kutokuanza mazungumzo haina kwamba mazungumzo hayafanyiki. ungelalamika na malalamiko yako yangekuwa na mashiko kama ungekuwa na andiko kutoka ACACIA au serikali linalosema mazungumzo hayatafanyika.

Ninadhani hujasoma thread yote na kama ungekuwa umeisoma na kuielewa vizuri basi ungefahamu kuwa hoja zako zimejibiwa vizuri sana.
 
Huna jipya ww na Kabudi sioni tofauti wote mnaishia kuingiza maneno ya kizungu kuwakoga majuha lakini hayana tija. Lengo na matumaini ya wananchi ni kulipwa 108t na wala sio kuogopwa kushitakiwa. Watu tumebaki na matumaoni makubwa kuhusu kulipwa na wala sio hofu ya kushitakiwa. Lengo la kuzuia makinikia ilikuwa ni kulipwa madini tunayoibiwa. Tukaishia kubezana humu majukwaani na nchi kwa ujumla huku kuanzia mkulu mpaka wafwata mkumbo wakionyesha tunalipwa tena hela nzito. Kwa hiyo yale maandamano ya kumpongeza rais na wengine wakaishia kusema rais aongezewe muda ni hiyo kuzuia kushitakiwa na Acacia? Najua umejitosa kwenye hii mada lakini unasikia aibu ya mwaka. Hoja ni kulipwa 108t na sio kuogopa kushitakiwa. Sasa imedhihirika hata hayo tunayojadili hayawahusu wezi wa sasa bali ni wapya watakao kuja anbao hatuna hakika kama watakuja.

Bless hour heart.
 
Nakubaliana naye mia kwa mia.

Yaani ukisikia baadhi ya maoni ya watu humu kwa jinsi wanavyoonyesha uoga kisa tu sijui kwenye bodi kuna William Cohen na Newt Gingrich, unabaki unatikisa kichwa tu.

Vyovyote vile itakavyokuwa, the sky won't fall.

Sioni sababu ya kuogopa hususan kama unajua kuwa unachokifanya ni sahihi hata kama huko nyuma kilikosewa.

Wengine tulilisema hili Ngosha, kinachosikitisha ni kuwa upinzani ndio tuliamini wanazo gololi za kusimamia mbele ya hawa wakubwa. Sasa sijui wenzetu wangekuwa madarakani wangefanya nini. Sidhani kama hata robo ya kilichofanywa sasa wangethubutu.
 
Tunajua sana kuongea, kulaumu, na kunung'unika.

Watu tumelalamika weee...sasa hayo malalamikio yanafanyiwa kazi, watu wanaanza kutetemeka [tena baadhi ya hao wanaotetemeka eti wanajiita sijui wasomi-mawakili]...ooh mmeona waliopo kwenye bodi ya sijui Acacia...mara sijui tutashitakiwa...mara hivi...mara vile!

Okay, fine...but so what?

You would think it's Armageddon the way some of these people tremble in apprehension!
Kinachoshangaza zaidi wanaotetemeka ndio wale ambao wanashinda mahakamani wakitetea watu wenye makosa.

Kama watu wangekuwa wanaogopa mahakama basi hata kazi za mawakili zisingekuepo hapa duniani.

Kazi ya mahakama ni kutafsiri sheria na lazima awepo mshindi na mshidwa.

Some of them just playing politics and stoking fear to poor Tanzanian.
 
Wengine tulilisema hili Ngosha, kinachosikitisha ni kuwa upinzani ndio tuliamini wanazo gololi za kusimamia mbele ya hawa wakubwa. Sasa sijui wenzetu wangekuwa madarakani wangefanya nini. Sidhani kama hata robo ya kilichofanywa sasa wangethubutu.
Uzalendo sio kufanya mambo kisiasa.
 
Kabudi endelea kumfurahisha jamaa yako wa chato.kumbuka hata samaki wa magufuli Tanzania tulilipa kwa uzembe wa huyo mpangusa kamasi in second.

Swissme
Huko ccm sijui huwa yanafanywa nini haya masomi yetu? Yaani hata li porofesa na mdigrii yake likishaingia huko linakuwa pumbavvvv la kutupwa! Huyu mbweha anataka kutuaminisha kwamba eti tuna-flex muscles kwa giants huku anasahau tayari wamesha-succumb kwa kusema sheria hii haitagusa mikataba iliyokwishasainiwa! Sasa hapo bingwa ni sisi au ACACIA? NYOKO HAWA!!
 
Tindo
Hakuna aliyesema tutalipwa 108 trilioni. Kuwa na madai ni suala moja, kukubaliwa madai ni suala jingine.

Rais alisema tutafanya majadiliano ili kufikia muafaka wa madai yetu.

Kutokuanza mazungumzo haina kwamba mazungumzo hayafanyiki. ungelalamika na malalamiko yako yangekuwa na mashiko kama ungekuwa na andiko kutoka ACACIA au serikali linalosema mazungumzo hayatafanyika.

Ninadhani hujasoma thread yote na kama ungekuwa umeisoma na kuielewa vizuri basi ungefahamu kuwa hoja zako zimejibiwa vizuri sana.

Mkuu msemajiukweli ni hivi sipingi utetezu wako bali ninachoongelea hapa ni picha iliyojengeka tuna deal na wezi na kitakachoendelea ni wao kutulipa. Lakini kwa maelezo ya leo ya Kabudi naona ameingiza baridi na anachotuletea ni historia sijui wajerumani zamani walikataliwa na Nyerere, mara sijui waingereza na €5m na hadithi za namna hiyo, lakini sio leo tutalipwa lini.

Hizo sheria zinasaidia nini wakati wizi unaendelea na wala mikataba hii haiwagusi wezi wetu zaidi ya wezi watakaokuja baadae? Ni kwa nini iwe ya hati ya dharura wakati sio ya wezi wapya? Tulitahadharisha hapa kwamba wananchi wanapewa matumini makubwa lakini kinachochezwa ni siasa tu na hakuna uzalendo wowote. Nikuulize Mwinyi mpaka anasema rais aongezewe muda na Warioba kuandamana na wananchi kumpongeza rais huku wengine wakitaka aongezewe muda ni hii miswaada ya dharura? Bi dhahiri watu waliandamana wakijua tumeshika wezi na tutalipwa. Lakini chini ya hao walioaminisha watu hakuna kinachoendelea huku wezi Acacia wakiendelea na kazi zao kama kawa na hao watz waliotajwa na ripoti wote wanadunda tu. Ni hivi mnatuchezea siasa zisizo na tija na bado muda kidogo watu watashitukia hii siasa nyepesi wanayochezewa.
 
Kinachoshangaza zaidi wanaotetemeka ndio wale ambao wanashinda mahakamani wakitetea watu wenye makosa.

Kama watu wangekuwa wanaogopa mahakama basi hata kazi za mawakili zisingekuepo hapa duniani.

Kazi ya mahakama ni kutafsiri sheria na lazima awepo mshindi na mshidwa.

Some of them just playing politics and stoking fear to poor Tanzanian.

..anayetetemeka ni serikali ya Tz.

..acacia wamekamatwa " redi hendedi"[kwa sauti ya bwana mkubwa] wakituibia, halafu tunapatwa kigugumizi kuwapeleka mahakamani/miga. WHY?

..unapofanya mazungumzo na mwizi, badala ya kumpeleka kwenye vyombo vya sheria, maana yake unamlinda mwizi huyo.
 
Maelezo ya Prof Kabudi anatambua kwamba We are fighting against Giant, anachojaribu ni kutuhamasisha ili tusijihisi wanyonge. Nadhani nae pia anaungana na mamia ya Watanzania wanaotaka umakini zaidi katika kila hatua ya Serikali ili kuepusha hasara inayotazamiwa.
Binafsi ninachokiona mpaka sasa ni as if tumefanikiwa sana kuwaweka Acacia mezani ili kujadiliana nao wakati hilo ndio limekuwa hitaji LA Acacia toka kuzuiwa kwa Makanikia yao.
Pia, Ile dhana ya kwamba Acacia imehalalishwa na mkutano wa Rais Ikulu kwa Kukubali negotiatation na watu waliotajwa kutokutambulika kisheria.
Acacia mpaka sasa bado wameendelea kusafirisha gold bars bila kizuizi chochote licha ya ufeki wao.
Kama kweli taarifa za kamati ni sahihi, Tanzania ndio tulipaswa kuwashitaki Acacia, na baada ya kuwashinda ndio tungewaleta mezani kwa kuwa nguvu yetu ingekuwa kubwa.
 
Ditto!

Kuhusu CCM na wabunge wao, hilo ni kweli.

Ni CCM pekee ndo waliotufikisha hapa tulipo.

Na umekuwa msimamo wangu wa muda mrefu sasa kwamba CCM wanapaswa kutuomba radhi Watanzania.

Sasa naanza kuona nidhamu inarejea. Uliingia kichwakichwa kujifanya mtetezi wa ccm huku ukijifanya wapinzani wanapinga kila kitu. Saa hii umeujua ukweli umepatwa na aibu ya mwwka. Sikutarajia uongee kwa upole hivi. Ukiacha Tindu Lisu kuongea kwa kejeli lakini kwenye hili yeye ndio yuko sawa. Kuanzia sasa uwe na nidhamu kwani kinachofanywa na awamu hii kuna maigizo mengi kiasi kwamba hujui kipi ni kipi na maisha yamekuwa magumu kwa maelezo matamu. Bwaaahaaaaaaa bwahaaaaahaaa.
 
Wameshatunyonya sana acha mikataba yote irudiwe upya. Na siyo ya madini tu nahisi kwenye gasi ndo kumejaa uozo. Mikataba yote irudishwe bungeni.

Ila wabunge haswa wa CCM hata siwaelewi, ni kama bendera fuata upepo tu. Wao walikaa na kupitisha miswada yote ya madini kwa kura ya ndiyo. Wapinzani walipowapinga wakabakia kuzomea. Sasa hivi walichokuwa wanahoji wapinzani ndo kinawatokea puani.

Tukiacha mihemko na uchama tukaweka nchi yetu mbele nina uhakika kabisa Taifa letu litasonga mbele. Ila kama sheria zitapitishwa tu kwa sababu tunataka ushabiki wa chama chetu ushinde tutatambukia shimoni.

Nakubaliana kabisa Prof Palamagamba alichosema ni vyema tukaenda mbele kwa ujasiri mkubwa na kuangalia upya mikataba iliyowekwa ya madini na kutengeneza mikataba mipya kuliko kuweka mkia katikati ya mapaja.

Liwalo na liwe tu. Ama zao ama zetu. Hata tukiliwa basi tujuwe pia tumejaribu kurudi kwenye mstari ikashindikana na siyo kubakia kulia lia tu.
Ninakubaliana na wewe.

Matatizo haya yametokea ndani ya utawala wa CCM nani lazima wabebe lawama.

Kazi ya CCM kwa sasa ni kujirekebisha baada ya kupewa nafasi ya kuongoza tena taifa.

Kuna baadhi ya watanzania wanasema lazima CCM iombe msamaha kwa kuruhusu hali hii itokee. Nadhani madai yao ni halali lakini ikumbukwe kuwa neno SAMAHANI ni geni katika jamii ya Tanzania achilia mbali siasa za Tanzania. Sioni CCM wakiomba msamaha!
 
Sasa naanza kuona nidhamu inarejea. Uliingia kichwakichwa kujifanya mtetezi wa ccm huku ukijifanya wapinzani wanapinga kila kitu. Saa hii umeujua ukweli umepatwa na aibu ya mwwka. Sikutarajia uongee kwa upole hivi. Ukiacha Tindu Lisu kuongea kwa kejeli lakini kwenye hili yeye ndio yuko sawa. Kuanzia sasa uwe na nidhamu kwani kinachofanywa na awamu hii kuna maigizo mengi kiasi kwamba hujui kipi ni kipi na maisha yamekuwa magumu kwa maelezo matamu. Bwaaahaaaaaaa bwahaaaaahaaa.

Ni wazi hunijui vizuri.

La, una kumbukumbu fupi sana.

Sijawahi hata siku moja kuwa mtetezi wa CCM mimi.

Na sijaanza leo kusema kuwa CCM wanapaswa kutuomba radhi Watanzania.

Nimeshawahi hadi kuanzisha uzi kuhusu hilo.

Nimeshawaponda sana CCM humu. Nimeshawaponda na CHADEMA pia.

Hiyo aibu ya mwaka unayoizungumzia ipo kichwani mwako tu.

Nimeanza kuyazungumzia hayo mambo ya CCM kuwaomba radhi Watanzania zaidi ya mwaka sasa.

Bofya hapo uone

CCM waombeni radhi Watanzania
 
Wengine tulilisema hili Ngosha, kinachosikitisha ni kuwa upinzani ndio tuliamini wanazo gololi za kusimamia mbele ya hawa wakubwa. Sasa sijui wenzetu wangekuwa madarakani wangefanya nini. Sidhani kama hata robo ya kilichofanywa sasa wangethubutu.

Hoja yako ni nini kwenye hili au na ww aibu imekushika kwa kutoamini unachosikia? Ni hivi hili suala kwangu limeingiza siasa kiasi kwamba hata ukweli hausemwi. Leo ripoti za makinikia zimeombwa bungeni zikagomewa. Sasa kama ripoti hata bungeni haipelekwi huoni ni siasa tu hapo? Mzee mwanakijiji kujitosa kwenye hili ni kujidhalikisha tu, kuna taswira inajengwa kwamba kuna uzalendo, lakini ripoti za muhimu zinapogeuzwa ni siri kwenye jambo zito hivi tunaona ni kick za kisiasa tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom