Prof. Kabudi: Watanzania tuache uoga, hakuna atakayeshitakiwa na ACACIA

Hizo ripoti zenyewe mnaficha hata wabunge mnashindwa kuwapa!

Madai mengine ACACIA wametujibu mpaka aibu alafu sijui mnajisifu nini!
Hili jamaa litakupotezea nda bure, waambie watoe ripoti zote 2, vinginevyo this sense ' professorial rubbish ' TL
 
Dollar billion 80 ndizo report za wataalam unaowaamini wewe walitamka, tena wakasema kwa kiwango cha chini. Wewe unasema inaweza kuwa dollar billion 10. Lakini wenye ufahamu wa sekta hii, tunasema kuwa hakuna hata billion moja (1) tutakayoipata. Kama hutaki kuamini, kaa usubiri, muda ni muamuzi mzuri.

Kilichofanywa na kamati ya Mruma ni sawa na kumwambia mtu kuwa kuna mahali umetokea wizi wa tani 500 za sukari. Halafu mtu akaja kukuambia kuwa mwizi tumemkamata akiwa amepakia sukari tani 500 kwenye lorry lake lenye uwezo wa kubeba tani 3. Wenye uelewa watajua ni upuuzi, wajinga watashangilia kuwa kazi kubwa imefanyika kwa kumkamata mwizi na sukari yote iliyoibiwa.
Hii ni shule kubwa sana, I like the logic, sukuri tani 500 imepakiwa kwenye gari la tani 3 lakini bado mazuzu yanashangilia
 
Sasa ndugu yangu JokaKuu, hiyo miswada iliyopelekwa bungeni nayo inahusu hayo mapanki tu?! Punguza mahaba ndugu yangu!

..hapo nilikuwa najibu a specific question.

..ulitakiwa usome kwanza niliyemjibu alikuwa amesema nini.

..kwangu mimi dhararu ni mikataba iliyoko sasa hivi ambayo inatuumiza, siyo miswada iliyopelekwa bungeni.
 
Huyu profesa anajichanganya! Bila shaka amechanganyikiwa! Ni kweli accasia hawawezi kutushitaki kwa sababu tumeamua kutokugusa mikataba yao! Huyu profesa ameshasema sheria MPYA haiwahusu wawekezaji waliopo.
Huyu profesa ninamwuliza kwa nini asiamue kuvunja mikataba yote na accasia kama kweli ana ushahidi kuwa wanatuibia?
Toa kauli ya kuvunja mikataba, hiyo ndiyo kauli pekee inayokubalika!
 
Ni wezi au si wezi??? Do you negotiate with thieves?? Wamesajiliwa au hawajasajiliwa? Do you negotiate with illegal business entities??? Ongeeni vitu vinavyo make sense....
Mbona una hasira sana ndugu?
 
Hilo lipo wazi hatuwezi kushitakiwa kwa kuwa hiyo miswada iliyopelekwa Bungeni haivunji Mikataba mibovu iliyosainiwa hapo awali na mikataba hiyo ndio inayowanufaisha Barik na hao ACACIA bila kusahau na CCM. Kama hiyo miswada ingeonyesha kuvunjwa kwa hiyo mikataba ya zamani sidhani kama huyu Paramagamba angekuja na kauli hii.
TATIZO NYIE KWA KUSHABIKIA UJINGA MNASHINDWA KUELEWA HAYO MAIGIZO YANAYOFANYIKA.
Hujui ukisemacho, subiria matokeo.

Kauli ya yule muoga wa kwanza ilikuwa tutashitakiwa tutashindwa na tutalipishwa mapesa mengi.
 
Ni wezi au si wezi??? Do you negotiate with thieves?? Wamesajiliwa au hawajasajiliwa? Do you negotiate with illegal business entities??? Ongeeni vitu vinavyo make sense....
Inashangaza sana! Mwizi ni wa kupelekwa mahakamani! SAA hii wangekuwa wamesimamishwa kufanya shughuli yoyote maana hawajasajiliwa! Mwizi akiwa anajua amekuibia halafu unataka kujadiliana naye sijui anakuonaje? Accasia walitegemea kushitakiwa, kinyume chake tunataka kujadiliana Nao!
 
Inashangaza sana! Mwizi ni wa kupelekwa mahakamani! SAA hii wangekuwa wamesimamishwa kufanya shughuli yoyote maana hawajasajiliwa! Mwizi akiwa anajua amekuibia halafu unataka kujadiliana naye sijui anakuonaje? Accasia walitegemea kushitakiwa, kinyume chake tunataka kujadiliana Nao!
Siku Brela watakaponionesha usajili wa kampuni ya Coca-Cola au Pepsi ndio nitaamini taarifa ya Prof Mruma. Badala yake utakutana na Kwanza limited, Bonite Botlers na Nyanza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom