Prof. Kabudi: Watanzania tuache uoga, hakuna atakayeshitakiwa na ACACIA

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,976
Hayo yamesemwa na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi wakati akiwasilisha hoja na kujibu maswali mbali mbali kwenye Kamati nne za kudumu za bunge kuhusu miswada mitatu inayohusu raslimali za Taifa.

Prof. Kabudi amesema Serikali sio naive na inafahamu dunia ilivyo kuhusu economic order. Tunajua we are fighting giants but we cannot be afraid of giants. Tunatumia akili nyingi, hekima na busara katika vita hii.

Aliendelea kusema, ‘’We know there will be an attempt to sabotage, definitely na kama tuki-succumb kwamba we are fight a giant busi tukae, tutakuwa hatulitendei haki Taifa’’.

‘’This country has survived sabotage, miaka mingi tu, na sisi lazima tujaribu kuliko kukaa chini na ku-succumb’’ alisema.

Aliendelea kusema‘’Hatuwezi kuwa na wawekezaji ambao hatufaidiki nao nani bora madini tuyaache badala ya kuyachimba ili tusubiri hao kizazi kijacho watakaokuwa na busara na akili kwa sababu sisi tumeshindwa. Madini huwa hayaozi’’

‘’Sheria hii tutakayotunga haiwafukuzi bali inawakaribisha kwa mazungumzo, waje tuongee, tutaelewana na uzuri mambo tunayoyadai yamo ndani ya sheria za kimataifa, hatuyazui wenyewe. Mikataba ya sasa itaangaliwa, tutajadiliana nao. Hatufukuzi mtu na hawawezi kufunga migodi kwa sababu tunafahamu wanapata faida’’.

‘’Yes, we fighting giant, biashara ya dhahabu inafahamika nani ana control lakini huyo giant unapomfikisha anarusha ndege kuja nchini kujadiliana na Rais, hayo ni mafanikio’’

‘’Kama Botswana yenye wananchi milioni 2 inaweza ku-flex its muscles kwenye maliasili zake, sisi Watanzania ambao ni 50 millions, we are lame ducks and toothless bulldog. It's incredible’’.

‘’Tusisahau kuwa nchi hii ime survive kwa vitisho vikubwa kuliko leo. Mwaka 1964, Mwalimu angetetereka kwa Wajerumani waliokuwa wanatupa hela nyingi, akawasikiliza, Tanzania isingekuwepo kama Jamhuri ya Muungano. Kwa msimamo wa Mwalimu, tulipoteza Deutsche Mark milioni 35 lakini Mwalimu akawaambia pack and go’’.

‘’Mwaka uliofuata, 1965 kulitokea Unilateral Declaration of Independence (UDI) in Rhodesia ambapo nchi zote za Afrika zilikubaliana lazima Uingereza imuondoe Prime Minister, Ian Smith ama sivyo nchi zote zitavunja uhusiano wa kibalozi na Uingereza. Baada ya Uingereza kukataa, nchi mbili za Tanzania na Ghana ndizo zilivunja uhusiano wa kibalozi ambapo gharama yake ilisababisha Rais wa Ghana kupinduliwa huku Tanzania tukikosa msaada wa pound milioni 5’’.

‘’Malengo ya mifano yangu sio kwamba turudie hayo bali kuonyesha kuwa Taifa hili limepita vipindi vigumu kwa sababu lilikuwa na uongozi unaothubutu na kusimamia maslahi ya watu ili liweze kuvuka. Hiki ni kipindi kingine cha kuvuka’’.

‘’Tusiogope na kuanza kuulizana kuwa tutaweza au hatutaweza? Wawekezaji watatishia kuwa wataondoka lakini ninasema hawataondoka’’.

Prof. Kabudi amesema watu wa ACACIA kinachowasumbua siyo sheria bali ni integrity yao kwa sababu kampuni inayovunja integrity pledge hupelekea kushitakiwa kwa kosa la fraud. kampuni inayofanya fraud na ikadhibitika kisheria, mali zake hutaifishwa. Hiki kinafanyika hata kwenye nchi zao za Ulaya na Marekani’’.

Alisema, ‘’Ukiona ACACIA wanavyohangaika ambapo mara ya kwanza waliomba kuonana na Rais ambaye maombi yao aliyakataa. Wakaomba tena mara ya pili na kukubaliwa kupitia Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambaye ni mmiliki mkubwa wa hisa 63.9 wa Kampuni ya Acacia Mining, Profesa John Thorton’’.

‘’Kwao integrity ni muhimu sana kutokana na heshima ya kampuni ambayo wajumbe wa bodi ni viongozi wastaafu wenye heshima kubwa duniani’’.

Alimaliza kwa kusema, Watanzania tunatakiwa tujiamini kwa sababu nchi yetu ime train watu wengi katika fani mbali mbali pamoja na fani ya madini lakini tatizo lililopo ni kutowathamini, kuwadharau na kutowatambua. Hatukuwatumia na wameondoka kwenda kusaidia nchi nyingine. Kwa mfano, Nchi ya jirani tunayoisifu kuwa miji yake imepangwa vizuri, wataalam waliochora ramani ya miji hiyo wametoka Tanzania. Director of finance wa Air Tanzania ndio alikuwa Director of finance wa Air Rwanda. Ndiye ameiwezesha Air Rwanda kufika hapo ilipo. Key staff wa Air Rwanda ni Watanzania ambao baadhi yao wamekubali kurudi. Tatizo letu watanzania tunajidharau wenyewe wakati uwezo tunao’’.

Kwa maelezo zaidi angalia video.
 
msomi akishateuliwa serikalini tayari anaacha usomi wake pembeni. anajuaje hatutashitakiwa?
Maelezo ya kwa nini hatushitakiwi yapo kwenye thread.

Nadhani umesoma heading tu na kutoa komenti kama ilivyo kwa baadhi ya Watanzania.

Katika nchi mojawapo yenye wananchi wavivu wa kusoma/kujisomea, Tanzania inaweza kuwa ndani ya kumi bora. Inashangaza mtu akiona andiko lefu anasoma heading na kuanza kutoa komenti/maoni ambapo mara nyingi utakuta ni nje ya mada au hoja zake zinakuwa zimeishapatiwa majibu kwenye thread.

Kinachoshangaza zaidi unakuta komenti wanazotoa ni nusu mstari au mstari mmoja tu.

Mtanzania ukimwaambia aongee bila kuandika, anaweza hata akamaliza siku nzima akiongea lakini maongezi yake mara nyingi ni pumba tupu!

Kwa mtaji huu, inashangaza tunashangaa kwa nini tunasainishwa mikataba mibovu ambayo technicality inakuwa kwenye small print
 
Nakubaliana naye mia kwa mia.

Yaani ukisikia baadhi ya maoni ya watu humu kwa jinsi wanavyoonyesha uoga kisa tu sijui kwenye bodi kuna William Cohen na Newt Gingrich, unabaki unatikisa kichwa tu.

Vyovyote vile itakavyokuwa, the sky won't fall.

Sioni sababu ya kuogopa hususan kama unajua kuwa unachokifanya ni sahihi hata kama huko nyuma kilikosewa.
 
..Prof anatuchezea tu akili zetu.

..sisi ndiyo tunapaswa kuwashtaki acacia MIGA kwasababu tuna ushahidi uliokusanywa na wasomi wetu unaothibitisha kwamba wametuibia.

..negotiations zifanyike baada ya acacia kupatikana na hatia. baada ya hapo watatulipa na tutakuwa ktk nafasi nzuri ya ku-negotiate nao the way forward.

..Again, baada ya ripoti za Prof.Mruma na Prof.Osorro anayepaswa kuogopa miga ni acacia, siyo Tanzania.
 
Yaani tunashindwa vita vya kiuchumi kabla hata ya kuanza mapambano kwa sababu tunatanguliza porojo nyingi na kudhani tunajua wakati hatujui.

Watanzania tunajua sana kuongea lakini kutenda ni zero.
 
Anasema hatuwezi kuwa na wawekezaji ambao hatufaidiki na hapohapo anasema sheria mpya haitekelezwi kurudi nyuma,anataka kutwambia kuwa sheria hii mpya itawafanya wawekezaji waone huruma kutuibia na kuacha wizi kwa hiari yao?
Ni wapi amesema sheria haitekelezwi kurudi nyuma?

Naomba video yake kuhusu madai yako.
 
..Prof anatuchezea tu akili zetu.

..sisi ndiyo tunapaswa kuwashtaki acacia MIGA kwasababu tuna ushahidi uliokusanywa na wasomi wetu unaothibitisha kwamba wametuibia.

..negotiations zifanyike baada ya acacia kupatikana na hatia. baada ya hapo watatulipa na tutakuwa ktk nafasi nzuri ya ku-negotiate nao the way forward.

..Again, baada ya ripoti za Prof.Mruma na Prof.Osorro anayepaswa kuogopa miga ni acacia, siyo Tanzania.
Kama umejua prof. anakuchezea akili, achana naye! Shughulika na hoja za watu wasiokuchezea akili!

Umejuaje kama hatuwezi kuwashitaki iwapo mazungumzo hayatafanikiwa?

Kwa nini unataka negotiations zifanyike baada ya acacia kupatikana na hatia? Kwenye masuala ya madai, hata mahakama huwa zinawaomba wadai wafanye mazungumzo nje ya mahakama kabla ya kushitakiana mahakamani kwa sababu ya kupunguza gharama za mashitaka.
 
Wameshatunyonya sana acha mikataba yote irudiwe upya. Na siyo ya madini tu nahisi kwenye gasi ndo kumejaa uozo. Mikataba yote irudishwe bungeni.

Ila wabunge haswa wa CCM hata siwaelewi, ni kama bendera fuata upepo tu. Wao walikaa na kupitisha miswada yote ya madini kwa kura ya ndiyo. Wapinzani walipowapinga wakabakia kuzomea. Sasa hivi walichokuwa wanahoji wapinzani ndo kinawatokea puani.

Tukiacha mihemko na uchama tukaweka nchi yetu mbele nina uhakika kabisa Taifa letu litasonga mbele. Ila kama sheria zitapitishwa tu kwa sababu tunataka ushabiki wa chama chetu ushinde tutatambukia shimoni.

Nakubaliana kabisa Prof Palamagamba alichosema ni vyema tukaenda mbele kwa ujasiri mkubwa na kuangalia upya mikataba iliyowekwa ya madini na kutengeneza mikataba mipya kuliko kuweka mkia katikati ya mapaja.

Liwalo na liwe tu. Ama zao ama zetu. Hata tukiliwa basi tujuwe pia tumejaribu kurudi kwenye mstari ikashindikana na siyo kubakia kulia lia tu.
 
Kama Raisi alikataa kuonanano sasa mnataka muonaneo nao ili iweje?
Hoja yako imejibiwa hapa;
Alisema, ‘’Ukiona ACACIA wanavyohangaika ambapo mara ya kwanza waliomba kuonana na Rais ambaye maombi yao aliyakataa. Wakaomba tena mara ya pili na kukubaliwa kupitia Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambaye ni mmiliki mkubwa wa hisa 63.9 wa Kampuni ya Acacia Mining, Profesa John Thorton’’.
 
Kama umejua prof. anakuchezea akili, achana naye!

Umejuaje kama hatuwezi kuwashitaki iwapo mazungumzo hayatafanikiwa?

Kwa nini unataka negotiations zifanyike baada ya acacia kupatikana na hatia? Kwenye masuala ya madai, hata mahakama huwa zinawaomba wadai wafanye mazungumzo nje ya mahakama kabla ya kushitakiana mahakamani kwa sababu ya kupunguza gharama za mashitaka.
Hizo ripoti zenyewe mnaficha hata wabunge mnashindwa kuwapa!

Madai mengine ACACIA wametujibu mpaka aibu alafu sijui mnajisifu nini!
 
Nakubaliana naye mia kwa mia.

Yaani ukisikia baadhi ya maoni ya watu humu kwa jinsi wanavyoonyesha uoga kisa tu sijui kwenye bodi kuna William Cohen na Newt Gingrich, unabaki unatikisa kichwa tu.

Vyovyote vile itakavyokuwa, the sky won't fall.

Sioni sababu ya kuogopa hususan kama unajua kuwa unachokifanya ni sahihi hata kama huko nyuma kilikosewa.
Go back home Dude

Swissme
 
Watanzania tunajua sana kuongea lakini kutenda ni zero.

Tunajua sana kuongea, kulaumu, na kunung'unika.

Watu tumelalamika weee...sasa hayo malalamikio yanafanyiwa kazi, watu wanaanza kutetemeka [tena baadhi ya hao wanaotetemeka eti wanajiita sijui wasomi-mawakili]...ooh mmeona waliopo kwenye bodi ya sijui Acacia...mara sijui tutashitakiwa...mara hivi...mara vile!

Okay, fine...but so what?

You would think it's Armageddon the way some of these people tremble in apprehension!
 
Maelezo ya kwa nini hatushitakiwi yapo kwenye thread.

Nadhani umesoma heading tu na kutoa komenti kama ilivyo kwa baadhi ya Watanzania.

Msemaji ukweli sitaki kuamini yale matumaini mliyowapa watu saa mnatuona majuha mnaanza kugeuza hoja ni kutokushitakiwa. Hoja ilikuwa ni kulipwa na wala sio hofu ya kushitakiwa. Mliiaminisha watu tutalipwa 108t, leo mnaanza kutuletea hadithi za kutoshitakiwa? Halafu nimejaribu kufuamfuatilia Kabudi, nimegundua hana jipya, kila mara akiongea anaishia kuongea historia na kiswangilish kisicho na tija lakini hana suluhisho la matatizo ya nchi.

Kwa ufupi huyo huyo Kabudi ni mwalimu wala sio mtu wa kumtegenea kwenye uchumi wetu. Pamoja na maelezo yake yote na kutumia vijimaneno vya kizungu hakuna mahali anapozungumzia hizo hela za malipo zaidi ya kuonyesha hatutashitakiwa. Kwani hao Acacia lengo lao ni kutushitaki? Wao iwapo wataendelea kuvuna hawana muda wa kutushitaki ila iwapo tutawazuia kuvuna wanaweza kutushitaki.

Nimegundua hata hiyo mnayosema sijui hawajasajiliwa Brela si lolote si chochote kwani mpaka sasa Acacia wapo nchini na wanaendelea na kazi zao. Hivi ingekuwa ni kampuni ya mtanzania na haswa mpinzani itamkwe haijasajiliwa leo ingekuwa bado inaendelea kufanya kazi? Tuliaminishwa baada ya wiki hao Barrick wanarudi kuja kujadili kurudisha chetu, mpaka hawajatokea, badala yake tunakimbizana na miswaada ya dharura kumbe hata yenyewe ni ya wawekezaji wapya na wala sio hawa mnaowata wezi. Duuuu aibu gani hii, na kwa kauli hizi sintoshangaa yale macontainer 277 ya makinikia tukalipishwa gharama za kuyazuia.
 
Hoja yako imejibiwa hapa;
Alisema, ‘’Ukiona ACACIA wanavyohangaika ambapo mara ya kwanza waliomba kuonana na Rais ambaye maombi yao aliyakataa. Wakaomba tena mara ya pili na kukubaliwa kupitia Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambaye ni mmiliki mkubwa wa hisa 63.9 wa Kampuni ya Acacia Mining, Profesa John Thorton’’.
Walifanya hivyo kwasababu ya mauzo ya hisa zao yalikuwa yanaporomko na ili kutuliza wana hisa na zaidi walitaka muwape hizo ripoti ambazo mpaka sasa mnazifanya siri(ajabu kabisa)

Kama mliweza kutuambia wamekubali kulipa kitu ambacho si kweli, mtashindwaje kutuambia walikuwa wanawambeleza/wanahangaika?

Mambo ya kuandamana ndio yametudhihirishia mlikuwa mna malengo ya kisiasa maana inashangaza watu wazima wanaandamana kwa jambo ambalo hata bado halijafika mwisho.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom