Prof Kabudi ni hazina kwa taifa letu akiweka siasa za uchawa pembeni

Babyloni

Senior Member
Dec 17, 2020
191
509
Taifa letu limejaliwa kuwa na wabobezi wengi katika nyanja mbali mbali kama siasa, uchumi n.k.

Nikiri kuwa siasa za nchi hii zinawaharibu wataalamu wetu wengi kwa ambao tumebahatika kumfahamu prof Kabudi kabla ya kuingia katika siasa za CCM watakubaliana na mimi kuwa huyu prof ni smart sana na anaweza kulisaidia taifa letu katika mambo kadha wa kadha ya kisheria.

Ombi langu kwako prof Kabudi na wana taaluma wengine tumieni taaluma zenu kulisaidia taifa letu kwa ujumla na sio kwa manufaa ya kikundi cha watu
 
..Prof.Kabudi ana siasa na mitizamo ya kizamani wakati wa vita baridi.

..Pia amechafuka kwa kuwa mtetezi kinara wa utawala wa kikatili wa Magufuli.

..Mimi ningemuona Prof.Kabudi ni hazina na mwenye msaada kwa nchi yetu kama angesimama upande wa HAKI na kupinga udhalimu uliokuwa ukifanywa na Magufuli.
 
Ni kweli ni msomi lakini ana mitizamo ya ajabu na diplomasia hajui. A leader should have moderate views on things.
 
Huyo mzee nilimdharau sana alivyokubali kutumika na Magufuli kama mtu asiye na elimu kabisa. Kitendo cha yeye kutumwa kwenda Madagascar kuchukua dawa ya Covid isiyo na udhibitisho wa kimaabara, kisha akaja kunywa mbele ya wananchi, ile ilikuwa ni hatua ya mwisho kabisa ya kuanika ujinga wake. Halafu akawa anaongea kwa sifa za kijinga, eti huko Madagascar rais ndio anagawa hiyo dawa, akidhani tunaona rais ni cheo cha maana sana.
 
Lakini kitendo cha mbowe kulilia lock down ulikiona Cha kishujaa?
 
Wewe umemjua kabudi juzi labda uyo mzee ni zao la Tanu youth

Alijiweka mbali na siasa baada ya Nyerere
 
Lakini kitendo cha mbowe kulilia lock down ulikiona Cha kishujaa?

Kwa taarifa yako Magufuli pamoja na udhalimu wake na ushenzi wake wote, katika vitu niliona alichukua uamuzi wa maaa ni kutokutuweka lockdown. Na yote hayo nimekiri humu humu jf, sasa ningeionaje msimamo wa Mbowe ni sahihi?
 
Taifa letu limejaliwa kuwa na wabobezi wengi katika nyanja mbali mbali kama siasa, uchumi n.k.

Nikiri kuwa siasa za nchi hii zinawaharibu wataalamu wetu wengi kwa ambao tumebahatika kumfahamu prof Kabudi kabla ya kuingia katika siasa za CCM watakubaliana na mimi kuwa huyu prof ni smart sana na anaweza kulisaidia taifa letu katika mambo kadha wa kadha ya kisheria.

Ombi langu kwako prof Kabudi na wana taaluma wengine tumieni taaluma zenu kulisaidia taifa letu kwa ujumla na sio kwa manufaa ya kikundi cha watu
Watanzani wengi wana sifa kubwa zinazofana bila kujali chama au elimu yao.
1.Kulalamika: happinex index inaonyesha watanzania hawana furaha kwa sababu wanapohojiwa kazi kulalamika tu
2. Kusifia na kupamba bila kujali uhalisia. Waliomsifia sana Magu leo wamemgeukia maza.
3. Uchawa. chunguzeni... hapa lengo ni maslahi binafsi.
4. Unafiki: hii ni tabia hatari sana inayokula taifa letu...
Kwa hiyo kwa vyovyote profesa ameathiriwa na sifa moja au zaidi kati ya hizo na hii inamfanya asiaminike hata kama alifaulu sana kitaaluma.
 
HANA LOLOTE HUYO MZEE MNAFIKI SANA HUYO MZEE WA KANYABOYA hana tofauti na MWEBDAZAKE KWA UONGO
1664915659087.jpg
 
Magu alisema anampigia saa nane za usiku na kumuita Mpumbavu ingawa ananizidi umri

Alishindwa kuacha kazi kulinda heshima yake ila kwa tamaa za madaraka akawa kainama na kukubali kudhalilishwa

Simkubali kabisa wala sipendi mtu anaekubali kudhalilika kisa maslahi yake hata kwa matajiri hivyo hivyo wanawafanyia wajinga na wanakubali kutukanwa na hata kuzabwa makofi kisa anapewa hela
 
Watanzani wengi wana sifa kubwa zinazofana bila kujali chama au elimu yao.
1.Kulalamika: happinex index inaonyesha watanzania hawana furaha kwa sababu wanapohojiwa kazi kulalamika tu
2. Kusifia na kupamba bila kujali uhalisia. Waliomsifia sana Magu leo wamemgeukia maza.
3. Uchawa. chunguzeni... hapa lengo ni maslahi binafsi.
4. Unafiki: hii ni tabia hatari sana inayokula taifa letu...
Kwa hiyo kwa vyovyote profesa ameathiriwa na sifa moja au zaidi kati ya hizo na hii inamfanya asiaminike hata kama alifaulu sana kitaaluma.
Mwana mapinduzi Che Guevara alipata kusema “ its better to die standing than to live kneeling 🧎‍♀️ “
 
Back
Top Bottom