Prof. James Mdoe: Serikali itafanya jitihada za uhamasishaji wa usomaji wa vitabu nchini

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Serikali imesema itafanya jitihada za uhamasishaji wa usomaji wa vitabu nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe wakati akifunga tamasha la 31 la vitabu lililomalizika leo katika viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa sasa ni wakati wa kuendeleza ushirikiano na sekta binafsi ambao ni waandishi na wachapishaji katika kuhakikisha wanarejesha ari ya usomaji wa vitabu nchini.

"Kwa kweli niwapongeze kwa jitahada za kuhakikisha tamasha hili linafanyika japokuwa kuna mapungufu ambayo kwa ushirikiano tutaweza kuyatatua katika matamasha mengine yajayo," amesema Prof. Mdoe.

Prof.Mdoe amesema kuwa utamaduni wa usomaji nchini umeshuka kwa kiasi kikubwa hivyo lazima kuwe na mbinu za kuhakikisha unarejea kama ilivyo kawaida.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Habari na Machapisho Bw. Kwangu Masalu ameshukuru Uongozi wa PATA kuweza kuwashirikisha katika maonesho haya .

Amesema wataendelea kufanya kazi kwa karibu na PATA katika kuhakikisha kazi ya uandishi na uchapishaji inafanyika vizuri kwa weledi.

Maonesho yajayo yatakuwa makubwa ambayo yatasaidia katika uhamasishaji wa usomaji wa vitabu nchini na Watanzania kupata fursa ya kusoma machapisho mbalimbali kutoka kwa wachapishaji binafsi.
IMG-20221016-WA0001.jpg
IMG-20221016-WA0005.jpg
IMG-20221016-WA0002.jpg
IMG-20221016-WA0006.jpg
IMG-20221016-WA0003.jpg
IMG-20221016-WA0004.jpg
IMG-20221016-WA0007.jpg
 
Watu waache kushinda Facebook, Instagram, TikTok, Whatsapp n.k waanze kujikita na mavitabu yenye kurasa kuanzia 100+. Kiufupi, watanzania wa sasa (wengi wao) hawapendi kuuchosha ubongo, kusumbua akili eti Kwa ajili ya kuyafahamu mambo kiundani zaidi. Wanataka posts na comments fupi fupi ili ubongo usichoke.
 
Sharti la kwanza mtu asome kitabu na kukielewa asiwe na stress, lakini kama mtu kichwa kimevurugika anawaza tozo hawezi kushawishiwa asome kitabu akatenda, muhimu kwanza serikali ingejitahidi kupunguza stress walizonazo wananchi wake, ili vitabu vianze kusomwa hata bila kushawishiwa.
 
Back
Top Bottom