Prof Euphrase Kezilahabi: Mwanazuoni anayehitajika kwenye ujenzi wa taifa hili

Mkuu Ukabila huo
 
Namkumbuka sana mwalimu wangu wa shule ya msingi castam mrs mkama ni mkerewe pia naye alikuwa na kipaji cha kutunga mashairi kwa kiwango cha juu
 
Mkuu Ukabila huo
Unanikumbusha tabia za viongozi wa Afrika. Ukimwambia ana akili kuliko raia wote, hufurahi sana ingawa siyo ukweli. Ukisema kweli kwamba anaongoza vibaya au ni dhaifu, nguvu za dola zinakuangukia.

Tukubali, kuna watu wana talents za ziada kuliko wengine.
 
kweli, lakini sio kabila fulani
 
mkuu jinsi ulivyoandika inaonesha wewe sio bora kuliko hao wa shule zetu za kata. hebu angalia ulipoweka hizo brackets zako kama kweli umeelimika.
 
Dah! Jamaa angekua padri sahivi,ila ndo alishatimuliwa bahada ya hapo ikabidi alipize kisasi kwa kutoa kitabu cha Rosa Mistika


Yap, Jamaa angekua padri ila kusoma soma sana kulimfanya akutane na maandishi ya Albert Camus ambayo kwa kiasi kikubwa yalimfanya aanze kujiuliza upya ju ya dhana ya maisha na maana yake.

Lakini kufukuzwa kwake upadri kukawa ni mwanzo wa hisia mpya za kifalsafa.

Ni watu wachache sana wanaothubutu kujaribu kutafuta maana ya maisha, wengi huogopa kwa kushiriki kifo cha kifalsafa.
 
Ukerewe ni kisiwa ambacho kilikuwa na Maprofesa wengi ,akina Prof.Machunda,Prof Makene,Prof Bwahato,hao niliwasikia nikiwa primary
 
Kuna Kezilahabi aliyekuwa idara ya mapato; yule sasa ni marehemu!!
 
Najua wengi mnaikumbuka riwaya ya 'Rosa Mistika' au ile 'Kichwa maji' zilizoandikwa na Profesa Euphrase Kezilahabi.
Mmenikumbusha mbali, enzi za Roza Mistika!. Primari, nilisoma darasa moja na binti yake Regina Kezirahabi, sijui siku hizi yuko wapi?.

Paskali
 
Nilikisoma mkuu Rosa alichaguliwa kujiunga na chuo cha ualimu
 
Siyo kwamba ni kwa sababu ya kanisa katoliki? Maana kanisa lilimjia juu kwa kutumia jina la Rosa Mistika ambalo linamafungamano na Bikira Maria na kwa Tabia za Rosa Mistika wa kitabuni kanisa liliona limechafuliwa na kitabu husika.

Waandishi wa Tanzania hawapo huru hasa wakiligusa tabaka tawala
 
Waandishi wengi wamekimbilia huko kwenye lugha ya picha kuukwepa mkono wa dola siyo Kezilehabi peke yake
 
Yah kwenye litanies ya Bikira Maria Rosa Mistika ni Waridi lenye Fumbo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…