Prof Euphrase Kezilahabi: Mwanazuoni anayehitajika kwenye ujenzi wa taifa hili

Juzi kati nimesoma kitabu chake cha 'Nagona'. Ni kitabu ambacho kimebeba lugha nzito na yenye picha. Huwezi kuelewa kama umetokea shule zetu pendwa za (kata?)....

Zama hizi zimeishiwa watu wa aina yake, naungana na wewe kwamba angekuwepo nchini angeweza kurithisha ujuzi wake kwa kizazi za leo.

Mkuu naomba unitumie hicho kitabu cha Nagona hata kwa pesa nitakinunua. Usisahau pia kama una riwaya yake ya Mzingile
 
You are very very wrong! Prof. Kezilahabi is living. Kulikuwa na Kezilahabi mwingine akiwa Mapato, sijui kama yuko hai. Yaonekana wote ni wakerewe. Kabla ya kukujibu imebidi nimtafute. Wikipedia ina maelezo kidogo lakini muhimu ni update ya May 2015. Kezilahabi yuko hai, ktk umri wa kutosha maana yaonekana amezaliwa 1944. he must be at 71.

btw. Hawa wakerewe siyo ajabu kuwa na ubora wa kiwango hicho. Ni kabila ambalo wako poetic. Bila kujali majivuno ya kila kabila, hawa tuwasifu pale wanapostahili. Yupo mkerewe mwingine alishatoa kitabu chenye juzuu mbili ambacho pia ukikisoma kinatisha! Kinaitwa Myombekere na Bugonoka na Ntulanalwo na Bulihwali . Ni kitabu cha mwaka 1945 na kikachapishwa 1981! Fantastic book. Ongeza na mwingine Gabriel Ruhumbika ambaye nadhani yuko based US. Wote wakitokea kisiwani Ukerewe!

Gabriel Luhumbika yuko Canada
 
Najua wengi mnaikumbuka riwaya ya 'Rosa Mistika' au ile 'Kichwa maji' zilizoandikwa na Profesa Euphrase Kezilahabi.

Lengo la kuleta uzi huu ni kutaka kujua kama kweli Prof huyu alifukuzwa nchini kwa sababu ya kukashifu falsafa na siasa ya ujamaa wa Tanzania kupitia tamthiliya yake ya 'Kaptura la Marx' ambayo kupitia kwayo alijaribu kuonesha kuwa mwalimu alikurupuka kulivaa kaptura la Marx ambalo baadaye lilikuja kumpwaya.

Nasikia Prof huyu nguli wa falsafa za udhanaishi yuko Botswana akifundisha lugha za kiafrika.

Nchi yetu bado imepwaya kwenye maeneo mengi ya taaluma ambayo Prof huyu angeweza kuwa kiraka kama siyo suluhisho kabisa.
bora abaki huko huko ccm hawachelewi kumwekea zengwe kuwa mzimu wa nyerere haumwitaji, tanzania inaongozwa na mzimu huu hivyo mabadiliko hayana nafasi, hata lowasa mziu huu ulimponza
 
Wakuu, nafurahishwa na uchangiaji wenu, unanifunza mengi.

Ila ninachotaka kujua ni kweli Kezilahabi alifukuzwa nchini?
 
Wakuu, nafurahishwa na uchangiaji wenu, unanifunza mengi.

Ila ninachotaka kujua ni kweli Kezilahabi alifukuzwa nchini?

Hakufukuzwa, alistaafu kazi UDSM akaenda kufata GREEN PASTURES Botswana. Alikuwa anarudi na kufundisha kwa muda pale UDSM. Mwaka 2000 alikuja akatufundisha kozi ya Fasihi Simulizi akiwa amealikwa na mwanafunzi wake wa zamani, Prof. Fikeni Senkoro
 
Nimefika ukerewe kipindi flani hivi na kusema kweli kizazi hicho kiliibeba sana ukerewe. Wengine ni kina Profesa Machunda(rip), Yupo Askofu Lukanima (sina kumbukumbu sahihi sana), Pius Msekwa, Getruda Mongela kwa kutaja wachache. Ni kabila lenye watu wa IQ kubwa na ni wasiri sana ndo maana waliaminiwa sana na mwalimu hasa kwenye mambo nyeti hapo namkumbuka Mpambe/Close bodyguard wa mwl nadhani aliitwa Mkanzabi. Wana msemo wao mkelebhe ni mpelhe
 
Najua wengi mnaikumbuka riwaya ya 'Rosa Mistika' au ile 'Kichwa maji' zilizoandikwa na Profesa Euphrase Kezilahabi.

Lengo la kuleta uzi huu ni kutaka kujua kama kweli Prof huyu alifukuzwa nchini kwa sababu ya kukashifu falsafa na siasa ya ujamaa wa Tanzania kupitia tamthiliya yake ya 'Kaptura la Marx' ambayo kupitia kwayo alijaribu kuonesha kuwa mwalimu alikurupuka kulivaa kaptura la Marx ambalo baadaye lilikuja kumpwaya.

Nasikia Prof huyu nguli wa falsafa za udhanaishi yuko Botswana akifundisha lugha za kiafrika.

Nchi yetu bado imepwaya kwenye maeneo mengi ya taaluma ambayo Prof huyu angeweza kuwa kiraka kama siyo suluhisho kabisa.
 
Najua wengi mnaikumbuka riwaya ya 'Rosa Mistika' au ile 'Kichwa maji' zilizoandikwa na Profesa Euphrase Kezilahabi.

Lengo la kuleta uzi huu ni kutaka kujua kama kweli Prof huyu alifukuzwa nchini kwa sababu ya kukashifu falsafa na siasa ya ujamaa wa Tanzania kupitia tamthiliya yake ya 'Kaptura la Marx' ambayo kupitia kwayo alijaribu kuonesha kuwa mwalimu alikurupuka kulivaa kaptura la Marx ambalo baadaye lilikuja kumpwaya.

Nasikia Prof huyu nguli wa falsafa za udhanaishi yuko Botswana akifundisha lugha za kiafrika.

Nchi yetu bado imepwaya kwenye maeneo mengi ya taaluma ambayo Prof huyu angeweza kuwa kiraka kama siyo suluhisho kabisa.

Namkubali sana prof. kezilahabi kitabu chake cha kaptura la Marx kiliondolewa kwenye orodha ya Vitabu vya fasihi mashuleni.
Naomba kuuliza kwa maeneo ya Dar ni bookshops zipi naweza pata kitabu cha kaptura la Marx?
 
Wakuu, nafurahishwa na uchangiaji wenu, unanifunza mengi.

Ila ninachotaka kujua ni kweli Kezilahabi alifukuzwa nchini?

Hapana! Hawezi kuwa amefukuzwa wakati yeye ni mTZ. Hata hivyo aliondoka nchini tukiwa tayari ni vyama vingi, na ukomunisti ukiwa umeanguka. Labda tu tuseme ilikuwa ni kwa mkumbo ule wa waalimu wengi wa UD kuondoka wakifuata maslahi bora. Kumbuka mishahara ya vyuoni ilikuwa hailingani na sifa zao kabisa au jinsi nchi kama Botswana zilivyowathamini watu wa aina yake.

Tumuombe tu aingie JF atuchangamumshe maana baadhi ya hadithi zake! Dah! sijui kama aliwahi shuhudia mambo ya aina hii huku duniani.
 
Mkuu, ndugu yetu hapo juu ametaja jina la kitabu, Nagona.

Pia ameandika kitabu kingine kilicho katika mtindo wa 'novela' kinaitwa 'Mzingire'

Nguli huyu pia ni mshairi mzuri, na ndiye mwalimkuu wa mashairi yasiyo na vina, Masivina.

Ameandika kdiwani ya ushairi inayoitwa 'karibu ndani' katika diwani hiyo Prof Kezilahabi anawaasa washairi wa ushairi wa kimapokeo kujiunga naye katika mashairi yasiyojali ulari wa vina na mizani

Kaka upo vizuri
 
Back
Top Bottom