Mawazo ya Prof. E Kezilahabi kuhusu siasa za Ujamaa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,016
9,885
Kezilahabi amekuwa ni msomi wa zile enzi za Vita baridi (Cold war) wakati ambao wasomi wengi wa afrika walikuwa upande wa UJAMAA, japo baadhi waliamini hawafungamani na upande wowote.

Kutokana na vita ile vijana wengi wa Tanzania na wanaharakati wa enzi hizo walijivika ujamaa kiitikani kuanzia kwenye vyama vya siasa vilivyopigania ukombozi na majina wakajiita MAKOMREDI, Kwa maana ya mtu anayeamini ujamaa. CCM wameendelea kujiita makomredi au kusema wanaamini ujamaa japo hawauishi, ni kwa kuwa TANU ilianzishwa kipindi hiko vita baridi imepamba moto nayo ilijipambanua baadae kuwa inafuata siasa ya ujamaa.

Vitabu vilivyokuwa vinauzika kirahisi kwa kipindi hiko kwa wafrika vilikuwa ni vile vinavyosifia ujamaa, vitabu vya kina Rene Dumont, Paulo Friere na wengineo vilipata kusomwa zaidi na wajamaa waliokuwa wanasoma nje. ukisoma utangulizi wa kitabu cha Pedagogy of the Oppressed cha Paulo Friere kimeandikwa hivyo kwenye utangulizi.

Kwa enzi hiyo ya vita baridi kwa kuwa Afrika ilikuwa ipo katika kundi la oppressed ilitegemewa sana wasomi kuukubali ujamaa, sio ajabu kuona wasomi wengi wa enzi zile kuwa wajamaa na wasikuwa wajamaa kupata masaibu kama ambayo aliyasimulia mmoja kati ya watu ambao hawakuamini ujamaa, Ludovick Mwijage kwenye the dark side of Nyerere.

Wasomi wengi katika harakati walikuja Afrika na Tanzania kwa ujumla ili kuweka mawazo ya kiujamaa kwa waafrika, akiwemo Walter Rodney ambaye amehudumu katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Profesa Euphrase Kezilahabi mbali na kujua kuwa ujamaa ulikuwa ni wa enzi yake, yeye alitumia riwaya, tamthiliya na mashari kwenye kuweka uwazi wa mawazo yake na alionyesha uhalisia wa tabia ya mwanadamu. Kezilahabi hakuwa mfuasi wa ujamaa. na alipoandika kitabu cha Kaptura la Marx, akidhihaki wanaojaribu kuvaa mawazo ya Carl Marx kuwa haliwatoshi, kitabu kile hakikuchapishwa hadi miaka ya 1999.

Siasa ya ujamaa Tanzania, imejadiliwa kwa kina kwenye vitabu vingi vya Kezilahabi, vitabu kama Gamba la nyoka, Dunia uwanja wa fujo na Kaprula la marx vimejadili hayo kwa undani wake.

Kaptula la Marx, ndio tamthliya iliyotamba Zaidi kwa kuonyesha jinsi ujamaa unavyompa mzigo mtu wa chini, mkulima. Lakini pia ujamaa unaamini katika usawa, kitu ambacho Kezilahabi anaamini hakiwezekaniki. Ukisoma maelekezo ya Korchnoi Brown alivyokuwa anamuelekeza raisi Kapera jinsi ya kufika nchi ya Usawa, utaona kitu.

Kuna mara aliwaambia …mtakuta bahari, hakuna mtumbwi wala ngalawa, itabidi muogelee… na sio kama wakimaliza kuogelea watakuwa wamefika usawa. Nadhani Kezilahabi ni kati ya wasomi ambao ile vita baridi haikumgusa moja kwa moja. Na ndio sababu alijiuliza kwenye kitabu cha Nagona kama falsafa zingalipo au tumebaki kuswagwa kwenye madukagati.

Dunia uwanja wa fujo ni riwaya iliyomuonyesha Tumaini alivyomuua Mkuu wa wilaya kwa kutokubaliana na ujamaa, maneno yake alipotembelewa mara ya mwisho alisema “….sijutii, kama nimetenda kosa, vizazi vijavyo vitaamua” stori hii inashabihiana kiasi na stori ya Saidi Mwamwindi aliyemuua Dr. Kleruu, hii yote ni kuonyesha jinsi gani vita baridi iliyopiganwa maktaba na shuleni ilivyoshindwa kuwafikia wananchi, na kuacha wasomi kuwa mstari wa mbele katika sera ambazo wananchi walikuwa hawazielewi.

Gamba la nyoka imeonyesha kwa ujumla jinsi wananchi walivyoamua kupigana na serikali kupinga hiyo kitu iliyoitwa ujamaa, japo walishindwa kwa kuwa nguvu ya serikali ni kubwa. Kupitia Gamba la Nyoka, Kezilahabi anatuambia ujamaa tunao, kwa kuwa tunafahamiana na kujaliana katika matatizo. Na sio kukaa katika vijiji vya ujamaa kunakoweza kufanya watu waweze kujaliana.

Katika kitabu cha mzingile, pia ametaja kidogo kuhusu ujamaa alipoenda kuongea na mzee. Mzee(huyu tutamjadili tukijadili dini) alishangaa kusikia usawa, kwa kuwa sio muundo aliouweka ndio maana alisema “..nyote mu wanyonyaji..” alipoleta mjadala kuhusu hilo mzee alimuuliza kama naye anacheza ngoma yao, hapo alibaki kimya.

Siasa ya ujamaa katika afrika ilikuwa kwa kasi sana kutokana na ile vita baridi, Kezilahabi alilijua hilo, ila kama ilivyo kawaida mtu kutaka kubaki katika comfort zone, wakuu hawakutaka kukosolewa na ndio sababu ya kufukuzana nchini kwa kuwa mtu haamini katika ujamaa wa kukaa katika vijiji nk. Swala la kutokukubali kukusolewa limeonyeshwa kwenye tamthiliya ya Kaptula la Marx.

Kezilahabi, katika vitabu, mzingile na nagona ametumia neno KICHAA kumaanisha mtu wa fikra, lakini kwa kuwa haeleweki na jamii ndio maan ameona atumie neno KICHAA. Katika mzingile anasema “Daima nilitaka kuwa kichaa”

Alipokitaja kitabu cha Karl Marx, Das Kapital, aliandika hivi “kitabu gani hiki? Das Kapital,….wiki moja imepita tangu nianze kukisoma kitabu hiki na wanasema hali yangu nafuu kidogo” hapo anaonyesha katika ukichaa, ukianza kuamini ujamaa kwa enzi zile ndio unaonekana umeanza kuwa vyema. Ilikuwa kawaida kwa SOVIET REGIME kumuita kichaa msomi yeyote asiyeamini ukomunist, nadhani hata jina la ukichaa la Kezilahabi lilitoka huko, na aliona jinsi wasomi wanavyoswagwa kwenye madukagati bila wao kuwa na fikra.

Lakini Kezilahabi anatambua tuna ujamaa ndani yetu kama waafrika, na wala hahitaji kuona unyonyaji uliokithiri, au kuweka pesa mbele dhidi ya utu. Haya utayaona kwenye mzingile. Japo anaonekana kutokuwa muumini wa ujamaa, yapo mambo katika ujamaa ambayo alikuwa anayakubali, kuhusu das kapitali alisema kuna mambo mengi mazuri, lakini falsafa yake inasema …..maisha ni kama mkufu, unachukua kipande hiki na kile unakiunganisha. Kipande kimoja kikikataa unakiacha unatafuta kingine, hicho kitamfaa mwingine……kamwe usitegemee kuokota mkufu uliokamilishwa kwa ajili yako”

Tutaendelea kujadili jinsi Kezilahabi alivyofikiri kuhusu vitu vingine.
Salaam!
 
Asante sana kiongoiz

Similar Discussions

Back
Top Bottom