Prof Euphrase Kezilahabi: Mwanazuoni anayehitajika kwenye ujenzi wa taifa hili

Saint Changas

Member
Dec 19, 2015
24
32
Najua wengi mnaikumbuka riwaya ya 'Rosa Mistika' au ile 'Kichwa maji' zilizoandikwa na Profesa Euphrase Kezilahabi.

Lengo la kuleta uzi huu ni kutaka kujua kama kweli Prof huyu alifukuzwa nchini kwa sababu ya kukashifu falsafa na siasa ya ujamaa wa Tanzania kupitia tamthiliya yake ya 'Kaptura la Marx' ambayo kupitia kwayo alijaribu kuonesha kuwa mwalimu alikurupuka kulivaa kaptura la Marx ambalo baadaye lilikuja kumpwaya.

Nasikia Prof huyu nguli wa falsafa za udhanaishi yuko Botswana akifundisha lugha za kiafrika.

Nchi yetu bado imepwaya kwenye maeneo mengi ya taaluma ambayo Prof huyu angeweza kuwa kiraka kama siyo suluhisho kabisa.
 
Juzi kati nimesoma kitabu chake cha 'Nagona'. Ni kitabu ambacho kimebeba lugha nzito na yenye picha. Huwezi kuelewa kama umetokea shule zetu pendwa za (kata?)....

Zama hizi zimeishiwa watu wa aina yake, naungana na wewe kwamba angekuwepo nchini angeweza kurithisha ujuzi wake kwa kizazi za leo.
 
Juzi kati nimesoma kitabu chake cha 'Nagona'. Ni kitabu ambacho kimebeba lugha nzito na yenye picha. Huwezi kuelewa kama umetokea shule zetu pendwa za (kata?)....

Zama hizi zimeishiwa watu wa aina yake, naungana na wewe kwamba angekuwepo nchini angeweza kurithisha ujuzi wake kwa kizazi za leo.

Naomba jina la kitabu mkuu
 
Hahahhhhaaa
Mbele ya Hukumu: ROSA MISTIKA kwanini umejiua?
Rosa Mistika: Ni kwasababu ya maudhi ya Baba yangu....
Mungu: Nitauuliza Ulimwengu

Hahahhhahaaaaaaaa kitabu kizuri sana sana kiliwahi kupigwa marufuku Tanzania, ukikisoma hutakaa ukiache daima
 
Naomba jina la kitabu mkuu

Mkuu, ndugu yetu hapo juu ametaja jina la kitabu, Nagona.

Pia ameandika kitabu kingine kilicho katika mtindo wa 'novela' kinaitwa 'Mzingire'

Nguli huyu pia ni mshairi mzuri, na ndiye mwalimkuu wa mashairi yasiyo na vina, Masivina.

Ameandika kdiwani ya ushairi inayoitwa 'karibu ndani' katika diwani hiyo Prof Kezilahabi anawaasa washairi wa ushairi wa kimapokeo kujiunga naye katika mashairi yasiyojali ulari wa vina na mizani
 
Ndugu yangu Elli, kwa sasa kwa kweli taifa halina watunzi mahiri wa riwaya. Ni kweli kabisa kama alivyosema hapo juu, ukianza kusoma kitabu hicho, hutakiweka chini hadi umalize kukisoma! Kezilahabi hakika ni moja kati ya watunzi mahiri sana kuwahi kutokea Tanzania.
 
Kama ni mzee kezilahabi ninayemfahamu,Alishafariki kitambo tuu.RIP Mzee Kezilahabi!
 
Euphrase Kezilahabi (born 13 April 1944) is a Tanzanian novelist, poet, and scholar.[SUP][1][/SUP] Born in Ukerewe, Tanganyika (now in Tanzania), he is currently based at the University of Botswana, where he is an Associate Professor at the Department of African Languages.[SUP][2][/SUP]
He writes in Swahili, and has delivered talks on subjects such as 'Aesthetic Ambivalence in Modern Swahili' and 'The Concept of the Hero in African Fiction'.
His works include:

  • Mzingile - 1991
  • Nagona - 1990
  • Karibu Ndani - 1988
  • Rosa Mistika - 1988
  • The Concept of the Hero in African Fiction - 1983
 
Kama ni mzee kezilahabi ninayemfahamu,Alishafariki kitambo tuu.RIP Mzee Kezilahabi!

You are very very wrong! Prof. Kezilahabi is living. Kulikuwa na Kezilahabi mwingine akiwa Mapato, sijui kama yuko hai. Yaonekana wote ni wakerewe. Kabla ya kukujibu imebidi nimtafute. Wikipedia ina maelezo kidogo lakini muhimu ni update ya May 2015. Kezilahabi yuko hai, ktk umri wa kutosha maana yaonekana amezaliwa 1944. he must be at 71.

btw. Hawa wakerewe siyo ajabu kuwa na ubora wa kiwango hicho. Ni kabila ambalo wako poetic. Bila kujali majivuno ya kila kabila, hawa tuwasifu pale wanapostahili. Yupo mkerewe mwingine alishatoa kitabu chenye juzuu mbili ambacho pia ukikisoma kinatisha! Kinaitwa Myombekere na Bugonoka na Ntulanalwo na Bulihwali . Ni kitabu cha mwaka 1945 na kikachapishwa 1981! Fantastic book. Ongeza na mwingine Gabriel Ruhumbika ambaye nadhani yuko based US. Wote wakitokea kisiwani Ukerewe!
 
[h=1]Euphrase Kezilahabi[/h]
euphrase-kezilahabi_285x0.jpg
Euphrase Kezilahabi, Tanzanian poet, novelist, and scholar, is perhaps the most widely known and acknowledged contemporary Swahili author. He was one of the first African writers to publish a collection of free verse poetry in Swahili, and he has had a great impact on the development of the genre of the novel in Swahili.

Kezilahabi was born in 1944 in Namagondo, a village on Ukerewe Island in Lake Victoria. He got his primary and secondary education in Ukerewe, and his BA and MA degrees at the University of Dar es Salaam, completing his MA degree in 1976. Later Kezilahabi continued his studies at the University of Wisconsin, in Madison, USA, finishing his second MA in 1982 and his PhD in 1985. Nowadays Kezilahabi is working as professor of African literature at the University of Botswana.

Kezilahabi's first poem collection, Kichomi (Twinge) was published in 1974. Except for one poem (written in shairi metre) it is written in free verse and with modern content, dealing with topics traditionally regarded as taboos. The publication of Kichomi created a fiery debate on poetry as conservationists and modernists argued over whether free verse poetry can be called Swahili poetry. Traditionally, Swahili poetry was written by native Swahili speakers, Muslims living on the coast of East Africa. Suddenly there were some young university students from interior Tanzania, for whom Swahili was not their mother tongue and who wrote poems in Swahili in a way that no-one had before. The phenomenon was connected to a change in the body of Swahili speakers: instead of the language of a limited Muslim community living on the coast, as it had been, Swahili was becoming the lingua franca of the whole East Africa, spoken by more than one hundred million speakers.
Kezilahabi's further poem collections, Karibu ndani (Welcome Inside, 1988) and Dhifa (Feast, 2008), are also in free verse. Important themes in Kezilahabi's poetry are death, life, existence, silence, and time. He frequently uses onomatopoeia and other sonic devices, drawing influence from the oral literature of his mother tongue, Kerewe.
Kezilahabi's poetry is seminal not only in its form but also in its content, giving voice to new, more individualistic and Western-educated Tanzanians, at the same time being connected to ordinary people due to the usage of Swahili. Kezilahabi's literature is also significant for the way it discusses philosophical ideas and conveys philosophy through fiction.
[h=2]Poems by Euphrase Kezilahabi[/h]
 
[h=3]EUPHRASE KEZILAHABI, KAPTULA LA MARX NA SAFARI YETU YA KUELEKEA NCHI YA USAWA[/h]


  • Kaptula la Marx ni tamthiliya makini dhati iliyoandikwa na Euphrase Kezilahabi (aka Shaaban Robert wa pili) zamani. Inasemekana kwamba tamthiliya hii ilimletea matatizo na ilipigwa marufuku kuchapishwa nchini Tanzania.

  • Baada ya miaka mingi ya ukiritimba wa chama kimoja na udumishaji wa fikra "sahihi" za mwenyekiti wa chama hatimaye tamthiliya hii ilichapishwa mwaka 1999 na Dar es salaam University Press (DUP). Nilifurahi nilipoiona katika maktaba hapa chuoni, nikaiazima na ndiyo tu nimemaliza kuisoma. Sasa najua ni kwa nini tamthiliya hii ilikaa katika makabrasha ya wachapishaji kwa muda mrefu.

  • Katika Kaptula la Marx kuna safari ndefu ya kwenda katika nchi ya ahadi – nchi ya usawa. Safari hii inaongozwa na Rais Kapera akiungwa mkono na mawaziri wake wote. Njia ya kwenda katika nchi ya usawa, hata hivyo, ni nyembamba sana na mawaziri wake ni wanene futufutu kiasi kwamba wanapata shida kutembea katika njia hiyo.

  • Raisi Kapera ameamua kuvaa kaptula kubwa la Marx ambalo kusema kweli halimwenei sawasawa na anaonekana kama kichekesho. Isitoshe, rais huyu pamoja na mawaziri wake hawajui kabisa njia ya kuelekea katika nchi hii ya usawa na hawana ramani. Kwa hivyo wamepotea.

  • Hatimaye linatokea jitu refu pandikizi linalojiita mtu jitu au beberu. Jina kamili la jitu hili ni KORCHNOI BROWN. Rais na mawaziri wake wanaliuliza kama linafahamu njia itakayowafikisha katika nchi ya ahadi – nchi ya usawa. Jitu hili linamhakikishia rais na mawaziri wake kwamba linaifahamu njia hiyo na linawapa maelekezo yafuatayo:
"Mtakwenda! Halafu mtapinda, mtapinda tena, halafu tena mtapinda, mwishowe mtapindapinda hadi mtakapofika mabonde yenye matope. Mtapita katikati ya matope. Halafu milima, halafu misitu yenye miiba hadi mtakapofika jangwani. Kutoka jangwani mtaingia tena bondeni chini kwa chini hadi baharini. Hakuna mitumbwi wala ngalawa. Mtaogelea, ingawa kuna papa wengi. Mkishavuka mtafika nchi iitwayo Svoboda. Kabla ya kuondoka katika nchi hii itawabidi kupambana na majitu yanayofanana na mimi. Mkitoka hapo mtafika kwenye njia nyembamba. (Akiwaonyesha mawaziri) Hawa hawatapita hawa! Njia hiyo itawafikisha katika nchi iitwayo Fraternite. Kutoka Fraternite mtafika Usawa. Ulizeni tu watu watawaonyesha! Mkifika Usawa mtawakuta Waswahili wenzenu wameketi nje ya ikulu ndogo ya Ravensto" Kaptula la Marx (uk). 20)

  • Kwa hivyo usishangae ni kwa nini baada ya miongo mitano ya uhuru bado hatujaifikia nchi ya ahadi. Inavyoonekana safari yetu ya kuelekea katika nchi hii ilikuwa ndiyo-siyo hata kabla haijaanza. Usishangae kama Ujamaa na Kujitegemea bado ndiyo falsafa na dira yetu elekezi ya kutufikisha katika nchi ya ahadi. Usishangae kamaahadi za wanachama wa chama cha Rais Kapera bado ni zile zile. Usishangae kama kinachoropokwa na wenye mikrofoni leo hakifanani na matendo yao. Usishangae kama "fraternite" ya watu wachache wanaofaidi maziwa na asali ya nchi ya usawa "kwa niaba" ya walio wengi inazidi kuimarika na kujitandaza. Usishangae kama (kama anavyosema George Orwell katika riwaya yake ya Shamba la Wanyama), wanyama wote ni sawa lakini wanyama wengine ni sawa kuliko wanyama wengine. Usishangae………..!
*******************************

  • Msikilize Euphrase Kezilahabi hapa chini akisoma mojawapo ya shairi lake; na huyu mwanafunzi akisoma shairi la Chai ya Jioni ambalo limo katika diwani ya Kezilahabi ya Karibu Ndani.
 
Kibanga, naomba ule mstari kwenye 'Kaptula la Marx 'unaosema anaiona/anaikaribia "Egalite"
 
Back
Top Bottom