DOKEZO Prof. Esther William Dungumaro na Ubadhirifu wa Fedha MUCE

DOKEZO Prof. Esther William Dungumaro na Ubadhirifu wa Fedha MUCE

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Sooth

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2009
Posts
3,922
Reaction score
5,626
DNG.png

Profesa Esther William Dungumaro ni Mkuu (Principal) wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa (MUCE). Kwa namna anavyoendesha chuo hiki cha umma, inaleta mashaka juu ya uadilifu wa uongozi wake katika masuala ya fedha. Taasisi za umma zinaendeshwa kwa mpango kazi wa kila mwaka na bajeti ya kila kazi inayopangwa kufanyika ktk mwaka husika.

Kwanini chuo kinashindwa kuwalipa wafanyakazi na watoa huduma wengine kwa zaid ya miez 6, kwa shughuli ambazo ni za msingi kwa taasisi? Unaendeshaje taasisi bila kutenga pesa kwa ajili ya shughuli za msingi za taasisi? Mbona pesa ya kuwakirimu viongozi wa kisiasa wanaokuja Iringa kwa ajili ya masuala yao binafsi anatoa kuanzia pesa mpaka magari?

Hakuna nia ovu katika kuweka wazi jambo hili. Kwakuwa linaathiri taswira ya taasisi ya umma na kushusha morali ya kazi, nashauri viongozi wafuatao wafanye uchunguzi wao kujiridhisha juu ya tuhuma hizi na kuchukua hatua:
  • Makamu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam: Prof. William Anangisye kwa sababu jambo hili linaathiri taswira ya chuo kizima cha UDSM na vyuo vyake vishiriki.
  • Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia: Prof. Adolf Mkenda kwa sababu jambo hili linaathiri ufanisi wa huduma za ufundishaji, utafiti na ushauri kwa jamii.
  • Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali. Kuna ishara za matumizi mabaya ya fedha au matumizi nje ya bajeti inayokuwa imepitishwa. Itakuwa vyema kama CAG atajiridhisha kama pesa ya umma inaenda ktk maeneo yenye tija.
 
duu huyo ESTA anamdomo mzurisana nimevuta picha Fulani itakuwa na mashavu mazuri sana
 
Si kwa maana ya kumtetea, lakini ukweli wa mambo vyuo na taasisi nyingi za Umma ziko taabani kiuchumi.
1. Vyuo kwa kiasi kikubwa vinajiendesha kwa mapato ya ndani ambayo ni ada za wanafunzi. Ada yenyewe ni ndogo mno. Kwa mfano shahada nyingi ziko chini ya shilingi 1,500,000 na haijawahi kupanda kwa zaidi ya miaka kumi. Utaendeshaje taasisi kubwa kama chuo kwa hali kama hiyo?
2. kushindwa kwa serikali kuviendesha hivi vyuo kumesababisha anguko kubwa la vyuo vya Tanzania kwenye redional and global rankings. Wahadhiri wamepoteza morali ya kazi kwa kukosa motisha na malimbikizo ya madai.
wahadhiri hawajihangaishi tena kufanya tafiti na kuchapisha kwenye majarida ya kimataifa (kumbuka university ranking kwa kiasi kikubwa huamuliwa na research publications).
3. swali la kujiuliza: je elimu ya chuo kikuu hapa Tanzania ni kwa ajili ya watu wote? is it universal kama ilivyo elimu ya msingi?.
kwa maoni yangu ni vema serikali ikaacha siasa kwenye elimu. tujikite kwenye quality na sio quantity.
 
Back
Top Bottom