Huyo mama Tibaijuka,katumia ile mbinu ya kisaikolojia tuliyokuwa tunaitumia enzi za utoto wetu, tulipokuwa tunawachokoza wakubwa waliotuzidi umri, na kuwapiga 'mkwara' na kuwaambia kuwa ukinipiga umenionea na ukiniacha umeniogopa!Watanzania wote tunajua kuwa leo ijumaa ni siku ambayo rais Kikwete atazungumza na taifa kukata mzizi wa fitina(hata kama ataumwagilia instead ya kuukata),cha kushangaza na kujiuliza ni kwanini Prof Anna Tibaijuka kaitisha press conference saa chache kabla kuzungumzia tuhuma zake zinazomkabili na kuweka msimamo kuwa hawezi kujiuzulu? kuna nini hapa? alikuwa wapi siku zote toka atuhumiwe? sio kujaribu kumchanganya Kikwete ili abadili msimamo wake alio kuwa nao kwa mtu huyu? NAONA PROF ANNA TIBAIJUKA KAFANYA SHAMBULIO LA KIFIKRA KWA RAIS..
Kumbuka kwamba fedha aliiombea shule akiwa fundraiser wa Barbro Johansson school na hayo yote yapo katika taarifa ya Balozi Rupia. Tusilazimishe tu mambo kwa sababu tunataka kuonekana kwamba tumeshinda. Suala la kumshupalia huyu mama wa watu lina sababu nyingine zaidi ya fedha za shule. Pesa hiyo pia asingeweza kuigawa ienmde popote kwa sababu ni ya shule ya Barbro na aliikabidhi kama lilivtotakiwa. Tuache ushabiki ambao hautusaidii lolote.Mama kwa nini hakupeleka angalau kahela ka ugoro kwenye jimbo lake kuchangia zile shule maarufu za kata?
Ningemuheshimu sana na kumuona wa maana sana kwenye elimu.
Lakini kusema yeye amefanya kazi Umoja wa Mataifa so what? Yaani huko UN ni kama mbinguni kuko kusafi kabisa?
Na zile issues za procurement kwenye idara yake aliyokuwa anaongoza vile ziliishia vipi?
Kwanza waTZ lazima tujiulize swali moja la msingi, ni kwa nini wale wote waliohusika na wizi huu wa kutisha wa mabilionii ya Escrow, wamekuwa na kiburi cha hali ya juu, kugoma kata kata kuwajibika na kujiuzulu nyadhifa zao?"Sijiuzulu ng'oo, na akinifukuza nitasema kuhusu nani hii .......... Shauri yenu "
View attachment 212062
View attachment 212063
Kwa hiyo!!!?
Tatizo ni kwamba Kikwete haheshimiwi kabisa na subordinates wake ndio sababu mama fisadi Tibaijuka kathubutu kuitisha mkutano na waandishi wa habari na kuongea kwa kuonyesha kiburi cha hali ya juu siku moja kabla ya Mkuu wake wa kazi kulihutubia Taifa kuhusu issue ambayo huyu mama fisadi Tibaijuka anahusika. Huwezi ukapokea mali ya wizi kisha kutaka kujifanya wewe ni mtakatifu. Je, alipopokea hii pesa alimtaarifu Mkuu wake wa kazi kwamba amepokea karibu bilioni 2 toka kwa Ruge? Je, alieenda Tume ya maadili ya viongozi kutoa taarifa kwamba amepokea pesa nyingi toka kwa Ruge kama zawadi/ruzuku!? Kwanini aliamua kumficha Mkuu wake wa kazi au Tume ya maadili kuhusu kupokea pesa hizo!?
Huyu mama fisadi Tibaijuka ni mwizi, ukiachilia mbali tuhuma za kupokea pesa chungu nzima za wizi pesa ambazo ni za walipa kodi, pia ana tuhuma nyingine za kujipatia viwanja mbali mbali nchini na kisha kuviuza kwa mwendo wa kuruka. Huyu mama hastahili kuendelea kuwemo ndani ya baraza la mawaziri kama walivyo mawaziri wengi kwenye baraza hilo.
Ufukuzwe uwaziri mara moja.
Kasema yeye na Muhongo ni majembe ya Mh. Rais Dr.JK. Na wanategemewa sana.