Prof. Anna Tibaijuka atolea Ufafanuzi sakata la Escrow, agoma Kujiuzulu

Watanzania wote tunajua kuwa leo ijumaa ni siku ambayo rais Kikwete atazungumza na taifa kukata mzizi wa fitina(hata kama ataumwagilia instead ya kuukata),cha kushangaza na kujiuliza ni kwanini Prof Anna Tibaijuka kaitisha press conference saa chache kabla kuzungumzia tuhuma zake zinazomkabili na kuweka msimamo kuwa hawezi kujiuzulu? kuna nini hapa? alikuwa wapi siku zote toka atuhumiwe? sio kujaribu kumchanganya Kikwete ili abadili msimamo wake alio kuwa nao kwa mtu huyu? NAONA PROF ANNA TIBAIJUKA KAFANYA SHAMBULIO LA KIFIKRA KWA RAIS..
Huyo mama Tibaijuka,katumia ile mbinu ya kisaikolojia tuliyokuwa tunaitumia enzi za utoto wetu, tulipokuwa tunawachokoza wakubwa waliotuzidi umri, na kuwapiga 'mkwara' na kuwaambia kuwa ukinipiga umenionea na ukiniacha umeniogopa!
 
Mama kwa nini hakupeleka angalau kahela ka ugoro kwenye jimbo lake kuchangia zile shule maarufu za kata?

Ningemuheshimu sana na kumuona wa maana sana kwenye elimu.

Lakini kusema yeye amefanya kazi Umoja wa Mataifa so what? Yaani huko UN ni kama mbinguni kuko kusafi kabisa?

Na zile issues za procurement kwenye idara yake aliyokuwa anaongoza vile ziliishia vipi?
Kumbuka kwamba fedha aliiombea shule akiwa fundraiser wa Barbro Johansson school na hayo yote yapo katika taarifa ya Balozi Rupia. Tusilazimishe tu mambo kwa sababu tunataka kuonekana kwamba tumeshinda. Suala la kumshupalia huyu mama wa watu lina sababu nyingine zaidi ya fedha za shule. Pesa hiyo pia asingeweza kuigawa ienmde popote kwa sababu ni ya shule ya Barbro na aliikabidhi kama lilivtotakiwa. Tuache ushabiki ambao hautusaidii lolote.
 
Tatizo ni kwamba Kikwete haheshimiwi kabisa na subordinates wake ndio sababu mama fisadi Tibaijuka kathubutu kuitisha mkutano na waandishi wa habari na kuongea kwa kuonyesha kiburi cha hali ya juu siku moja kabla ya Mkuu wake wa kazi kulihutubia Taifa kuhusu issue ambayo huyu mama fisadi Tibaijuka anahusika. Huwezi ukapokea mali ya wizi kisha kutaka kujifanya wewe ni mtakatifu. Je, alipopokea hii pesa alimtaarifu Mkuu wake wa kazi kwamba amepokea karibu bilioni 2 toka kwa Ruge? Je, alieenda Tume ya maadili ya viongozi kutoa taarifa kwamba amepokea pesa nyingi toka kwa Ruge kama zawadi/ruzuku!? Kwanini aliamua kumficha Mkuu wake wa kazi au Tume ya maadili kuhusu kupokea pesa hizo!?

Huyu mama fisadi Tibaijuka ni mwizi, ukiachilia mbali tuhuma za kupokea pesa chungu nzima za wizi pesa ambazo ni za walipa kodi, pia ana tuhuma nyingine za kujipatia viwanja mbali mbali nchini na kisha kuviuza kwa mwendo wa kuruka. Huyu mama hastahili kuendelea kuwemo ndani ya baraza la mawaziri kama walivyo mawaziri wengi kwenye baraza hilo.
 
"Sijiuzulu ng'oo, na akinifukuza nitasema kuhusu nani hii .......... Shauri yenu "
ImageUploadedByJamiiForums1418939623.396466.jpg
ImageUploadedByJamiiForums1418939891.268884.jpg
 
"Sijiuzulu ng'oo, na akinifukuza nitasema kuhusu nani hii .......... Shauri yenu "
View attachment 212062
View attachment 212063
Kwanza waTZ lazima tujiulize swali moja la msingi, ni kwa nini wale wote waliohusika na wizi huu wa kutisha wa mabilionii ya Escrow, wamekuwa na kiburi cha hali ya juu, kugoma kata kata kuwajibika na kujiuzulu nyadhifa zao?

Lakini kutokana na picha hiyo ambayo mkulu anaonenekana yupo 'beneti' na bilionea Ruge, ni ushahidi tosha wa mazingira kuwa ukwapuaji huu wa Escrow ulikuwa na 'kolabo' ya prominent figures wengi ndani ya nchi hadi ndani ya Magogoni!

Kwa hiyo ni kama vile akina mama Tiba wanajisemea kimoyomoyo kuwa wewe mkulu ukiamua kumwaga ugali nasi tutalazimika kumwaga mboga!
 
Mama ana uso wa kauzu kweli ,halafu nao wandishi wa habari wetu hata kumuuliza maswali ya msingi hakuna halafu wengiwa hao waandishi nikama wameokotwa pale nje kuwa jamani njoo mjaze ukumbi kuna soda na vipapatio vya bure,nyingi ya sura zile sio za waandishi wa habari.
 
Naona mama anatafuta sympathy kwa wanahabari akubali kosa aachie ngazi kwani waliopita mbona walijiudhuru kwani walikosea moja wa moja kwa mfano waziri mkuu mstaafu Lowasa na wengine weengi tu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kikwete ashitakiwe haraka sana na akibainika kafanya huu uhuni basi arudishe hizo hela na kunyongwa ili tuweke historia na fundisho kwa marais wengine watakaokuja hapo baadaye.
 
Naona kafanya hivyo kwa maagizo ya prof J.K kwamba aanze kutoa ufafanuzi halafu yeye atamalizia.
 
Tatizo ni kwamba Kikwete haheshimiwi kabisa na subordinates wake ndio sababu mama fisadi Tibaijuka kathubutu kuitisha mkutano na waandishi wa habari na kuongea kwa kuonyesha kiburi cha hali ya juu siku moja kabla ya Mkuu wake wa kazi kulihutubia Taifa kuhusu issue ambayo huyu mama fisadi Tibaijuka anahusika. Huwezi ukapokea mali ya wizi kisha kutaka kujifanya wewe ni mtakatifu. Je, alipopokea hii pesa alimtaarifu Mkuu wake wa kazi kwamba amepokea karibu bilioni 2 toka kwa Ruge? Je, alieenda Tume ya maadili ya viongozi kutoa taarifa kwamba amepokea pesa nyingi toka kwa Ruge kama zawadi/ruzuku!? Kwanini aliamua kumficha Mkuu wake wa kazi au Tume ya maadili kuhusu kupokea pesa hizo!?

Huyu mama fisadi Tibaijuka ni mwizi, ukiachilia mbali tuhuma za kupokea pesa chungu nzima za wizi pesa ambazo ni za walipa kodi, pia ana tuhuma nyingine za kujipatia viwanja mbali mbali nchini na kisha kuviuza kwa mwendo wa kuruka. Huyu mama hastahili kuendelea kuwemo ndani ya baraza la mawaziri kama walivyo mawaziri wengi kwenye baraza hilo.

Naskia ana bifu na Mchechu (NHC) kwasababu alilazimisha dili lake dogo akacheua
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kasema yeye na Muhongo ni majembe ya Mh. Rais Dr.JK. Na wanategemewa sana.

Ukiniambia anategemewa kwenye kupanga madili ya kuiaba pesa nitakubaliana naye. Lakini kama ni wizara kuna majembe kibao. Huyu mama ni mzigo mkubwa katika nchi hii kiburi kitamuisha
 
kasema yupo tayari kurudisha fedha alizochukua, uwaziri mtamu bwna....akikumbuka king'ora!
 
Nakumbuka msamiati mpya uliletwa na Dr Mwakyembe wakati wa Richmond, nao ni "ujasiri wa kifisadi." Ati Waziri anatajwa kuhusika na kashfa ya wizi wa fedha za umma, iwe kweli ama si kweli, lakini kitendo cha kuitisha mkutano na waandishi wa habari na kutamka waziwazi mimi sijiuzulu ati kwa kufanya hivyo Rais (aliyemteua) atamshangaa sana. Ati yeye ni mwaminifu hivyo hawezi kujiuzulu. Ati yeye aliwahi kuwa boss huko UN na akijiuzulu lazima aende New York kuwaeleza (uuuuuwi!!!). Mungu wangu Tanzania imefika pabaya. Jeuri ya huyu mama Tibaijuka inatoka wapi? Hakuna anayesema Prof Tibaijuka kaiba bali mazingira ya uchotwaji wa fedha za Escrow na hatimaye kugundulika kwamba naye alinufaika kumempaka matope, kama mtu wa kimataifa kama anavyodai, ni vyema kuwajibika. Tabia hii inapandisha hasira wananchi na hata wana CCM wenyewe. Prof Tiba, umeonyesha kiwango cha juu sana cha utovu wa nidhamu na dharau kwa Rais wako na watanzania. Au alitumwa na JK? Hakika huu ni ujasiri wa kifisadi!
 
Back
Top Bottom