Prof. Anna Tibaijuka atolea Ufafanuzi sakata la Escrow, agoma Kujiuzulu

Kilaza

JF-Expert Member
Feb 28, 2013
3,324
1,377
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka, leo Alhamisi atarajia kukutana na waandishi wa habari saa tano asubuhi katika hoteli ya Grand Hyatt (Kilimanjaro).

Taarifa zilizothibitishwa na Prof Tibaijuka mwenyewe, zinasema waziri huyo atazungumzia ukwapuaji wa mabilioni ya Sh. Katika akaunti ya Escrow na jinsi anavyohusishwa kunufaika nayo.

"Ni kweli nimelekeza wasaidizi wangu wizarani waniandalie mkutano na waandishi, ninataka kuzungumzia kwa kina, tuhuma ninazohusishwa kuhusu mimi kunufaika na fedha zenye utata kwente akaunti ya Escrow," alieleza Prof. Anna Tibaijuka kwa njia simu.

Prof. Anna Tibaijuka hakutaka kuingia kwa undani kuzungumzia juu mapendekezo ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyotaka kujiudhuru wadhifa wake wa uwaziri.

Aliishia kusema, "Wewe si mwandishi? Si umenusa na ukajua kuwa nina mkutano na waandishi habari kesho? Subiri mambo yatajulikana hapo," alisema Prof. Anna Tibaijuka huku akicheka.

Mytake:naona mzee wetu muheshimiwa kuliko wote Tanzania ameshakuwa mtaalamu wa "chenga za mwili"kwasababu na yeye yupo kwenye mgao wa mlungula hivyo hawezi kuwafukuza kazi lakini alishajadiliana nao hivyo alivyotuambia "nitawawajibisha kwanzia wiki ijayo" wewe ulidhani atawawajibishaje???? ndio hivyo sasa

Swali lililobaki ni je, mama Tibaijuka atafuata nyayo za Werema?

=================================


UPDATES
attachment.php

Prof. Anna Tibaijuka akiwa kwenye Press Conference Hyatt Regency Hotel Dar es Salaam leo


-Anatolea ufafanuzi wa Msaada wa fedha uliotolewa na Rugemalira kwenye Shule yake

-Anasema watu wanaona kujiuzulu ni 'fashion' ila yeye hayuko katika 'fashion' hiyo

-Nikijiuzulu hata Rais atanishangaa maana katika yale mapendekezo ya Bunge hakuna sehemu iliyonitaka kujiuzulu.

-Amesema kaja kufafanua sakata, hawezi Kujiuzulu

-Lengo la kuzungumza na Waandishi wa habari ni kuzungumza yale niliyokosa nafasi ya kujitetea wakati wa sakata la TegetaEscrow

-Yeye aliomba mchango wa Shule, akijiuzulu anasema atakuwa hajaitendea haki jamii

*Hajajiuzulu na sasa ni kipindi cha maswali na Majibu


SIKU chache kupita baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema kumwandikia Barua Rais Jakaya Kikwete ya Kujiuzulu na Rais kuridhia kujuzulu kwake na kumshukuru kwa kazi aliyofanya.

Naye Waziri Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka amekuja Juu na kuwavaa wanaotaka yeye ajiuzulu na kusema hawezi kufanya hivyo kutokana na kutohusika katika wizi huo.

Na kusema pesa alizopewa zaidi ya Bilioni 1.6 na Mbia wa Kampuni ya IPTL bwana James Rugemarila ilikuwa kwa ajili ya kusaidia kuboresha elimu ya mwanamke na kumkomboa kutoka kwenye hali duni ya elimu.

Kauli hiyo ambayo imekuwa ni Tofauti na Matarajio ya Wengi imetolewa Mda leo jijini Dar Es Salaam na Waziri huyo wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka wakati wa mkutano na waandishi wa Habari Pamoja na Mambo Mengine Waziri Tibaijuka akizungumza kwa uchugu alisema hawezi kujiuzulu kutokana na yeye kutohusika katika ufisadi huo.

"Mimi Nijiuzulu kwa sababu gani? yaani kwa sababu ya mafanikio ya kuwakomboa wanawake kwenye Elimu ndio mimi nijuzulu,maana kujiuzulu kunasababu, na hakuna sababu ya mimi kufanya hivyo na sitofanya hivyo kwani wanaodai mimi nijiuzulu ni wanafiki wenye nia mbaya na mimi ,na mimi sijiuzulu ng'o na nikifanya wanavyotaka Rais atashangaa "alisema Waziri Tibaijuka.

Waziri Tibaijuka aliongeza kuwa madai anayodaiwa kupewa pesa zaidi ya Bilioni 1.6 na Mbia wa Kampuni ya IPTL bwana james Rugemalira ilikuwa kwa ajili ya kuinua elimu ya wanawake kwa kuikomboa shule ya Barbro Johansoon ambapo waliochangia kwenye Shule hiyo ni wengi kuliko bwana James Rugemalira.

"Leo natuhumiwa na kila mtu kwamba nimepewa pesa na Rugimalira kwamba ni za kifisadi,Jamani tuwe wa kweli kuhusu madai haya maana nimepewa pesa na Rugemalira kwa ajiri ya shule hizi na sio huyo pekee alliyechangia kwani waliochangia pesa hizi ni watu wengi ikiwema Rais wa Awamu ya Tatu,Benjamin Mkapa,Mfanya Biashara Maarufu Reginald Mengi na wengine wengi,inakuwaje leo mchango wa Rugumarila kwa Ajiri ya Elimu kwenye Shule hii ndio iwe nongwa"

"Kwasababu ukisema ni pesa alizonipa ni za ufisadi wa Escrow sio kweli,kwani Bodi ya Shule ilimuomba Bwana Rugemalira pesa kwa kutumia Kampuni yake ya Mabibo Wine na kipindi kile ndio alikuwa kiongozi, sasa hawa watu wanaozani ni za ufisadi inakuwaje jamani tuwe wakweli"Aliongeza Waziri Tibaijuka.

Waziri Tibaijuka akiongea kwa uchungu huku kama akitaka kulia alivishangaa vyombo vya Habari hususani Magazeti kumtuhumu kana kwamba ndio Mhusika wa Ufisadi wa Escrow

"Taifa la Ujerumani liliteketea kwa Uwongo uliokuwa ukienezwa,na Tanzania ndio tunaelekea huko yaani Magazeti yananituhumu mimi kwamba mimi ni mhusika wa Escrow,hivi haya Magazeti yana nini jamani hivi kweli huyo ni Mwandishi wa Habari kweli,na gazeti linaandika Escrow ya Tibaijuka,hivi msaada wangu wa kuwakomboa Wanawake kielimu ndio imekuwa haya jamani mbona hatuna hofu ya Mungu?"alihoji Waziri Tibaijuka.
 

Attachments

  • tiba.jpg
    tiba.jpg
    27.4 KB · Views: 30,839
Huyu mama anapenda sana madaraka tusitarajie kujiuzulu, huyu mama ana mdomo mrefu nakusudia ni muongeaji na mtaalam wa kupanga maneno na kujaribu kupangua hoja. Labda tumtegemee JK kwa huyu mama kuwajibika otherwise yeye kama yeye never..
 
Mkutano umeandaliwa na wasaidizi wa wizara je ni mkutano wa kikazi au binafsi,

Kama ni wa kikazi ina maana anaitetea wizara kupewa 1.6b na Rugemarila,
kama ni wa binafsi nani atalipa gharama na kwa nini uandaliwe na wizara.

Huu ni mwendelezo wa matumizi mabaya ya ofisi ya umma.
 
Naona safari hii upepeo umekuwa mbaya!
Wamesubiri kupima upepeo sasa mmoja anajitosa baharini ilikumsefu nahodha na chombo cake wasizame.Lakini meshasababishia madhara chombo kwa kuitoboa toboa na bado safiri ni mdefu mpaka chombo kitie nanga 2015 ,chombo kitakuwa kimezama jumla na nahodha.
 
Huyu mama anapenda sana madaraka tusitarajie kujiuzulu, huyu mama ana mdomo mrefu nakusudia ni muongeaji na mtaalam wa kupanga maneno na kujaribu kupangua hoja. Labda tumtegemee JK kwa huyu mama kuwajibika otherwise yeye kama yeye never..

kuna taarifa jk aliwaomba sana wajiuzulu wenyewe ameanza werema nadhani huyu anafwata
 
wanacheza na kafulila? wallahi wataisha wote, na maumivu lazima yamfikie mkuu wa kaya
 
wanacheza na kafulila? wallahi wataisha wote, na maumivu lazima yamfikie mkuu wa kaya
kaka ogopa haya maneno :Namwachia Mungu: wananchi walisimama na kusema hayo maneno sasa ndo mambo yanatokea.Kama ulishuhudia uchaguzi wa serikali za mitaa watu walionyesha walichokuwa wanataka kuonyesha.
 
Lazima ajiuzulu, anajikaza kibibi bomba, akileta za kuleta nguvu ya umma inamwondoa, kibibi bomba jiizi sana hiki....fisadi jike..angefaa kunyongwa kabisa...!!
 
Lazima ajiuzulu, anajikaza kibibi bomba, akileta za kuleta nguvu ya umma inamwondoa, kibibi bomba jiizi sana hiki....fisadi jike..angefaa kunyongwa kabisa...!!

mkuu una hasira nini shida ...!!! hivi kweli bado ujazoea EPA RICHMOND RADA BUZWAGI ...etc hili dogo tu kibillioni 360 kinakupa presha....mbona ni vijisenti tu hivyo wala usikasirike..
 
Back
Top Bottom