Mnyonge Namba1
JF-Expert Member
- Jan 27, 2012
- 402
- 81
Katika hali ambayo vibaraka wa ccm hawataweza kuipotosha na CD zao za Udini na Ukabila, jana Prof aliudhihirishia umma wa Watanzania na dunia kuwa, kwenye harakati za ukombozi wa nchi kupitia M4C sisi sote ni ndugu, tatizo ni ccm peke yake kwa mustakabali wa taifa hili na watu wake.
Utayarishaji wa kesi ya kupinga Ushindi feki wa Dr. Kafumu Igunga, ufuatiliaji na usimamiaji wa hoja zote za kesi hii ulifanywa kizalendo sana na Prof Safari.
Bila shaka CCM watakuwa walijaribu kumshawishi Prof kwa sera zao za Ukabila na Udini au kumpa rushwa ili alegeze kamba lakini Prof aliamua kuupuuza ujinga wao, akafuata njia iliyosahihi na ya haki, kwa sababu anaipenda nchi yake na watu wake, lakini zaidi anakipenda chama chake cha CHADEMA. Ndiyo maana jana na leo tunasherehekea nchi nzima ushindi wa haki dhidi ya dhuluma jimbo la Igunga.
Wito wangu kwa Watanzania wote wanaopotoshwa na ccm kwa sera yao ya Ukabila na Udini au fedha, wapuuzeni hao ccm na muwe wazalendo wa kweli kama Prof. Safari ili sote kwa pamoja tuikomboe nchi yetu mapema iwezekanavyo.
!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! SISI SOTE NI NDUGU, TATIZO LETU SUGU NI CCM !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!