Prof. Abdallah Safari, uzalendo wako ni wa kupigiwa mfano ndani ya CHADEMA

Katika hali ambayo vibaraka wa ccm hawataweza kuipotosha na CD zao za udini na ukabila, jana Prof aliudhihirishia umma wa wa watanzania na dunia kuwa, kwenye harakati za ukombozi wa nchi kupitia M4C sisi sote ni ndugu, tatizo ni ccm pekee yake kwa mustakabali wa taifa hili na watu wake.
Utayarishaji wa kesi ya kupinga Ushindi feki wa Dr. Kafumu Igunga, ufuatiliaji na usimamiaji wa hoja zote za kesi hii ulifanywa kizalendo sana na Prof Safari.

Bila shaka CCM watakuwa walijaribu kumshawishi Prof kwa sera zao za ukabila na udini au kumpa rushwa ili alegeze kamba lakini Prof. aliamua kuupuuza ujinga wao, akafuata njia iliyosahihi na ya haki, kwa sababu anaipenda nchi yake na watu wake, lakini zaidi anakipenda chama chake cha CHADEMA. Ndiyo maana jana na leo tunasherehekea nchi nzima ushindi wa haki dhidi ya dhuluma jimbo la Igunga.

Wito wangu kwa Watanzania wote wanaopotoshwa na ccm kwa sera yao ya Ukabila na Udini au fedha, wapuuzeni na muwe wazalendo wa kweli kama Prof. A.Safari ili sote kwa pamoja tuikomboe nchi yetu mapema iwezekanavyo.



!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! SISI SOTE NI NDUGU, TATIZO LETU SUGU NI CCM !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


Well spoken; A Big up Prof Safari, you have shamed the devil.
 
Bila shaka CCM watakuwa walijaribu kumshawishi Prof kwa sera zao za Ukabila na Udini au kumpa rushwa ili alegeze kamba lakini Prof aliamua kuupuuza ujinga wao, akafuata njia iliyosahihi na ya haki, kwa sababu anaipenda nchi yake na watu wake, lakini zaidi anakipenda chama chake cha CHADEMA. Ndiyo maana jana na leo tunasherehekea nchi nzima ushindi wa haki dhidi ya dhuluma jimbo la Igunga.
Binafsi namwamini sana Prof. Safari kwani ni mtu makini, asiye na papara, mwaminifu, anayeichukia dhulma kwa dhati, mwenye mapenzi ya kweli kwa imani yake na nchi yake na si mnafiki. Natamani angekuwa mbunge wa jimbo fulani nina uhakika angelichangamsha sana bunge kwa hoja zake zisizo za kinafiki na kujipendekeza kwa watawala. CHADEMA ina kila sababu za kujivunia timu yake wa wapiganaji wenye weledi, makini na wenye mtazamo wa mbali tofauti na wenzao ambao kwa bahati mbaya wamesheheni watu wanaotumia matumbo kufikiri na kuamua!
 
Baba Prof Journey, you have shown us a rightous way to follow our journey!!!!!!!!
 
Katika hali ambayo vibaraka wa ccm hawataweza kuipotosha na CD zao za Udini na Ukabila, jana Prof aliudhihirishia umma wa Watanzania na dunia kuwa, kwenye harakati za ukombozi wa nchi kupitia M4C sisi sote ni ndugu, tatizo ni ccm peke yake kwa mustakabali wa taifa hili na watu wake.
Utayarishaji wa kesi ya kupinga Ushindi feki wa Dr. Kafumu Igunga, ufuatiliaji na usimamiaji wa hoja zote za kesi hii ulifanywa kizalendo sana na Prof Safari.

Bila shaka CCM watakuwa walijaribu kumshawishi Prof kwa sera zao za Ukabila na Udini au kumpa rushwa ili alegeze kamba lakini Prof aliamua kuupuuza ujinga wao, akafuata njia iliyosahihi na ya haki, kwa sababu anaipenda nchi yake na watu wake, lakini zaidi anakipenda chama chake cha CHADEMA. Ndiyo maana jana na leo tunasherehekea nchi nzima ushindi wa haki dhidi ya dhuluma jimbo la Igunga.

Wito wangu kwa Watanzania wote wanaopotoshwa na ccm kwa sera yao ya Ukabila na Udini au fedha, wapuuzeni hao ccm na muwe wazalendo wa kweli kama Prof. Safari ili sote kwa pamoja tuikomboe nchi yetu mapema iwezekanavyo.



!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! SISI SOTE NI NDUGU, TATIZO LETU SUGU NI CCM !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Nakubaliana na wewe ya kwamba huwezi kuwa MZALENDO ama kudai Uzalendo kama utapingana na jitigada za chama cha CDM ktk kumkomboa Mtanzania. Lakini fahamu ya kwamba Uzalendo unatokana na imani ya Utaifa wetu kwa kuenzi tamaduni na mila zetu. Hivyo yule mkristu aliyeko Chadema lakini anapingana na tofauti zake na Waislaam ktk ujenzi wa Tiafa hili huyu sii Mzalendo..

Kama unakataa kumsikiliza Muislaam kwa sababu za kiimani huo Uzalendo wako ni fake, sawa na yule anaye tangaza tofauti hizi kujenga hoja. Bora wale wanaopiga makelele ya kulaani vitendo viovu vya Udini wanakuwa sii wadini wabaya, kuliko yule anayekaa kimya lakini anaamini dini na kabila yake ni bora zaidi ya mwingine. Uzalendo huu sisi wengine utatushinda maana kila siku hapa JF matusi ni kwa waislaam lkn tunaambiwa ndio Uzalendo...

Hapana haikubaliki, ikiwa vijana wa Chadema wanaamini ktk Usawa (equal opportunity) kwa nini wanapingana na madai ya Waislaam wanapoitaka haki na usawa maana Uzalendo sii kupuuza ama kuwakwaza wananchi wengine kwa kuwapachika Imani ya Uzalendo unaofuta ama kupingana na utamaduni, mila na desturi zao. Ifahamike wazi kwamba sisi pamoja na Profesa Safari tumejiunga na Chadema kwa sababu ya Uzalendo wetu kwa kutambua Utaifa wetu na sii vinginevyo. Hatuwezi kukubaliana na sera, ilani, sheria ama kanuni zinazowakwaza waislaam badala ya kuwawezesha kama wanavyowezeshwa wengineo..

Tunawapongeza viongozi wetu kwa Uzalendo walituonyesha toka Mbowe alipokamata uongozi japokuwa kuna migogoro baina yao..Tunatetea M4C kwa sababu inawalenga Watanzania wote ktk ujenzi wa Natinalism lakini kama hatuna majibu ya madai ya Waislaam basi Uzalendo huu hauna manufaa kwetu..Tumechoka na matusi yanayotolewa humu JF kuhusu Uislaam kwa sababu tu wameweka madai yenye kuitaka haki na Usawa.

Udini sio Propaganda tupu. Udini sio kutoa maoni na fikra za madai bali Udini ni kuwakwaza wanaoweka madai yao. Udini ni kuwadhalilisha wengine kutokana na imani yao ili kuwalazimisha wafuate yenu. Hivyo kuna ukweli mkubwa kwamba vijana wa Chadema ndio wana UDINI kwa maana ya kwamba wanaona Uislaam ni imani chafu na imani ya kishetani pamoja na mtume wao..Waislaam hawafikirii hivyo na wala sio madai yao kuhusu Yesu ama mafundisho yake. Badilisheni fikra zenu na mjenge Uzalendo wa kweli tutaweza kuwa pamoja ktk mapambanao haya...
 
Tatizo letu SUGU... ni CCM.

Sijui Sugu naye ataweza kusema hilo?

On the real though, this is a distinction from "tatizo letu CCM".
 
Tatizo letu SUGU... ni CCM.

Sijui Sugu naye ataweza kusema hilo?

On the real though, this is a distinction from "tatizo letu CCM".

we mchizi huwa unanifurahisha sana yaani siku zote huwa unakuja kwa ajili ya kubisha. Lakini mchizi una kipaji aisee!
 
we mchizi huwa unanifurahisha sana yaani siku zote huwa unakuja kwa ajili ya kubisha. Lakini mchizi una kipaji aisee!

Shukran,

Leo nimewapa heko kwa kutofautisha "Tatizo letu CCM" (iliyoletwa jana hapa na nikai-critique) na hii mpya ya "Tatizo letu sugu ni CCM" ambayo ipo karibu zaidi na ukweli.

CHADEMA hawahitaji cheerleaders zaidi kwani wanao kibao.

Wanahitaji critical analysis na constructive criticism ili wajijenge wasiturudishe kwenye haya tunayoyakataa huko CCM.

Katika nchi ambayo taasisi za umma hazijaimarika sana bado, na tuko susceptible to "strongmen centered systems" ni muhimu kuwa na watu wanaokataa kuimba chorus na wanaoangalia mambo kwa principles zaidi na kina kirefu.
 
Mkandara siku zote mimi huwa nashindwa kuelewa ni yepi madai ya Watanzania na ni yepi madai ya Waislamu na ni yepi madai ya Wahindu na ni yepi madai ya wapagani?

Nategemea mtu mkongwe kama wewe usifunikwe na kilemba cha dini kwa kila mtu ana uhuru wa kuabudu, kinachotakiwa wote tukipioganie ni Equal Rights & Justice for all.

Haya mambo ya madai ya Waislamu mimi kwangu naona ni ku entertain mambo ya udini tu.
 
Last edited by a moderator:
cdm bana,leo mahakama wanaisifia kesho ikila kwao wanaiponda haya,tuheshimu mahakama,ilinikera sana pale Arusha ilipokula kwao walisema Ikulu ilitoa maagizo.
 
Mkandara siku zote mimi huwa nashindwa kuelewa ni yepi madai ya Watanzania na ni yepi madai ya Waislamu na ni yepi madai ya Wahindu na ni yepi madai ya wapagani?

Nategemea mtu mkongwe kama wewe usifunikwe na kilemba cha dini kwa kila mtu ana uhuru wa kuabudu, kinachotakiwa wote tukipioganie ni Equal Rights & Justice for all.

Haya mambo ya madai ya Waislamu mimi kwangu naona ni ku entertain mambo ya udini tu.
Utaweza vipi kuweka equal rights pasipo kujali madai ya makundi yetu?..Utawezaje kusema ELIMU sawa kwa wote lakini usijali tofauti zilizopo baina ya wanawake na wanaume?. Justice itaweza tu kutumika kwa kutambua kwamba wanawake wamedai kutoshirikishwa ktk maswala ya elimu na ujenzi wa taifa isipokuwa wakiambiwa mahala pao ni jikoni, halafu kwa kumbeza madai yoyote ya kutokuwa na elimu ni kutokana na yeye kukaa jikoni wakati watu wengine wanakwenda kusoma. Hivi ndivyo tunavyowasikia nyie Mkitutukana waislaam wakati tunajua mnaamini kuwa Waislaam sio watu wa kuthaminiwa sawa.

Udini ni vitendo vya kumdharau mwenzako na sio yule anayelalamika hapa ndipo mnapokosea sana. Sisi tunadai equal rights, vitu kama Muafaka wa MoU tunaambiwa ati na nyie ombeni sasa nani atamuombea Mpagani walio asilimia 30 ya wananchi?. Kifupi baina ya Wapagan na waislaam tupo asilimia sii chini ya 60 lakini Muafaka wa MoU umejengwa kuwapa uwezo kanisa kuendesha maswala ya Elimu na Afya nchini bila ridhaa ya makundi haya.

Unazungumzia equal rights! kwa nini shule za makanisa na hospital zisiwe Private zikijiendesha zenyewe kama zilivyo shule na Hospital za wengine. Kwa nini serikali iweke mkono wake ndani, kuziwezesha hizi zifanye kazi wakati inaacha shule na Hospital za Wapagani kina Kariuki..Kwa nini tusiwe na mfumo mmoja kwa shule na Hospittal zote private nchini bia kujali dini zao?..Sijui wewe unatazama vipi Udini lakini hapa hakuna equal rights wala justice maana sio swala la mlengwa hata Mabeberu wanakuja chimba madini yetu wanasema ni kwa faida ya Watanzania ilihali wanatuibia maliasili zetu. Ukimuuliza Mzungu hatakuelewa kabisa kama wanatutawala kiuchumi..Think large!
 
...tumeona mchango wa Godbless Lema (CHADEMA) aliyevuliwa ubunge wa Arusha. Vipi mchango wa Aeshy (CCM) aliyevuliwa ubunge Sumbawanga mjini? Karibu Kafumu usaidie kuiimarisha CCM yetu inayozidi kuporomoka kila kukicha

Hahahahahahaha hapo tu.. Lazima Kujinyonga mwaka huu
 
Hivi nyie huwa mnaanza na viroba kabla ya kuandika? Kwani mtu kuwa mzalendo maana yake ni kutolipwa?

Narudia kauli yangu ya awali "SERIKALI YA CCM PIGA MARUFUKU VIROBA AU WAAMURU WATENGENEZAJI WAPUNGUZE ALCOHOLIC CONTENT YAKE".

hahahahahahahaha
 
Back
Top Bottom