Prof. Abdallah Safari, uzalendo wako ni wa kupigiwa mfano ndani ya CHADEMA

Mkuu Mkandara kwanza kabisa nikiri kwamba wewe ni mmoja kati ya watu ninaowaheshimu sana hapa JF kwa comments zilizo na ujazo na tena uko objective sana on issues of our national interests. Na kwahakika najifunza mengi sana toka kwako na maandiko yako hapa JF.

Samahani lakini mkuu, unaonaje ukitumia kipaji chako, taaluma yako, uzoefu wako, ujuzi wako na nguvu zako kujaribu kutoa suluhisho la matatizo/maswaibu/malalamiko ya waislamu ili kuwasaidia wale wasiofahamu exactly ni mambo gani yanayodaiwa na waislamu ambayo yanahitaji kuungwa mkono na wazalendo wote.

Nadhani ni muhimu sana usikwame kwenye tope la kuwa mlalamikaji, kama walivyo viongozi wetu; DC analalamika, RC analalamika, Waziri analalamika, Waziri mkuu analalamika na Raisi naye analalamika! Naomba utusaidie kutoa/kupendekeza suluhu ya matatizo hayo ili tupate pa kuanzia.
Kwa sasa naomba kuishia hapa kiongozi wangu.
 
Last edited by a moderator:
...tumeona mchango wa Godbless Lema (CHADEMA) aliyevuliwa ubunge wa Arusha. Vipi mchango wa Aeshy (CCM) aliyevuliwa ubunge Sumbawanga mjini? Karibu Kafumu usaidie kuiimarisha CCM yetu inayozidi kuporomoka kila kukicha
Aeshy sasa anauza unga na ulezi na kafumu ameahidi anarudi kutuingiza mkenge kwenye mikataba ya madini. SIASA hawaziwezi, hela ya kukusanya watu kwenye malori hawana!...
 
kweli usipoelewa ushabiki wa siasa utaishia kushangaa kila siku, ukishinda haki imetendeka, ukishindwa wamependelea, loh!
unabwabwaja sana,una fangasi mdomoni,hisia za kukata rufaa au kukubali yaishe ni vyema mkaangalia court precedence,logic ya ushahidi,ya igunga huwezilinganisha na evidence za burian,judgment ilifanyika kwa hisia bila hata visible evidence,ukibarehe ama kuvunja ungo ukue na akili pia,
 
Mkuu Mkandara kwanza kabisa nikiri kwamba wewe ni mmoja kati ya watu ninaowaheshimu sana hapa JF kwa comments zilizo na ujazo na tena uko objective sana on issues of our national interests. Na kwahakika najifunza mengi sana toka kwako na maandiko yako hapa JF.

Samahani lakini mkuu, unaonaje ukitumia kipaji chako, taaluma yako, uzoefu wako, ujuzi wako na nguvu zako kujaribu kutoa suluhisho la matatizo/maswaibu/malalamiko ya waislamu ili kuwasaidia wale wasiofahamu exactly ni mambo gani yanayodaiwa na waislamu ambayo yanahitaji kuungwa mkono na wazalendo wote.

Nadhani ni muhimu sana usikwame kwenye tope la kuwa mlalamikaji, kama walivyo viongozi wetu; DC analalamika, RC analalamika, Waziri analalamika, Waziri mkuu analalamika na Raisi naye analalamika! Naomba utusaidie kutoa/kupendekeza suluhu ya matatizo hayo ili tupate pa kuanzia.
Kwa sasa naomba kuishia hapa kiongozi wangu.
Kwanza nashukuru kama unanifuatilia maana sii rahisi kuwa na wafuasi wanaopenda kujifunza ama kukosoana maana janvi hili linatuweka pamoja kutafuta suluhu ya matatizo/maswaibu na malalamiko yetu..

Mkuu wangu nimeandika sana humu JF kuhusiana na swali lako..Na sii tu kuweka malalamiko bali hata jinsi ya kuyatatua lakini imekuwa sumu kwa wengine. Na sii kwamba nalalamika mimi kwa sababu ni Muislaam isipokuwa athari za mfumo wenyewe ndio unapelekea mimi nikubaliane na malalamiko yaliyoletwa na waislaam kwa maana kwamba hata ingekuwa ni Wakristu waliolalamika bado ningewaunga mkono. Hivi Ndivyo nilivyo ktk mitazamo yangu.

Mkuu wangu sisi wote ni maskini sana na naelewa na kumkubali mwalimu Nyerere aliposema maadui wetu ni watatu yaani UMASKINI, UJINGA na MARADHI hivyo jukumu la kupambana na maadui hawa ni la Kitaifa na letu sote. Sasa inanishangaza sana ilipofika mwaka 1992 chini ya rais mstaafu Mwinyi (muislaam) alipobadilisha mfumo wa ELIMU na AFYA na kuuweka chini ya kikundi cha watu kwa madai ya kwamba serikali yetu ilishindwa kuendeleza elimu na Afya (Japokuwa hii ni tungo za watu)..

Sasa jiulize ikiwa serikali ilishindwa kuhudumia elimu na Afya na kanisa lina uwezo huo inakuwaje serikali isiyokuwa na uwezo na iliyoshindwa kuhudumia ndiyo inatakiwa leo kutoa fungu la fedha za bajeti yake pamoja na vyanzo vyake kuwapa kanisa wenye uwezo kuendesha elimu na Afya?. Yaani ndugu yako asiyekuwa na uwezo anapokuomba umsaidie kuwasomesha watato wake inawezekana kweli wewe ndio umtoze yeye fedha za hata kuendesha maisha yako ilihali wewe ndiye mwenye uwezo!. Hii kweli imekaa sawa?

Kwa hiyo dhana ya kwamba serikali ilishindwa sii ya kweli isipokuwa tulichezewa akili maana ilikuwa deal la watu. my case in kwamba kama ingekuwa kweli serikali isinge endelea kujenga shule zake na Hospitali na hata kutoa huduma hiyo kwa asilimia 50 hadi leo na wameongeza huduma hizo kwa asilimia zaidi ya 300 yoka 1992. Wanaendelea kujenga mashule na Hospital na zaidi ya hapo serikali inalazimika kuwasomesha walimu wanaoletwa na kanisa bure ktk vyuo vyake..Asilimia 80 ya matumizi ya ELIMU na AFYA ni katika matumizi ya ndani sio ya maendeleo ilihali navyosikia bajeti yetu japokuwa inapata support ya asilimia 40 kutokana na wafadhili lakini asilimia tena zaidi ya 70 inakwenda ktk shughuli za elimu na Afya hvyo kuyafanya makanisa kuwa wadau wa fedha hizo..

Ubora wa Elimu na Afya nchini umeshuka sana, tunaona migogoro kila siku walimu na madaktari wakigoma kutoa huduma kwa madai halali kabisa kwamba hawalipwi mishahara mizuri, hawana vifaa wala posho kwa kazi kubwa wanayoifanya. Hapa tunaathirika sote sii waislaam wala wakristu lakini naposema huu mfumo uloletwa ndio sababu kubwa ya kushindwa kwetu. Watu wanachukia kwa sababu nimeligusa kanisa. Hivyo kama tunavyopinga posho na mishahara mikubwa kwa wabunge na viongozi ni lazima pia tukemee matumizi mabaya ya fedha za umma ktk kupambana na Umaskini. haijalishi fedha hizo wanapewa kanisa, msikiti au baba yangu mzazi.

Na nasema tena hata wangekuwa wamepewa waislaam ningepiga vita kwa sababu lengo la mfumo huu sii kuboresha elimu na Afya nchini bali kuna watu wanataka kutumia makanisa kujipatia Umaarufu. Lowassa alianza kazi hii toka mwaka 1990 na amefanikiwa kwa kiwango kikubwa sana kufika hapo alipofika. Hana imani ya dini wala kupenda sana wananchi wake isipokuwa anajua Siasa za Tanzania pasipo support ya watu huwezi kufanikiwa. Na amelitumia kanisa muda wote wa maisha yake ndani ya siasa za Tanzania. Ni mchezo unaofanywa na baadhi nya viongozi wa CUF kwa kutumia Uislaam na Uzanzibar kujaribu kujenga umaarufu wao wenyewe na sii kwamba inawauma sana..

Kwa hiyo mkuu wangu, ELIMU na AFYA virudishwe chini ya mamlaka ya serikali..Halafu wenye kufungua shule private iwe kanisa, msikiti, Hindu ama Wapagani watakuwa na sheria moja kwa wote. Kama serikali itatoa ruzuku basi ruzuku hiyo ihusiane na kuwawezesha watoto wetu kusoma shule hizo na sio kuendesha ujenzi na shughuli za shule hizo. Serikali yetu haina fedha za kuwalipa walimu na madaktari lakini ina fedha za kuwagawia makanisa wenye uwezo mkubwa kuendesha shule zao. .Hii kweli inaingia akilini, badala ya haya makanisa kuisaidia serikali hata kutoa huduma za Elimu na Afya karibu na bure maana wanapewa fungu la fedha zilizokopeshwa serikali yetu na tutalipa deni hilo sisi wote. Makanisa wana fedha na nakuhakikishia Vatican hawashindwi kuendesha shule zake na tumeona nchi zote wanakowekeza ni msaada zaidi ya biashara isipokuwa Tanzania tu. Na sidhani kama waliomba jkusaidiwa isipokuwa kuna viongozi hapa nchini ngozi nyeusi wanalitumia kanisa kujinufaisha wao kisiasa na kifedha.
 
Mkandara lets assume kwamba Makanisa na Wakristo wanapendelewa, je hili linaweza kuwa sababu ya Waislamu kuwa na chuo kimoja tu kikukuu tena majengo ni ya Umma, pili matokeo mabaya kwa shule zinazomilikiwa na Taasisi za Kiislamu yanatokana na mfumo kristo?

Kwa Mfano watu wote makini tunampinga Lowasa, lakini je huoni Lowasa makanisa yanavyomtumia kufanya Harambee za Mamilioni kwa ajili ya vyuo na Maospital ya kanisa?

Hivi Mkandara hawa kina Agha Khan ni Waislamu wa division two, au wote mtume wao ni SWA? kwa nini Waislamu hawa mambo yao safi na tatizo ni kwa Waislamu hawa ambao ukiwaita kwa majina yao stahili utasema tunawakashifu? mimi naomba tu kujuwa kwamba hawa siyo waislamu?

Hivi mtu mwenye msimamo kama yule aliyemzaba kibao Mzee Mwinyi hivi mtu wa namna ile mtakaa muelewane naye kitu gani jamani to be honnest?
 
unabwabwaja sana,una fangasi mdomoni,hisia za kukata rufaa au kukubali yaishe ni vyema mkaangalia court precedence,logic ya ushahidi,ya igunga huwezilinganisha na evidence za burian,judgment ilifanyika kwa hisia bila hata visible evidence,ukibarehe ama kuvunja ungo ukue na akili pia,

Mkuu hapa tunaelemishana tu, hatugombani! inakuwaje unanirushia maneno kama hayo? mbona mimi sijakutukana?
 
Mkandara lets assume kwamba Makanisa na Wakristo wanapendelewa, je hili linaweza kuwa sababu ya Waislamu kuwa na chuo kimoja tu kikukuu tena majengo ni Umma, pili matokeo mabaya kwa shule zinazomilikiwa na Taasisi za Kiislamu yanatokana na mfumo kristo?

Kwa Mfano watu wote makini tunampinga Lowasa, lakini je huoni Lowasa makanisa yanavyomtumia kufanya Harambee za Mamilioni kwa ajili ya vyuo na Maospital ya kanisa?

Hivi Mkandara hawa kina Agha Khan ni Waislamu wa division two, au wote mtume wao ni SWA? kwa nini Waislamu hawa mambo yao safi na tatizo ni kwa Waislamu hawa ambao ukiwaita kwa majina yao stahili utasema tunawakashifu? mimi naomba tu kujuwa kwamba hawa siyo waislamu
Matola mbona unarudia yale yale nilokwisha yajibu miaka mingi tu.. UISLAAM ni imani ya kumwabudu MUNGU haina jukumu la kuelemisha watu. Sitaki kwenda kuzungumzia mfumo wa Ukristu kwa sababu sii imani yangu kabisa. na sikubaliana na msikiti kufungua shule za kufundisha elimu dunia kwa watu wote kwa sababu hii sio kazi yao ila kufundisha dini. hao waliofungua Tanzania ni kutokana na mfumo uliopo. Hivyo matokeo ya makanisa au misikiti kufundisha elimu dunia imewa brain wash watoto wakubali kwanza imani ya dini zao..

Mimi nilikuwa mmoja wa watoto waliolazimika kubadilisha jina na Kuijiita Emmanuel ili kuwa registered Namibu Primary school mwanzo mwa miaka ya 60.. Hivyo hadi Nyerere alipotaifisha shule za makanisa ndipo nilipoweza kurudi na kutumia jina langu halisi..Misikiti ni ya IBADA, dini ni ya kumwabudu Mungu sio ya kueneza elimu dunia wala kuendesha shughuli za Afya. Tunazo serikali na watu binafsi wanaoweza kuifanya kazi hiyo na ndilo jukumu lao kwa sababu hii sii kazi ya kiroho wala msaada bali ni kutokana na mahitaji ya kidunia.

Matokeo mabaya ya shule za kiislaam ni kwasababu shule hizi zinapokea watoto waliokwisha shindwa (kabuntasi) watoto walioshindwa mitihani ya darasa la 7, 12, na 14 hivyo wana kazi kubwa ya kuwafundisha watoto walioshindwa pamoja na yule aliyesoma shule ya kanisa na akashindwa. Hawa wiote wanakwenda shule za waislaam haijalishi dini yake na hataweza kushinda maana kichwani hamna kitu. Lakini kwa ujumla wake nchi nzima elimu imeshuka kwa sababu tuna shule za watoto wenye akili wakienda kusoma shule za serikali na kanisa halafu wale kabuntas wanaenda kusoma shule za Waislaam na private pasipo kutihaniwa..Hata mtoto anayefanya vizuri ukimweka na kundi hili inawezekana kabisa akaishia kuwa failure.. Huu ndio mfumo kristu tunaozungumzia.

Hivyo huwezi kunambia shule za kiksritu zinafanya kazi vizuri zaidi wakati haichukui watoto walio fail mitihani hali wakijiita Private. Naomba siku moja wachukue watoto walio fail darasa la 7, 12 na 14 Halafu shule za kiislaam zichukue wale walioshiinda kisha tuone kama kweli kanisa litaweza kubadilisha matokeo mwisho wa mwaka. halafu mkuu wangu hatushindani hapa kuona mbora yupi isipokuwa tunawajenga Watanzania.

Kwani hao Mapadre wenyewe wanashindwa kufanya harambee hadi aje Lowassa? mbona kila Jumapili kuna Harambee makanisani iweje kanisa linamhitaji Lowassa wakati watu wanazitoa fedha zao kwa sababu ya kanisa na sio Lowassa!..Think again who is using who?

Unazungumzia AghaKhan huyu ni mfanya biashara. tajiri aliyerithi utajiri mkubwa wa wazazi wake ambao wali dedicate fungu la utajiri wao kusaidia watu wao. Ni sawa na sadaka anayoitoa Bill Gates huwezi kusema ndivyo Waamerika wote wanatakiwa kuwa kama yeye. Uislaam hauna mahusiano yoyote na AghaKhan, hizi ni fedha zake anafanya biashara zake na kati ya faida zake ndio hupeleka ktk misaada. He is a businessman first na imekuwaje shule zake hakurudishiwa?
 
Mkandara sasa umediscus vitu objectively and fact, nadhani watu wenye busara husema kwamba kuligunduwa tatizo ni nusu ya kulitatuwa tatizo hilo, mimi napenda kujifunza kutoka kwa mtu nitakayeamini kama ana material ambayo napaswa kuchota busara zake kama wewe.

Kumbe mimi nilichokigunduwa hapa tutapigizana kelele kila siku na kutengana kwa misingi ya kidini kumbe tatizo watu wengi hawajalitambuwa, tatizo siyo sisi, sisi sote ni ndugu ila tatizo ni CCM, hii mifumo yote inayolalamikiwa ni tatizo la CCM na wala siyo la Wakristo wala kanisa.

Kama nimekuelewa vizuri dini ya Kiislamu ilivyoingizwa nchini ilikuwa ni kwa ajili ya Elimu akhera tu, lakini Missionary walivyokuja walikuja na Elimu, Shule, na Afya. hapa ndipo msingi wa Serikali yetu baada ya Uhuru ndipo makosa yalipofanyika, maana Uislamu haukuja kuleta Elimu Dunia wala Huduma ya Afya.

Hapa sasa ndipo panapohitajika hekima maana ni vigumu kutumia zile hekima za Nyerere kwamba mtoto wa Lindi akipata pass max 60 na mtu wa kaskazini akipata pass max 80 basi inabidi achukuliwe huyu wa max 60 ili kubalance, hii haiwezi kufanya kazi kwa sasa.

Kinachopaswa sisi kama Taifa tubadili mindset kwanza, lakini silioni hilo kama linawezekana maana CCM ndio beneficiary wa utengano wa Kitaifa, kwenye Mshikamano wa kitaifa kamwe CCM haiwezi kupumuwa, CCM ina viongozi njaa wake inaowatumia kama Bakwata na Wachungaji uchwara wa makanisa mbalimbali wakiwemo Mzee wa Upako na wakati wa nyuma kanisa katoliki.
 
WAKATI Chama Cha Mapinduzi kikisema kwamba kitakata rufaa kupinga hukumu, Wakili Profesa Abdallah Safari aliyekuwa akimtetea mgombea wa Chadema, Joseph Kashindye katika kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Igunga, amesema haikuwa kazi rahisi kukibwaga chama tawala.

Kauli ya Profesa Safari imekuja siku moja baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, kutengua matokeo ya ubunge wa jimbo hilo yaliyompa ushindi mgombea wa CCM, Dk Dalaly Peter Kafumu.

Profesa Safari ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema alisema ugumu katika kesi hiyo ulitokana na mashahidi wengi kuwa waoga. Profesa Safari alisema jana kwamba mashahidi wengi walikuwa wakiogopa kutoa ushahidi dhidi ya viongozi ambao walihusishwa kwenye kesi hiyo.

“Katika kesi hii, mashahidi wengi walikuwa waoga hasa kwa kuwa walikuwa wakitoa ushahidi dhidi ya viongozi kwa mfano, ukimwambia mtu atoe ushahidi dhidi ya Rais Mstaafu Benjamin Mkapa anaogopa,” alisema na kuongeza;
“Kwa mfano, ushahidi dhidi ya maneno aliyosema Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama ulifanikishwa na waandishi wa habari kwa kuthibitisha kuwa alitamka maneno yale.” Alisema kesi hiyo imekigharimu Chadema hicho fedha nyingi.
Jitihada za gazeti hili kumpata Kashindye ziligonga mwamba baada ya Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Igunga, Khamis Majimoto kusema kuwa ni mgonjwa.

“Huyu bwana anaumwa na hata hukumu ya jana hakuhudhuria lakini kwa taarifa zozote zinazohusu suala hilo mimi ndiye mzungumzaji,” alisema. Alisema baada ya hukumu Chadema kinajipanga kwa ajili ya mikutano ya hadhara kuwashukuru wananchi wa Igunga ambao walichangia zaidi ya Sh5 milioni kufanikisha kesi hiyo na kwa ushahidi kilioupata. CCM rufaa

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema chama chake kitakata rufaa kupinga uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora kumvua ubunge Dk Kafumu.
“Chama Cha Mapinduzi kimetafakari hukumu ya kesi ya uchaguzi iliyotolewa Agosti 21, mwaka huu na Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora, chama kimejiridhisha na kufanya uamuzi wa kukata rufaa dhidi ya hukumu ya kesi ya uchaguzi, dhidi ya Dk Kafumu,” alisema Nape na kuongeza:

“Kusudio hilo linatokana na kutoridhishwa na hukumu hiyo.” Awali, Mweka Hazina wa CCM, Mwigulu Nchemba alisema kuwa chama hicho tawala kinaheshimu uamuzi huo wa Mahakama na kwamba kinajipanga kwa ajili ya uchaguzi mwingine. Nchemba ambaye alikuwa Meneja wa Kampeni wakati wa uchaguzi huo mdogo uliompa ushindi Dk Kafumu alisema CCM kinaheshimu uamuzi wa Mahakama lakini akasema kilikuwa kinasubiri kauli ya mwanasheria wa chama hicho kabla ya kutoa msimamo wake.

Nchemba ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi, alisema CCM kipo vizuri pande zote na endapo uchaguzi utarudiwa, kina uhakika kuwa Dk Kafumu au mwingine yeyote wa CCM atashinda. “Kwa jinsi uamuzi ulivyotolewa na hali halisi ilivyo, nina uhakika hata uchaguzi ukirudiwa kesho, basi Dk Kafumu atashinda. Kitakachobadilika ni kuwa Dk Kafumu atavunja rekodi kwa kuwa kiongozi aliyeapa mara nyingi katika Bunge,” alisema.

Alisema ingawa Dk Kafumu mwenyewe amekiachia chama uamuzi wa kukata rufaa au vinginevyo, ana uhakika kuwa watakuwa naye bungeni Novemba akiendelea kuchapa kazi.

Sheria ibadilishwe

Wakizungumzia hukumu hiyo, baadhi ya wasomi wamesema umefikia wakati wa kuwa na sheria itakayolifanya taifa kutoingia katika chaguzi za mara kwa mara kwa kuwa zinagharimu fedha nyingi ambazo zingeweza kutumika katika shughuli nyingine za maendeleo. Profesa Gaudence Mpangala wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), alisema umefikia wakati Tanzania kuwa na utaratibu kama unaotumika Afrika Kusini ambao mbunge wa chama husika akifariki au kupokwa ushindi, aliyemfuatia kwa kura ndani ya chama chake ndiye anayechukua nafasi. “Utaratibu huu kwa kiasi kikubwa unaondoa gharama za uchaguzi…sioni umuhimu wa Tanzania kuendelea na utaratibu wa sasa kwa kuwa fedha zinatumika nyingi katika uchaguzi,” alisema Profesa Mpangala. Kuhusu hukumu ya Igunga alisema:
“Pamoja na hayo ninamsifu aliyetoa hukumu.
Hii ndiyo misingi ya kidemokrasia tunayoitaka.”

Kwa upande wake, Dk Kitila Mkumbo alisema: “Kama ikitokea mbunge kafariki au amebainika kushinda katika njia zisizostahili, basi yule aliyekuwa wa pili katika kura za maoni za chama husika ndiye awe mbunge.”
Mhadhiri mwingine wa UDSM, Bashiru Ally alisema ni muhimu kwa jambo hilo kujadiliwa wakati huu wa kupata Katiba Mpya ili kuepusha matumizi makubwa ya fedha katika chaguzi ndogo.

“Tunatakiwa kuwa na mfumo wa uwiano na ijulikane wazi wananchi wanachagua nini kati ya chama na mgombea,” alisema Bashiru na kuongeza: “Kura za uchaguzi mkuu ndizo zinazoamua mgombea wa chama gani kashinda, kama ndiyo hivyo basi kuwe na utaratibu wa yule aliyeshika nafasi ya pili katika kura za maoni ndani ya chama chake awe mbunge ikitokea mbunge wa eneo husika amefariki, ambaye pia ni wa chama hichohicho.

” Alisema tangu mfumo wa vyama vingi uanze, imeshafika miaka 20, hivyo kuna umuhimu wa kulijadili suala hili ili fedha zinazotumika katika chaguzi ndogo zipelekwe katika shughuli nyingine za maendeleo. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria (OuT), Profesa Tolly Mbwete alisema kufanyika kwa chaguzi za mara kwa mara ndiyo gharama ya demokrasia lakini akasema suala hilo linaweza kujadilika ili kuja na mfumo mzuri zaidi. “Hili ni jambo ambalo taifa linatakiwa kuamua, inawezekana kama Watanzania wakiamua” alisema Prof Mbwete.
 
Jamani MWITA MARANYA, MATOLA na MKANDARA mbona mnaenda nje ya mada?. Hebu tujadili maudhui ya uzi husika, msijikite udini tu wakati hilo sio kusudio la mleta mada.
 
Watanzania wote ni ndugu tufikirie mustakabali wa taifa. Kama mfumo wa kiutawala uliopo unatukandamiza ni muhimu tutambue hilo na tuanze kuushughulikia ili tuuangamize na kujiwekea mfumo utakaotufaa bila kujali matabaka ya kiitikadi, kidini, kikabila nk.
 
Wasomi waliopo ccm magarasa tu wameshindwa kukisaidia chama na nchi
 
sasa mbona lugha gongana wao kwa wao

Nape - tutakata rufaa
Mwiguru - tutarudia uchaguzi

nani bosi ?? hivi hiki chama hakina msemaji mkuu wa chama ?? wapi katibu mkuu duh !! kweli kimejifia
 
Naona maprofesa na madaktari wote wanaotoa maoni juu ya kupunguza gharama za uchaguzi kwa kumkaimisha mshindi wa pili katika kura za maoni za vyama husika wanakosea na pengine hawajafikiria zaidi ya upande mmoja.
1.Washindi wa kura za maoni hupigiwa kura na wanachama na wapenzi wa chama husika.
2.Wagombea ubunge hupigiwa kura na makundi mbalimbali, kuna uwezekano aliyepiga kura akawa kapiga kura kwa sababu ni mwanachama wa chama husika au akawa si mwanachama na vilevile wapo wanaopiga kura kwa kuwa wana imani na mahaba kwa mgombea, mwisho wapo wanaopiga kura kwa kuwa tu wamepewa takrima au chochote kitu.
Kama ukiitafakari hii kauli yangu namba mbili,binafsi ninaamini kabisa, mbunge kama akifariki au akivuliwa ubunge, mwakilishi wa chama kinachoshika nafasi ya pili ndio akaimishwe nafasi iliyoachwa wazi.
 
Back
Top Bottom