Precision Air, hii ndio Customer Care mliyofunzwa?

Precision Air, hii ndio Customer Care mliyofunzwa?

Kwenye ndege kuna kitabu chao yule mama CEO anajisifu kuwa ameweza kutatua tatizo la delay na cancelation kwa 80%...upuuzi mtupu maana ndege za Zanzibar na Mwanza ndo zinaongoza kwa delay.. Wanatabia ya kuleta watu toka mwanza ndege ya saa12 wanawaleta saa5 usk wanafika dar saa8 usk...wamefilisika kiela na kihuduma
 
mbali na matatizo haya ya Precision Air pia watanzania tuna mapungufu katika suala la huduma kwa watejal. Ndo maana kuna mahotel kibao mjini wanaajiri wakenya.

Inahitaji akiri kidogo kwa yeyote bila hata kuambiwa kuchukua juhudi hata za kutoa taarifa. Mwanzoni aliyonza huyu MD mpya mmama,walijaribu lakini naona naye ilikuwa nguvu ya soda. hata hivyo uenda wakisoma haya, watayafanyi kazi.
 
PW must chance their name to UNPRECISION-AIR.
In short PW sucks big time.
 
...

.....pole Preta !!!!

......mimi waliniuzi sana ila nilicho kifanya hawatasahau !!!
 
Ukiwa mteja wa PW yakupasa uwe mvumilivu sana.... Vinginevyo panda tu Ngorika ili kuepuka kadhia kama hizi.
 
kwa sababu wanajua hapa kwetu hakuna wa kumlalamikia.......sasa wasubiri hao walioenda kwao sijui watarudi na maoni gani........

Wazungu ni wabaya sana kwa fitna watapajua pa kuwashughulikia lazima hii biashara ya kiccm ife
 
Hilo shirika linaonekana tatizo ni uongozi mbaya tena sana,
Sasa jiulize mtu anabishana na mteja anasababishwa mteja ashushwe eti shirika la ndege huu ujinga uongozi ndio unasababisha wafanyakazi wawe na vibri.

Kwakitendo chakumzalilisha doctar Rweyetama na rudisha likadi lao la umember ship na un subsribe email yangu wasinitumie offer zao ntapanda Aibus fastjet na isamilo huu ni upuuzi mafanyakazi hayana adabu na roho mbaya.
 
Nimebook flight ya wageni wangu kutoka Arusha kwenda Zanzibar na kurudi Arusha.....mmewapeleka vizuri........siku ya kurudi nimere-confirm na mkanihakikishia hiyo flight ipo.......wageni wangu wamecheck in saa 1215......kumbe mmecancel hiyo flight lakini hamkuwaambia........kwa nini wakati wana check in hamkuwaeleza wakarudi kufanya shuguli zingine.....?....hilo mnalijua wenyewe......

Watu wamekaa airport kuanzia saa tano mpaka saa kumi na mbili jioni kusubiri flight ya kutoka Zanzibar-Dar-Jro.....na route ilikuwa ni Znz-Dar-Ars.....nyie ni kina nani mpaka muharibu mipango ya watu.....?......kwa shingo upande walikubali huo upuuzi wenu kwa sababu hawakuwa na la kufanya......

Wamefika Dar wakaconnect vizuri mpaka JRO.....wamefika saa nne usiku.....hapo mliwahakikishia kuwa shuttle yenu itawasubiri kuwapeleka mjini kwa sababu kwanza mmewapotezea muda na mmewachosha......kufika JRO mnawaambia kuwa shuttle imeshaondoka kwa hiyo wakodi tax....really.....!!......bahati mbaya mlikuta wapo ngarangari.....likawashuka.....mkawakodia tax....ok wapeni basi mizigo yao waende.....khaaa....mmeiacha Dar.......what the f**k was that....!!....saa sita usiku.........kweli mmefuzu taaluma ya u-customer care.........kesho yake mkawaletea mizigo yao but hamkuwaomba hata radhi ya usumbufu.......man***na.......

Sasa basi.....wageni hao hao baada ya week na nusu wanarudi kwao.......wanakwenda Nairobi kuconnect international flight....mmewahakikishia shuttle yenu itaondoka saa tisa na nusu usiku kuwapeleka JRO.......tisa kamili wawe wamefika kituoni kwenu......usiku kama huo mtu hajalala.......ameamka kwenda kuwahi flight......kumbe hiyo shuttle haipo....mmecancell bila kusema.....mnapigiwa simu hampokei.....kweli......?......mlitegemea mtu afanye nini wakati huo ili hali taarifa hamkumpa.......?

Siwaharibii biashara lakini siku nikisikia mtu anasema anataka kufly na nyie......nitamkataza hata kwa kuvua nguo.......

ASANTENI SANA KWA HUDUMA YENU NZURI.......
Naamini kupitia JF ujumbe wangu umewafikia..........


it happens once in a while, safari ni hatua....

to me precisionair is probably the best we have in Tanzania
 
Kwenye ndege kuna kitabu chao yule mama CEO anajisifu kuwa ameweza kutatua tatizo la delay na cancelation kwa 80%...upuuzi mtupu maana ndege za Zanzibar na Mwanza ndo zinaongoza kwa delay.. Wanatabia ya kuleta watu toka mwanza ndege ya saa12 wanawaleta saa5 usk wanafika dar saa8 usk...wamefilisika kiela na kihuduma
Hapo ktk bold nilisoma na kushangaa sana, nilikuwa natoka Arusha kwenda Dar via Zenji. Nilikumbwa na dhoruba ya delays na kukosa deals kibao.
 
Kama nawaona vileee wahusika wa PW wanasoma hii mada na kukenua meno kwa kejeli mwisho wanamalizia na msonyoo na kijitusi cha kufumbia jicho.
 
Nyangau kabisa hawa kuna siku ndege ya kuondoka saa saba tuliondoka saa kumi mbaya zaidi wako kimyawala hawasemi
sijui wanakuwa hawajui yaani kama mabasi ya kwenda ikwiriri,msata,nkasi
 
Wazungu ni wabaya sana kwa fitna watapajua pa kuwashughulikia lazima hii biashara ya kiccm ife

Kuna mama alikuwa anahojiwa katika redio.........basi kila baada ya maneno kadhaa, anaingiza neno 'promise' !
Naona na wewe umeathirika na neno CCM !
 
Ndo madhara ya kuua air tanzania

Pw watawatia wabongo vidole vya macho, maana hawajali na wanajua hawana ushindani mkubwa. Fill dharau
 
Pole sana shit happened
Tulibook flight ya Tbr -Dar, reporting time 9oclock kufika saa mbili na dkk 40 ndege inafunga mlango wakasema mabadiliko yalikuwepo ilikuwa uambiwe simple as that aaaaaggggggh
 
Back
Top Bottom